ELININO KUUKUMBA MKOA WA PWANI, MINGENEYO
MASIKA KUIKUMBA MKOA WA PWANI, MINGENEYO
NA TANPRESSTZ,
MKOA wa Pwani ni miongoni mwa mikoa kadhaa itakayo kumbwa na mvua kubwa ‘Elinino’ kuanzia mwezi Oktoba hadi kufikia Disemba Mwaka huu 2023 Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imetangaza.
Kwa mjibu wa taarifa hiyo iliyotolewa wiki hii na TMA, wananchi wa mikoa hiyo, wanapaswa kujiandaa na mafuriko, huku wakulima wakijiandaa vyema na kilimo cha vuli kwani mvua itakuwa ya kutosha katika kipindi hicho cha kuelekea mwishoni mwa Mwaka.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Meneja wa utabiri Hali ya Hewa, Julai 19, 2023, Dk.Mafuru Kantamla, imesema kuwa hadi sasa uhakika ni asilimia 90 kwamba mvua kubwa ya El nino itanyesha kuanzia kipindi cha vuli.
ametaja mikoa hiyo kuwa ni Pwani ikiwemo Arusha,Manyara,Kilimanjaro,Dar es Salaam, Tanga,Lindi na Mtwara…
ngezeko la mvua linasababisha kutabiri uwepo wa El Nino, mfano kipindi cha kipupwe tumeona imeanza kujitengeneza athari zake hatutegemei kipindi hiki ongezeko la mvua kubwa,"amesema Dk Kantamla.
Pia, Dk Kantamla amesema El Nino haitaathiri wakazi bahari ya hindi pekee itasambaa hadi maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani.
“Katika kipindi hiki cha kipupwe TMA inaendelea kufuatilia kwenye mchakato wa kuelekea msimu wa mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza Oktoba hadi Desemba mwaka huu na kuangaliwa athari za El Nino kwa ufasaha Ili kuifahamisha jamii kwa ujumla,”amesema.
Nini maana ya El Nino
Ni hali ya uwepo wa ongezeko la joto la bahari ya katika eneo la kati ya kitropiki la bahari ya Pasifiki, hali hii inapokuwepo kunakuwa na madhara mbalimbali katika maeneo tofauti ya duniani.



