Monday, December 18, 2023

CEVEDE; Vicoba havijabadili jina, usiposajiliwa faini hadi Mil.10

CEVEDE; Vicoba havija-badilishwa jina, usipovisajili faini hadi Mil.10

Na Tanpresstz,Arusha


KITUO cha Vicoba na Maendeleo ya Vikundi (COVEDE) kimetoa taarifa kwamba vikundi vinavyo tumia mfumo wa VICOBA havijafutwa ila vinatakiwa kusajiliwa chini ya sheria rasmi ya huduma ndogo ya fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019 kama vikundi vya kijamii vya huduma ndogo ya fedha.

kwa mjibu wa taarifa iliyosambazwa na mkurugenzi wa COVEDE,

Evance Chipindi  amesema kuwa amesoma Makala mtandaoni yenye kichwa cha habari kwamba kuna sheria mpya imebadili jina la Vicoba na kuitwa C.M.G. jambo ambalo sio sahihi.

“Sheria hiyo imetenga watoa huduma za fedha katika madaraja makuu manne. Daraja la kwanza ni taasisi zinazoruhusiwa kuchukua amana, ambazo pamoja na sheria hii wanatakiwa kutumia pia sheria ya Benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006, daraja la pili watoa huduma za mikopo ambaalo linajumuisha (Taasisi, Kampuni na watu binafsi), daraja la tatu ni vyama vya ushirika wa akiba na mikopo na daraja la mwisho ni daraja la nne linahusika na vikundi vya kijamii vinavyo jihusisha na shughuli za  kukusanya fedha na kukopeshana wenyewe. Daraja hili linahusu vikundi vyote vinavyo tumia mfumo wa VICOBA, VSLA, SILC, IFOGONG’O, Saving Club na vingine”alisema Evance Chipindi

 Aliongeza kuwa yule afisa mendeleo aliyetoa taarifa kwenye kongamano la CHALINZE WOMAN TALK kwamba Vicoba vimebadili jina nakuitwa Community Money Group alipotosha jamii, alitakiwa kuwapa elimu na kuwasisitizia wajasiriamali kwenda  kusajili,  vikundi vyao, ili kuepuka adhabu kama sheria inavyotaka.

“Nisisitize kwa mujibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 ibara ya 28 imeainisha taratibu za usajili wa kikundi na ibara ya 52 ibara ndogo ya (b) imeainisha adhabu. Nanukuu mtu yeyote atakaye jihusisha au kuendesha kikundi bila kusajiliwa atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja na isiyozidi milioni kumi au kifungo jela kisicho pungua miezi mitatu na kisichozidi miaka miwili au kutumikia adhabu zote mbili kwa wakati mmoja”alisema Evance Chipindi

 Anasema Sheria hiyo imetoa mamlaka kwa Benki Kuu ya Tanzania kukasimisha jukumu la Daraja la nne ya vikundi vya Kijamii vya huduma ndogo ya fedha kwa Mamlaka ya serikali za mitaa kwa kufanya kazi ya usajili na usimamizi. Kila halmashauri imeteua msajili wa vikundi mwenye jukumu la kusajili vikundi vyote bila kujali ni VICOBA, VSLA na majina mengine ili mradi vinaendesha shughuli za kuweka na kukopa.

VICOBA ni mfumo ambao unatoa utaratibu wa uendeshaji, usimamizi, uongozi, utunzaji wa kumbukumbu, udhibiti wa fedha, utatuzi wa migogoro na CMGs hii ni sheria ya usajili na usimamizi wa vikundi vyote vinavyo toa huduma ndogo ya fedha na ambayo imetoa mwongozo katika mambo machache sana ya uendeshaji wa vikundi. 

Ametoa wito wadau kuendelea na vicoba huku akiwataka kuzingatia sheria na taratibu ikiwemo kusajiliwa, kupata mafunzo sahihi kutoka kwa wawezeshaji wenu na kuhakikisha taarifa zenu za fedha mnakaguliwa mara kwa mara ili kuepusha upotevu wa fedha.

 tujikumbe awali Akitoa elimu kwenye kongamano la akinamama Women Talk Chalinze, Afisa Maendeleo Wilaya ya Chalinze,Ramadhani Mumba, alisema kuwa sheria imebadili rasmi vikundi vinavyoitwa,Village Community Bank maarufu kama Vicoba, sasa vinaitwa Community Microfinance Group kifupi (C.M.G) hiyo ni kwa mjibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya Mwaka 2019/2020 na kanuni zake.

“Vikundi vya vicoba vimebadilishwa jina kutokana Village Community Bank na sasa vinajulikana kama vikundi vya kijamii vinavyotoa huduma ndogo za kifedha CMG na uendeshaji wake unafuata sheria kwahiyo lazima visajiliwe,

….. vicoba ni kitu kikubwa, kwa mjibu wa sheria hiyo ukikutwa unashiriki kikundi ambacho hakijasajiliwa faini kuanzia mil.1 hadi 10 au jela miezi 6”alisema Mumba


 

 

 

Labels: