Friday, October 10, 2008

KUBENEA: SERIKALI IMEDHAMIRIA KUANGAMIZA MWANAHALISI.

Awasilisha utetezi wake kwa Serikali
Adai ana ushahidi wa Kikwete kungo’lewa na wenzake 2010.
Ahoji kwanini Rai haikubanwa kama MwanaHalisi
Asisitiza MwanaHalisi kuendelea kuikosoa serikali

Na. Mwandishi wetu

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers inayochapisha magazeti ya MwanaHalisi na Mseto, Saed Kubenea, amesema sasa ni wazi kwamba serikali imedhamiria kuangamiza gazeti la MwanaHalisi kwa kulituhumu, isivyo halali, kuwa linafanya uchochezi.

Kubenea aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye ofisi za gazeti hilo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, na Idara ya Habari (MAELEZO), kulalamika na kulitaka gazeti hilo lijieleze kwanini lisichukuliwe hatua kufuatia habari yake ya jumatano iliyopita, kuwa kuna njama za kumng’oa Rais Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010.

Alisema habari ya MwanaHalisi inayolalamikiwa haina uchochezi ndani yake, ni habari ya kweli yenye ushahidi wa kutosha tena unaoweza kuthibitishwa.

“Rweyemamu anasema tuliandika “porojo” ili kuganga njaa. Tunasema siyo porojo. Lakini kuna porojo ngapi mitaani na katika vyombo vya habari ambazo hazijaitikiwa kwa kishindo hiki? Alihoji Kubenea.

Alisema kitendo cha Wizara hiyo, MAELEZO, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, kulalamikia habari hiyo na kuutaka uongozi wa gazeti hilo ujieleze, kinashangaza na kuchekesha kwani gazeti la Rai la Aprili 10 hadi 16, mwaka huu 2008, liliandika habari kama hiyo, iliyokuwa na kichwa cha habari “Waziri aanza mbio kumngo’a JK 2010”, lakini si Rweyemamu, MAELEZO, wala Wizara ya habari iliyojitokeza kulaani na kulitaka gazeti hilo lijieleze kama wanavyofanya sasa dhidi ya MwanaHalisi.

Akipitia kidogo nakala ya gazeti la Rai lililoandika habari hiyo, alisema Rai liliandika, “Waziri mmoja aliyepo katika serikali ya Rais Kikwete, ameanza harakati za kugombea urais mwaka 2010, akitumaini kumuangusha rais aliyeko madarakani”

Akilinganisha habari hiyo ya Rai na habari ya MwanaHalisi inayolalamikiwa, alisema tofauti iliyopo kati ya neno “kuangusha “ na “kung’oa” yaliyotumika kwenye habari hizo, ni ya uchaguzi tu wa neno lipi litumike kwa shabaha ya kuweka uzito, lakini serikali ilikaa kimya.

Alisema walitarajia serikali ingesema inachunguza habari iliyochapwa na kutafuta ukweli wake na kuombwa msaada na wahusika katika uchunguzi huo.

“Tulitarajia Rweyemamu aseme hajapata taarifa za kikundi au watu binafsi kufanya njama, kwa hiyo anahitaji taarifa zaidi, badala ya kukimbilia kudai kuwa hakuna njama.

“Tulitarajia wale walioguswa kulalamika na hata kwenda mahakamani ili watafute, siyo tu ukweli, bali haki mbele ya chombo cha kutoa haki kikatiba”. Alisema Kubenea.

Alisema dhamira ya serikali kutaka kulifungia gazeti hilo inabainishwa na uharaka wake katika kudai maelezo, hususani kitendo cha MAELEZO kukataa kabisa kumpa muda mhariri mkuu wa gazeti hilo, Jabir Idrisa, kuwasilisha utetezi wake jumatatu, licha ya kutolewa sababu ya msingi kuwa mhariri huyo yuko safarini, Zanzibar.

Akifafanua zaidi kuhusu uharaka huo wa serikali, alisema;

“Taarifa ya wizara iliyosambazwa jumatano kwa vyombo vya habari ilitupa siku tatu hadi leo (jana) tuwe tumejieleza kwa nini tusichukuliwe hatua kwa kuandika hivyo pamoja na madai mengine ya serikali.

Siku hiyo hiyo, Mkurugenzi wa MAELEZO, ambaye kwa nafasi yake ndiye Msajili wa Magazeti, alituandikia akitaka tujitetee kwa nini tusichukuliwe hatua kwa kuandika habari hiyo. Tofauti na wizara iliyotaka maelezo katika siku tatu, MAELEZO ilitaka utetezi kesho yake (juzi) kabla ya saa 9.30. Tofauti ya muda wa utetezi inaweza kutafsiriwa kuwa ni nia ya haraka ya kutaka kuzima gazeti letu”. Alisema Kubenea.

Alisema hata walipoomba muda wa kujibu hadi Jumatatu, kwa sababu mhariri wao ambaye kimsingi ndiye aliyeandikiwa barua hiyo, yuko safarini Zanzibar, MAELEZO ilikataa kwa maandishi kuwa lazima wajibu juzi hiyo hiyo, kwa hoja kuwa hata kama mhariri amesafiri bado wanapaswa kujieleza kwa kuwa ofisi za gazeti hilo ziko wazi.

Hata hivyo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa pamoja na kushinikizwa kutoa utetezi haraka, tayari wameshatoa utetezi huo na aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanaweza kupata maelezo yao huko huko MAELEZO.

Alipoulizwa haoni kuwa ombi lao la kutaka kuongezewa muda halikuwa na msingi kwani tayari wameweza kuwasilisha utetezi huo haraka kama walivyotakiwa, alisema;

“Barua ya MAELEZO ilitumwa kwa mhariri mkuu wa gazeti letu, Jabir Idrissa, ambaye ndiye alitakiwa atoe utetezi. Yeye hayupo, yupo safarini Zanzibar na ninaomba ieleweke vizuri kuwa mimi si mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, mimi ni Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers. Kwa hiyo tuliwaomba watupe muda ili mhariri wetu awasilishe utetezi jumatatu wakakataa. Sikuwa na namna, ikabidi mimi niwasilishe utetezi …..na tena nimewaambia kwenye utetezi huo, kuwa ungekidhi haja zaidi kama ungeandaliwa na kuwasilishwa na mhariri wetu”

Alisisitiza kuwa MwanaHalisi itaendelea kuandika habari za kweli, sahihi, zinazopendwa na watu na zinazoikosoa serikali kwani kazi ya gazeti hilo si kusifia serikali.
Alisema gazeti hilo linajiendesha kitaasisi na hata kama yeye akifa bado litaendelea kufanya kazi na haamini kama serikali inayoheshimu uhuru wa wananchi wake kupata habari italifungia gazeti hilo.

Jumatano iliyopita Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, na Idara ya Habari MAELEZO ziliitaka MwanaHalisi, kujieleza kufuatia kuandika habari iliyodaiwa ya uchochezi, kuwa kuna njama zinazofanywa na baadhi ya Mawaziri na viongozi wa Chama cha Mapinduzi ili kumngo’a Rais Kikwete asigombee tena kipindi cha pili cha urais ifikapo 2010.

Wednesday, October 8, 2008

upinzani upo viongozi ndio wamekufa

PRofesa Saffari:upinzani unashamiri viongozi ndio wamekufa kisiasa

na njemba njemba

WAKATI mageuzi ya Demokrasia yanaaingia hapa nchini mwanzoni mwa miaka ya 1990 ilikuwa ni vigumu kumkuta msomi anayetegemea kazi za Serikali akitamka wazi kuwa yeye ni muumini mzuri wa siasa za mageuzi.

Lakini leo ikiwa ni miaka zaidi ya 15 tangu kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini sio jambo la ajabu kwasasa kumkuta mhadhili wa Chuo kikuu akitamka wazi kuwa yeye ni mwanachama wa chama cha upinzani na atasimama kugombea nafasi ya juu katika chama hicho.

Hata hivyo wasomi ambao wanathubutu kusema hivyo hadi sasa wengi wao ni wanataaluma wa chuo kikuu, bado ni vigumu kwa wasomi wa kada ya chini ambao kipato chao kinategemea serikali kutamka kuwa yeye ni mwanachama wa chama cha upinzani.

Miongoni mwa wasomi wa elimu ya juu ambao wamejitokeza wazi na kubainisha kuwa ni waumini wa kubwa katika siasa za kambi ya upinzani ni Prof.Abdallah Safari ambaye amefanya mahojiano na Tanzania daima wiki hii nakubainisha kuwa anayo matarajio makubwa ya kukuleta magezi katika siasa za hapa nchini.

Prof.Safari ambaye naye ni miongoni mwa wahanga walioachishwa kazi serikalini katika miaka ya hivi karibuni baada ya kubainisha nia yake ya kuunga mkono Chama cha Wananchi CUF anasema kuwa amedhamiria kuibua Vuguvugu la mageuzi.

Akiwa Ofisi kwake anapojishughulisha na utunzi wa vitabu vya Riwaya na Sheria huku akisubiri Chama cha CUF kutangaza tarehe ya Uchaguzi ili aweze kuwania nafasi ya uenyekiti wa taifa ameweka wazi kuwa yuko mbioni kuachana na kazi yake ua uwakili ili awatumikie wananchi.

“ siku hizi najishughulisha sana na uandishi wa vitabu nataka kuachana na uwakili kwasasa..nimebakiwa na kesi chache tu mahakamani nataka kuwatumikia wananchi kwa namna nyingine’ alisema Prof.Safari alipoulizwa kama kuanza kuachana na kazi ya sheria ni moja ya mikakati ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kumrithi Profesa Mwenzake Haruna Lipumba ambaye anaongoza CUF.

Hata hivyo anajua kazi kubwa iliyopo mbele yake kuhakikisha napata Uongozi kwenye Chama hicho kikuu cha upinzani, “sina pesa za kuzunguka mikoani nakuanza kuomba kura nasubiri siku itakayopangwa ifike nitatumia muda mchache tu pale buguruni kuwaeleza wajumbe nia yangu kwa kutumia taaluma ya sheria na ualimu naamini watanielewa”anasema

kitu kinachomtofautisha na viongozi waliopo madarakani ni msimamo dhabiti amabao anaamini utasababisha apedwe na wafuasi wa CUF ambao wamekuwa na sifa ya kupigania haki bila kuogopa nguvu ya dola.

Anabainisha hayo pale anaposema kuwa akifanikiwa kushinda uongozi hata jumuiya ya Ulaya zitajua kuwa mwanamageuzi wa kweli ameingia madarakani kwani hatathubutu kushiriki uchaguzi wowote ule unaosimamiwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi bila kuundwa Tume huru na katiba mpya ya jamhuri ya Tanzania.

“nimmejaribu kuwashaauri wenzangu wasishiriki uchaguzi wowote hadi Tume huru ya auchaguzi iundwe sambamba na Katiba ya jamhuri ili wawe kuiondoa CCM madarakani kiurahisi lakini hawanielewi, Tunduru wameshiriki,

Kiteto nako wameunga mkono CHADEMA pote wameambulia patupu na sasa ni huko tarime, nawambia huwezi ukashinda kwa sababu Kwenye uchaguzi CCM Ndio majaji na Uchaguzi ndio kesi unategemea nini?anahoji

Anasema yeye atakapopata nafasi ya kuongoza atahakikisha Katiba mpya inapatikana kwanza na tume huru ndipo wanashiriki uchaguzi vingenevyo uchaguzi utakuwa ndoto hapa nchini.

Mwanasheria huyo mashuri nchini anasema kuwa zaidi ya Miaka 15 tangu mfumo wa vyama vingi uingie hapa nchini CCM imeendelea kuwepo madarakani kutoka na kukosekana kwa wanasaisa makini wa upinzani wenye nia ya dhati kufanya hivyo.

Prof.Safari anaweka wazi kuwa viongozi wa sasa waliopo madarakani wamekufa kisiasa na kupoteza mwelekeo wa kuitia madarakani wamebaki tu bila kuwepo na jambo jipya la kuleta mabadiliko.

“alipoingia madarakani Rais Jakaya Kikwete yaliibuka maneno kuwa uponzani umekufa nikaamua kufanya utafiti wangu nikagungua kuwa upinzani na unazidi kuota mizizi viongozi ndio wamekufa na kupoteza mwelekeo”anasema

Anasema kuwa kutokana na kufa kwa viongozi kisiasa ndio maana zimekuwa zikipatikana fursa nyingi za kuindoa CCM madarakani anakosekana kiongozi wa kusiamama aseme wazi kuwa ondoka.

Hali hiyo inadhihirisha kuwa wapinzani wameipakata kwenye miguu CCM iendelee kukaa madarakani kwani vingenevyo zinapoibuka sikendo kubwa kama mkataba wa kitapeli Richmond, kashfa ya IPTL, Rada, Mkataba wa umeme nchini Tanesco ilitosha kuimrisha CCM bila kuipa muda iondoke madarakani.

Licha ya hivyo Profesa anasema kuwa alishangazwa siku aliposikia Rais Kiwete anavunja katiba kwa kuwasameheme mafisadi wa waliopora pesa Benki kuu kupitia kitengo cha Madeni ya nje (EPA) na viongozi wa upinzani wakashindwa kumwambia ajiuzulu.

“ile kauli ya kutamka hadharani kuwa anawapa muda warudishe pesa ilitosha kumwambia Rais Pale pale leo hulali Ikulu kwasababu umevunja katiba uliyoapa kuilinda na sasa umekiuka kipengele kinachosema kila mtu anahaki mbele ya sheria, nasasa unafanya tuamini kuwa mahakama na magereza ni sehemu za wanyonge”anabainisha frusa za kutoa Rais Ikulu.

Hawa wanaipakata CCM na wala hakuna dalili zozote za kuing’oa madarakani wala sioni kiongozi yeyote mwenye nia ya kuing’oa” anasema kuwa watu wanaoweza kuleta mabadiliko hapa nchini ni wasomi wanaotokea kwenye familia za daraja la kati (sio masikini wala matajiri sana) lakini anaonya kuwa haitoshi kusoma tu lazima ujito mhanga.

“nikiwa mwenyekiti kazi yangu ya kwanza ni kuwaunganisha wasomi wote waingie CUF na wale wakurugenzi waliopo Makao makuu nitahakikisha wanabaki kama wana Shahada vingenevyo niawaondoa niingize wenye elimu ya juu, hawa akina Lipumba wamekosa mwelekeo wanashindwa waende wapi?

“Mimi ni mwanasheria suala la migodi ,EPA kwenye nchi ya demokrasia hai ilitosha kuingoa CCM Madarakani Kikwete ameleta ubaguzi watu wanatuibia anawasemehe wakati katiba inasema toa haki sawa”

Nitakiimarisha chama kwanza kiwe cha kitaifa sio kilivyo hivi sasa ambapo kinaonekana kama cha kanda ya pwani, tu nitahakikisha ninafungua mashina nchi nzima na kuimarisha matawi kwa kusambaza pikipiki na mabaiskeli kwani kura zipo huko sio mijini!

Anambeza Prof.Lipumba kuwa ameshindwa kuimalisha chama kitaifa amebaki akitegemea maamuzi kutoka Zanzibar jambo linalozolotesha chama kisiingie madarakakani haraka.

“kama kuna mtu anaongoza chama kikubwa kama CUF halafu anashindwa kupata mbunge hata mmoja bara alipaswa ajiuzulu siku hiyo hiyo inaonekana ameshindwa”anasema naakuongeza kuwa mimi siogopi wapiga kura naogopa watu wanaohesabu kura na mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga wa watanzania nitakuwa nakazi ya kutoa elimu ya uraia.

Migogoro mikubwa imekuwa ikiibuka hata kuathiri vyama vingi kutokana na kugombea ruzuku Prof.Safari amejipangaje kulikabili hilo “kwa Ruzuku sio kitu cha kutegemea niendeshe cha ili niingo’oe CCM madarakani”anasema nakuonongeza kuwa kama TANU ingetegemea Ruzuku isingeweza kumng’oa Mkoloni.

Anahoji kuwa inakuwaje CCM inaendelea kushinda wakati haina viongozi makini mfano Mwenyekiti wake ambaye ni Rais Jamhuri ya muungano ameweka rekodi ya kuingia Ikulu ya marekani ‘white house’ mara saba nakujiweka kwenye kundi la vibaraka wa Georg Bush anawezaje kuongoza chama kikawa na nguvu za kushinda upinzani

Anamaliza kwa kusema Viongozi wa upinzani hawajafanya lolote ndio maana CCM haijaona hatari yoyote inayoikabili kwani kuna nafasi nyingi ambazo zinajitokeza lakini zinashindwa wanabaki kuwa wachekeshaji.

Profesa safari alikuwa mkurugenzi wa masomo na mipango katika chuo kikuu cha Diplomasia Kurasini hadi alipoachishwa kwa sababu anazosema ni za kisiasa ,amezaliwa June 3 Mwaka 1951 ni mwislamu aliye na wake na watoto wawili.

Alimaliza elimu ya Sekondari Mwaka 1969 na kidato cha sita Mwaka 1972 kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha M
limani Mwaka 1979 akichukua shahada na kisha shahada ya juu ya Sheria Mwaka 1985 katika chuo hicho.

Baadaye mwaka 1995 alikwenda kusoma uingereza chuo cha Sussex akizama zaidi kwenye sheria na kutunukiwa hashima ya Sheria Mwaka 2000
Alipopewa Uprofesa.

Amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo kufanyakazi mahakama kuu kuanzia 1987 kama wakili hadi leo, amewahi kuajiliwa kama mtafiti msaidizi katika tasisi yaa uchunguzi wa Kiswahili 1972 hadi 1974 na kuwa mhariri wa nyumba ya uchapaji (TPH)1974 hadi1976 ,mwanasheria wa Serikali katika wizara ya sheria 1979 hadi 1986.

Mwaka 1987 alikuwa afisa mtafiti wa kituo cha uhusiano wa nje ,1988 hadi 1991 alikuwa mhadhili wa sheria baadaye Mwalimu mkuu wa Sheria hadi anaondoka pia Mwaka 2000 alikuwa mtaaluma mwandamizi wa sheria katika kituo cha uhusiano wa mambo ya nje.

Zipo nafasi nyingi ambazo ameshika au kusomea kama tukiziandika hapa itaihitaaji makala nyingine lakini kwasasa ni wakili wa kujitegemea anayemiliki Firm ya Saffari na ni mtunzi muzuri wa vitabu kwasasa anaandaa kitabu kinachoelezea hatima ya Demkrisia na chaguzu za hapa nchini

Mawasiliano .mobinsons@yahoo.com

Labels: