Thursday, September 20, 2012

Rais anapokuwa na makengeza kifo cha mwandishi lakini kwa balozi safi

na Mobini Sarya RAIS wa Jamhuri ya watu wa Tanzania,Jakaya Kikwete ameonyesha masikitiko makubwa kutokana na kifo cha balozi wa Marekani nchini Libya aliyeuwawa wiki iliyopita kwa mlipuko wa mabomu kutokana na wandamanaji wanaopinga filamu ya kifedhuli inayoukashfu uislam. Rais kupitia wizara ya Mambo ya nje amenukuliwa akimtumia salam za rambi rambi Rais Barack Obama wa Marekani kutokana na kifo hicho ambacho amedai kimemsikitisha na kumshtusha hivyo kuwaahidi wamarekani kuwa atahakikisha analinda ubalozi wao uliopo hapa nchini yasitokee yaliyotokea huko,Libya. rais Jakaya ametuma salamu za rambirambi Washington Marekani,ikiwa ni takribani wiki tatu zipite tangu mwanahabari wa kituo cha chaniel ten, Daud Mwangosi auwawe kikatili na askari Polisi mkoani Iringa septemba 2 Mwaka huu. Tangu mwanahabari huyo auwawe , watu mbalimbali zikiwemo taasisi zitoe matamko makali ya kulaani, lakini hakuna kiongozi wowote wa serikali wala ofisi ya Rais aliyejaribu kutoa tamko la kulaani mauaji hayo au kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu achilia mbali viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa au mkurugenzi wa chanel ten. Tangu Rais Kikweke aingie madarakani Mwaka 2005 amekuwa akisifiwa kuwa ni mtu wa watu na amekuwa kijitokeza kwenye misiba mbalimbali inayotokea kwa wananachi wake na kuwajulia hali familia za wafiwa kama mila za kiafrika zilivyokawaida. Kubwa zaidi Rais Kikwete alijitokeza nyumbani kwa msanii nguli wa filamu,Steven Kanumba alipofariki dunia jijini Dar es salamu,akatoa pole kwa familia ya marehemu kabla ya kupishana na waziri wake akipeleka pesa za rambirambi zinazofikia shilingi milioni 10. lakini tangu kifo cha mwandishi huyo kitokee katiaka mazingira ya kutatanisha Rais ameshindwa kutuma salam, za rambi rambi wala wasaiidizi wake kujitokeza hadharani kuwafariji wafiwa kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwenye misiba mingine. kwanini kimya kwa mwangosi. Inamaana Rais Kushindwa kutuma salam, za rambirambi wala wizara ya habari kushindwa kufanya hivyo anajiweka katika kundi la waovu waliohusika na ukatili huo,jambo ambalo linadhidi kumjengea chuki aendapo kustaafu,kwasababu anaonekana kuwa ni kiongozi anayenyamazia maovu kwenye utawala wake. lakini leo tunajiuliza inakuwaje katika mwezi huu matukio yanayofanana katika nchi tofauti yatokee Rais ashindwe kutuma salamu za rambi rambi kwenye msiba wa nyumbani kwake tena kwa mwandishi wa habari ambaye tunaamini amekuwa akifanya naye kazi kila anapokwenda mkoani Iringa kwenye safari za Kiserikali badala yake akumbuke kutuma Marekani. baadhi ya watanzania ambao wamezungumzia hoja katika mindao mbalimbali ikiwemo mtandao maarufu wa jamii forums wamekwenda mbali na kutania rais kuwa pengine alidhani mwandishi aliyefariki nchini kwake labda alikuwa mkenya na wala tukio halikufanyika hapa nchini ndio maana hakujishughulkisha nalo. wapo ambao wamesema kuwa ukimya wa Rais katika kifo hicho umeonyesha kuwa mapenzi ya Rais kwa wananchi wake yamepungua kwa kasi zaidi kadri anavyomaliza muda wake ikulu,wanaamini kuwa rais wa sasa sio yule ambaye alichaguliwa miaka saba iliyopita ambaye alijitokeza hadharani na kuunda tume kila janga lilipowakuta watu wake. Walikumbushia jinsi ambavyo aliunda tume siku chache baada ya kuingia madarakani ikashughulikia kashfa ya mauaji iliyokuwa inawakabili askari Polisi akiwemo mkuu wa upelelezi wa kanda maalum ya Dar es Salaam,wakati huo Abdallah Zombe ambaye hatimaye walikutwa na hatia wakapandishwa kizimbani kwa kuuwa wachimba madini wa ifakara Morogoro. ingawa baadaye watuhumiwa hao walishinda kesi hiyo kwa kukosa ushahidi wa moja kwa moja wa kuwatia hatiani lakini kwa nafasi ya Rais alionyesha uwajibikaji kwa kuunda tume hiyo, ambayo siku za hivyo karibuni amekua akiombwa aunde lakini anashindwa kufanya hivyo. jamii imekuwa inamuomba raisi aunde tume kama hiyo kuchunguza mauaji yanayoendelea hapa nchini lakini anashindwa kufanya hivyo licha ya kwamba Polisi wamekuwa wakifanya makusudi ya kutumia nguvu kubwa katika maeneo ambayo haikutakiwa kufanya hivyo. leo Rais amefikia hatua ameshindwa kabisa kuhudhuria msiba wa mtu mhimu kama mwanahabari ambaye anafanya kazi zinazojulikana hadi nje ya nchi,amekuwa akitangaza nchi yetu sawa wanavyofanya wasanii anao wahusudu yeye. Serikali yake imekaa kimya wala wakuna kiongozi yeyote kutoka taasisi mhimu ya serikali aliyejitokeza hadharani kutoa hisia zake hata Pole kwa ndugu na family ya marehemu achilia mbali vyama na kituo cha habari cha chanel 10 ambacho marehemu alikuwa anakitumikia enzi akiwa hai. Nadhani hata familia yake itakuwa imesikitishwa sana na ukimya wa rais Jakaya Kikwete kushindwa kutuma salam, za rambirambi kama ambaavyo amekuwa akifanya kwenye misiba mingine na wakati mwingine hufika kutoa pole moja kwa moja. Tumemuona akifanya hivyo katika misiba mbalimbaali,alijitokeza kumjulia hali Mkurugenzi wa Halihalisi Publishers,Sued Kubenea alipomwagiliwa tindikali na maadui wa uhuru wa habari,pia alijitokeza kumjulia hali mbunge wa Rombo Selasini alipolazwa baada ya kupata ajali mbaya iliyogharimu ndugu zake. Wanajiuliza vipi mwandishi wa habari ambaye ni mpiga kura wake, mjenga nchi auwawe katika mazingira yenye kutia hofu na kuichafua nchi Rais ashindwe kutumia msiba huo kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoambatana na uonevu unaogharimu maisha ya watanzania kama ambavyo yamemkuta mwanahabari huyo. Sio kwamba Rais Kikwete hajui thamani ya wanahabari.anaijua fika.anakumbuka mchango wao Mwaka 2005 jinsi walivyotumika kwenye mtandao wa kusaidia kuingia Ikulu wakati huo, ambapo alilazimika kuacha shughuli zote na kuketi karibu nao wakitengeneza mikakati ya ushindi. leo ameingia Ikulu amesahau fadhira hizo anawaona watanzania kama hawana thamani sawa na wamarekani.Rais anaapa kwamba atahakikisha anawalinda wamarekani waliopo hapa nchini yasiwakute kama yaliyowakuta hao waliokuwa Benghazi Libya ambapo watatu kati yao walifariki sambamba na balozi wao. mbona kauli hiyo nzito alishindwa kuitoa kwenye vyombo vya habari vya hapa nchini kuwafariji wanahabari wake?kuwaambia kuwa 'baasi nyamazeni,nitahakikisha kuwa hakuna tena mwandishi anayeuwawa katika mazingira ya kazi' ukimya wake unabainisha kuwa kuna mwandishi mwingine atauwawa akienda katika mazingira kama yale. Rais ameshindwa kukemea vitendo vinavyosababishwa na Polisi wake kwasababu anaamini wanamlinda yeye, lakini anadhudhubutu kuwakemea waislam waliokerwa na filamu inayoukashfu uislam ambayo imeandaliwa na mmarekani na wao wakaamua kulipa kisasi. swali ambalo sasa watanzania wanahoji na wataendelea kuhoji hadi majibu yapatikane ni kwa jinsi gani Rais jakaya ameshindwa kutuma salamu za Rambirambi iringa kutokana na kifo cha mwanahabari huyo lakini ametuma salam hizo kwa kifo cha kuwawa kwa balozi wa ,marekani. Tunalojiuliza ni kwa namna gani Rais ameshindwa kutolea tamko hata la kulaani tukio hilo,hivyo kupingana na waziri wake wa mahusiano,Seteven Wassira aliyetangazia umma kupitia shirika la TBC kuwa kila binadamu anathamani sawa. wengine tunapinga kauli hiyo kwani Kama kauli ya Waziri ingekuwa sawa leo Rais angetuma mwakilishi kwenye msiba huo au salam za rambi rambi kwa kituo cha televisheni cha Chan.10 alichokuwa anafanyia kazi marehemu pamoja na Klabu ya wandishi ya Iringa (IPC)kama ambavyo Rais amefanya kwa wamarekani.tutaendelea kuhoji hadi tupate majibu. Waziri Wassira amesema kuwa misiba yote inayotokea inalingana tusiupe uzito zaidi huu,sawa lakini Wassira hajatuambia mbona serikali yake imekaa kimya kwenye msiba huu,tafauti na misiba mingine ambayo wamekuwa wakitoa ubani kama ule wa marehemu Steven Kanumba au tuamini kwamba serikali imehusika moja kwa moja na kifo hicho?.na tuhoji.