Ufugaji wa kuku ni utajiri wa haraka,magonjwa ni kikwazo
Na
Mobini Sarya,Tanpress
WAKATI
kuku wakiendelea kuteketea kwa kuvimba
macho,kupofuka na kutoa makamasi hatimaye kufa watalam wa mifugo wamepishana
kauli kuhusiana na aina ya ugonjwa huo.
katika maeneo ya vijiji mbalimbali vya jimbo la Chalinze,mkoani Pwani wataalum,wafugaji
wa kuku wamepata hasara baada ya kuku wao kupoteza maisha baada ya kupofuka na
kushindwa kuona chakula.
Afisa
Kilimo na mifugo Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba wilayani, Bagamoyo,Rashid Ali
Ramadhan,amesema kuwa tayari kuku kadhaa wamekwisha kufa huku ugonjwa huo
ukizidi kusambaa haraka.
“Huu ni
ugonjwa ambao unatusumbua katika ukanda huu wa pwani kila mara hivi sasa
umelipuka na wafugaji wengi wamepata hasara”anasema Ramadhani
Akiuelezea
ugonjwa huo anasema kuwa wakulima wanaofuga kuku wanapaswa kuwachanja wakiwa na
wiki nne tangu wazaliwe ili kuweza kudhibiti maambukizi hayo.
Ramadhani
anasema kuwa kuku au ndege akishapata ugonjwa huo macho huvimba na kupofuka
hivyo kushindwa kula chakula na baadaye hufa kwa njaa.
Baada ya
kuku kuugua mfagaji anatakiwa kumsafisha kuku macho kwa kutumia mafuta ya kula
na kumpaka mafuta ya taa kila mara ili aweze kuona chakula vingenevyo anakufa
na njaa.
“hakuna
dawa nyingine ambayo anaweza kupewa lakini kama bado ni mdogo unaweza kumchanja
dawa aina ya Chicken pox
Vaccine,..uhakika ni asilimia 80 kwamba hawataugua ugonjwa huo”anasema Rashid
Hata
hivyo kauli hiyo imepingwa na mfugaji wa kuku mkazi wa kijiji cha Lunga,
Seleman Rashid, ambaye amepoteza kuku 150 kutokana na ugonjwa huo.
Seleman
anasema ugonjwa huo sio ndui bali ni mafua ya kuku ambayo humshambulia kuku kwa
kutiririsha maji na machozi huku macho yakivimba nakuziba kabisa.
“unajua
watalaamu wanatofautiana, mara ya kwanza hata mimi walinimbia ni ndui
nikajiuliza mbona vifaranga vikitotolewa tu navichanja imetoka wapi
ndui?”anahoji Rashid
Hata
hivyo anasema baadaye aliwapiga picha na kwenda nayo kariakoo katika maduka
makubwa yanayouza dawa za mifugo, walipoona tu hiyo picha wakamwambia hayo ni
mafua ya ndege na alipopewa dawa ya ugonjwa huo wakaanza kupona.
Mtaalam
mwingine aliyezungumzia ugonjwa huo ni John Chiwaligo ambaye amesema kuwa sio
ugonjwa bali ni upungufu wa vitamin ndio unaosababisha kuku wanavimba macho.
Chiwaligo
ambaye ni afisa ugani kata ya Lugoba amewashauri wafugaji wanaokumbana na
ugonjwa huo wawape vitamin aina Multrivet.
“hiyo ni
dalili kwamba kuku hao wanaukosefu wa vitamin mwilini,mfugaji anapaswa kuwapa chanjo ya vitamin aina ya
Tetrs Colvit au Multvet anawawekea kwenye maji wanakunywa”anasema Chiwaligo
Mtaalam
huyo ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha wataalam wa mifugo nchini,
anasema kuwa kuku akivimba macho anatakiwa kusafishwa kwa maji masafi na
kuwekewa dawa aina ya macho aina ya Waund Powder.
UGONJWA WA MAFUA YA KUKU (INFECTIOUS
CORYZA
OR FOWL CORYZA
Ugonjwa
wa kuku ni ugonjwa wa kuambukiza unaoshambulia zaidi mfumo wa juu wa upumuaji
kwa kuku na baadhi ya ndege wa porini mfano njiwa.
Ugonjwa huu
unasababishwa na bakteria wanaojulikana kitaalamu kama Avibacterium paragallinarum
(zamani
aliitwa Hemophilus paragallinarum )
.
Ugonjwa
wa mafua ya kuku unaweza kuwapata kuku wa umri wote lakini zaidi wale wa umri
wa kati na wakubwa.
Aidha
unajitokeza zaidi kwa kuku wanaotaga na wale wanaokaribia
kutaga
mayai na mara chache hujitokeza kwa kuku wa nyama.
Uenezwaji
Ugonjwa huu huenea kutoka kuku mmoja kwenda kwa kuku mwingine au kutoka banda/shamba
moja kwenda jingine kwa njia ya kugusana kati ya kuku na kuku au watu wenye
wadudu au kwa njia ya hewa kupitia chembe chembe ndogo za vumbi na pia kupitia
maji ya kunywa.
Uenezwaji
kwa njia ya vyombo vya chakula pia unawezekana.
Ugonjwa
unaweza ukaanza na kuku wachache huku ukienea taratibu na kuishia na kuku
wachache au uk
aenea kwa
kasi na kushambulia kuku wengi.
Ugonjwa unapatikana sehemu mbalimbali duniani
na baadhi ya maeneo hujitokeza mara kwa mara. Kwa Tanzania ugonjwa huu
hujitokeza hasa kuanzia mwezi wa tano hadi wa nane.
Dalili za
Mafua ya kuku Kufuatia maambuzi ya ugonjwa huu, dalili huanza kujionyesha tangu
siku ya 1 hadi ya 4. Dalili zake ni kama ifuatavyo:
-
Kwa ugonjwa
wenye madhara madogo, dalili zinazoweza kuonekana ni kuzubaa, kuchuruzika mafua
mepesi na mara chache kuvimba uso kwa kiasi kidogo.
-
Wakati
ule ugonjwa mkali hujionyesha kwa kuvimba kwa kiasi kikubwa maeneo ya masikiona
macho bpamoja na uwepo wa
maji
kwenye nyama zinazozunguka maeneo ya macho inayopelekea kufumba kwa jicho moja
au yote.
Kutoa
makamasi mazito yaliyochanganyika na usaha puani
na
mdomoni, vigubiko vya macho hushikana kwa ute mzito ambao huonekana pia ndani
ya macho. Kwa kuku dume uvimbe unaweza kwenda hadi kwenye upanga/ndevu. Uvimbe
huwa
mkubwa
kati ya siku ya 10-14.
Dalili
nyingine ni pamoja na kukohoa, kupumua kwa shida kunakosababisha watoe sauti ya
mkwaruzo
(kukoroma),kuku
kutoa machozi, kupungua kwa hamu ya kula
kunakowapelekea
kushusha uzalishaji (ukuaji na utagaji wa mayai),kuharisha pia kunaweza kutokea , kudhoofika na hatimaye
kufa.Utagaji wa mayayi hushuka kwa
asilimia
kuanzia 14 hadi 40. Kuku akipasuliwa
-
Utando
mwepesi au mzito ndani ya pua, macho na masikio
wenye
rangi ya njano,Uvimbe wenye maji maji maeneo ya usoni,
upanga/ndevu,na
upande wa chini wa shingo
-
Uwepo wa
wekundu na ukahawia au uchafu mweupe n
dani ya
ngozi inayofunika
jicho
-
Uwepo wa rangi
nyekundu kwenye kuta za koromeo la juu na ute mzito ndani yake,mara chache
mapafu nayo huathirika.
Pia ufugaji
kuku wakienyeji una faida kubwa zifuatazo; kuanzisha mradi hakuhitaji mtaji
mkubwa sana, Kuku wa kienyeji hawahitaji eneo kubwa sana, kuku wa kienyeji wanastahimili
mazingira magumu, Kuku wa kienyeji hawaugui mara kwa mara.
aidha kuku wa kienyeji wana soko kubwa sana, kuku wa kienyeji ana bei kubwa sokoni,Mayai ya kuku wa kienyeji ni mazuri sana, Mayai ya kuku wa kienyeji yana soko kubwa.
Faida ya kuku wa mayayi huanza kuonekana pale mfugaji
anapokuwa na kuku 500 ambapo anakuwa na uhakika wa kukusanya trei 10 za mayai
kwa siku.
Ukiweza kukusanya kiasi hicho cha mayai ya kienyeji unakuwa
na uhakika wa kuuza kati ya shilingi 900 hadi 12000 kwa trei moja sawa na
shilingi 90,000 kwa siku.
Hivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja kama mfugaji atakuwa
anauza kwa shilingi 90,000 ana uhakika
wa kuvuna kati ya shilingi milioni 2,700,000 hadi milioni 3,60,000 kwa mwezi.
Pesa ambayo hata kama akitoa nusu yake kwa ajili ya kulipia
gharama ya chakula na dawa bado mfagaji ana uhakika wa kubaki na kipato kikubwa
zaidi ya wafanyakazi walioajiliwa au wafanyabiashara zingine
CHANJO
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
Kuku wapewe chanjo ya kideri/mdondo kila baada ya miezi mitatu chanjo hii hupatikana nchini kote ukifika dukani ulizia chanjo ya newcastle, utapata maelekezo ya jinsi ya kuwawekea kuku kwenye maji ya kunywa, chanjo hii wapewe kuku wazima tu na wagonjwa watengwe mbali
MINYOO
Kuku hunyweshwa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu, kuna dawa kama piperazine na nyinginezo ambazo huwekwa kwenye maji
CHAWA NA UTITIRI
Unaweza kutumia dawa za kuogeshea mifugo kama ecotix au dawa ya unga unga ya kunyunyuzia kama akheri powder, dawa ya akheri unaweza kuimwaga bandani na kisha kumnyunyuzia kuku mwilini ukiwa umemning’iniza kichwa chini miguu juu ili mayoya yaacha nafasi ya dawa kuingia
MAGONJWA YA MAPAFU
Kuna magonjwa mengi yanayoshambulia mfumo wa hewa, dawa ya tylosin inauwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa karibu yote, wape dawa hii mara tu unapoanza kuona dalili za mafua
Mayai
ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote.
(madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana
kwa afya ya watu hasa watoto wachanga.
Pia hutupatia protini,Kinyesi cha kuku ni mbolea safi pia ni
kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga.
Gharama za kuanzisha na kuendeleza miradi ni nyepesi, kitoweo
chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au
miwili na kumalizika.
Jogoo hutumika kama saa inapowika,manyoya ya kuku hutumika
kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro.
Kuku ndiye mnyama wa kipekee
anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa.
Ufugaji wa kuku ndio shughuli
inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri
vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo
binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu.
Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na
huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza
kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu.
Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia
chakula nje huongeza idadi ya mayai
(kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%).
TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA
MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara
katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha
afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya.
Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada
ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:
Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na
kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi
na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni
shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.
Kinyesi chaweza kuwa na rangi ya kijani
kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa
chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata katika nchi za hari
kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa muda.
Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na
tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula,
mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu
ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni piperazine, phenothiazine na
butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1 kwa
kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga).
Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur
au dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila
baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri
husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara
ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi.
Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito
wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion
kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa mashimo) pulizia kila kuku
ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku 150).
Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu,
waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu.
Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion
kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia
inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya kikohozi. Ugonjwa huu
huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa wingi.
Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua.
Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale
walipouzwa. Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu.
Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha kuku
mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara
kutokana na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza
kutekeleza kwa wakati mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo.
Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya
4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa
kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili
Labels: MAKALA


