Saturday, March 3, 2012

wananchi CHUNYA wamechoma nyumba za polisi

Wananchi wilayani CHUNYA wamechoma nyumba nne za polisi kutokana na mwanafunzi kuuliwa kwa kipigo na polisi akiwa selo inasemekana kuwa mwanafunzi huyo alikwapua simu ya bwana mmoja na polisi kuchukua sheria mkononi kwa kumpa kisago hadi kupoteza maisha nimekubari wananchi wamechoka sasa,hawaogopi kupigwa risasi na pilisi tena na utafika wakati polisi na wananchi itakuwa ni kama osama na USA tusubiri tu tutaona On Sat, Mar 3, 2012 at 2:38 AM, Yona F Maro wrote: Sasa wanadhani wanaweza kupata haki zao kweli kwa kuvunja haki za wengine hao wananchi ? kwanini wasingetumia vyombo vya sheria vilivyopo ili kuweza kupata haki zao za msingi ? hivi huyo mwanafunzi aliyewekwa sero ya polisi tunajuaje kama ameuwawa kwa kipigo cha polisi na sio wananchi hao hao wenye hasira kali wanaouwa watuhumiwa kila kikicha tena kwa kuwachoma moto ? Kufuata sheria ni jambo zuri sana Yona lakini unafuataje sheria ahali wasimamizi wa sheria si waaminifu tena. Muundo mzima umekuwa mbovu na mwananchi wa kawaida hana imani tena na hivyo vinavyoitwa vyombo vya sheria. Polisi wamekuwa miungu watu kiutendaji katika hali ya kawaida siwezi shangaa kila naposoma mambo ya ajabu yanayofanywa na wananchi. Kwa ujumla utawala wa kisheria umeshindikana na ni anguko kwa serikali kwa kushindwa kutimiza wajibu wake. Kazi ya ziada inabidi kufanyika lakini ugumu unakuja kuwa wale waliotufikisha hapa kila siku wanaweka mbinu za kuwafanya wakae juu milele na milele amina. Serikali imechukua likizo muda mrefu lakoini na sie wananchi tunasehemu kuubwa sana tunachangia kwa kila jambo linalotokea, kama kila uchaguzi tutasema ni kwa ajili ya wanasiasa na hayatuhusu basi tusilalamike yanayotendwa na wanasiasa On Mar 3, 10:24 am, ibrahim mtolera engmtoleraibra...@gmail.com> wrote: