Sunday, June 1, 2008

MZEE Mpema;Kada wa TANU anayejitosa kumaliza mgogoro wa CCM,CUF

.
*Asema siasa chafu zilianza enzi ya Nyerere

Na Mwandishi wetu

WAKATI Chama cha Wananchi CUF kikigoma kurejea kwenye Mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa Kisiasa Zanzibar,kati yake na CCM, Mzee mmoja amejitokeza nakutaka kuwa mpatanishi atakayekutanisha mahasimu hao wawili aweze kuleta maelewano.

“unapotaka kuwapatanisha wanaogombana kwanza unakutana na upande mmoja unausikiliza na kupima kiwango cha hasira kisha unatoa ushauri kuwa kushusha hasira zile ili iwe rahisi kukutana na upande wa pili vingenevyo watapigana mbele yako” ndivyo anavyoaza kwa kusema Mzee huyo ambaye aliwahi kuwa Kada maarufu wa Chama cha TANU,

Mzee Paul Mpema aliyezaliwa 1924 ambaye amezungumza na Tanzania Daima wiki hii nakushauri atafutwe msuluhishi haraka ili awapatanishe mahasimu hao wawili wa kisiasa Zanzibar.

Mzee Mpema alikuwa akizungumza na Tanzania daima kwenye mahojiano maalum, nyumbani kwake Kigamboni alisema kuwa yuko tayari kuwakutanisha, katibu mkuu wa CUF Maalim Seif na Rais wa Zanzibar Aman Karume ili kumaliza mgogoro huo unaoweza kuleta ,maafa.

Mzee huyo amesema kuwa kwa uzoefu wake alionao kwenye mambo ya siasa ni vigumu vyama hivyo vikafikia kutokana na chuki, dharau waliyojingea kwa kipindi kirefu hivyo kila mmoja hamwamini mwezike.

Alisema kuwa tatizo la mpasuko Zanzibar linazidi kuwa kubwa kutokana na ufahamu mdogo wa Viongozi wa CCM na CUF ambao kila mmoja anasumbuliwa na tatizo la unazi wa kiitikadi.

“CCM inasumbuliwa na Ukereketwa kutokana namatatizo waliyonayo viongozi wake kukumbatia Ukeretwa kila Mwanaccm anapokuwa anazungumzia Mgogoro wa Zanzibar anatanguliza ukeretwa hivyo hata akikosea anajiona yuko sahihi”alisema mzee huyo nakuongeza kuwa tatizo la CUF ni ufurukutwa hivyo ni wananchama wake wanajihisi wanadhulumiwa kila uchaguzi’

Kutokana na ufurukutwa uliojengekeka miongoni mwa Viongozi wa CUF wamekuwa wakilalamikia CCM kuwadhulumu kila uchaguzi ingawa na CCM haitaki kukubali makosa kutokana na Ukereketwa wake.

Anakumbushia kuwa hata yalipofanyika mauwaji kule Zanzibar Mwaka 2001, CCM haikutambua kuwa ni kosa lao limesababisha mauwaji hayo, hata CUF katika kujihisi kuwa imedhulumiwa haikutafuta njia iliyobora kudai haki baadala yake ikaamua kutumia Ubabe wa jino kwa jino CCM ikajibu kwa Dola damu ikamwagika.

Mpema anasema kuwa kama CUF wangetumia njia iliyo bora kama Mahakama kutafuta haki yasingetokea ,lakini wakabaki wanatumia maneno kuwa tutaingia barabarani bila kuwa na silaha huku wakitambua kuwa CCM inadola inayoweza kuwadhibiti.

akizungumzia Mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kwa miezi kumi na nne anasema yameshindwa kupata ufumbuzi kutokana kuwa ya kinafiki na kufanywa siri ya watu wawili ambao ni mahasimu bila kushirikisha vyama vya upinzani ili kuwa mashahidi na kinachozungumzwa.

“CUF na CCM kujifungia wawili eti wanatafuta muafaka wakati wanachukiana ni unafiki hivyo ni vema akatafutwa mpatanishi akawakutanisha wote wawili.. …hata mimi nipo tayari kuwa mshuluhishi wakinichagua kuwapatanisha viongozi hao ili kumaliza mgogoro huo ambao tayari CUF wameonyesha kutumia mbinu zozote kufanikiwa huku CCM ikijivunia dola”anaonya Mpema

Mzee Mpema anasema kuwa hata kama sio yeye atakuwa mpatanishi ni vizuri tasisi mbalimbali zikajitosa kupatanisha vyama hivyo, ingawa yuko tayari kufanya hivyo ,kutokana na uzoefu wa kutatua migogoro aliona kwani anaamini vyama hivyo haviwezi kupatana bila kuwepo msuluhishi kutokana na unafiki wake ambapo wakikutana kwenye vikao hawaaminiani.

“Mwaka 2000 walifikia Muafaka lakini CCM ilishindwa kutekeleza madai ya CUF na Mwaka huu wametuambia kuwa wamefikia muafaka lakini hakuna anayeamini kama kweli madai ya CUF ni ya kweli kwani walifanya siri katika kipiondi chote walichokuwa wanazungumza …
katika ufahamu wangu hawa watu walitakiwa wapate msuluhishi akae nao awapatanishe kabla maafa hayajatufikia” anasema mzee huyo nakusema kuwa kilichopo Zanzibar ni mgogoro sio mpasuko wa kisiasa kama wanavyouita wanasiasa

Akizungumzia mgogoro ulioibuka katika kisiwa cha Pemba anaonya kuwa kutokana na msimamo ulioonyeshwa na wakazi wa kisiwa hicho wakitishia kujivika mabomu Serikali ya CCM isipojirekebisha na kutafakari kwa kina madai yao wanaweza kusababisha mauwaji makubwa nchini.

“tumefikia sehemu mbaya wale wanaotaka kujifunga mabomu watauwa hata wasio kuwemo”nakuwataka chama cha CCM kuacha ulevi wa Madaraka na kuitafakari kauli hiyo ya wapemba kutaka kujilipua huku akionya kuwa kauli hiyo ilitolewa baada ya CCM na CUF kushindwa kufikia muafaka jambo ambalo limerudisha hata maendeleo ya jamii nyuma.

Mzee huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Somangira Kigamboni na Makamu mwenyekiti Wilaya ya Temeke anasema kuwa kama watamwitaji anaouwezo wa kuwakutanisha Viongozi mahasimu Rais Amani Karume wa Zanzibar na katibu Mkuu wa Cuf Seif Shaarif Hamad ili kumaliza kabisa mgogoro huo kwani inaonekana wanashindania uhai wa watu.

“unapotaka kuwapatanisha wanaogombana kwanza unakutana na upande mmoja unausikiliza na kupima kiwango cha hasira kisha unatoa ushauri kuwa kushusha hasira zile ili iwe rahisi kukutana na upande wa pili vingenevyo watapigana mbele yako” anasema mzee Mpema (84) ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke anasema siasa za chuki hazikuanza leo.

Anasema kuwa wakati akiwa kijana wa TANU tawi la Kigoma wao ndio walikuwa wanamsaidia Mwalimu Julias Nyerere kueneza chama hicho kwa watu wakifanya kampeni kwa siri kwa kumuogopa Gavana wa kiingereza.

Anasimulia kuwa Mwaka 1961 uliitishwa uchaguzi mkuu chini ya Serikali ya Mwingereza ambapo vyama viliwili vilikuwa vinaongozwa na waafrika vilikuwa mahasimu kama ilivyo sasa kwa CCM na CUF vyama hivyo vilikuwa ni TANU ya Mwalimu Nyerere na Congress cha Zuberi Mtemvu.

Katika uchaguzi huo ambao nafasi ya juu iliyokuwa inagombewa ni uwaziri mkuu, Chama cha Tanu kiliamua kutumia mbinu chafu kumpaka matope mgombea wa Congress ili asichaguliwe na wananchi.

“mbinu iliyotumiwa na Nyerere kumshinda Mtemvu kirahisi ni kutumia karatasi ya kupigia kura kumchora Simba baadala ya picha halisi ya Mtemvu na Nyerere akachorwa amekaa amekipakata kitufe cha nchi….vijana wa Tanu tukaanza kupita usiku nyumba hadi nyumba tunawaambia wananchi wasimchague Simba atawatafuna bali wamcague Nyerer ndiye alikuwa Mlezi”

Mzee huyo anasema kuwa mbinu hiyo ilitumika kumpa ushindi mkubwa Mwalimu Nyerere lakini baada ya uchaguzi Mtemvu alibaini mchezo huo akaamua kupinga lakini Serikali ya Tanu chini ya Mwalimu Nyerere akiwa Waziri Mkuu iliwatia mbaroni wafuasi wa Congress kwa kuwaita Wahaini.

“Baada ya Mtemvu kufahamu kampeni hizo wafuasi wake wakaanza kudai uchaguzi huru ,Nyerere akawaita Wahaini akaanza kuwakamata waliosalimika walikimbilia nje waliobaki wakasweka ndani jela zikajaa mahabusu ,Serikali ikajitapa ‘tunataka kujenga jela zaidi ili waishie gerezani’na Mwaka 1962 Nyerere alipotawazwa kuwa Rais akapiga marufuku vyama vingi ili kuwavunja nguvu.

Mzee mpema anamaliza kwa kusema kuwa hakushangaa kusikia hivi karibuni wapemba waliojitokeza kudai Serikali ya Shirikishi wakiitwa wahahaini hata hivyo anasema amesikitishwa na kauli zilizotolewa na wapemba kuwa wapo tayari kujilipua huku serikali ikidharau kuwasikiliza madai yao ambayo kimsingi yanamantiki na yanaweza kuleta madhara makubwa kwenye jamii yasiposikilizwa na kutekelezwa nakumaliza kwa kusema Mwenye hekima hakosi Busara.

Mobinsons@yahoo.com .. …0712 17 16 23

Labels:

Katiba ya Tasisi ya Kaya na Familia (TAKAFA)

1.0 UTANGULIZI

Hii Tasisi imeanzishwa kwa lengo la kusaidia watanzania wote ambao ni masikini, jina la Tasisi hii limebuniwa na muasisi wake …

Jina hilo linafaa sana kutumika kwa kuwa linalenga walengwa ambao ni kutaka kuboresha maisha ya familia za watu masikini na makazi yao.

Hiyo inamaana kuwa tasisi hii itakuwa inasaidia familia na watu masikini watakaojiunga nayo wawe wanachama kwa kuboreshewa maisha.

Hii inatokana na kuwa Kaya nyingi za watanzania ni masikini hivyo kama wataweza kujiunga kwenye tasisi ya Kaya na Familia watasaidiwa kuondolewa umasikini.

Tasisi ya kaya na familia (TAKAFA) sio ya kiserikali imeanzishwa na wananchi masikini ili waweze kusaidiana kwa shida na raha.

Watu watakaofaidika nayo ni wanachama watakaojiunga na Tasisi hii kwa hiari yao wenyewe.

2.0 SEHEMU YA KWANZA

2.1.1 JINA ,ALAMA,ANUANI ,ENEO,NEMBO NA MUHURI.

2.2 JINA
Jina la Tasisi linajulikana kama Tasisi ya Kaya na Familia (TAKAFA)imeandikishwa chini ya sheria za vyama vya kijamii ,sheria namba …kwa jina la Tasisi ya Kaya na Familia.

2.3 ANUANI YAKE NI
TASISI YA KAYA NA FAMILIA
S.L.P
DAR ES SALAAM
TANZANIA.

2.4 EMAIL ; Mwema.shaurimoyo@gmail.com
2.5 SIMU ; 0753 399 579

2.6 ENEO;
Tasisi hii itakuwa na makao yake Karakata Kipawa ,Manispaa ya Ilala Dar es Salaam.

2.7 NEMBO;
Tasisi itakuwa inatumia kifupi cha TAKAFA kwa kuanza na TK kubwa kisha zinafuata herufi zingine ndogo za familia zikiwa na rangi ya blue zikikolezwa na nembo ya TK yenye rangi ya Kijani kiwiti ikitoa matumaini ya maisha mapya.

2.8 ALAMA
Barua yoyote ya kiofisi lazima iwe na kichwa cha habari kinaoitambulisha Tasisi ya Kaya na Familia.

2.9 MHURI; mhuri utakuwa na mandishi ya yanayotaja cheo cha kiongozi wa Tasisi na Nembo yake.

3.0 WAANZILISHI
Hili jina la Tasisi ya Kaya na Familia limekubaliwa kwa kuidhinishwa Mei-2008 na

1.Mobini Sarya
2.John Daniel
3.Mariam Gesagero
4.Amina Said

Watu hawao ambao majina yao yametajwa ndio waliohusika kuasisi Tasisi ya Kaya na Familia hivyo watakuwa na maamzi ya mwisho.

Pia watanzania wengine masikini watakuwa wanajiunga bila ubaguzi wa rangi au kabila.

3.1 MAANA
A. Tasisi hii itakuwa inafahamika kwa mjibu wa katiba kama TAKAFA

B.Katika Tasisi watu wenye kipato cha chini kabisa watasaidiwa

C.Tasisi itaundwa na kuimarishwa na Wanachama waanzilishi.

D. Wanachama waanzilishi ni wale walioasisi Tasisi

E. Tasisi haiendeshi shughuli zake kisiasa bali kijamii

4.0 SEHEMU YA PILI

4.1 MAJUKUMU YA TASISI
Tasisi ya TAKAFA sio Kampuni ya Kibiashara bali ni chombo ambacho kimeundwa kwa lengo la kuinua kipato cha watu masikini.

Lengo la TAKAFA ni kuwa kiunganishi kati ya masikini na masikini ili wawe na Sauti ya kupata mitaji kwenye Tasisi za Fedha bila kuwa na Dhamana ya mtu binafsi.

watu wote wenye kipato cha chini ,wakijiunga na TAKAFA watakuwa wanachama wake.

Hivyo kila mwanachama atatakiwa kuwa katika kikundi cha watu kumi ili kuwa rahisi kujuana na kusaidiwa.

Misaada ambayo wanachama watafaidika nayo ni

a.kuwezeshwa kukopa kwenye tasisi za pesa bila masharti

b.kupata huduma za kijamii bure au kwa kuchangia kidogo, kama Elimu,Afya na Maji safi.

c. kusaidiwa kwa hali na mali pale mwanachama anapopatwa na matatizo.

d.wanachama wote watakakuwa ndugu na TAKAFA itakuwa Imani kwao.

5.0 SEHEMU YA TATU

5.1 DIRA YA TAKAFA
Katika nchi nyingi za Dunia ya tatu zinakabiliwa na maadui watatu ambao ni Umasikini, Ujinga na Maradi.

Dira ya TAKAFA ni kuwaunganisha wanyonge Ili kushinda maadui hao.

6.1 SEHEMU YA NNE

6.1 LENGO LA TAKAFA

A.Kuwaunganisha masikini wote wawe na Sauti ya pamoja.
B .Kufanya maisha ya kila mwanachama yaboreke
C.Kuunda mtandao nchi nzima wa mtu kwa mtu
D. Kuhakikisha kila mwanachama anajiodoa kwenye kundi la masikini.

7.0 SEHEMU YA TANO

7.1MTAZAMO WA TASISI

TAKAFA ni wakala wa Maendeleo hapa nchini , kwa hiyo itafanya shughuli zake ikijikita kwenye Sekta binafsi.

Kwa mtazamo wake ni kwamba masuala yote yataamliwa na wananchama wenyewe.

8.0 SEHEMU YA SITA

8.1 VYANZO VYA MAPATO

TAKAFA itakuwa inapata Pesa kwa njia zifuatazo;

a.kuchangishana wanachama wenyewe au kutoka kwa wasisi.

b. Shughuli za Tasisi /miradi itakayoanzishwa.

c. harambee kutoka kwa watu ambao sio wananchama

d. wafadhili,Serikali na Mikopo kutoka kwenye Tasisi za Pesa.

e. kukusanya michango kutoka kwa wanachama wake.

9.0 SEHEMU YA SABA

9.1 MHIMILI WA BODI

Zifuatazo ni kazi na muundo wa Bodi ya TAKAFA.

A.VIONGOZI wa Tasisi, Mwenyekiti ,Katibu Mkuu na Afisa Mipango pamoja na waanzilishi wengine watatu.

B.WANACHAMA,wote wanakuwa chini ya Tasisi ambayo inaongozwa na Mwenyekiti.

C. SHUGHULI zote za Tasisi zitakuwa zinaendeshwa na Utawala wa Bodi.

D.KUSAINI mikataba na kuingia makubaliano masilahi ya Tasisi.

E.KUBEBA dhamana ya Mali zote za Tasisi.

F.MWENYEKITI wa Bodi,Katibu mkuu,Afisa Mipango na Mhadhini ndio watakaokuwa wanasaini nyaraka za Tasisi.

G.KUDHIBITI mapato yatokanayo na vyanzo mbalimbali.

H.MATUMIZI ya saini yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ya kiwanza ‘A’ na ‘B’ katika sehemu ya kwanza ‘A’ SAHIHI lazima iwe ya Mwenyekiti (2) Katibu Mkuu.

Kwa sehemu ‘B’ SAHIHI itatumika ya Afisa Mipango na Mhasibu.

Katika masuala yanayohusu kuchukua pesa sahihi inayotambuliwa ni ya Mwenyekiti au Mhasibu.

9.2 KAMATI NDOGO ZINAZOUNDA TASISI

A.Kutakuwepo kamati tatu ambazo zinatokana na mapendekezo ya Bodi kwa ajili ya kuendesha Shughuli za Tasisi na kushughulikia masuala mbalimbali.

B. Wajumbe wa kamati hizo watatokana na wale wanaounda Boda na majina yake yatapendekezwa na Boda.

C. Wajumbe wa kamati hizi watakuwa wanateuliwa kutoka moja hadi nyingine chini ya Mwenyekiti.

D.Kila kamati itakuwa na Mwenyekiti ,Katibu Mkuu na wasisi wengine watatu.

9.3.0 MUUNDO NA MAJUKUMU YA VIONGOZI WA TASISI

9.3.1 MKURUGENZI WA TASISI NDIYE;

A.Mwenyekiti wa Bodi ya Tasisi
B.Anakuwa na mamlaka kwenye mkutano
Wa Bodi.

C.Msemaji mkuu wa Tasisi na mamlaka zote zipo chini yake

D.Anachagua wajumbe wa mikutano ya Tasisi
E. Alama ya Tasisi

F.Mwenye dhamana na utawala wa mali za Tasisi.

9.3.2 KAZI ZA KATIBU MKUU NI;
A.kutunza kumbukumbuku za Tasisi
B.kuandaa agenda za mikutano
C.kuandaa taarifa za mkutano wa Boda kwa
Mwaka.
D.kuandaa na kuitisha mikutano ya Tasisi
Akishauriana na Mkurugenzi.
E.kila shughuli inayofanywa na Boda lazima
Ahusike.

9.3.3 AFISA MIPANGO ATAKUWA;

A.kuandaa mipango ya kuwafikia wanachama na kuwaunganisha
B.kuhamasisha watu wajiunge na Tasisi pamoja na kuwapatia elimu.

C.kuunda timu ya kuandaa mipango ambayo itasaidia kuinua kipato cha washirika (wanachama)

9.3.4 MHASIBU ATAKUWA

A.kupokea/ kutunza mali zote za Tasisi pamoja na kufanya mahesabu ya matumizi.

B.kudhibiti mapato na matumizi ya Tasisi

9.3.5 KAMATI NDOGO ZITAKUWA

A.zinapanga na kuendesha miradi/shughuli zilizopendezwa na Bodi
B.kuandaa taratibu na kanuni ndogo za uendeshaji wa Tasisi.

C.kuwa chini ya Mkurugenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tasisi.

9.4.O MTANDAO WA WANACHAMA NCHI NZIMA

9.4.1 VIONGOZI WA MATAWI,MASHINA,HADI TAIFA

A.KIKUNDI-kutakuwepo na kiongozi anayeongoza kikundi cha
Wanachama kumi atajulikana kama Kiongozi.
B.SHINA- ni mkuu wa vikundi kumi vyenye wanachama 100 atakuwa
Atatokana na wale viongozi kumi ataitwa BALOZI
C.TAWI- ni mkuu wa mabalozi 100 wenye wanachama 1000 atakuwa
Anachaguliwa miongoni mwa mabalozi.
D.GAVANA-ni mkuu wa jimbo/wilaya
10.0 SEHEMU YA NANE

10.1 WAANZILISHI

i.ni waasisi wa kweli katika Tasisi
ii. wapo aina mbili za waanzilishi

a.Waasisi- ni wale waliotumiwa muda wao mwingi kutafakari na kutoa wazo la kuanzisha pia kuhakikisha linakubalika kwa waanzilishi.

b.Waanzilishi- hao ni wale washirika wa kwanza kupokea wazo la kuanzisha tasisi na kujiunga kulieneza.

c.idadi ya waanzilishi itategemeana mapendekezo ya waasisi

d.idadi ya watu wanaounda bodi ya Tasisi sio chini ya 6 na sio zaidi ya 10

e.ushirika wa waasisi utakoma pale wanapofariki dunia vingenevyo watabaki kuwa waasisi na wajumbe wa bodi bila kikomo.

f. wasisi wana mamlaka ya kuchagua na kumweka katika nafasi yoyote wanaoona inafaa.

g.waasisi na washirika waanzilishi wote watakuwa na haki ya kuunda boda ya Tasisi lakini mamlaka na nguvu zote zitabaki mikononi mwa waasisi.

10.1.3 USHIRIKA WA WAANZILISHI
10.1.4 ushirika wa wanachama waanzilishi utakoma pale;

a.atakapojiuzulu mwenyewe

b.atakapofanya kosa na kufukuzwa

c.atakaposhindwa kuhudhuria mikutano (4)bila sababu wala maelezo

d. endapo atafariki dunia
e. hawezi kuendesha wala kusadia shughuli za tasisi

f.kufukuzwa na mkutano mkuu wa Bodi

11.0 SEHEMU YA 9

11.1 MIKUTANO

a.kutakuwepo mkutano mkuu wa bodi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya Tasisi

b.mwenyekiti wa Bodi anaweza kuitisha mkutano wa dharura wakati wowote

c.kamati ndogo zitakuwa zinakutana kila miezi mitatu kujadili maendeleo ya washirika wanavyoongezeka

d.ili mkutano ufanyike lazima mahudhurio ya wajumbe yatimie 2/3

12.0 SEHEMU YA KUMI

12.1 UTUNZAJI WA PESA NA MAHESABU

A.pesa zote za tasisi lazima zitunzwe benki na wakati wa kuchukuliwa mwenyekiti atie saini.
b.vitabu vya mahesabu lazima vitunzwe ofisi kuu

c.itakuwepo kamati ndogo ya mahesabu ili kukagua mapato na matumizi ya Tasisi.

d.Mkaguzi wa mahesabu kutoka nje atakuwa anaitwa baada ya Mwaka kumalizika na taarifa yake itakuwa inakabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Bodi .

13.0 SEHEMU YA 11

13.1 KANUNI NA TARATIBU NDOGO;- Bodi ya
Tasisi inamamlaka ya kutunga kanuni ndogondogo zinazoendana na wakati.

14.0 SEHEMU YA 12

14.1 MABADILIKO YA KATIBA;-Katiba inaweza kubadilishwa na Bodi katika mkutano mkuu wa Mwaka ikiungwa mkono na 2/3 ya wajumbe

1.5 SEHEMU YA 13

16.1 LUGHA YA TASISI
Lugha ya Tasisi ni kiingereza na kiswahili
Lakini kiswahili kitatumika zaidi.

16.2 WALIOPITISHA KATIBA
Sahihi za watu waliohusika kupitisha mapendekezo na kukubali kuanzisha Tasisi

JINA ANUANI SAHIHI

1.MOBINI SARYA
2.JOHN DANIEL
3.MARIAM GESAGERO
4. AMINA SAID

5.
6
7
8
9
10.

Hii inadhibitisha kwamba leo tarehe… ya Mwaka 2008 maelezo yote ya TAKAFA yamedhibitishwa na wahusika mwezi…..

Tasisi ya Kaya na Familia (TAKAFA)

Fomu ya kuomba kujiunga na TAKAFA kuanzia ngazi ya shina na kuendelea.

*muombaji ajaze nakala mbili moja ni ya maombi ya awali na ya pili ni ya wanakikundi wake.

1.Mimi……………
(majina kamili kwa herufi kubwa)
Naomba kujiunga na ……………ngazi ya………… kuanzisha………

2.Utambulisho /kuzaliwa

Tarehe……....kijiji/Mji…….….Wilaya………..………Mkoa………….

uraia
a.mimi ni raia wa
b.baba alikozaliwa……………..mama alipozaliwa
c.mahali ninapoishi……………………
d.Shina……….Tawi…………..Kata/wadi……………
f.jina la kiongozi wa tawi……………………………..

3.Elimu;
Kiwango cha elimu nilichofikia…………….

4.Uanachama
i.siku niliyoingia TAKAFA……………

ii.namba ya kadi yangu………nimelipa Ada hadi………..

5.Kazi yangu
a.kazi inayonipatia mapato/ninayoitegemea zaidi ni…………………….
b.kijiji ,eneo, mjini ninapofanyia kazi………………….

6.Tabia

a.umepata kushtakiwa kwa kosa lolote na kupewa adhabu?
(jibu ndio au hapana)…………………
b. kama ndio taja makosa yaliyokufikisha kwenye sheria
. ………………………………..
c.je umepata kuwa mfanyakazi ukafukuzwa bila kulipwa?
………………………… ………………

7. Ujenzi wa Tasisi ya TAKAFA

Tangu nimejiunga na Takafa nimeshiriki kuendeleza kwa kuunda mtandao kama ifuatayao.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

8.Udhibitisho

Nathibitisha kwamba maelezo niliyoyatoa kwenye fomu hii ni ya kweli
………………………. …………………………
Tarehe saini ya mwombaji

9.Maoni kutoka kwa wajumbe wa Bodi ya Takafa

a.kikao cha awali……………………………….

Tarehe ………………….saini………………

Kikao cha kuidhinisha…………………..

Tarehe……………….. Saini ya Mwenyekiti wa Bodi……………….

Labels: