Friday, August 4, 2023

Wekeza kwenye kilimo cha alizeti Chalinze -frusa na.1

Wekeza kwenye kilimo cha alizeti Chalinze

Na Mojr Kaisarya


Tutaanza kutizama au kuangalia frusa moja moja zinazopatikana kwenye kilimo wilayani chalinze mkoa wa Pwani na leo tuanze kuitazama frusa ya kilimo cha alizeti.

Kilimo cha Alizeti hakijawa maarufu sana kwa wenyeji wa hapa kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakilima ufuta baada ya kuachana na Pamba miongo kadhaa iliyopita.

Baada ya upungufu wa mafuta ya kula ulioikumba dunia miaka michache iliyopita sehemu mbalimbali za nchi walianza kulima mazao ya kukamua mafuta miongoni mwao ni alizeti.

Zao hili limepiga hodi kwa kasi wilayani hapa, na bahati nzuri ardhi ya chalinze ina rutuba ya kutosha kwa ajili ya kilimo hicho, hivyo kuwanufaisha wakulima.

Bado zao la alizeti halijaanza kushambuliwa na magonjwa kama mazao mengine, hali ambayo inaongeza faida kwa mkulima na gharama za kuandaa zao hilo sio kubwa kama nitakavyoonyesha hapa chini.

Bajeti

Kukodi heka 5 za kilimo ni shilingi 35,000/@ heka =175000

Kulima kwa trekta @heka 60,000 jumla tsh.300,000

Mbegu kg 2 @heka ni 15000 jumla kg 10 tsh.75000

Kupalilia @heka ni tsh.50,000 heka 5 ni tsh.250,000

Jumla tsh 800,000/= +kuvuna tsh, 200,000 = mil.1

 

Mavuno faida


Heka moja ya alizeti inatoa wastani wastani wa gunia 7*5=35 inategemea aina ya mbegu.

Gunia 35 ukiuza ni shilingi 70,000 @moja sawa na 2,450,000

Ukikamua gunia moja linatoa wastani wa lita 20 za mafuta sawa na dumu moja au dumu 35 .

Ukiuza kila dumu ni shilingi lakini moja sawa na Milion.3.5

Toa gharama za kilimo

3500,000


-1000000

Mil.2,500,000 faida au 2450,000-100000 =mil.1500,000 faida

Kwa kipindi cha miezi mitatu tu, wasiliana nasi kwa ushauri 

0766 297097

 

Labels:

Kwa mahitaji yako ya viwanja, nyumba na mashamba, Bagamoyo na Chalinze

Wasiliana na Dalali wetu makini

0766 297097

Au Whatsaap 0656 938315

1.  Changamkia frusa za uwekezaji katika kilimo cha Alizeti, mtama , ufuta, mhogo na Mbaazi wilayani Chalinze, mashamba yapo ya kununua au kukodi.


2.  Nunua viwanja vyenye material ya ujenzi kwa gharama nafuu sana.

3.  Nunua nyumba zilizokamilika au za wapangaji katika mji wetu wa chalinze na maeneo yake. Wasiliana nasi haraka.

4.  Pata maeneo ya kuwekeza mgodi wa kokoto, mawe na chokaa kwa gharama nafuu.

5.  Agiza kokoto kwa bei nafuu!