Wednesday, May 25, 2011

Vuvuzela "huenda inaeneza maradhi"

Vuvuzela chombo kilichotumika kwa kushangilia hasa na mashabiki wa soka kwenye Kombe la Dunia la soka mwaka jana- sio tu inasababisha uchafuzi wa mazingira kwa kelele, lakini huenda pia ikasababisha maradhi, kwa mujibu wa wataalamu.

Vuvuzela likipulizwa
http://languagelog.ldc.upenn.edu/myl/vuvuzela2.jpg

Upulizaji kidogo tu wa Vuvuzela hutoa mate mengi sawa na yanayotoka wakati mtu akipiga chafya, yakisafiri kwa mwendo wa kasi ya mara milioni nne kwa sekunde moja kwa kila tone, hii ni kwa mujibu wa jarida la PLoS One.

Katika eneo lililofurika watu, mtu mmoja akipuliza vuvuzela linaweza kuwaathiri watu wengine wengi kwa magonjwa yanayosambazwa kwa kuvuta hewa kama mafua na kifua kikuu.

Waandalizi wa michezo ya Olympiki mjini London mwaka 2010 bado wanafikiria iwapo waruhusu vuvuzela kutumika au la.

Dr Ruth McNerney, aliyeendesha utafiti wa hivi karibuni katika shule inayohusika na masuala ya usafi na maradhi ya nchi za joto ya London - London School of Hygiene & Tropical Medicine, amesema "upulizaji wa chombo cha vuvuzela" huenda kinahitajika kuliko kukipiga marufuku.

"Kama ilivyo wakati wa kukohoa na kupiga chafya, hatua zinapaswa kuchukuliwa kuzuia uenezaji wa maradhi, na watu wenye maradhi ya kuambukiza washauriwe wasipulize vuvuzela zao karibu na watu", alisema.

Kamati yake iliyochunguza hatari zinazoletwa na upulizaji wa vuvuzela, waliwatumia watu wanane waliojitolea kupuliza vuvuzela.

Kwa wastani chembechembe zinazotoka kwenye mapafu, 658,000 kwa lita ya hewa zilitolewa kutoka kwenye vuvuzela.

Matone hayo ya mate yaliruka angani kwa kiwango cha mara milioni nne kwa sekunde.

Kwa kulinganisha, wakati watu hao waliojitolea walipotakiwa kupiga kelele, waliweza kutoa mate kiasi cha chembechembe 3,700 tu kwa lita kwa kiwango cha 7,000 kwa sekunde.

Labels:

Tuesday, May 24, 2011

Polisi inavyohatarisha amani Tarime

Mara

JESHI la Polisi nchini limeendeleza tabia yake ya kumiwa na serikali kwa ajili ya kuwandamiza watu wake kadri wanavyoona inafaa.

Hivi leo Mei 24 wameafurusha wanaharakati wa kutetea haki za binadamu pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wametua wilayani hapo kwa lengo la kuvuatilia mauaji yaliyotokea kwenye mgodi wa Nort Mara.

RPC wa TARIME/RORYA ,CONSTANTINE MASSAWE
Jana ilikuwa ni kazi ya kufanyia miili mine uchunguzi na upasuaji ambapo leo ilipangwa waagwe kwenye uwanja wa sabasaba kisha wakazikwe lakini cha ajabu Usiku wa kuamkia leo Polisi walifika katika Hospitali ya wilaya ya Tarime na kuwakamata viongozi wa CHADEMA kasha wakachukua kwa nguvu maiti wote nakuanza kuwasambaza kwenye vijiji wanavyotokea.

Lakini cha ajabu kila walipokuwa wanafika kwenye mji walikuwa wanakuta hakuna ndugu wa marehemu kwa sababu wamewaacha Hospitalini na walichokuwa wanafanya ni kutupa maiti hapo kasha wanaondoka zao.

Baada ya kupambazuka wandishi wa habari waliamua kufuatilia matukio hayo katika kijiji cha Nyakunguru karibu kabisa na Mgodi huo takribani KM 20 , lakini walizingirwa na Polisi wakakamatwa na kupelekwa kwenye kituo kikuu cha Polisi Nyamwaga.

Na Habari zuilizopatika hivi Punde zimeweka wazi kuwa akina Tundu lisu na wanaharakati wa kituo cha sheria na haki za binadamu wamenyimwa dhamana hadi kesho kesi yao itakapoitajwa tena ,huku wandishi wa habari wanne waliokuwa wamekamatwa kijiji Nyamwaga wameletwa wilayani ilipo ofisi ya Kanda maalum kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao.

nakujua kama watapewa dhamana au wasubiri kesho kupanda mahakamani,aidha taarifa zingine kutoka wilayani Serengeti zinadai kuwa Mkuu wa wilaya hiyo amenusurika kuchomwa mishale baada ya kukubali kusindikiza gari la Polisi lililopeleka maiti usiku katika kijiji cha Bonchugu na kuwaacha ndugu wa Marehemu wilayani Tarime, ndipo yowe ikapigwa watu wakatoka na mishale, maiti imetupwa vichakani baada ya Polisi kulipua mabomu 30 wakimuokoa DC na wao kujisalimisha mjini Serengeti