Monday, April 9, 2007

BARUA YA MALIMA KWA SPIKA


Malima: Sikubali Spika kunipatanisha na Mengi





Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima



Nimepata muda wa kupitia na kutafakari kwa kina maelezo yako yaliyokuwemo ndani ya uamuzi wako wa tarehe 8 Februari 2007 wakati ukiwasilisha bungeni uamuzi huo katika suala hili.

Aidha, nimepata nafasi ya kurejea suala lote, ikiwa ni pamoja na matamshi yangu ndani ya Habari na Utamaduni na Michezo pamoja na barua yangu kwako nikiomba muongozo.

Kabla sijawasilisha maoni yangu kuhusu uamuzi wako huo, naomba nieleze masikitiko yangu kuhusu matamshi uliyonukuliwa kutoa kwenye gazeti la RAI, toleo namba 701 la tarehe 15-21 Machi 2007. Gazeti hilo limekunukuu ukisema kwamba nashauriwa vibaya katika maamuzi yangu na kwamba unalaumiwa kwa kutonichukulia hatua.

Aidha, Spika amenukuliwa akisema ninapotafutwa na ofisi yake, simu yangu inazimwa kwa taathira, yaani ninazima simu kwa makusudi ili nisipatikane.
Mheshimiwa Spika, naomba nikuhakikishie kwamba tangu sakata hili limeanza sijawahi kuzungumza na vyombo vya habari kwa kuwa ninaamini si mahali sahihi pa kulitafutia ufumbuzi. Hivyo sikuona sababu ya Spika kutoa matamshi ambayo hayanitendei haki bila kupata nafasi ya kupokea maoni yangu. Niseme tu kwamba wakati mnanitafuta nilikuwa jimboni kwangu Mkuranga, kwanza katika kampeni ya uchaguzi mdogo wa kata ya Shungubweni na baada ya hapo katika usimamizi wa shughuli za ujenzi wa shule za sekondari.

Maeneo mengi ya Mkuranga hayana mtandao wa simu, kwa hiyo inawezekana kwamba wakati mnanitafuta nilikuwa nje ya mtandao. Taarifa hiyo niliifikisha ofisi ya Katibu wa Bunge. Hivyo, naomba nikuhakikishie kwamba sikuwahi kuzima simu yangu kwa makusudi ili kukwepa kuwasiliana na Ofisi yako.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme yafuatayo kuhusu uamuzi wa Spika wa tarehe 8 Februaru 2007:

Spika wa Bunge ameamua kwamba mimi ni muongo, na kwamba kauli yangu ndani ya Bunge ilikuwa ya kubuni iliyolenga kumgonganisha Bwana Mengi na viongozi wakauu wa kitaifa. Uamuzi huo ulishinikizwa na ushauri tofauti wa Wabunge Mh. Christopher ole Sendeka, Mb na Mh. Anne Kilango Malecela.

Spika wa Bunge ameamua nikutanishwe na Bwana Mengi wa IPP ofisini kwake, kwa ajili ya kutafuta suluhu baina yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nikukumbushe tu kwamba mimi nilipata bahati ya kukaa kwenye kamati ya maadili uliyoikabidhi jukumu la kufanyia kazi suala hili kwa muda wa wiki sita. Kwenye kamati tulipata nafasi ya kusikia maoni ya pande zote, pamoja na kusikiliza maelezo ya mashahidi wa pande zote. Naomba nikufahamishe kwamba kamati hiyo, kama ulivyosema menyewe, ilifanya kazi kwa umakini mkubwa, ilifikia uamuzi kwamba sikukosea katika matamshi yangu na kwamba nilikuwa ndani ya taratibu na kanuni za matamko ya wabunge katika utekelezaji wa majukumu yao, na hivyo sikumkosea Bwana Mengi.

Licha ya maamuzi hayo ya kamati, busara ya Spika imeona ichukue maoni ya ushauri tofauti wa Mh. Ole Sendeka ambaye naamini hakuelewa yaliyokuwa yanasemwa ndani ya kamati ama hakusikiliza maelezo ya utetezi, na yamezingatia ushauri tofauti wa Mhe. Anna Kilango Malecela ambaye hakuhudhuria hata kikao kimoja cha kamati ambapo mimi, Mengi na mashahidi wetu tulifika kutoa maelezo yetu.

Naamini kwamba uamuzi wa Spika haukuzingatia ukweli wa nia na madhumuni ya matamshi yangu bungeni, na badala yake umenihukumu kwa tafsiri ya taathira (interpretation by implication), hali ya kwamba matamshi yangu yalikuwa wazi, bayana ambayo hayakuwa na tafsiri za kujificha na barua yangu kwa Spika inajieleza vya kutosha, na hivyo uamuzi wa Spika haukunitendea haki.

Naomba nikuhakikishie kwa dhati kabisa kwamba nakuheshimu sana kama Spika wangu, kama kiongozi wa juu wa chama changu na mwisho kama mzee wangu.

Hata hivyo, Bwana Mengi hakunithibitishia kwamba anaelewa uzito wa tuhuma zake juu yangu, na wala kwamba ana nia ya kurekebisha kauli zake za kashfa dhidi yangu ambazo si tu zimenikashifu mimi, lakini pia zimewakashifu wabunge wenzangu wote.

Naomba nitamke, kwa maana hiyo basi, kwamba kwa taratibu, misingi na vigezo ulivyotumia kufikia maamuzi yako ya tarehe 8 Februari 2007, sina nia ya kukutana na Bwana Mengi kwa lengo la kupatanishwa naye kwa ugomvi usiokuwepo, isipokuwa labda ugomvi kama anao ni wa kwake aliyetengeneza kwa mashaka yake na kutojiamini kwake. Nikiridhia kukutana naye kwa lengo la kupatanishwa nitakuwa sijitendei haki mimi mwenyewe kwa kuwa nitakuwa nafanya hivyo kinyume na imani ya misingi ya wajibu wangu kama Mbunge, lakini pia nitakuwa sikuwatendetea haki Wabunge wenzangu.

Naomba kuwasilisha,

Adam Kighoma Ali Malima, Mb
MBUNGE WA MKURANGA.

Labels: ,

WENGI KUNUFAIKA NA RFV,KWELI KUFA KUFAANA

Na Mobini Saarya

kweli katika Dunia hii maajabu hayaishi ndivyo sasa tunavyoshudia ,kila siku

yakiibuka matukio ya ajabu na yakustaajabisha, ikiwa utakuwa hujawahi

kukumbana nalo ukilisikia utafikiri kwamba ni hadithi ,lakini kwa wale wanaokuwa

wamelishuhudia inakuwa ni jambo la kawaida.

katika dunia hii ni vema binadamu sasa afahamu kuwa zimepita zile zama za

hadithi ya hapo zamani palikuwepo na kitu fulani, sasa hivi tunachokisikia na

kukishudia ni visa na mikasa ya kweli inayotokea kwenye jamii ambayo inakuwa

vigumu kuvikubali kwa yule anayekuwa hajakumbana nayo.

kwa mfano habari za kuwepo kiumbe anayejulikana kama Popobawa limekuwa ni

jambo linalopingwa na watu kuwa huo ni uvumi , lakini kwa wale ambao

wameshudia au kuathiliwa na kiumbe hicho hawana cha kupinga, mfano ilifikia

hatua huko zanzibar wakauwa binadamu mmoja aliyekuwa anaendesha baiskeli

wakimfananisha na Kiumbe cha Popo Bawa.

tukio hilo linafananasha na tukio lililotokea Septemba 11 Mwaka 2001 kule

Marekani wakati Maadui wa Marekani wanaopachikwa jina la Magaidi walipolipua

kituo cha Kimataifa cha Biashara Word Trade Centre 'W.T.C' kwa Ndege

walizoteka na kuzigeuza Mabomu ili kutimiza Azima yao iliyofaniwa na

kuushangaza ulimwengu hata kuingia kwenye Rekodi ya Dunia.

baada ya tukio hilo ilidaiwa kuwa huko Marekani kila alikuwa anaonekana kuwa na

Ndevu nyingi alikuwa anakamatwa na kunyanyaswa akihusishwa kuwa ni mfuasi

wa Magaidi wakimfananisha ndevu zake na za Sheikh Usamah bin Laden yule

Kaptein wa Alqued na Jemadari wa vita ya kushtukiza.

wakati hayo yakionekana kuwa tayari yametokea kumeibuka ugonjwa mpya hapa

Tanzania ambao umepewaa jina la Homa ya Bonde la Ufa kwa kingereza RVF

wakimaanisha kuwa chimbuko la ugonjwa huo ni 'mikoa ya Bonde la ufa' na

maana ya Bonde la ufa ni bonde la asili linaloanzia Kaskazini mwaKenya hadi

Tanzania kupitia mikoa ya kaskazini kuelekea kusini kisha Maghaaribi mwa

Tanzania yaani ziwa Tanganyika.

jinsi bonde hilo lilivyopita ndivyo ugonjwa huo unavyoambaa na kuathiri maisha

ya viumbe wa Dunia kama wanyama na Binadamu, hali hiyo imesababisha ibuke

Michapo kuwa ni njama za wanya kutaka kujinusuru na hasira za binadamu kwa

kuwafanya kitoweo kila Mara ndio maana wameamua kujigeuza sumu amabayo

imesababisha wasichinjwe.

walianza kuku wakidaiwa kuwa wanamafua ya Ndege ,kutokana na ugonjwa huo

binadamu wakagopa kuwachinja aina zote za Ndege wakihofia kufa kwa Homa ya

Ndege sasa wanyama kama ng'ombe wamekuja na RVF, tumeshuhudia Pasaka

nzima mabucha yakiwa yameganda nyama na mengine yakiwa yamefungwa,

nakumbuka mtu mmoja aliyekuwa anabatiza watoto wake alichinja Mbuzi lakini

wageni wakagomea kitoweo hicho ikaamuliwa waletewe maharage na mchicha

watumie kwenye wali.

baada ya kero hizo kuibuka za hapa na Pale wamekuja watu wanajiita ni wataalamu

waliosomea magonjwa ya wanyama ya kuambukiza kwenda kwa Binadamu

wakiwa na mchapo mkali wakisema wako tayari kuwaondolea binadamu hofu ya

kula nyama ya RVF ikiwa tu Serikali itawaruhusu kufanya hivyo.

wataalamu hao wanasema kuwa wanataka serikali iwape ruhusa wafungue vituo

vya zahanati za wanyama katika maeneo mbalimbali ya nchi kisha serikali itunge

sheria ya kuwalazimisha watu kila anayenunua mbuzi,ng'ombe au kondoo kabla

hajaenda kumchinja sharti apitie kwenye zahanati hizo mnyama achukuliwe damu

kwanza kisha apimwe choo kama yuko safi.

baada ya hapo mlaji akiwa amelipia gharama zote za upimaji wa vipimo vya Homa

ya Rift Valley atahakikishiwa kuwa kitoweo chake ni salama kwa kuliwa,

ataruhusiwa kwenda kuchinja, lakini kama atakutwa na ugonjwa huo atarudishiwa

wa pesa zake za upimaji kisha ataacha yule mnyama hapo, ili asiende kuambukiza

wengine majumbani.

kwa hiyo ikiwa wataalamu hao watafanikiwa kupewa kibali hicho wanatarajiwa

kuvuna kiasi kikubwa cha hela kutoka kwa wachinjaji na walaji wa majumbani

,mtandao wa mobinday.blogspot.com. umebaini na kunawasiwasi mwingine kuwa

huenda wapimaji wakaamua kuwaandanganya walaji kuwa kitoweo chao kina

maradhi ili mlaji akiache pale wao wakajichane 'tunahamu ya kuona uadilifu

wao'anasema mlaji mmoja.

habari zaidi soma; www. mobinday.blogspot.com. 0753 399 579

Sunday, April 8, 2007

KWA MCHEZO HUU UKIMWI HAPONI MTU

Na Mwandishi Maalum.

kumbe katika katika Dunia hii kuna watu hawapo tayari kuona ugonjwa wa Ukimwi siku moja ukitoweka kabisa,kwao itakuwa hasara kubwa kuliko kwaida kama inavyoonekana sasa.

tumekuwa tukifutilia yanapofanyika matamasha Mambalimbali wanayoita makongamano ya kuelimisha rika namna ya kuipambana na Ugonjwa huo hatari lakini kinyume na matarajio ya walengwa yamekuwa yakitumika kuchochea ugonjwa huo, ni ukweli usio na kifani kwamba hayo makongamano hayasaidii kwa njia yoyote kumzuia mtu siambukizwe ukimwi.

hata ukiwauliza waandaji wa Makongamano hayo kuwa tume takwimu ya watu ambao walikuwa katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi lakini nyie katika makongamano yenu mkafaniwa kuwaokoa, hawana, lakini ikitokkea kabla ya kongamano wakapimwa watu wote waliohudhuria hilo onyesho kisha baada ya miezi mitatu walewale watu wakatafutwa wakapimwa idadi ya walioambukizwa itakuwa imeongezeka!

hiyo inatokana kuwa kila wanapokutana vijana pamoja muonekano wao na mavazi wanayokuwa wamevaa katika kongamano la ukimwi huwa hakuna tafauti na watu wanaokwenda Disko usiku hali hiyo hutia vishawishi na siku kama hivyo vijana wengi hupata wapenzi wapya!

tulishudia katika maadhimisho ya Disemba Mosi Mwaka jana yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana CCM jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Leders Club, kwa wale walioshuhudia walijua kuwa Vita ya ukimwi bado haijanza kinachofanyika ni 'Mwaliko wa harusi Matangani'

katika kongamano lile akili za vijana wa pale zilionekana kuzama na kufurahi zaidi kusikiliza zile nyimbo za wasanii wa kizazi kipya kuliko kuelewa ile maantiki ilikuwa imewapeleka pale, hakuna alikuwa anaonekana kujali na zaidi, Tamasha liligeuka 'siku ya uzinduzi wa kondom mpya na kushudiwa vijana wakipanga foleni kutaka mgao!

hatujui zile kondomo vijana walizokuwa wanagombea walikuwa wanakwenda kufanyia nini kuchezea kama puto au kufanyia ngono na zinauimara kiasi gani kuzuia maambukizi ya ukimwi.

hiyo ni kwa upande wa dunia tuangalie Makanisani, April 7 ilikuwa ni siku yaMkesha wa Pasaka kwa wakiristo ambao wanaamini kuwa ni siku ambayo Yesu Kristo 'Mwana wa Mungu' alishinda na kulala kwa hiyo tulitegemea kuona wakiwa watulivu katika hali ya maombolezo ya kuvaa nguo nyeusi Pasaka nzima, kwani mkombozi wao alikuwa amekufa.

kinyume na Matarajio katika Mkesha tulishuhudia watu wakielekea makanisani wakiwa na mawazo mengine kabisa wengine wanakwenda kutafuta wapenzi ni katika hali kama hiyo ulikuwa unakita waumini wengine wapo makanisani wanasali wengine wapo kwenye kona nje ya kanisa wanatongozana huku mavazi waliyovaa yakiwa ndivyo sivyo.

na hali kjadhalika haikuishia hapo Pasaka nzima ikiendelea wanadamu wengine walikuwa wanaendeleza uzinzi hadi Pasaka ikakamilika, bila kujua maana yake nini kupoteza umhimu wa siku yenyewe na wengine kujikuta wanakuwa mawakala wa kupokea na kusambaza virusi vya Ukimwi.

ili kunyesha kuwa sasa watu wameanza kuuzoea Ugonjwa huo, hata viongozi wa Makanisa nao katika Mahubiri ya Pasaka walijitenga kukemea vitendo vya Uzinzi ambavyo husababisha maambukizi na badala yake mahubili yao yaligeuka Hutuba zilizokaa kisiasa na kiuchumi, huku wakikwepa kuzungumzia hata umaskini wakisema 'Maskini tunao hapa duniani siku zote'

hakuna sasa kiongozi wa Dini anayeonekana kukemea au kuipambana kikamilifu na ugonjwa huu hatari wa Ukimwi unaoonekana kunana dhahiri shairi na Ugonjwa wa Ukoma ambao uliwatesa watu wazamani ingawa hadi sasa upo lakini sio tishio tena.

katika hali kama hiyo tunaona ni vyema Serikali ikaingilia kati ikaamua kubadilisha namna ya kupambana na ugonjwa huu,kuna haja serikali ikaanza kwa kupiga marufuku matamasha yote yanayohusiana na Ukimwi kisha ikajaribu kufuatilia kama kuna haja ya kuendelea kuwepo na Mikesha makanisani.

ni hali ya kushangaza kuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,anaacha majukumu yake Ofisini anakwenda kupambana na Makahaba wa uwanja wa Fisi manzese, wakati wahusika wakuu wapo, hivi kazi ya Tume ya Taifa ya kupambana na Ukimwi TAKAIDS ni nini?

kila mwaka inatengewa bajeti nono lakini umhimu wa kuendelea kuwa na tume hii hatujauona, kwa watanzanaia kuendelea kuteteketea kwa ugonjwa huu,Takaids,Wizara ya Utamaduni na Viongozi wa Dini wanabebeshwa lawama moja kwa moja kwani maisha ya watanzania yanawategemea wao.

kwa mfano wizara ya habari ,utamaduni na Michezo imekuwa ikizembezea na kutazama utamaduni wetu ukiharibiwa na wageni bila ya wao kuchukua hatua yoyote ile, huku utamaduni wa kigeni ukizidi kushika kasi ya kuchochea ukimwi.

leo tunanyosheana vidole kuwa yule ana ukimwi lakini itafikia Kipindi ambacho, wakati kila mmoja ataonekana ameathirika na kitakachokuwa kinafanyika ni kujaribu kuokoa wale wachache ambao hawajaupata ili waendelee kuzaliana kuokoa hiki kizazi.

itafikia wakati ambapo idadi kubwa ya wanadamu watakuwa wameathilika mbapo sasa tutarudi kuwanyoshea vidole wale ambao hawajaathilika kwa kusema yule inawezekana hajaathilika, hapo ndipo Dunia itajikuta imechelewa.

historia ya ugonjwa wa Ukimwi inaanzia pale Latin Amerika miaka ya 70 wakati huo unjwa huo ulifahamika kama unjwa wa mashoga, ulioletwa na Mungu kama pigo kwa watu waliokuwa wanajihusisha na vitendo vichafu, lakini baadaye walijikuta wakiambukizwa hata wale ambao hakuwa mashoga hapo kosa lilifanyikia.

kama binadamu wakati huo angechukua tahadhari dhabiti leo tungepona au hata uliporipotiwa kuwa umepiga hodi mkoani Kagera mwaka 1982 Serikali ingechukua hatua ya kuweka karantini na kuzuia kuhakikisha wageni wote waliokuwa wanaingia nchini wamepimwa na wanavyeti leo hii ugonjwa huu tungekuwa tunasikia.

kinachoonekana sasa hapa ni kwamba Dunia haijaamua kupambana na ugonjwa huu kwani kuna watu wanaonekana wanafaidika na wasingependa kuona ugonjwa huu ambao wengi wameugeza uchumi ukiisha,kama dunia iliweza kupambana na kimeta kwa muda mfupi au Ugonjwa wa mafua ni kwanini huu?.

ikiwa serikali kama ya Tanzania sasa inapamba na Homa ya Bonde la Ufa RVF kwani isitumie mbinu kama zile kupambana na ukimwi, watu wanapenda Nyama lakini wameweza kujizuia iweje washindwe uzinzi kwani ni wangapi wameshuhudia mgonjwa wa RVF lakini mbona wa Ukimwi tunawashudia majumbani mwetu.

watu wamegeuza ugonjwa wa ukimwi kuwa ni uchumi kwao wanasema wanawasaidia wenye ukimwi, kumbe wanavuna chao wenye ukimwi wakifa wakamalizika wanawageukia yatima walioachwa kwamba wanawasaidia watoto yatima, hapo pia wanavuna chao halafu leo walale waamke wambiwe ukimwi umetoweka itakuwaje?

tusitegemee matamasha wala makongamano,tusiitegemee Kondomu kama kinga ya maisha yetu,kondomu sio Bima ya Afya, tubadilike kwanza ni bora umri uwekwe kila mmoja akiufikisha anaingia kwenye ndoa kwa maana nyingine ni kwamba kwa sababu ya tamaa zetu ni bora kila mmoja awe na mke au mme wake mwenyewe hiyo ni kinga imara.
pia ni bora sheria ya kupambana na wazinzi ikatungwa polisi na mgambo wakapewa uwezo wa kuingia kwenye magesti na kuwatoa nje wale wote ambao hawana vyeti vya ndoa lakini wanafanya uzinzi, wenye vinguo vifupi washughulikiwe kikamilifu wakiwemo mashoga.
ni bora ifahamike kuwa wakati oparesheni ya kutokomeza ugonjwa huu inaendeshwa ni bora kuachana na dhana ya Haki za Binadamu,ili kuweza kupambana kikamilifu na mawakala wa Ukimwi, njia kama hizo zilitumika kule Uganda wakaweza kuutokomeza ugonjwa huo kwa kuwachapa makahaba wote bakora na kuwafurusha huko.


uganda imetajwa karibuni hapa kuwa ongezeko la ugonjwa huo limeanza baada ya kupunguza mapambano na matumizi ya kondomu kuripotiwa kuingezeka nchini humo, ni vema serikali ibadilishe mapambano kwani hali ni mbaya hadi makanisani.

0753 399 579kwa msaada wa.website; mobinday.blogspot.com.

VIONGOZI WAASWA ASKOFU

Na mwandishi wetu

VIONGOZI wa Serikali wa ngazi za chini wakiwemo wakuu wa Mikoa, wilaya wametakiwa kutosubiri maagizo toka kwa Rais Kikwete na badala yake wajitume wao wenyewe.

Hayo yalisemwa jana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya, Evaristo Chingula wakati akihubiri katika ibada ya misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka iliadhimishwa kitaifa Mkoani humo katika kanisa la Bikira Maria wa Fatma, kanisa la Hija lililoko Mwanjelwa.

Askofu chingula alisema kuwa leo hii mpaka maelekezo yatoke Ikulu kwa viongozi wa ngazi za juu ndipo mambo yaanze kufanyika.

"Leo mpaka habari itoke Ikulu, kwani sisi hatuoni shida ambazo zipo katika mazingira yetu, kuna watoto wengi ambao wapo katika mazingira yetu hawajaenda shule lakini mpaka mtu wa juu aseme kuna tatizo la watoto ambao hawajaenda shule ndipo maelekezo mengine yanafuata kwani sisi hatuoni shida hizi? Alihoji

Alisema kuwa yapo matatizo mengi ambayo hayapaswi kusubiri maagizo toka Ikulu na kwamba viongozi wa ngazi hizo ndio wenye wajibu katika kushughulikia kwani wapo katika mazingira ambayo wanayaona matatizo hayo.

" Hatuna mpangilio, katika mazingira yetu nenda katika baadhi ya mitaa hapa Mwanjelwa, kipindupindu kikifika anakuja mtu anasema kimefika" alisema

Aidha alisema kuwa kuna tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali kupiga marufuku baadhi ya shughuli fulani mpaka tatizo litokee.

"Tuangalie vijana wanaoendesha mikokoteni wakigonga mtu ndio waseme hapana lazima tuwe na mpangilio, tuwatafutie sehemu ya kuwawezesha wao wenyewe kujiajiri na kuweza kujipatia kipato ndipo tupige marufuku.

Wakati huo huo Askofu Chingula amezishutumu Taasisi zisizo za Kiserikali NGO's zinazojishughulisha kulea watoto yatima kuwa baadhi ya Taasisi hizo zimeanzishwa kwa manufaa ya kuneemesha watu fulani na si kulea watoto hao kama ilivyokusudiwa.

Alisema wengi wanaoanzisha Taasisi hizo huanzisha kwa lengola kujipatia kipato wao wenyewe.

"Wapo wengine ambao hujipatia watoto yatima kwa kuanzisha vituo kwa ajili ya kuwalea, kumbe ni njia ya kujitafutia mishahara kwa ajili ya manufaa yao binafsi" alisema Askofu Chingula.

Alisema kuwa kuna watu ambao wapo tayari kusimama juu ya migongo ya watu fulani ili tu kufaidika kupitia migongo ya watu hao.

Alisema kufanya hivyo hasa kwa wakristu ni kwenda kinyume na watu wa Mungu.

Awali katika mahubiri yake Askofu Chingula alisisitiza upendo ndani jamii.

Alisema upendo ni pamoja na kujitolea kwa ajili ya watu wengine wenye matatizo mbalimbali.

"Mfanyakazi lazima afanye kazi si kwa kujitafutia fedha tu bali ni kutafuta njia ya kusaidia wahitaji, wale wanaohangaika hii ni kusaidia kueneza upendo wa Kristo" alisema

Alisisitiza kuwa maisha yetu si ya binafsi bali lazima yaonekane kwa wengine.

Aidha alisema kuwa katika bara la Afrika mambo ya huruma, haki na upendo havipo hivi sasa

Alisema viongozi wa dini wanatarajia kufanya mkutano barani Afrika kuzungumzia masuala ya Amani.

"Watafanya mkutano huo kuonesha kuwa hatuna huruma, upendo hatutaki kuwa watu wa amani".

Alisema jamii ina wajibu wa kulinda na kuthamini upendo na kusisitiza kuwa watu wa ndoa ndio ngazi ya kwanza ya kuonesha upendo wao kwa kulea watoto katika maadili.

Askofu Chingula alisema kuwa wajibu wa kulea watoto si wa Serikali ni wa mzazi wenyewe na kama mtoto akiharibika basi mzazi hakutekeleza wajibu wake.


MWISHO.