Sunday, April 8, 2007

KWA MCHEZO HUU UKIMWI HAPONI MTU

Na Mwandishi Maalum.

kumbe katika katika Dunia hii kuna watu hawapo tayari kuona ugonjwa wa Ukimwi siku moja ukitoweka kabisa,kwao itakuwa hasara kubwa kuliko kwaida kama inavyoonekana sasa.

tumekuwa tukifutilia yanapofanyika matamasha Mambalimbali wanayoita makongamano ya kuelimisha rika namna ya kuipambana na Ugonjwa huo hatari lakini kinyume na matarajio ya walengwa yamekuwa yakitumika kuchochea ugonjwa huo, ni ukweli usio na kifani kwamba hayo makongamano hayasaidii kwa njia yoyote kumzuia mtu siambukizwe ukimwi.

hata ukiwauliza waandaji wa Makongamano hayo kuwa tume takwimu ya watu ambao walikuwa katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi lakini nyie katika makongamano yenu mkafaniwa kuwaokoa, hawana, lakini ikitokkea kabla ya kongamano wakapimwa watu wote waliohudhuria hilo onyesho kisha baada ya miezi mitatu walewale watu wakatafutwa wakapimwa idadi ya walioambukizwa itakuwa imeongezeka!

hiyo inatokana kuwa kila wanapokutana vijana pamoja muonekano wao na mavazi wanayokuwa wamevaa katika kongamano la ukimwi huwa hakuna tafauti na watu wanaokwenda Disko usiku hali hiyo hutia vishawishi na siku kama hivyo vijana wengi hupata wapenzi wapya!

tulishudia katika maadhimisho ya Disemba Mosi Mwaka jana yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana CCM jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Leders Club, kwa wale walioshuhudia walijua kuwa Vita ya ukimwi bado haijanza kinachofanyika ni 'Mwaliko wa harusi Matangani'

katika kongamano lile akili za vijana wa pale zilionekana kuzama na kufurahi zaidi kusikiliza zile nyimbo za wasanii wa kizazi kipya kuliko kuelewa ile maantiki ilikuwa imewapeleka pale, hakuna alikuwa anaonekana kujali na zaidi, Tamasha liligeuka 'siku ya uzinduzi wa kondom mpya na kushudiwa vijana wakipanga foleni kutaka mgao!

hatujui zile kondomo vijana walizokuwa wanagombea walikuwa wanakwenda kufanyia nini kuchezea kama puto au kufanyia ngono na zinauimara kiasi gani kuzuia maambukizi ya ukimwi.

hiyo ni kwa upande wa dunia tuangalie Makanisani, April 7 ilikuwa ni siku yaMkesha wa Pasaka kwa wakiristo ambao wanaamini kuwa ni siku ambayo Yesu Kristo 'Mwana wa Mungu' alishinda na kulala kwa hiyo tulitegemea kuona wakiwa watulivu katika hali ya maombolezo ya kuvaa nguo nyeusi Pasaka nzima, kwani mkombozi wao alikuwa amekufa.

kinyume na Matarajio katika Mkesha tulishuhudia watu wakielekea makanisani wakiwa na mawazo mengine kabisa wengine wanakwenda kutafuta wapenzi ni katika hali kama hiyo ulikuwa unakita waumini wengine wapo makanisani wanasali wengine wapo kwenye kona nje ya kanisa wanatongozana huku mavazi waliyovaa yakiwa ndivyo sivyo.

na hali kjadhalika haikuishia hapo Pasaka nzima ikiendelea wanadamu wengine walikuwa wanaendeleza uzinzi hadi Pasaka ikakamilika, bila kujua maana yake nini kupoteza umhimu wa siku yenyewe na wengine kujikuta wanakuwa mawakala wa kupokea na kusambaza virusi vya Ukimwi.

ili kunyesha kuwa sasa watu wameanza kuuzoea Ugonjwa huo, hata viongozi wa Makanisa nao katika Mahubiri ya Pasaka walijitenga kukemea vitendo vya Uzinzi ambavyo husababisha maambukizi na badala yake mahubili yao yaligeuka Hutuba zilizokaa kisiasa na kiuchumi, huku wakikwepa kuzungumzia hata umaskini wakisema 'Maskini tunao hapa duniani siku zote'

hakuna sasa kiongozi wa Dini anayeonekana kukemea au kuipambana kikamilifu na ugonjwa huu hatari wa Ukimwi unaoonekana kunana dhahiri shairi na Ugonjwa wa Ukoma ambao uliwatesa watu wazamani ingawa hadi sasa upo lakini sio tishio tena.

katika hali kama hiyo tunaona ni vyema Serikali ikaingilia kati ikaamua kubadilisha namna ya kupambana na ugonjwa huu,kuna haja serikali ikaanza kwa kupiga marufuku matamasha yote yanayohusiana na Ukimwi kisha ikajaribu kufuatilia kama kuna haja ya kuendelea kuwepo na Mikesha makanisani.

ni hali ya kushangaza kuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,anaacha majukumu yake Ofisini anakwenda kupambana na Makahaba wa uwanja wa Fisi manzese, wakati wahusika wakuu wapo, hivi kazi ya Tume ya Taifa ya kupambana na Ukimwi TAKAIDS ni nini?

kila mwaka inatengewa bajeti nono lakini umhimu wa kuendelea kuwa na tume hii hatujauona, kwa watanzanaia kuendelea kuteteketea kwa ugonjwa huu,Takaids,Wizara ya Utamaduni na Viongozi wa Dini wanabebeshwa lawama moja kwa moja kwani maisha ya watanzania yanawategemea wao.

kwa mfano wizara ya habari ,utamaduni na Michezo imekuwa ikizembezea na kutazama utamaduni wetu ukiharibiwa na wageni bila ya wao kuchukua hatua yoyote ile, huku utamaduni wa kigeni ukizidi kushika kasi ya kuchochea ukimwi.

leo tunanyosheana vidole kuwa yule ana ukimwi lakini itafikia Kipindi ambacho, wakati kila mmoja ataonekana ameathirika na kitakachokuwa kinafanyika ni kujaribu kuokoa wale wachache ambao hawajaupata ili waendelee kuzaliana kuokoa hiki kizazi.

itafikia wakati ambapo idadi kubwa ya wanadamu watakuwa wameathilika mbapo sasa tutarudi kuwanyoshea vidole wale ambao hawajaathilika kwa kusema yule inawezekana hajaathilika, hapo ndipo Dunia itajikuta imechelewa.

historia ya ugonjwa wa Ukimwi inaanzia pale Latin Amerika miaka ya 70 wakati huo unjwa huo ulifahamika kama unjwa wa mashoga, ulioletwa na Mungu kama pigo kwa watu waliokuwa wanajihusisha na vitendo vichafu, lakini baadaye walijikuta wakiambukizwa hata wale ambao hakuwa mashoga hapo kosa lilifanyikia.

kama binadamu wakati huo angechukua tahadhari dhabiti leo tungepona au hata uliporipotiwa kuwa umepiga hodi mkoani Kagera mwaka 1982 Serikali ingechukua hatua ya kuweka karantini na kuzuia kuhakikisha wageni wote waliokuwa wanaingia nchini wamepimwa na wanavyeti leo hii ugonjwa huu tungekuwa tunasikia.

kinachoonekana sasa hapa ni kwamba Dunia haijaamua kupambana na ugonjwa huu kwani kuna watu wanaonekana wanafaidika na wasingependa kuona ugonjwa huu ambao wengi wameugeza uchumi ukiisha,kama dunia iliweza kupambana na kimeta kwa muda mfupi au Ugonjwa wa mafua ni kwanini huu?.

ikiwa serikali kama ya Tanzania sasa inapamba na Homa ya Bonde la Ufa RVF kwani isitumie mbinu kama zile kupambana na ukimwi, watu wanapenda Nyama lakini wameweza kujizuia iweje washindwe uzinzi kwani ni wangapi wameshuhudia mgonjwa wa RVF lakini mbona wa Ukimwi tunawashudia majumbani mwetu.

watu wamegeuza ugonjwa wa ukimwi kuwa ni uchumi kwao wanasema wanawasaidia wenye ukimwi, kumbe wanavuna chao wenye ukimwi wakifa wakamalizika wanawageukia yatima walioachwa kwamba wanawasaidia watoto yatima, hapo pia wanavuna chao halafu leo walale waamke wambiwe ukimwi umetoweka itakuwaje?

tusitegemee matamasha wala makongamano,tusiitegemee Kondomu kama kinga ya maisha yetu,kondomu sio Bima ya Afya, tubadilike kwanza ni bora umri uwekwe kila mmoja akiufikisha anaingia kwenye ndoa kwa maana nyingine ni kwamba kwa sababu ya tamaa zetu ni bora kila mmoja awe na mke au mme wake mwenyewe hiyo ni kinga imara.
pia ni bora sheria ya kupambana na wazinzi ikatungwa polisi na mgambo wakapewa uwezo wa kuingia kwenye magesti na kuwatoa nje wale wote ambao hawana vyeti vya ndoa lakini wanafanya uzinzi, wenye vinguo vifupi washughulikiwe kikamilifu wakiwemo mashoga.
ni bora ifahamike kuwa wakati oparesheni ya kutokomeza ugonjwa huu inaendeshwa ni bora kuachana na dhana ya Haki za Binadamu,ili kuweza kupambana kikamilifu na mawakala wa Ukimwi, njia kama hizo zilitumika kule Uganda wakaweza kuutokomeza ugonjwa huo kwa kuwachapa makahaba wote bakora na kuwafurusha huko.


uganda imetajwa karibuni hapa kuwa ongezeko la ugonjwa huo limeanza baada ya kupunguza mapambano na matumizi ya kondomu kuripotiwa kuingezeka nchini humo, ni vema serikali ibadilishe mapambano kwani hali ni mbaya hadi makanisani.

0753 399 579kwa msaada wa.website; mobinday.blogspot.com.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home