Wednesday, September 13, 2023

Tawa WamiMbiki wamuokoa mtoto wa tembo Chalinze

 




Na Mobini Sarya, Tanpresstz

ASKARI wa uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) wamefanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo anayekadiriwa kuwa na umri wa Mwezi mmoja, baada ya kuzama katika shimo lenye matope katika kijiji cha Kwamsanja, Kibindu, wilayani Chalinze, Pwani.

Tukio hilo limetokea Septemba 11 Mwaka huu, katika kijiji hicho jirani na Pori la Akiba la WamiMbiki, baada ya raia mwema kutoa taarifa kwa askari hao.

“Taarifa ya motto huyo aliyetelekezwa na kundi la tembo kisha kuangukia shimoni zilitolewa na raia mwema aitwaye Manase Thomas Baha mkazi wa kijiji cha Kwamsanja, nakumlazimu Kamanda wa Pori la Akiba, WamiMbiki, Emmanuel Lalashe kutuma haraka msaada wa askari 4, walioshilikiana na askari Mgambo sita, kwenda kumuokoa” imesema taarifa kuoka WamiMbiki.


Akizungmza baada ya zoezi la uokoaji huo kukamilika Kamanda Lalashe, aliwashukuru wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ya WamiMbiki, kwa ushirikiano wanaoutoa katika kulinda rasilimali za nchi yetu, zilizopo katika hifadhi hiyo.

“hususani rasilimali wanyamapori ambazo ni chachu ya shughuli za utalii na pato la nchi” alisema Lalashe nakuongezea kuwa mahusiano mazuri yaliyojengwa kati ya wahifadhi wa hifadhi ya WamiMbiki na wananchi wanaoishi vijiji jirani na hifadhi hiyo umekuwa na manufaa makubwa siku za karibuni,

 kwani wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika shughuli za uhifadhi.

Aidha ametoa wito kwa wajasiriamali wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya utalii kuchangamkia frusa za hoteli  kwenye hifhadhi hiyo na utalii wa boti kwenye mito ndani ya hifadhi hiyo inayo zungukwa na mkoa wa Pwani na Morogoro ambayo imefunguliwa hivi karibuni.

    

  

Labels: