Friday, March 23, 2007

JE UNGEPENDA MWANAO AISHI MAISHA KAMA HAYA?

WATOTO WETU, HADITHI NA VITIMBI NA SALAAM.



WATOTO WETU, HADITHI NA VITIMBI NA SALAAM.

Jina lake kamili ni Louis Goodlack,anamsalimu mama yake Shani Mshana,baba yake Goodluck Mramba,Babu yake mzaa baba Pamphili Pesambili Mramba,bibi yake Honorina Mramba.

Wengine ni bibi mzaa mama yake Majui Mshana,Mjomba wake Issa Mshana,Shangazi yae Jasumin Abdallah, na bibi yake mdogo Halima Mshana.

Akiwa mkubwa angependa awe mtumishi wa Mungu (Padri).

Ujumbe,ameitaka jamii kumcha Mungu daima.
Atangaza kuuza simu baada ya kutokupigiwa.


MTU mmoja ameshangaza watu baada ya kutangaza kuuza simu yake ya mkunoni ili apate pesa akanywee Pombe, baada ya kuona inamgarimu pesa nyingi kuwa nayo.

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina moja la Dina ambaye ni mfanyakazi katika Mgahawa mmoja jijini Dar es Salaam, aliwambia watu kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona hakuna ndugu wala jamaa anayempigia simu ispokuwa niyeye tu anawapigia.

“nimelazimika kuchukua uamzi huu, najua utawashangaza wengi lakini hakuna sababu ya kuendelea kuumia hapa,ninapoteza pesa nyingi kuwapigia maradiki simu lakini wao hawanipigii, zaidi ya kuishia kunibip”alilalama dada huyo.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Freemedia umebaini kuwa watu wengi nchini Tanzania wananunua simu pasipokuwa na mpango, wanashindwa kuelewa kuwa simu inatumika kwa utaratibu hasa wa kibiashara,mtu anatumia pesa kuzungumza akijua atapata pesa na wala simu sio kwa ajili ya anasa.

Mkuranga bora kukumbana na RiftValley kuliko Popobawa.

WAKAZI wa mkuranga mkoani Pwani wamesema katu wao hawataacha kula kiti moto kwa sababu ya kuepuka kukumbwa na homa ya Rift Valley baadala yake wataendelea kukitumia kwa ajili ya kujikinga na popobawa anayeendelea kuwaingilia sehemu nyeti.

Wakiongea kwa masikitiko na Mtandao wa Freemedia huku wameshika Shavu, wakazi hao wamesema kuwa hajui kama ni kiama chao kimefika kwani kwa muda sasa wamekuwa wakisumbuliwa na Kiumbe cha ajabu kinachowaingilia usiku wamelala na kuanza kuwalawiti, bila kujali jinsia wala mtoto na wamekuwa wakila nyama ya nguruwe kama kinga sasa wanaambia wasiitumie ina homa.

‘kama ni kiama chetu kimefika bora tufe kuliko kuishi, tumekuwa tukitegemea kitimoto kama kinga ya Popo bawa, sijui amesuka njama sasa ammeingia hata kwenye
dawa ya kumdhibiti, hatuwezi kuwaacha bora tufe kwa RiftValley kuliko kukumbana na aibu ya Popobawa” walisema wakazi hao.

Kwa muda sasa wakazi hao wamekuwa wakisumbuliwa na kiumbe hicho cha ajabu kinachodaiwa kuwa kililetwa na Mpemba mmoja baada ya kuibiwa mali yake kijijini hapo ili kiwashughulikie wale wote waliohusika na wizi huo baada ya kumaliza kazi sasa kimewageukia na wenginem tayari watu kadhaa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kujeruhiwa.


Wanyama kuachiwa huru na binadamu?ni baada ya kuibuka bonde la Ufa.

Baadhi ya Makabila yanayojihusisha na Ufugaji wa wanyama mbalimbali kama Ng’ombe na mbuzi Afrika Mashariki, wanapanga kuachia mifugo hiyo itoke katika makazi ya Binadamu ikaishi Porini baada ya kuleta maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Rift Valley inayoangamiza maisha yao.

Habari zilizochapishwa na Mtandao wa Freemedia leo zimekariri kwamba baadhi ya makabila hayo maarufu kwa ufugaji kama wamasai na wasukuma wanapanga kukutana ili kuamua kama kuna haja ya kuendelea kukaa na wanayama hao majumbani kwasasa wakiingia gharama za kuwafuga bila faida.

Imeelezwa kuwa wanyama hao wameonekana hawana faida kutokana na nyama yake kukosa soko ikidaiwa kuwa inavimelea vya ugonjwa huo unaopatikana sana kwenye sehemu za Bonde la ufa linalotokea nchini Kenya hadi Tanzania kupitia mkoani Arusha hadi ziwa Tanganyika.

Habari zilizopatika wikii hii kutoka katika mikoa ya kaskazini Mwa Tanzania zimebainisha kwamba tayari watu wanne wamekwisha kufa na ugonjwa huo huku wengine wakiwa wawili wakiwa Hospitali,hali iliyosababisha nyama kukwama mabuchani na Maziwa kumwagwa baada ya kukosa soko kwa hofu hiyo.

Ikiwa wafugaji hao watakuwa wamefikia uamzi wa kuacha kufuga hao wanyama itakuwa ni mara ya kwanza kwa Historia ya dunia binadamu kuacha kuwanyanyasa wanyama kwa kuwachinja kikatili ili apate kitoweo na wengine akiwatumia kwa kilimo,lakini pia inaweza kuwa mwisho wa wanyama hao duniani kama Ngo’ombe kutokana na kutoweza kuishi peke yake kwa kujitafutia maji na nyasi kama wanya wengine wa porini.

kanisa latoa Roho za watu kwa Maombi

KANISA moja kutoka nchi jirani ya Kenya limeibuka wilayani Serengeti na kufanya mahubiri ya Ajabu yanayodaiwa kuwa waumini walikuwa wanachapwa bakora na vitu visivyo julikana.

Kanisa hilo la ajabu ambalo bado halijajulikana jina lake liliendesha Maombi yanayodaiwa kuwa ya miujiza katika kijiji cha Nyichoka wilayani hapa ambayo yaliwavuta watu kutoka sehemu mbalimbali na waliofika walikuwa wanachapwa na vitu visivyojulikana hadi wanasema madhambi yao.

Katika kipigo hicho walichokipata tayari mtu mmoja ameuwawa baada ya kuchapwa na wengine kadhaa kujeruhiwa, imedaiwa kuwa Oktoba 13 Mwaka huu Ryoba Jeremia (50) mkazi wa msati wilayani Serengeti alifika siku hiyo kwenye mahubiri kwa ajili ya kusikiliza.

Habari zinasema kuwa Ryoba ambaye kwasasa ni marehemu baada ya kusikiliza maombi hayo ya ajabu anadaiwa kusema madhambi yake ikiwa ni pamoja na kuwa alikuwa mchawi na alipoombwa ataje wenzake anaoshirikiana nao aligoma kuwataja hali iliyofanya mchungaji wa kanisa hilo ambaye kwasasa nasakwa na Polisi kumuaru ataje kwa lazima na alipokataaa kutaja alichapwa hadi akakata roho.

Imedaiwa na Polisi kuwa Mhubiri ambaye anadaiwa kuwa ni anatokea Kenya na sasa anasakwa na jeshi hilo aliamuru mtu huyo aendelee kuchapwa hadi akakata roho bila kuwataja washirika wake n Maiti iliokotwa eneo la tukio na Polisi ikiwa imevunjwa mguu na makovu mwilini.

Tayari mtu mmoja Ryoba Yusuph (48)anayedaiwa kuwa mmumini wa kanisa hilo mkazi wa kijiji hicho amekamatwa na kufikishwa mahakamani wilayani hapa kufuatia tukio hilo,kanisa hilo linadaiwa kuingia hapa likitokea nchi jirani lilipenya kwenye kijiji cha Kenokwe na Nyichoka pembeni hali ambayo haikuwa rahisi kujulikana hapa.

Labels:

WATOTO WETU, HADITHI NA VITIMBI NA SALAAM.

Joseph Ntezimana ,anasoma darasa la kwanza ,Shule ya Msingi Chang’ombe anawasalimu baba na mama yake, baba yake Chrispin Luvinga akiwa katika kijiji cha Kitowo (Dabaga)Iringa na rafiki zake wote popote walipo.
Yeye anasema akiwa mkubwa anapenda kuwa mwanajeshi.

Fadi jamali (5)
Anasoma shule ya nasari Kigogo jijini Dar es Salaam, anawalimu mama yake Amina ,baba yake Jamali wote wakiwa jijini na mama yake mdogo tinna akiwa kigogo , mama halima akiwa ilala na mama mwingie Shadafa akiwa Temeke na Rafiki yake Eva.
Ujumbe anawambia watoto wenziwe waheshimu wakubwa.

Mseto

Mobini na Mashirika habari

London,Uingereza

Watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi wameijia Duania wamneijia juu serikali ya Uingereza wakidai kuwa imetunga sheria ya kuwanyanapaa wathilika wa HIV, wasiweze kuingia kwenye nchi hiyo ya ulaya kwa kisingizio kwamba inadhibiti kifua kikuu (TB) .

Katika habari zilizokariria na Mashirika ya habari wiki hii, Nchi ya uingereza imeamua kutunga sheria inayolazimu watu wanaotaka viza ya kuingia nchini humo wawe wamepima kama wanakifua kikuu,wakipatikana na ugonjwa huo hawataruhiswa kupewa viza.

Katika nchi ambazo tayari zimewekwa katika utaratibu huo, kama majaribio ni Kenya, Afrika kusini na China kisha utaenea duania nzima,utaratibu huo umewakera sana watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini Kenya na tayari Mratibu mmoja anayetetea haki za wanawake walioathilika nchini humo amesema tasisi yake inautafakari uamzi huo inao uona kama unalengo la kuwabagua waathilika kwani Ukimwi ni swahiba wa TB.

Waathilika hao wamesema kuwa huwezi kuutenganisha Ukimwi na kifua kikuu labda wanalengo la kutuizuia tusiinge nchini humo, tunajaribu kuasiliana ili kutafakali uamzi huo tunaouona kama wa kutunyanyapaa, madai ambayo yanakanushwa na Serikali ya uingereza kwa maelezo kuwa wanalenga kuutokomeza ugonjwa wa kifua kikuuu.

WATOTO WETU, HADITHI NA VITIMBI NA SALAAM.

Maelezo

Ratifa Yakubu (2)wa Kigamboni DSM anawasalimu, mama yake Hawa Ally na Baba yake Yakubu Ally na Bibi zangu Mariam Mohamed Mzinga na Bibi Lukia Sulum Lata wote wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.anapenda chakula cha Matunda na Nyama Pamoja na Soda ya Fanta.

Ujumbe; Baba na Mama Mnitunze vizuri.


Na ANKO Mobini

Leo watoto wazuri baada ya Anko wenu Kusubiri mtume hadithi mmeshindwa kufanya hivyo ameamua kuwataolea hadithi nyingine tamu inayohusu kisa cha kuku kuwa na uhasama na Mwewe.

Je Watoto Mnamfahamu huyu Ndege anayeitwa Mwewe na Mnafahamu kisa cha kuwa na uadui na huyu Ndege mwinge wa kufugwa anayeitwa Kuku? Hebu fuatana nami.

Hapo zamani za Kale katika Milima ya Uluguru palitokea njaa Kali iliyowakumba wanayama wote walikao na watambaao, lakini katika Kijiji kimoja kulikuwa na Mkulima aliyekuwa amejihifadhia nafaka Nyingi, kwa hiyo njaa ilipotokea akaanza kuwauzia wenye njaa na wengine kuwapa Msaada kwa wale wasiojiweza.

Wakati huo Kuku na Mwewe walikuwa marafiki wakubwa wakaambizana Rafiki kwanini kukae huku tukifa kwa njaa pamoja na familia zetu wakati kuna Habari kuwa katika Kijiji kimoja kuna chakula kinauzwa tusiende kukinunua Mwewe alimwambia Rafiki yake Kuku.

Kutokana na Habari hiyo Kuku akaona ni wazo Zuri akamwambia Rafiki yake haya na tuanze safari mara moja kwenda kutafuta hicho chakula mahala kinapopatikana.

Safari yao ikakamilika wakaenda hadi kule chakula kilipokuwa kinauzwa na kweli wakamkuta yule Mkulima akawauzia kadiri ya mapatano yao, Mara baada ya kumaliza kuwapimia Mwewe aliruka na chakula chake akamwacha kuku anakuja nyuma.

Kumbe baada ya Kuku kumaliza kupimiwa alimpa yule Mkulia asante mkulima akafurahi akamuongeza chakula kingine bure akiwa ameondoka alifika kwenye mti mkubwa uliokuwa njiani akapumzika kivulini kumbe juu ya Mti alikuwa anapumzika Mwewe, hapa chini kuku alikuwa anapumzika huku amenyanyua mguu mmoja juu.

Mwewe alipomtaza aliona anachakula kingi kuzidi cha kwake akamuuliza Rafiki yangu mbona wewe unachakula kingi zaidi ya kwangu umeongezewa? Kuku akamjibu nilimwabia yule mkulima anikate mguu mmoja ili aniongeze chakula akafanya hivyo, kuku alikuwa akiongea hivyo huku amenyenyua Mguu wake juu Mwewe asiuone.

baada ya Mwewe kuambiwa Hivyo aliruka kwa Hasira kurudi kwa yule Mkulima alipofika akamwambia kuwa yuko tayari kukatwa mguu ili amuongeze chakula, yule Mkulima aliposikia hiyo habari hakuwa na lingine zaidi ya kuchukua Panga na kufanya hivyo kisha akamuongeza chakula, kutokana na kumkata Mguu Damu iliendelea kutoka kwa wingi sana lakini akaajaitahidi hivyo hadi Nyumbani kwake akiwa haoi.

Alipofika alikuwa ametoka Damu nyingi akawapa watoto wake chakula hicho kabla hajakata Roho akawamabia kuwa Wanaagu kuku amenifanyia haya yote kwa kunidanganya kuanzia leo kila mkimuona au watoto wake ni kuwauwa baada ya maneno hayo akafariki dunia tangu siku hiyo Mwewe na Kuku ni uadui

Webste;www.mobinday.blogspot.com

Labels:

MWANAFALSA AOMBA MJADALA WA KITAIFA

SERIKALI imeombwa kuanzisha mjadala wa kitaifa utakaosaidia kurudisha maadili ya Taifa.

Wito huo ulitolewa na mwana falsafa wa falsafa za Hayati Mwalimu J.K Nyerere alipokuwa akiongea na Tanzania Daima Jijini Dar es salaam.

Alisema sasa hivi watanzania imewapasa kuelewa kwamba wamemuasi mwalimu nyerere kwa kutofuata yale ambayo alikuwa akiyafanya badala yake wanakuwa ni watu wenye ahadi nyingi bila utekelezaji.

" Tuelewe kuwa baada ya kumuasi mwalimu inakuja laana , na mtu ukikaa kwenye laana elewa kwamba unapoelekea ni kubaya afadhali Raisi Kikwete aitishe mjadala wa taifa ambao watu watajadili ni jinsi gani ya kuweza kurudisha heshima ya nchi ambayo sasa hivi inapotea kutokana na laana ya Mwalimu " alisema

Alisema kwa sasa hivi hakuna mtu mwenye uchungu na nchi yake kwa sababu hakuna mtu mweye kitambulisho cha uraia kinachomtambulisha kama yeye ni raia wa Tanzania.

Alisema Tanzania kwa hivi sasa haina mwenyewe ndiyo maana inaporwa na kila mtu na hakuna hata mtu wa kusimama na kutetea kwamba isiporwe kwa sababu uzalendo na maadili ya mwalimu Nyerere vimetoweka.

" Kwa kukosa vitambulisho tumemuasi Nyerere , Nyerere alikuwa ni kitambulisho cha utaifa kwa sababu kila alichokifanya alikifanya kwa maslahi ya Taifa "alisema

Aidha alisema ili tuweze kufanikiwa ni lazima malalamiko na kero za wananchi zishughulikiwe haraka na pia raia watambulike kwa uraia wao ili wajione huru wenye nchi yao, ambao watakuwa tayari kutetea na kulinda maslahi ya nchi yao .


MWISHO

Miaka30 ya CCM imedhihirisha inaanguka kwa kishindo

Miaka30 ya CCM imedhihirisha inaanguka kwa kishindo, nani kuiokoa?

Na Mobini Sarya

chama cha Mapinduzi(CCM)wiki hii kimeadhimisha miaka 30 ya kuundwa kwakwe, maadhimisho ambayo kitaifa yalifanyikia Uwanja wa Jangwani Jijini Dar esSalaam,yakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete.

awali maadhimisho hayo yalikuwa yafanyike 5 February Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Tarehe halisi ambayo imezoeleka kila mwaka lakini tarehe hiyo ilibadlishwa na kuwa February 4 siku ya Jumapili kwa maelezo kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwapa nafasi wananchama wao ambao ni wafanyakazi serikali waweze kupata nafasi ya kuhudhuria Sherehe hizo zilizokuwa zimeandaliwa kwa kishondo.

sababu nyingine ambayo haikuwekwa wazi nikwamba jumapili watu wengi hupumzika hususanijijini Dar es Salaam, kwa hali hiyo walitarajia wakazi wengi wangejitokeza kwenye maadhimisho hayo yaliyokuwa yamepambwa na kila aina ya ngoma za wasanii na vivutio vingine,hizo ndizo zilikuwa ndoto kamili za CCM huku wakiwa wammewaalika Mabalozi wa Nchi mbalimbali ilikuja kujionea pamoja na ukongwe wa Miaka 30 ya chama hicho bado kinapendwa.

ili kuhakikisha kila Mwananchi aliyetaka kufika kweneye maonyesho hayo anayashudia Vema wakaamua kuyaweka uwanja mpana wa jangwani ambao upo jirani kabisa na mjinin na usafiri wake ni rahisi kufikika wakiwa na kumbukumbu nzuri kichwani kwamba miezi miwili iliyopita yaani Disemba 9 katika sikukuu ya uhuru wa Tanganyika watu wengi walishindwa kuyaona maadhimisho hayo kutokana na uwanja wa Taifa kufulika,ndio maana CCM wakapeleka Jangwani.

lakini pamoja na kufanya maandalizi ya kila aina kwa gharama kubwa chama hicho kikongwe kililishindwa kusumbua akili yake kusoma majira ya Saa na Nyakati, wakashindwa kutambua kuwa siku chache baada Mgombea wao kutangazwa kuwa Mshindi wa Tsunami kwenye uchaguzi mkuu wa 2005,Chama cha CUF Kiliandaa maandamano ya kumshinikiza Rais Kikwete amfute kazi Mkuu wa Polisi wakati huo IGP Mahita,Maandamano ambayo yalihudhuriwa na wananchi wengi.

lakini wiki mbili kabla CCM haijaadhimisha miaka 30 yake Vyama mbalimbali vya upinzani hapa nchini viliandaa maandamano ya kulaani serikali kununua rada kwa bei kubwa wakishinikiza uchunguzi wa kina ufanywe ili kuwabaini walihuskia na biashara hiyo, lakini wananchi hawakujitokeza kama ambavyo walijitokeza kipindi CUF iliandaa maandamano pamoja na kwamba hata hayo yalihusisha wanacuf.

jambo ambalo CCM ha

Waandishi Tuiambie Serikali isishiriki ufisadi

Udikteta Gumzo la WIKI

Na Mobini Sarya

SERIKALI Ya Awamu ya nne kwa Mara nyingine imejidhihirisha wazi kuwa imeamua kuwatupa Wazawa wanyonge na kuwakumbatia wageni wenye pesa hasa katika sekta zinazohusu Maslahi ya wazalendo kwatika uwekezaji.

Siku chache baada ya Mgodi wa Buhemba Gold Mining kufungwa kutokana na kumalizika kwa Dhahabu bila Taifa kupata Manufaa yoyote ,tukio ambalo limewaacha aibu kubwa, Serikali imeamua kuwafukuza wachimbaji wazawa waliokuwa wakichimba pembeni ili kuipatia Kampuni ya Makaburu Land Gold kutoka afrika kusini.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma (D.C) Saveli Maketa ameyabainisha hayo wikii hii Mjini Musoma alipokuwa akihojiwa na Tanzania Daima, kuthibitisha kuwa Serikali inajiandaa kikamilifu kutumia Nguvu ya Majeshi ili kuwaondoa wachimbaji hao Wazalendo wapatao 6000.

Kauli hiyo ya DC imekuja siku chache baada ya kutolewa kauli ya Kamishina wa Madini Nchini Piter Kafumu alipotembelea Mgodi huo, kukutana na wachimbaji hao kisha akawataka waondoke haraka kwenye Mgodi huo ili kumpisha Mwekezaji, pia aliwatuhumu wachimbaji hao kuwa ndio wamechangia Mwekezaji kufunga Mgodi.

Kafumu aliwapa Amri hiyo ya kuwataka waondeke eneo kwa Madai kwamba Alikuwa anatekeleza Amri ya waziri Mkuu Edward Lowassa aliyoitoa wakati alipofanya Ziara Mkoa wa Mara,akawalaumu kwamba kuendelea kwao kukaa pale ni kuitia Serikali Hasara kwani wao hawaingizii serikali mapato yoyote na pia ni wachimbaji haramu.

Katika mahojiano yake na Gazeti hili DC wa Musoma amesema kwamba wamepata taarifa kuwa Wachimbaji hao wameandaa silaha Mbalimbali kama vile mishale na mapanga ili kukabiliana na polisi kwa hiyo inabidi Serikali itumie majeshi yote ili kuwaondoa, kwani wapo katika eneo kinyume na sheria, hawana leseni wala hawajamilikishwa eneo hilo na serikali.

Mkuu huyo ametoa kauli inayopingana na dhamira yake anapodai kuwa wachimbaji hao hawana faida yoyote kwa Serikali huku akijua kuwa, wachimbaji hao ni watu wenye familia ambao wamefika hapo kwa ajili ya kutafuta ada za watoto wao wa shule, nguo na chakula.

Pia amesahau kuwa Serikali imeamua kuwatuika mzigo mzito wa Elimu wananchi kwa kuwalazimisha kuchangia kujenga Madrasa ya sekondari na Shule za Misingi bila kujali kuwa ilianzisha Mpango wa Elimu ya Sekondari (MES)ambao ulitakiwa uboreshwe kwa kutumia fedha za wafadhili na zile ambazo serikali imesamehewa Madeni kwa kuboresha Elimu hapa nchini baadala ya kuwapa mzigo huo wananchi, ambao kwao maisha ni magumu.

Serikali imeahidi kutumia jeshi lenye silaha kupambana na wananchi wake kwa kuwaita wachimabaji haramu, sawa na inavyopambana na wahamiaji haramu kutoka kwenye mikoa iliyompakani na nchi za Rwanda na Burundi, jambo linaloiweka mbali na wanchi wake.

Hatua ya serikali kutangaza vita na wanchi wake kwa kuwahamisha kutoka eneo ambalo walikuwa wawnajipatia pesa kidogo kwa ajili ya kuchangia elimu hapa nchini, kwa madai kuwa kuwepo eneo lile ni kuitia serikali hasara kinaonekana kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaopaswa kulaumiwa na kila mtu kwani ikumbukwe kwamba ni siku chache zimepita baada seriukali kuwanyanga wakulima wa mpunga eneo na kumpa Mwekezaji.

Tabia ya serikali kuwanyang’anya wananchi maeneo ya mali na kuwapatia wawekezaji wa kigeni inahesabika sawa na mzazi kumtoa mtoto chakula na kumtupia mbwa kisha akampa makombwe eneo walilokuwa wananchimba wachimbaji hao ni eneo ambalo awali mwekezaji alilipima akaona halina mali akaweka uzio kwelile aliloona linadhabu sasa amemaliza wanyonge wanaambiwa waondoke apatiwe hii haitavumilika.

Ikumbukwe kuwa baada ya Serikali kutangaza kuwaondoa Wazawa kwenye eneo ambalo walikuwa wanapatia Riziki, akina Mama wajane zaidi ya 500 walikuwa wanasafisa dhahabu hapo watakosa kazi, vijana waliomaliza shule na kukosa ajira zaidi ya 3000 watapokosa Riziki na wazee zaidi ya 1000 walikuwa wanapasua mawe watapoteza ajira.

Akina mama na Vijana wadogo zaidi ya 900 walikuwa wanasomba maji na kuosha dhabu kuomba mifuko yam awe watapoza ajira bila kuwasahau, Machinga na Mamalishe zaidi ya 600 walikuwa wamehamia katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya biashara ya na kujiingizia kipato kwa kuuza vyakula.

Bila kusahau kuwa kuwepo kwa machimbo hayo ya wazalendo kumesaidia saana kupunguza uhalifu kwani wananchi wengi mawazo yao yamezama huko wanakopata riziki yao

Waandishi Tuihurumie Serikali tusishiriki ufisadi



na Mobini Sarya

YAANI kama ningekuwa mimi Mhariri nisingediriki kushikiriki ufisadi huu yaani kama ningekuwa mhariri wa chombo chochote cha habari ningethubutu kushirikiana na viongozi wa Serikali katika ufisadi kama huu.

yaani unakuta kionogozi wa Serikali anaondoka kwenda kufanya ziara mikoani anaongozana na wanahabari kutoka Dar es Salaam, kama vile anakwenda ulaya nukusahahu kuwa huko mikoani aendako kuna wanahabari kama anaoondoka nao jijini.

yaani kiongozi wa Serikali anaamua kuongozana na wanaandishi lukuki kutoka Dar es Salaam, kwa Gharama kubwa ya kula na kulala kwenye hoteli kubwa wanazofikia na kusahau kuwa huko mikoani kuna waandishi tena ambao hawahitaji hata kulipiwa vyumba kwani wapo nyumbani kwao.

kwanini Mhariri ukubali kutoa waandishi jijini waongozane na kiongozi kwenda mikoani ambako unajua chombo chako kina mwakilishi unayemtegemea,humwamini je waandishi wa Dar ndio wana taaluma kuliko wa mikoani?

kwanini wanahabarai tusiihirumie serikali yetu kiongozi anaandamana na kundi la Waandishi kwenda mikoani hata kama hakuwapa posho akirundi Ofisini anaandika kwamba alitumia Mamilioni ya Hela kuwalipa waandishi wakati kumbe niuongo lakini kwa sababu aliiongozana nao anakuwa amepata mwanya wa kufanya ubadhilifu ambao unaonekana kwamba wahariri wamekuwa wammeshiriki moja kwa moja.

yaani kama ningekuwa Mhariri na Kigogo yeyote akaleta mwaliko Ofisini wa kutaka waandishi kwenda nao Ziara mikoani ningemwambia akachukue hukohuko mkoani kwani tunaye mwakilishi,kuliko kukubali serikali kuingia Gharama ya kuwasafirisha waandishi utafikiri wajumbe wanaokwenda kusuruhisha mgogoro wa mpaka kule kagera.

Yaani kama ningekuwa Mhariri nisingekubali Mwandishi aatoke 'NewsRoom'kwenda mikoani kwenye ziara ya waziri au nani wakati najua wapo waandishi huko wanaofanyakazi katika mazingira Magumu ya kazi, halafu leo kiongozi anafanya ziara huko wanaonekana hawafai.

yaani kama ningekuwa mimi nisingedhubutu kushiriki umangimeza huu, tunajua wanandishi wa Dar es Salaam, hata kama hawana kipato cha kuridhisha lakini wanafanyia kazi katika mazingira Mazuri kwani hukawiii kuwasikia wakaigombea mishiko lakini kwa mikoani hiyo ni nadra kutokea.

leo waziri anaodoka kwenda mikoani anaongozana na kundi la wanahabari bila kujua huo ni ufisadi na wale wa mikoani kuonekana hawafai kitu kinachowavunjia heshima kwenye jamii inayowazunguka hasa pale anaonekana mwandishi wa chombo chake ametoka Dar es Salaam,na yeye kukosa kazi ya kufanya.

hii tabia hutumika sana katika kipindi cha uchaguzi kwa baadhi ya wagombea kutembea na waandishi huku wale wasio kuwa na uwezo wa kukodi waandishi wanakoswa kuandikiwa habari zao kwani wale wanahabari wa mikoani hususa kuandika hizo habari baada ya kuona wagombea wengi wanaongozana na waandishi kutoka jijini.

na hii tabia ya kukodi waandishi toka Dar es Salaam, kwenda nao mikoani imekuwa ikiwanyima wananchi haki ya kutoa na kupata habari za uhakika,hebu tujiulize mwandishi aliyekodiwa kutoka Dar na Wizara ya madini kwenda kuembelea mgodi Madini ataweza kuandika kweli baya lolote la mgodi huo kama utakuwa umempa waziri Rushwa.

hatabaki kuufagilia mgodi huo kutokana na kwamba 'Bosi' aliyengalimikia safari hadi kumfikisha huko naye amepewa kiatu cha Madini, vipi kama na mwanadishi atakuwa amepewa mlungula unaotokana na mgodi huo hata wananchi watoe kilio kwenye mkutano wa hadhara na waziri akakipuuzia Mwandishi atakiandika si atabaki anaandika waziri amesema!!!

Kama nindekuwa mimi kiongozi wa Serikali ninakwenda kufanya ziara mkoani kabla ya kukutana na viongozi wa eneo hilo ningekuwa nakutana na wanadishi wa eneo hilo kwanza wananipa taarifa na maendeleo ya viongozi wa pale.

kwani uzoefu unoenyesha tena na tena kwamba wanandishi wa Mikoani aawanaelewa mambo mengi kuliko hata viongozi waandamizi wa huko kwaani kero zote za wananchi wanazifahamu vema, utakuta mwanadishi anahusika kikamilifu kuwatetea wananchi kuliko hata mbunge.

kuna mahala fulani nilikwenda nikamkuta Mwanandishi mmoja wananchi wa Pale wamemgeuza kama Mbunge wao au Mwamuzi mwenye hekima jinsi walivyokuwa wanajipanga asubuhi kibandani kwake kumweleza shida sikuamini kama sababu ya uandishi wake kutokana na maswala mengine magumu.

niliwauliza mbona mambo mengine ni kimahakama kabisa kwanini msiyapeleke Mahakamani lakini wao walinivunja nguvu kwa madai kwamba unakuta wanamatizo wakitaka wakitoa taarifa kwa mtendaji au kiongozi wa mtaa kesho unamkuta yule mtendaji anakunywa pombe na mtuhumiwa wao, wakimuomba barua ya Polisi anawanyima, ukiwauliza kwanini msiende polisi watakuambia he tukifikisha na watu kama hao polisi wakati mwingine unakuta sisi ndio hukamatwa.

nilishangazwa na taarifa hizo kwamba hadi sasa hapa nchini kuna maeneo ambako kitu kama utawala Bora kwao ni ndoto wala hawaujui utawala bora ni kitu gani yaani unakuta mtendaji ni kama Mfalme.

ninazosababu ambazo zinanifanya nione kuwa hapafai mwandishi kuongozana na kiongozi wa Sereikali kutoka Dar es Salaam, kwenda naye mikoani wakati kuna waandishi kule zipo hata kama wewe utaziona hazifai lakini zichgukulie kama hivyo.

kwanza kama nilivyotangulia kusema kwamba kiongozi anapoandamana na waandishi kutoka jijini kwenda nao mkoani kunawafanya waandishi wa Mkoani wajione kuwa hawatambuliwi na kutahaminiwa na chombo chao wanachokitumikia, pia mwandishi aliyeongozana na kiongozi hawezi kuandika mabaya yatakayoibuliwa kwenye ziara hiyo asije akamkasilisha bosi aliyempeleka huko.

ukweli huo ulibainika Oktoba Mwaka jana wakati Mkoa wa Mara ulifanya maonyesho ya kutangaza fursa za uwekezaji zilipo humo ikiwemo utajiri wa Madini kwa kushirikisha wilaya zote Nne, lakini cha ajabu uongozi wa mkoa huo uliamua kuapuuza waandishi wa mkoa huo ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiutangaza na kuwaalika wa kutoka nje.

nini kilijili waandishi waliotolewa nje ya mkoa wa Mara walilipiwa vyumba ya kulala vya Gharama kubwa ikiwemo posho na chakula lakini yale maonyesho yalipoomalizika hakuna mwandishi aliyeandika makala ya kuelezea zile fursa kwani kila mmoja alifungasha vyake akaondoka huku akijiesabia alichovuna.,

kwa ujumla yale maonyesho pamoja na kwamba yalifunguliwa Rais lakini hayakufanikiwa, wandishi wa mkoa wa Mara waliona wamezarauliwa na uongozi wa mkoa hakuna alijishughulkisha kuwa julisha waandishi yaliyojili kwenye maonyesho hayo.

kutokana na kutokutangazwa ili wapate mafanikio wiki iliyopita Halmashauri ya Serengeti ililazimika kutumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuja jijini Dar es Salaam, ili kujitangaza katika sekta ya uwekezaji ambapo walionana na wenyeji wa Serengeti wanaokaa Dar es Salaam, hayo ndio matatizo ya kudharau waandishi.

wandishi wa mikoani wanaelewa habari zaidi pamoja na kwamba vyombo vya Habari vingi haviwajali na wanajaua siri ya mafanikio ,viongozi waache mara moja kutumia gharama za serikali kuwasafirisha waandishi kutoka Dar es Salaam na baadala yake wakifika mikoani kabla hawajazunguka wakutane na wandishi wa huko wawape siri za huko.

yaani mimi ningekuwa mhariri ningemuomba mkurugenzi wa kampuni awasaide usafiri waandishi wa amikoani ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa habari kisha kila mkoa ningewatumia Computer na internet hapo ningeonekana ninawajali sio kushiriki kuwakandamiza na kuwadharau nasema hayo kwa uchungu wala stanii kwani uzoefu upo.

mobinsons@yoo.com 0717328102