Dc. Okash awaomba radhi wafugaji Bagamoyo
Na tanpresstz, Chalinze
SIKU chache tu baada ya kutoa kauli nzito na za onyo kwa jamii ya wafugaji wilayani Bagamoyo, Mkuu wa wilaya hiyo (DC) Halima Okashi sasa amegeuka na kuwaomba radhi baada ya kukutana nao.
“Niwaombe radhi wafugaji wote kama kuna sehemu nimewakosea, kwa kauli zangu au kwa namna yoyote kwani mimi ni binadamu kama nyie naweza kukosea….nikikosea nirekebisheni mnisahihishe ntajirekebisha”alisema DC , huyo.
Ingawa hakufafanua sababu ya kuomba radhi lakini itafahamika kuwa siku mbili zilizopita alikuwa ametoa matamko mazito ikiwemo kaeripio kali kwa wafugaji watakao kamatwa mifugo yao ikirandarada mitaani.
aliwataka wafugaji wote wajisajili kwake na idadi ya ng’ombe walizonazo huku wakionyesha maeneo yao ya kuchungia kwani ataanza kukamata mifugo inayoranda randa mbarabarani na kwenye mashamba ya watu na kuichinja nyama zake anagawa kwenye taasisi.
“ukimiliki ng’ombe 100 uwe na heka 5 za kuchungia ndio maana nataka kila mfugaji ajisajili na anionyeshe eneo aliotenga kwa ajili ya kuchungia huna eneo huruhusiwi kufuga….na zoezi la kukamata mifugo yote inayoranda randa itaanza Julai Mosi Mwaka huu hakuna faini ni kukamata na kuchinja kisha kugawa nyama kwenye taasisi”alisema Dc Jumanne iliyopita alipokuwa akiongea na viongozi wa CCM kata ya Lugoba.
Katika kikao hicho Dc. Alionekana mkali hata kwa watoa kero ambao wengi wao ni wana ccm kwa kuwakatisha na kuwataka wakae chini ,tofauti ilivyokuwa kwa mkutano wa wafugaji ambao amesema ataunda kamati ya kushughulikia changamoto zinazowakabili wafugaji wilayani hapa.
Aidha aliwataka wale wote ambao wamejenga au kulima kwenye maeneo ya wafugaji wahame haraka huku akipuuzilia mbali agizo la kuwavunjia nyumba wakazi wa Diozile.
Awali akifungua mkutano huo wa wafugaji wote kutoka katika wilaya ya Bagamoyo uliofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba alijitanabaisha kwamba yeye ni Mmasai licha ya kukaririwa siku za nyuma akidai kwamba yeye ni msambaa kutoka Mkoani Tanga.


