Thursday, May 30, 2024

WEZI WAVUNJA KANISA CHALINZE, KUIBA VITI NA VYOMBO

WEZI WAVUNJA KANISA CHALINZE, KUIBA VITI NA VYOMBO Na Ripota wetu, Chalinze
WATU wanaosadikiwa kuwa wezi wamevunja milango ya Kanisa la TAG Mboga, kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze na kuiba viti zaidi ya 80, simu na vyombo vya mziki. Akizungumza na shirika la habari vijijini (TANPRESSTZ) Mchungaji wa kanisa hilo Chediel Msangi, amesema tukio hilo limetokea May 27 usiku 2024 katika kijiji cha Mboga baada ya wahalifu hao kuvunja mageti ya milango na kuingia ndani ya kanisa hilo.
Kanisa la TAG Mboga, kata ya Msoga linavyoonekana kwa nje “Hapa natokea kutoa taarifa Polisi Lugoba, nimepewa Rb No.LUG/RB/302/2024 WIZI, kanisa letu lina mageti lakini wamevunja wakaingia ndani wakachukua, simu ya muumini alikuwa ameilaza kwenye chaji, viti vya kanisa zaidi ya 80, vyombo vya mziki kama busta,mixer na sipika”amesema Mchungaji Msangi.
Jengo la kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mboga lililoibiwa viti linavyyonekana kwa ndani likiwa tupu. Mchungaji huyo amesema kuwa taratibu za kiuchunguzi wameachia jeshi la Polisi huku wao wakiendelea na maombi na kutoa wito kwa mtu mwenye taarifa zozote awasilishe Polisi au ampigie simu yake 0714684572 kwa taarifa

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home