Monday, October 8, 2007

Watahiniwa 199,274 waanza mtihani wa kidato cha nne nchini

WATAHINIWA 199,274 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne Tanzania
Bara na Visiwani (Zanzibar na Pemba).


Akitoa taarifa hiyo kwa wana habari mjini Tarime, mkoani Mara, juzi jioni, Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta, alisema mtihani huo utafanyika kwa
kipindi cha wiki tatu kinachoanzia Oktoba 8 hadi 30, mwaka huu.


Waziri Sitta alibainisha kuwa kati ya watahiniwa hao, 127,988 sawa na asilimia 64.2
wako shuleni na watahiniwa wa kujitegemea ni 71,286 sawa na asilimia 35.8 ya
watahiniwa wote waliosajiliwa.


Alifafanua kuwa kati ya watahiniwa hao wa shule, wavulana ni 71,012 sawa na
asilimia 55.5 na wasichana ni 56,976 sawa na asilimia 44.5.


“Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 71,286 waliosajiliwa kufanya mtihani huo,
wasichana ni 37,451 sawa na asilimia 52.5 na wavulana ni 33,835 sawa na asilimia
47.5,” alisema Waziri Sitta.


Katika mtihani huo wa mwaka huu kuna ongezeko la watahiniwa 51,682 sawa na asilimia
35 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa
aina hiyo ni 147,592.


Aidha, waziri huyo alisema watahiniwa 26,199 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa
Maarifa (Qualifying Test) ndani ya kipindi hicho, kati ya hao, wasichana ni 15,383
sawa na asilimia 58.7 wakati wavulana ni 10,816 sawa na asilimia 41.3.


Alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wasimamizi na waendeshaji wote wa mitihani hiyo
kuzingatia kwa ukamilifu maelekezo ya usimamizi na uendeshaji wa mitihani kama
yalivyotolewa katika semina walizohudhuria.


Aliwataka wasimmamizi hao kujiepusha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani
hiyo, badala yake wawe makini kwa kuhakikisha kuwa watahiniwa hawaingii na vitu
visivyoruhusiwa katika vyumba vya mitihani.


Sitta alihadharisha kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na
kisheria wasimamizi watakaokutwa na kasoro yoyote ile katika eneo la usimamizi.


“Natoa pia onyo kwa watahiniwa watakaofanya udanganyifu kuwa hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo yao yote ya mtihani,”
alionya.


Alisisitiza kuwa vyombo vya dola vitakuwa macho wakati wote kuhakikisha kuwa kanuni
na taratibu za uendeshaji wa mitihani zinazingatiwa. Alitoa wito pia kwa raia wema
kutosita kutoa taarifa pale wanapobaini kuwapo kwa udanganyifu na ukiukwaji wa
taratibu za uendeshaji wa mitihani hiyo.


Waziri Sitta alikuwa katika ziara ya siku moja wilayani Tarime ambako alifuatana na
Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Diodorus Kamala, kuelezea kwa wananchi mambo muhimu yaliyomo kwenye
bajeti ya serikali ya mwaka 2007/2008.


Mwisho.

HUKU YA SWAUMU

Makala.

SWAUMU NA HUKMU ZAKE

Na: Shaaban Mpalule

Sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema . sala na salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad pamoja na jamaa zake waliotoharika

Maana ya swaumu:-
Swaumu kilugha ni kujizuia, mafano Bibi Maryamu mama wa Nabii Issa, aliposema. “hakika mimi nimejizuia basi sitomsemesha yeyote leo hii”
Ama kiistilahi ni kujizuiya kufanya matendo maalumu, kwa muda maalumu, kwa watu maalumu, na mwezi maalumu,
Ama watu maalumu, ni kuwa muislamu balehge mwenye akili timamu, asiwe katika hedhi au ni nifasi kwa mwanamke asiwe safarini na awe ni mwenye swiha kamili.

Muda maalumu ni kuanzia asubuhi hadi kuzama kwa jua. mtu kujizuia na kula, kunywa na kufanya tendo la ndoa, ikiwa ni halali au la haramu katika muda wa mchana wa Ramadhani. Yaani kuanzia asubuhi ya Alfajiri hadi kuzama kwa jua.

Ulazima wa swaumu:-
Katika dini ya kiislamu, kuna nguzo tano ambazo ndio katiba ya dini ya kiislamu. Hutoitwa muislamu uliokamilika iwapo hutaitekeleza nguzo hizo:-
Ya Kwanza:- kuamini hapana apaswae kuabudiwa kwa haki ila ni MwenyeziMungu pekee.
Ya pili :- kusimamisha swala tano.
Ya tatu :- kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Ya nne :- kutoa zaka kwa menye uwezo.
Ya tano :- kuhiji makka kwa awezae na kuamini siku ya mwisho (kiama).
Hivyo swaumu ni nguzo ya tatu katika nguzo za kiislamu.


Dalili za ulazima wa kufunga Ramadhani.
Hakika kila nguzo katika uislamu zina manufaa yake kwa mtekelezaji na kwa jamii, na kuna madhara kwa mwenye kukiuka na kwa jamii kwa ujumla, mfano:-
Nguzo ya kwanza, faida yake ni kuwa, Muumini kutambua kuwa dunia hii hakuna muweza wa kufanya lolote isipokuwa ni Allah pekee, na hana mshirika katika hilo.
Nguzo ya pili, baada ya kutambua na kumjua Muumba, basi inakubidi umuamini na kumuabudu kwa kufanya yote aliyoamrisha kama kuswali swala tano, ambazo unatakiwa uziswali ili uwe ni mwenye kumkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara.
Nguzo ya tatu, faida yake ni kukumbuka shida ya njaa, ambapo tajiri na masikini inabidi wahisi shida hiyo, ambapo hapa tajiri nae anatakiwa ahisi maumivu ayapatayo maskini, ili kwamba akisikia maskini akilalama njaa basi aweze kutoa alicho nacho kwa masikini yule na kutoa kwa kila kilichozidi katika mali yake.
Nguzo ya nne, ni kwenda kuhiji Makka, ili kukutana na watu wa Mataifa mbalimbali duniani hali yakuwa ni wenye kufanana kimavazi bila ya kutambua huyu ana cheo gani anakotoka, pia kubadilisha mawazo na kujua matatizo yanayoikabili dini yao.
Mwisho ni kuamini kuwa dunia hii ni mahali pa kupita tu na ni wenye kusubiri hukumu siku ya kiama kwa kila yaliyotendwa duniani.
Hivyo hapa tunatambua ya kwamba swaumu ni miongoni mwa nguzo iliyokuwa muhimu sana katika uislam, na isipofuatwa basi uislam utakuwa haujakamilika.
Mwenyezi Mungu ana sema ndani ya Qur’ani:-
“Enyi mlioamini mmefaradhiwa (mmlazimishwa) kufunga kama ambavyo wamefardhiwa waliopita kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu.” (suratul Baqarah: 183)
Pia Mtume (s.a.w.w) anasema:- “fungeni mpate kuwa na afya”, hivyo swaumu kwetu ina faida nyingi sana.

Swaumu na masharti yake:-
Pindi uingiapo mwezi mtukufu wa Ramadhani ni wajib kwa kila muislamu kufunga na kutimiza yote yaliyo mlazimu (sharti) ili swaumu yake ipate kukamilika, masharti hayo ni:-
1. Mwenye kufunga ni lazima awe baleghe, mwanaume ni miaka kumi na tano, na mwanamke ni miaka tisa
2. Awe na akili timamu (asiwe chizi)
3. Awe ni mwenye afya njema (asiwe mgonjwa, au ugonjwa unaosababishwa na swaumu))
4. Awe ametoharika na Hedhi (damu ya mwezi) na nifas (damu ya uzazi)
5. Asiwe msafiri. Mwenye kufunga hali ya kuwa ni msafiri basi swaumu yake haitakubalika, na itamlazimu kulipa siku hiyo (hizo) baadae.
6. Mzee (anatakiwa atoe fidia ya chakula kila siku na kulipa kwake si lazima), mama mjamzito, na anayenyonyesha, kwao si lazima kufunga , lakini inawabidi walipe baadae.

Kuthibitka kwa mwezi wa Ramadhani:-
Hulazimika swaumu ya mwezi wa Ramadhani kwa kuonekana (kuandama) kwa mwezi, kwa njia zifuatazo:-
1. Auone mwenyewe.
2. kuthibitika kwa wanaume wawili waliowaadilifu.
3. kukamilika kwa siku thalathini za mwezi wa Shaaban
4. kuthibitika na kuwa na matumaini kwa kusikia toka mji wa jirani.

WABONGO WANAPOKANA TIBA ZETU

Na Vumilia Kondo



Kuna mkanganyiko mkubwa wa mawazo katika vichwani vya watu kuhusiana na neno “TIBA ASILI” , kuna maelfu ya watu ambao imani zao zimejengeka katika dini wanaamini kwa asilimia kubwa kabisa kuwa tiba asili ni uchawi lakini si kweli na h ii yote ni kwasababu hawana elimu ya kutosha juu ya neno hili.


Tlba asili sio uchawi ni tiba pekee ya mwafrika ambayo imekuwepo tangu enzi ya babu zetu na imekuwa msaada katika kupambana na magonjwa mbalimbali, tiba asili inatafsiliwa kuwa ni majumuisho ya maarifa, elimu na vitendovitumikavyo katika kugundua, kukinga au kuondoa maradhi kwa uzoefu uliokuwepo, taaluma hizi hurithiwa kwa uangalifu kutoka kizazi hadi kizazi kwa njia ya mafunzo au maandishi. Vilevile taaluma hiyo hutofautiana kati ya nchi na nchi kutokana na tofauti ya utamaduni, mila na destuli za watu na aina ya mitidawa inayopatikana katika jamii hiyo.


Watanzania kuanzia sasa wanatakiwa kuondokana na dhana ile ya kwamba tiba asili na kwenda kwa mganga wa jadi kupiga ramli la hasha, tiba asili inayozungumziwa sasa ni kwenda kwa mganga wa jadi na wewe mwenyewe kumueleza matatizo yako na kutokana na maelezo yako atagundua ugonjwa wako na kukupatia dawa za asili.


Changamoto nyingine ni kwa serikali kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na suala hili la tiba asili , ikiwemo kuwapatia semina wadau mbalimbali pamoja na wana habari kwani wao ndio waelimishaji wakubwa kwenye jamii, mawazo ya wanahabari yatasaidia watu kufahamu kusudio halisi la tiba asili na kuiamini.


Wakati wa kilele cha siku ya tiba asili ya mwafrika tarehe 31 agasti nilizungumza na waganga mbalimbali wa tiba asili ambao wengi walilala mikia
juu ya kutokuwepo uhamasishaji wa kutosha kuhusiana na suala zima la tiba asili , wananchi waliokuwa wakiudhuria maonesho hayo walikuwa wachache tofauti na maonesho mengine ambapo watu huwa wengi.


Waganga hao pia waliiomba Serikali iwe inapanga mapema ni wapi maonesho hayo yatafanyika Kitaifa kuliko kushutukiza kama walivyofanya nwaka huu, kwaniwaganga wengi walishindwa kufika na hivyo kufanya maudhurio yao kuwa hafifu na wengine walichelewa kufika.


Lakini kitu cha kufurahisha au kupendeza kwa wafrika ni shrika la afya Duniani(WHO)kutambuaumuhimu wa tiba asili ,katika maadhimisho hayo walituma salamu zilizosomwa na Rosemerry Shija kwa niaba ya doka Mohamedi Darhusi ambae ni mwakilishi wa WHO hapa nchini, wao walisema kuwa wapo tayari kusaidia utafiti mbalimbali watiba asili pamoja na magonjwa na tayari wameshatoa muongozo unaohusu usalama, uweZowa dawa na upimaji wa dawa hizo kwa magonjwa ya marelia, UKIMWI, kisukari na shinikizo la damu.


Shirika hilo lilitoa changamoto ya utafiti kwani kuna uhusiano mbovu kati ya watafiti, wahudumu na watumiaji wa dawa hizo na kutaka kuwepo uhasiano kati ya wataalamu wa tiba asili na wataalamu wa tiba za kisasa.


Kikubwa kinachotakiwa kufahamika sasa ni Bara la Afrika limeamua kusheuerekea siku hii ili kuthamini na kuienzi tiba asili ya mwaafrika ambayo itakuwa ikifanyika kila mwaka tarehe 31 agasti.. Madhumani ya tiba asili ya mwafrika ni kuthamini mchango mkubwa ambao tiba mbalimbali za asili zimekuwa zinaendelea kuitolewa kwa wananchi katika kupambana na magonjwa nchini . Vilevile kuamsha ari ilipofifia ya kuthamini tiba asili ili kuimarisha tiba hiyo, pia Serikari na wananchi kwa ujumla waweze kuzitambua.


Wananchi wanapaswa kufahamu hali halisi ya uoaji huduma ya afya hapa nchini ambapo huduma za afya zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ile ya kisasa na asili ,ambayo zaidi ya asilimia 60% ya watanzania hupitia kwa waganga wa tiba za asili kabla ya kwenda hospitali.



Pamoja na jamii kuthamini tiba asili pia yapo matatizo yanayotokana na huduma hii ambayo hayafai. Mauaji ya vizee na vikongwe na uchunaji wa ngozi za binaadamu,matangazo yasiyofuata maadili,kushilikiana na majambazi ,kuleta mifarakano katika jamii, kutumia viungo vya binaadamu katika tiba asili hudharilisha huduma ya tiba asili,ili taaluma hii iheshimike yapasa kufuata maadili na sheria za tiba asili.


Katika vitu ambavyo vinaonekana sasa mchango wa tiba asili katika kuboresha afya ya jamii ni mkubwa ,.kwa utaratibu huu waganga wa jadi wanatakiwa kusajiliwa kwa lengo la kuwatambua na kuboresha huduma zao kwa madhumuni ya kuzuia maambukizi ya magonjwa kama vile UKIMWI,kifua kikuu(TB) na mengineyo.


Aidha watendaji katika kutoa huduma hizo za afya za kisasa na za jadi wanatakiwa washirikiane na kuaminiana kwa huduma zitolewazo nchini, kwani matidawa pia inaonesha kuwa na mchango katika kuboresha afya za wananchi yakiwemo magonjwa mbalimbali kama vile UKIMWI,kisukari na magonjwa mengi yaliyopoatika jamii.


Ikumbukwe kuwa kabla ya ukoloni na ukoloni mambo leo tiba asili iliukuwamfumoawahuduma afya kwa wananchi wakati huo, wazee wetu walipambana na adui maradhi kwa kutumia waganga wa tiba asili pamoja na rasilimali ya mitlidawa. Wakoloni walikandamiza tiba asili na kufanya wananchi kunyanyapaa tiba asili kuyumba, kukosa dira na mwelekeo.


Katika jitihada ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi mkakati wa kutekeleza mabadiliko ya uendashaji wa huduma za tiba za kisasa hasa hospitali “Hospital reforms” uliandaliwa na hivi sasa unatekelezwa na Serikali. Mkakati huo unawenda sambamba na mabadiliko ya kuweka mfumo mzuri wa kukubili matatizo yalioathili huduma za tiba asili.


Wizara ya afya na ustawi wa jamii inatambua umuhimu wa mchango wa kuinua afya kwa wananchi. Niukweli usiopingika kuwa zaidi ya asilimia 60%ya wagonjwa wanaokwenda hospitali kupata matibabu huwa wanapitia kwenye huduma za tiba asili kwanza ,kwakuwa huduma hizi zilikandamizwa , kudhalauliwa ,kutolewa kiholela na kuleta madhara kwa wananchi , Serikali sasa kwa kupitia Wizara ya afya na ustawi wa jamii ,imeamua kusimamia ili kuziboresha kwa manufaa ya wananchi.


Katika jitihada za kuleta ubora wa utoaji wa huduma ya tiba asili kwa wananchi Wizara imeandaa muongozo wa utekelezaji wa sheria ya tiba asili. Sheria ya tiba asili ilpitishwa na Bunge la Jamhuri ya Tanzania mwezi Novemba mwaka 2002, chini ya sheria hii waganga pamioja na wakunga wa jadi wanatakiwa kusajiliwa kwa lengo la kuwatambua na kuboresha huiduma zao.


Mwisho kabisa inatakiwa tukubali kuwa yote yawezekana ,tushirikiane tuwe na lengo moja la kuondoa adui maradhi nchini kwa nia ya kuboresha afya ya wananchi ili wacvhangie maendeleo yao.
.

BONGO ;MISHAHARA YA MAKONDAKTA NA VIBARUA JUU

WAZIRI WA KAZI ,AJIRA MAENDELEO YA VIJANA, JOHN CHILIGATI AKIWA IDARA YA HABARI (MAELEZO)AKIMWAGA MISHAHARA MIPYA.


WAZIRI CHILIGATI AKIWA AMEONGOZA NA BAADHI WA YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUSHOTO NI KATIBU WA TUCTA ,NESTORY MUNGULLA

Serikali yadhubutu kutangaza kima cha chini cha mshahara wa mfayakazi sekta binafsi.



KILIO cha wafanyakazi wa Sekta Binafsi ambacho kilikuwa kinataka waboreshewe Mishara sasa kimesikika na Serikali imeamua kutangaza mishara mipya ya kima cha chini iliyopanda kutoka shilingi 48,000 hadi 65000 kwa mfanyakazi w a ndani bila kujali kama ni kijijini au mjini na shili 350,000 wa migodini.

Serikali kupitia Wizara ya Ajira ,Kazi na Maendeleo ya vijana imefikia hatua hiyo baada ya Waziri John Chiligati kuunda Bodi zilizokuwa na wajumbe wawili kila pembe ,waajiri, wajiriwa na Serikali kufanya uchunguzi na kutoa matokeo yaliyotumika kupanga mishahara.

Akitangaza Mishara hiyo Mipya itakayoanza kulipwa Novemba Mosi Mwaka huu mbele ya Wandishi wa Habari Waziri Chiligati alisema kua anatumia kifungu namba 41 (1)cha sheria namba 7 ya mwaka 2004 ambacho kinampa mamlaka ya kutangaza mapendekezo ya Bodi aliyopokea ndani ya siku 60 tangu akabidhiwe mapendekezo hayo vingenevyo itabidi akajieleze Bungeni.

mapendekezo hayo aliyapokea 27 Septemba Mwaka huu takribani Siku 10, yaliyotplewa na bodi nane alizounda ambazo ni Sekta ya Majini, Bahari na nchi kavu,Majumabani na mahotelini, Kilimo, Madini,ulinzi binafsi,Biashara na viwanda, Afya na Usafiri,Mawasiliano, pia ameonya kwamba wajiri wasipandishe kodi katika vitegauchumi vyao ili kufidia gharama za mishara mipya watakayoanza kuwalipa wafanyakazi w ao.

Chiligati alisema katika uchunguzi bodi , zilibaini mapungufu yafuatayo ,karibu 15% ya wafanyakazi hawana mikata ya Ajira, sehemu nyingi za kazi hakuna mikataba ya hali bora ya kazi baina ya mwajiri na mfanyakazi, wafanyakazi w anafanyizwa kazi kwa saa nyingi bila kujali saa za kazi na ziada.

mazingira kiafya na usalama wa wafanyakazi katika baadhi ya sehemu nyingi za kazi hayaridhishi,
kuna baadhi ya waajiri hawajaandikisha wafanyakazi wao mifuko ya hifadhi ya Jamii,kama NSSF,PPF,n.k.

na wafanyakazi wanaoumia wakiwa kazini wanacheleweshewa au hawalipwi malipo ya fidia ya kuumia kazini (Workmen's Compensation)na baadhi hawalipwi.

Waziri Chiligati akiwa ameongozana na viongozi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi na waajiri akiwemo katibu wa shirikisho la wafanyakazi TUKTA,Nestory Ngulla, alisema;

"mapendekezo ya kima cha chini cha mshahara yaliyoletwa na Bodi za kisekta na ambayo karibu yote nimeyakubali ,ispokuwa mapendekezo ya sekta ya huduma za usafiri na mawasiliano , kila sekta itakuwa na kima chake cha chini cha mshahara kwa kuzinagatia hali ya uzalishaji" .

"kima cha chini cha mshahara kitatumika kwa wafanyakazi wote katika sekta husika bila kujali kama ni wafanyakazi wa mjini au vijijini kwa hiyo’

Wafanyakazi wa Kilimo wataanza kulipwa kima cha chini cha mshara shilingi 65000 kutoka 48000 na wafanyakazi wa Sekta ya Majini;Baharini na Ziwani katika Meli kubwa za kimataifa watatumia mkataba wa ILO wa Mwaka 2006.

lakini wale wa Meli za mizigo na abiria watalipwa 225,000 Meli za uvuvi wa Ndani shilingi 196000,Makuli na wajenzi wa meli 30,000.
Sekta nyingine ni ya wafanyakazi wa majumbani na mahotelini ambapo wa majumbani wamegawanywa katika makundi matatu wapo w anaowafanyia kazi wafanyabiashara wakubwa na mabalozi watakuwa wanalipwa kima cha chini cha mashahara 90,000 wale w anaowafanyia maafisa wanaolipiwa huduma hii na waajiri wao watalipwa 80,000 na wengineo watakuwa wanalipwa 65,000.

hata hivyo w aziri akizungumzia Sekta hii ya ndani alisema kuwa watumishi wa ndani wanaoishi na kupata huduma ya chakula ,malazi na nyinginezo kutoka kwa mwajiri atakatwa asilimia 68 ya mshahara wake kwa ajili ya malazi ambapo chakula 56% na 12% matumizi mengine.

kwa wale wa mahotelini watakuwa w analipwa kima cha chini shilingi 150,000 hoteli za kitalii na Maahoteli ya kati 100,000 na hoteli ndogondogo , mabaa ,nyumba za wageni na migahawa shilingi 80,000.

katika Sekita ya madini upande wa migodi mikubwa watakuwa wanalipwa shilingi 35,000 kima cha chini lakini waajiri wanaoshughulika na chumvi au chokaa wataingia kwenye kundi la viwanda vidogo kwa kuwa uwezo w ao ni mdogo ukilinganishwa na wa migodi ya madini yenye thamani kubwa.

Sekta ya Ulinzi binafsi Serikali imesema kuwa katika uchunguzi wake imegundua kuwa makampuni mengi yanawalipa wafanyakazi wao pesa kidogo au kuwacheleweshea mshahara wakati w amewapa silaha hali inayowafanya wajiingize kwenye vitendo vya ujambazim kutokana na hali hiyo wamiliki wa makampuni hayo wameonywa kama watashindwa kuwalipa kima kipya wafunge makampuni yao mapema.

kutokana na hali hiyo makampuni ya wakubwa na makampuni ya kigeni itakuwa shilingi 105,000 na makampuni mengeineyo 80,000 Sekta nyine ni biashara na viwanda ambapo ni pamoja na mabenki kima cha chini kitakuwa shilingi 150,000 na viwanda vidogo na biashara ndogo itakuwa shilingi 80,000.

sekta nyingine ni Afya amabapo imegawanywa katika makundi mawili kuna ,Hospitali kubwa na maduka mshara kima cha chini kitakuwa 120,000 kwa hospitali ndogo na zahanati kitakuwa 80,000.

Sekta nyinge ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu ni usafiri na mawasiliano ambapo kuna vyombo vya habari na daladala zinazowahusu wandishi na makondakta katika s ekta hii wafanyakazi wa huduma za anga kima cha chini watakuwa wanalipwa 350,000, wasafirishaji wa mizigo (Clearing and Forwarding) kima cha chini ni 230,000.

kwa wafanyakazi wanaofanya katika mitandao mbalimbali ya mawasiliano ya simu (Telcom)shilingi 300,000 wengine niusafiri wa nchi kavu (Makondakta) kima c ha chini kitakuwa shili.20,0000.

katika vyombo vya habari waziri Chiligati alisema Vipo vya aina mbili vya kibiashara ambavyo kima cha kumlipa Mwandishi kitakuwa Shilingi 250,000 na kwa vile vya kidini ambavyo huwa vinatoa matangazo ya Dini kima cha chini kitakuwa 150,000, hata hivyo Chiligati amesema kima hiki hakimzuii mwajili kupandisha mshahara isipokuwa kinambana asilipe chini ya hapo.

kwa upande w a vibarua ambao hawajaajiriwa wsaajiri wametakiwa kugawanya mashahara wa kima cha chini katika siku 30 hiyo ndio itakuwa malipo ya kibarua kwa kutwa aidha kaWaziri Chiligati alisema kuwa nyongeza hii ya mishahara isiwe chanzo cha waajiri kupandisha bei ya bidhaa kwani kwa kufanya hivyo ni kuwaumiza w afanyakazi wao.

"Kwa mjibu wa tangazo (Wage Order) litakalotolewa katika gazeti la Serikali (GN)Viwango vipya vitaanza kutumika kuanzia Mwezi Novemba mwaka huu, tangazo hilo mara litakapotolewa kila mwajiri anatakiwa kulipa viwango vipya ,kinyume chake ni kukiuka kifungu namba 41(1)cha sheria na 7ya Mwaka 2004 na kwahiyo hatua kalizitachukuliwa dhidi ya mmwajiri yeyote atakatelipa mishahara chini ya viwango vilivyowekwa kwa mjibu w a sheria"alisema waziri.


Naye Hellen Ngoromera anaripoti kuwa

Akizungumza baadaye kuhusu tamko hilo la serikali, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), Nestory Ngulla, alisema TUCTA imeyapokea maamuzi hayo.

Awali kabla ya tamko hilo la serikali, Shirikisho hilo la wafanyakazi liliitaka serikali kuongeza mshahara wa kima cha chini na kuwa sh. 315,000.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa pamoja na tamko hilo, TUCTA itatafakari na kuona ni namna gani itafanya kuhusiana na suala hilo.

“Tumeyapokea haya… ingawa kiwango hicho cha mishahara kilichotangazwa hakijafikia kiwango tulichokitaka TUCTA inaona kuwa huo ni mwanzo mzuri

Hiyo siyo kazi ndogo, kiwango cha mishahara kilikuwa chini mno, toka sh. 35,000 hadi sh. 65,000, kwa kuwa mshahara mpya unatakiwa kuanza kulipwa Novemba mosi nasi kama shirikisho tutatumia nafasi kuanzia leo(jana) kuona tunafanyaje,”. Alisema Katibu Mkuu huyo.

Sakata la TUCTA kuidai serikali kima cha chini cha mishahara lilianza miezi michache iliyopita jambo lililosababisha shirikisho hilo kufanya mgomo ikiwa serikali haitatekeleza ahadi yao.

Hatua hiyo ililifanya shirikisho hilo kuipa serikali mwezi mmoja kushughulikia suala lao. Hata hivyo baadaye serikali ililifanyia kazi suala hilo na kuunda kamati ndogo kufuatilia suala hilo ambalo ndilo lilikamilisha kazi yake na kuifanya serikali kutolea majibu suala hilo jana.