Wapentekote wapingana uteuzi wa rais Kikwete
Na Tanpress
KANISA
la Pentecost Evangelist (PEC) limesema kwamba Mwenyekiti wa chama cha
Democratic Party (DP) Mchungaji, Christopher Mtikila,ameteuliwa na Rais Jakaya
Kikwete kuwakilisha mawazo ya wapentokoste,katika
bunge la katiba.
Akizungmza na wanahabari leo Dar es Salaam, Askofu wa jimbo
la nyanda za juu, Mbeya,William
Mwamalaanga amesema kuwa anasikitishwa na wale wanaolalamikia uteuzi wa
Rais Kikwete kwamba amewatenga wapentekoste wakati alimteua Mchungaji Mtikila.
“nawashangaa Wapentekoste wenzangu wanaodai kumlaani Rais
kwamba hajawateua wawakilishi kutoka kwenye kanisa letu , wakati kamteua
Mtikila ambaye anauwelewa mzuri kuliko wajumbe wengi kuhusu mambo ya katiba na
serikali ya Tanganyika”amenukuliwa
Askofu Mwamlanga ambaye amejitambalisha kuwa ni Mwenyekiti
wa kamati ya wanataaluma,haki za binadamu na mazingira inayoundwa na viogozi wa
dini amesema kwamba Mtikila alianza kutetea serikali ya Tanganyika tangu Mwaka
1986.
“Nimesikia kwamba baadhi ya wapentekoste wamemlaani Rais
Kikwete kwa kuwatenga katika bunge la Katiba,….sio kazi yetu viongozi wa dini kulaani serikali ….kazi yetu ni
kuombea na kutoa Baraka…mtu anayelaani serikali yake ni sawa na yule anayelaani
sahani anayotumia kulia chakula”amesema Mwamlanga.
Aidha amewatahadharisha viongozi wa dini kujitenga na siasa
kwani kama nchi ikichafuka kutokana na kauli zao hawatapata pa kukimbilia kwani
hata wao wataakuwa sehemu ya watanzania.
Askofu Mwamlaanga ametoa tamko hilo saa chache baada ya Askofu
mwenzake Zakary Kakombe kusambaza waraka wa kuilaani serikali kwa kitendo chake
cha kuwatenga wapentekoste katika bunge la katiba huku baraza la maaskofu wa
kipentekoste wakitajwa kumuunga mkono waraka huo.
