Mafua ya kuku yalipuka yashambulia bagamoyo
Na Mobini
Sarya,Tanpress
Ugonjwa wa
mafua ya ndege umelipuka na kuathiri ndege wakiwemo kuku katika jimbo la
Chalinze mkoani Pwani.
Afisa Kilimo
na mifugo Kijiji cha Saleni Kata ya Lugoba wilayani, Bagamoyo,Rashid Ali
Ramadhan,amesema kuwa tayari kuku kadhaa wamekwisha kufa huku ugonjwa huo
ukizidi kusambaa haraka.
“Huu ni
ugonjwa ambao unatusumbua katika ukanda huu wa pwani kila mara hivi sasa
umelipuka na wafugaji wengi wamepata hasara”anasema Ramadhani
Akiuelezea
ugonjwa huo anasema kuwa wakulima wanaofuga kuku wanapaswa kuwachanja wakiwa na
wiki nne tangu wazaliwe ili kuweza kudhibiti maambukizi.
Ramadhani
anasema kuwa kuku au ndege akishapata ugonjwa huo macho huvimba na kupofuka
hivyo kushindwa kula chakula na baadaye hufa kwa njaa.
Baada ya
kuku kuugua mfagaji anatakiwa kumsafisha kuku macho kwa kutumia mafuta ya kula
na kumpaka mafuta ya taa kila mara ili awe kuona chakula vingenevyo anakufa na
njaa.
“hakuna dawa
nyingine ambayo anaweza kupewa lakini kama bado
ni mdogo unaweza kumchanja dawa aina ya
Chicken pox Vaccine,..uhakika ni asilimia 80 kwamba hawataugua ugonjwa
huo”anasema Rashid
Aidha mmoja
wa wafugaji wa kuku ,Seleman Hamad ambaye ana kuku zaidi ya 600, amesema kuwa
awali wataalum wamuilwambia kuwa ugonjwa huo ni ndui lakini baada ya kwenda nao
kwa wataalam wengine akabaini kuwa ni mafua.
“Waliponiambia
kuwa ni ndui nikajiuliza mbona nilikwisha chanja , lakini baada ya kuwapiga
picha na kwenda nao katika maduka makubwa ya karaiakoo, wataalm walipoona tu
wakaniambia ni mafua ya ndege na kweli nilipoanzisha tiba wameanza
kupona”anasema Hamad.


0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home