Thursday, March 6, 2014

Wanakwenda wapi Watoto wa vituoni?



Na  Mobini   Sarya

SWALI ambalo pengine  msomaji umewahi kujiuliza ni kwamba;je wanakwenda wapi wale watoto wanaolelewa kwenye vituo maalum wanapofikisha umri wa miaka 18?.

Wakati mwingine vinajulikana kama vituo vya watoto yatima au vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Hilo ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kama ambavyo pengine na wewe umewahi kujiuliza lakini sasa linaweza  kuwa limepata majawabu.


 BCDSA tz,mkurugenzi wake, Mathew Shadrack anasema kuwa tangu kianzishwe Mwaka 2004,hawajapokea watoto wengine.

Nimekwenda vituo vitatu tofauti vya kulelea watoto hao, viwili vipo jijini Mwanza na kimoja cha KIWOHEDE Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na walezi au wasimamizi wa vituo hivyo nimegundua mambo kadhaa.

Katika kituo cha Upendo Daima kilichopo jirani na chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine,eneo la Malimbe Mwanza nakutana na Bi. Irine Kimaro ambaye ni msaidizi wa kituo hicho.

Katika mazungumzo yangu naye nagundua kuwa kituo hicho kilianza miaka ya 90, kilianzishwa na masisita wa kanisa Katoliki kwa lengo la kukusanya watoto wanaoishi mitaani na kwarejesha katika familia zao.

 Hiyo ndiyo falsafa ya kuanzisha vituo hivyo, kwamba siyo mpango wala nia ya serikali kuruhusu watu kutunza watoto katika vituo hivyo badala yake wanapaswa kuwakusanya na kuwarejesha makwao.

Masista hao walianzisha kituo kilichokuwa kinaitwa Day Care Centre ambapo walikuwa wanawatunza watoto kabla ya kuwarejesha makwao.

Hata hivyo baada ya ongezeko la watoto walianzisha kituo kingine ambacho kinaitwa Back to home hiki kituo kazi yake ni eneo la kungojea usafiri wa kuwapeleka watoto kwao mara baada ya kuwa wamejulikana wanapotoke.

“Sio lengo la kituo kulea watoto hapa, hiki kituo kilianzishwa kwa lengo la kuwakusanya watoto wanaotangatanga mitaani na kuwarejesha katika familia zao”anasema Bi.Kimaro

Hata hivyo hivi sasa kituo hicho kimelazimika kujipa jukumu la kuwalea na kuwasomesha baadhi ya watoto kutokana na kwamba wamegoma kurejea makwao.
   Swali la kujiuliza ni kwanini watoto hawataki kurejea majumbani kwao hata pale wanapoambiwa watasafirishwa kwa gharama za vituo?

Mmoja wa maafisa wanaofanyaka kazi ya kupeleka watoto majumbani kutoka kituo hicho Bw. Waryoba Nyamsenda anasema wanapowapata watoto wanaoishi mitaani huwarejesha nyumbani kwao na huwapatia shilingi 50,000 kama  pesa ya kununua vifaa vya shule.

 “Kwanza mtoto unakuta anafanya kosa halafu anakimbia kuogopa kuchapwa, pili migogoro ya kifamilia inayofanya mtoto kukosa malezi, tatu njaa inayokabili familia nyingi watoto wanamua kwenda kujitafutia au wanatumwa na wazazi wao”anasema mfanyakazi huyo.

“Unakuta mtoto anakwambia kuwa kwetu ni Shinyanga mnakata tiketi ya watu wawili kwenda huko, mkifika  anawageuka tena anawambia kuwa  kwetu ni Mara sio hapa hata jina anadanganya”anasema Bi. Kimaro.

Bi.Kimaro anasema kuwa watoto wanaokaa nao kituoni ni wale ambao wanagundua kuwa hata wakirejea majumbani kwao hawawezi kuendelea na masomo kutokana na umasikini au njaa kwenye familia zao.

Bi.Kimaro alisema wamepata barua kutoka Ustawi wa Jamii, hivyo tukiwapata mitaani wakifika hapa tunawapima uwezo wao kielimu halafu tunakwenda kuwaombea nafasi ya kusoma katika shule ya msingi Nyamalango”anasema Bi.Kimaro

tangu waanzishe mpango huo miaka michache iliyopita  wamefanikiwa kusomesha watoto 48 ingawa kituo kinauwezo wa kuwalaza watoto 50.

Mwandishi  wa makala hii alipotaka taarifa zaidi ya idadi ya wanaosoma, alipatiwa  kama ifuatavyo: darasa la kwanza watatu, la pili watatu, darasa la tano wanne, walioingia darasa la saba Mwaka huu saba.

“waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013 walikuwa watatu na wamefaulu wote kwenda shule ya upili (sekondari) lakini tunawachukua watoto wa kiume tu, kuanzia miaka 6 hadi 16” anasema Bi.Kimaro. 

Hata hivyo kuna watoto wawili waliokuwa wanasoma shule ya upili (sekondari) Kilango iliyopo wilayani Magu, wameacha masomo wakiwa kidato cha kwanza mwaka jana bila sababu hivyo kituo kimejitoa kuendelea kuwahudumia.

Wapo wale waliohitimu kidato cha tano Nyamilama Sekondari mwaka jana ambao ni watatu, wanaomaliza shule ya msingi wakashindwa kuendelea kidato cha kwanza hupelekwa katika vyuo vya elimu ya ufundi.

Kituo hicho kinao watoto wawili wenye vipaji vya mpira ambao wamechaguliwa kwenye mashindano ya kombe la dunia la watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Brazili, mwaka huu wakitoka gereji wanakwenda kufanya mazoezi ya mpira wa miguu, nao ni Maganga Khamis (14) na Majuto Madirisha (14).

Kituo hicho kimeendelea kuwasaidia watoto hao kusoma kadri wanavyoweza na tayari mmoja wao amefika chuo cha sanaa Bagamoyo (TASUBA)ambaye ni Bw.Agoustine Mgendi anasomea muziki na ngoma za asili.

“Kama unavyofahamu sio lengo letu kukaa na watoto kituoni hata wale wanaosoma ambapo hulazimika kuishi kituoni, wanapofunga  shule  huwapeleka likizo majumbani kwao, baadaye kabla ya likizo huwa tunakutana nao mitaani wakizurura”anasema mlezi huyo.

   


 
baadhi ya watoto wanaotokea katika familia zenye maisha magumu wakifundishwa elimu ya ujasirimali katika kituo cha KIWOHEDE Dar es Salaam.
Anasema kuwa watoto wengi wanatabia ya kukimbilia mitaani hivyo “tunawapa mazoezi ya akili,michezo,ngoma, sarakasi na mpira wa miguu.

Anaongeza kuwa idadi ya watoto wanaozurura mitaani ambao wangehitaji msaada wa kituo hicho ni kubwa lakini hawana uwezo huo ndio maana wanahitaji pesa za kujenga shule yao wenyewe itakayokuwa na uwezo wakusomesha watoto wengi.

Kutokana na tabia zao za kutoroka, kituo hicho kimelazimika kuajiri mshauri kubadili tabia pamoja na mtu anayewasimulia hadithi za kuwajenga kisaikolojia kila siku jioni.

Kituo hicho kinasema kuwa mkakati wake ni kuwarejesha watoto kwa wazazi wao wakasome, lakini kwa wale ambao wamebainika kuwa hawapo tayari kurejea makwao ndiyo watakaosomeshwa hadi wafikie umri wa kujitegemea.

Mwangalizi wa kituo hicho anatoa wito kwa serikali iwawezeshe wazazi ambao wanaishi kwenye mazingira magumu ili waweze kutunza watoto wao badala ya kuwaacha wakiahangaika mitaani.

Katika Kituo cha Kiwohede Dar esSalaam,Mshauri wa vijana katika kituo hicho,Bi.Stella Mwambeja anasema  kuwa kituo chao  hakikuanzishwa  kwa ajili ya kulea watoto kituoni  hapo bali kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Kituo hicho ambacho kilianzishwa chini ya mkurugenzi Bi.Jusita Mwaituka,Mwaka 1999 kimetoa taarifa yake kuwa;“walengwa ni wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 17  wanaoishi katika mazingira magumu lakini akija mvulana anaweza kusaidiwa.

Mwalimu wa kituo hicho Bw.Waryoba Nyamsenda anasema wanapowapata watoto wanaoishi mitaani huwarejesha nyumbani kwao kisha huwapatia shilingi 50,000 kama  pesa ya kununua vifaa vya shule.

“kazi ya kukaa na mtoto umshauri hadi akubali kurejeanyumbani kwao ni ngumu kuliko msaada  mwingine wowote”anasema Bw. Nyamsenda ambaye pia ni mshauri wa vijana.

Hata hivyo licha ya kwamba kituo hicho kina zaidi ya miaka 15 tangu kianzishwe wasimamizi wake walikosa takwimu zinaoonyesha idadi ya watoto waliowahi kurejeshwa majumbani kwao au wale walionufaika na kituo hicho.

Aidha katika kituo cha serikali kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam,imeelezwa na Kamishna wa ustawi wa jamii, msaidizi idara  ya watoto, Bw.JeanneNdyetabura kuwa, hawana kumbukukumbu  watoto hao wanakwenda wapi wakifikisha umri wa  miaka 18.

Kamishna  huyo licha ya kukiri kuwa serikali ina kituo kimoja tu kati ya vituo 287 vilivyoanzishwa nchi nzima, lakini ameweka bayana kuwa wale watoto wanaolelewa pale kituoni hutakiwa kuondoka wakifikisha miaka 18.

“Hatuna kumbu kumbu zozote lakini ninachojua wapo waliosoma hadi chuo kikuu na wakafanikiwa kupata ajira na kuoa wakahama kituoni.. lakini baada ya hapo hatu wafuatilii maisha yao”anasema Bw.Ndyetabura

Na kuongeza kuwa, kituo cha kurasini kinauwezo wa kuchukua watoto 70 wenye umri wa miaka mitatu  hadi 17 huku wakitegemea kituo cha Msimbazi  kuwapelekea watoto waliofikisha umri wa miaka 2 na kukosa walezi.

Bw.Ndyetabura aliongeza kuwa, ili kituo kipewe kibali cha kulea watoto lazima wamiliki wake waonyeshe mkataba wa pango uliolipiwa zaidi ya Mwaka na wawe na  uhakika wa kuwapatia  watoto chakula na malazi kwa muda wote watakaokaa kituoni.

“Kama kituo kitakuwa na watoto waliofikisha umri wa kuanza shule lazima  watafutiwe shule, wapewe malazi mazuri ,mahitaji ya lazima na bwana  afya akague kituo hicho kama mazingira yake ni safi”anasisitiza Kamishna huyo.

Katika utafiti wa serikali uliofanywa na maafisa ustawi wa jamii umebaini kuwa  kati ya vituo 282 vinavyotumika kulea watoto ni vituo 120 tu ndio vimesajiliwa huku vingine vikiwa vinajiendesha kinyemelea kutokana na kukosekana maafisa ustawi wajamii katika baadhi ya halmashauri.
0753399 579 break.news@yahoo.com











0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home