Wednesday, August 3, 2011

Igunga nafasi mhimu kwa vyama vichanga

Na Mobini Sarya

JIMBO la uchaguzi igunga mkoani Tabora lipo wazi, baada aliyekuwa mbunge wake Rostam Aziz kujiuzulu mwezi uliopita.

Wakati wowote kuanzia sasa tume ya taifa ya uchaguzi itatangaza tarehe rasmi ya kuanza kampeni ya uchaguzi ili kuziba nafasi hiyo.

mtemi wa wanyamwezi chifu Mirambo
Tayari vyama vitatu vya siasa vimeanza kupitia pita kwenye jimbo hilo huku kila kimoja kikidai kwamba hiyo nafasi ni halali yake.

Vyama vinavyoonekana kupigana vikumbo katika jimbo hilo ni CCM kilichokuwa kinaliongoza,CHADEMA na CUF ambacho kilisimamisha mgombea kwenye uchaguzi uliopita.

Vyama vingine vyenye uwakilishi bungeni kama TLP,UDP na Nccr- Mageuzi bado havijaamua kama vitaweza kusimamisha wagombea katika jimbo hilo.
Uchaguzi wa jimbo hilo ni mhimu kwa vyama vinavyoitwa vidogo kama vitaamua kushiriki kwa sababu ni nafasi pekee ya kujitangaza.

Kwa sasa kuna vyama vya siasa takribani 17 ambavyo vimesajiliwa na msajili wa vyama vya siasa hapa nchini.

Lakini kati ya hivyo ni vyama vitano tu ambavyo vimekuwa vikijitutumua angalau kushiriki uchaguzi wa mara kwa mara licha ya kwmaba ni vyama vitatu ambavyo vimeonyesha kuwa na ushindani kipindi cha kampeni.

Uchaguzi wa Igunga unanafasi kubwa na ya kipekee kwa vyama vidogo kama SAU,CHAUSITA,AFP UMD,DOKRASIA Makini,APPT-Maendeleo, Jahazi asilia na DP kama vitaamua kushiriki.

Ni nafasi muhimu kwa vyama hivyo kushiriki kwa sababu watapata frusa ya kujitangaza na kutathimini hali ya maenedeleo ya vyama vyao mkoani Tabora.

Uchaguzi huo mdogo ambao ni wa kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu ulipita utatoa frusa kwa vyama vyote vitakaoshiriki kujitanganza na kujitathimini zaidi.

Pia ni uchaguzi ambao vyombo vya habari vitaelekeza nguvu kule kwa kuwa ni uchaguzi ambao umetokana na mbunge kujiuzulu tafauti na chaguzi zingine ambazo zilikuwa zinasababishwa na mbunge kufariki au kuvuliwa uanachama.

Nawashauri vyama viongozi wa vyama vingi kujitahidi kushiriki kwenye uchaguzi huu ili watumie frusa ya kipekee kujitangaza kwasababu ushindani utakaokuwepo utaleta changamoto kubwa na ukuaji wa demokrasia.

Ikiwa chama hakina hata ofisi yoyote mkoani tabora kitaamua kuelekeza nguvu zake kule kitatumia frusa hiyo kuimarisha mfumo wa uongozi na kufungua ofisi jambo ambalo lisingefanyika kwa urahisi.

Litakuwa ni jambo la kushangaza kama vyama hivyo vitashindwa kusimamisha wagombea kwa lengo la kujitangaza bandala yake wabaki kuwa watazamaji.

Ni heri washiriki uchaguzi huo kwani kushiriki kuna umhimu wake hata kama mshiriki hataibuka mshindi lakini anapotajwa mshindi na mshikiri naye hutajwa.

Unaposhiriki sio lazima ushinde lakini hutumia frusa hiyo kusoma mbinu za mshindi ili kujiandaa na mashindano yanayofuata.

Lakini kama vyama hivyo havitashiriki uchaguzi huo na havina ofisi wilaya ya Igunga ni lini vitaimarisha mtandao wao nchi nzima kama havitaki kutumia frusa hiyo ya bure tena sambamba na matangazo ya vyombo vya habari.

Sasa ni wajibu wa vyama hivyo kupima uzito na kuona kama kuna umhimu wa kushiriki au kutokushiriki katika uchaguzi huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kisiasa.

Kwa wale wasiojua historia ya mkoa wa Tabora ni kwamba mkoa huo unaokaliwa na kabila la wanyamwezi kwa wingi ni moja ya maeneo ambayo hadi kufikia karne ya 19 yalikuwa yameanza kujitawala kidola.

Mkoa huo unahistoria yake katika biashara ya utumwa kwani ndio ulikuwa kitovu cha soko hilo afrika ya kati, walipokuwa wanakusanyiwa watumwa kabla ya kusafirishwa kwenda bagamoyo na warabu wa tabora.

Ndio eneo la kwanza kupigana vita kibila na wakoloni kati ya askari wa mtembi mirambo aliyekuwa anatumia askari wa kali waliojuliakna akama warugaruga dhidi ya bwana vita Tip tip ambaye alikuwa mfanyabiashara wa watumwa karne ya 18.

Hivyo tunapozungumzia siasa za mkoa wa Tabora hatuwezi kusahahu historia yake tangu mwaka 1700 hadi 1900 ambapo walizaliwa akina chifu fundikira karne moja baada ya kufariki mtemi asiyeshindikana Mirambo.

Labels:

Friday, February 18, 2011

Mabomu ya JWTZ yazalisha wakimbizi Dar

*Jeshi lasisitiza haliwezi kuhamisha kambi
*Wahofia ya Misri,Tunusia

MAELFU ya wakazi wa Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam, wameyakimbia makazi yao wakihofia kuendelea kulipuka kwa mabomu zaidi katika Kambi ya 511KJ Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la wananchi (JWTZ) likiwataka warejee makwao,

Shimbo akionyeshwa mabomu hayo

Msemamaji wa Jeshi la wananchi (JWTZ) Luten Kanali Kupambala Mgawe aliwaambia wandishi wa habari kuwa, wananachi wanapaswa kurejea makwao,kulinda mali zao kwani hakuna mabomu yatakayolipuka tena.

“Mabomu yaliyozagaa maeneo hayo ni aina ya rocket ambayo hayawezi kulipuka bila kulipuliwa, pia tunawashauri wanapoona milipuko ya namna hiyo wasiyakimbie bali walale chini”alisema Mgawe

Tukio hilo ambalo limetokea Februari 16, mwaka huu usiku baada ya maghala ya kuhifadhia mabomu kuteketea na kusababisha vifo vya Watanzania 20 kwa idadi ya awali na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa huku wakazi wa Jimbo la Ukonga wakiyahama makazi yao na kwenda kujikusanya kama wakimbizi katika uwanja wa Taifa.

Hatua ya wakazi hao kukimbia makazi yao ni baada ya kurejea Alhamisi asubuhi majumbani kwao na kukuta mabomu ambayo hayajalipuka yakiwa yamezagaa kwenye makazi yao hivyo wakawa na hofu kuwa huenda yakalipuka tena.
Luten Kanali Kupambala Mgawe amewataka wanachi hao kutoa taarifa wanapoyaona ili askari wakayakusanye mabomu hayo na nakuyategua.

“Sisi kama wataalam wa mabomu tunawaambia wananchi wote warejee kwenye makazi yao,hakuna tena mabomu yatakayolipuka tena, tumekwisha yadhibiti hakuna sababu ya kuyakimbia na yale yaliyotapaa mitaani wasipoyagusa hayawezi kulipuka,”alisema Kanali Mgawe

Hata hivyo pamoja na kusema hivyo huku akisaidia na askari Polisi waliokuwa wanapita na kipaza sauti kuwaambia watu warudi makwao, bado misururu ya wananchi iliendelea kumiminika barabarani wakikimbilia kwenye maeneo mengine hasa uwanja wa taifa.

Nipe habari imeshuhudia Misururu mikubwa katika barabara ya Mwalimu Nyerere ikiekelea Mjini ambapo magari yalikuwa kwenye msongamano mkubwa yakiwahamisha watu yakiwemo yale ya kubeba takataka.

Akizungumzia tukio hilo Luten Kanali Mgawe alisema kuwa ilikuwa Februari 16 saa 2:20 usiku ambapo bomu moja lilipuka kwenye ghala namba tano baada ya masaa mawili yakaanza kulipuka zaidi.

Maeneo yaliyoathirika zaidi na mabomu hayo ni Gongo la Mboto, majohe, Kipunguni ambako yalikuwa yakielekea nakusababisha nyumba nyingi kuangukana,Chanika na baadhi ya meneo ya Pugu.

Rais Kikwete ataembelea 511KJ

Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Jakaya Kikwete Februari 16, alitembelea Kikosi cha jeshi 511 eneo la Gongo la mboto ambapo kulitokea mlipuko mkubwa wa mabomu na kusababisha maafa makubwa.

Akitoa taarifa mbele ya Rais Mkuu wa Kikosi hicho Kanali Aloyce Mwanjile alisema kuwa maghala 22 ya kuhifadhia silaha yameteketea kwa mabomu pamoja na mabweni mawili ya askari makapera.

Ingawa alisema kuwa hakuna askari aliyeuwawa, lakini alisema watano walijeruhiwa wakati wanakimbia ,lakini alisema kuwa magari matano yakiwemo mawili mapya yameteketezwa kabisa na nyumba ya kuhifadhia mafuta pamoja na maghala ya kuhifadhia chakula

“Mheshimiwa Rais katika yale mabweni nguo na mali zote za askari zimeteketea kabisa na kitu kilichokuwemo ndani askari wamebaki bila kitu chochote,” alisema Mwanjile.

Akizungumzia hali hiyo Rais Kikwete amesema kuwa alipata taarifa hizo usiku baada ya kuarifiwa na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwanyange ambapo walikutana Ikulu usiku huo huo na kujadiliana jambo hilo.

“Nimekuja hapa kupata taarifa zaidi, nilipata usiku kwa mkuu wa majeshi…hili ndilo ghala letu kuu la silaha na limeteketea lote, leo mchana tutakutana baraza la usalama wa taifa kujadili tukio hilo,”alisema Rais Kikwete.

Amewataka Watanzania kuwa watulivu kwani kile kipindi cha hatari kimepita na taarifa rasmi zitaendelewa kutolewa na jeshi baada ya baraza hilo kukutana.

JWTZ hatuwezi kuhamisha kambi zetu

Jeshi la wananchi (JWTZ)limesisitiza kuwa haliwezi kuhamisha kambi zao zilizopo karibu na maeneo ya wananchi kama njia ya kuepusha maafa yataokanayo na milipuko kwasababu wananchi wenyewe ndio wamezivamia.

Msemaji wa Jeshi hilo, Luteni Kanari Mgawe alisema jana kuwa wakati kambi hizo zinajengwa Jijini Dar es Salaam, maeneo hayo yalikuwa mapori lakini baada ya ongezeko la watu wakaamua kuzifuata.

“Wanajenga karibu na eneo la Jeshi huku wakisogeza bikoni kwa madai kuwa sisi wanajeshi hatukosona hatujui mikapa sasa yakianza kulipuka wanatutaka tuhame,tukihama nani atailinda Dar es Salaam yakitokea yale ya Misri au Tunisia”?alihoji Mgawe .

Kauli hiyo ilirudiwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo, Abdarahiman Shimbo aliyewaambia wandishi wa habari kuwa kila kambi ina mabomu yanayoweza kulipuka wakati wowote lakini hawawezi kuhama labda wananchi wahame.

“Sisi tunazipenda kambi zetu hatuwezi kuzihamisha… zipo kwa ajili ya ulinzi wananchi ndio wanapaswa kuhama kwani kila kambi ya jeshi ina mabomu,”alisema Shimbo.

Kwa upande mwingine Nipe Habari limetembelea eneo la uwanja wa taifa na kushuhudia msururu mrefu wa watu waliokuwa wanapita mbele ya watoto zaidi ya 179 waliopotea na kukusanywa eneo hilo.

Baadhi ya watu na taasisi mbalimbali zilikuwa zimejitokeza eneo hilo kwa lengo la kutoa msaada wa maji na mikate ili kuwafaraji watu hao ambao walionekana kuchoka na kukata tamaa kabisa.

Labels:

Saturday, June 26, 2010

WANDiSHI WATIWA MBARONI DODOMA

Na Mwandishi wetu Dodoma

WANDISHI nane wa habari kutoka katika vyombo mbalimabali juzi walijikuta matatani baada ya kutiwa mbaroni na mamafisa usalama wa taifa wa kituhumiwa kuingia bungeni bila kibali cha bunge.

http://tarishi.files.wordpress.com/2008/08/img_1626.jpg

Wandishi waliokamatwa na kushikiliwa kwa masaa kadhaa ni wale waliopelekwa na Taasisi ya kutetea uhuru wa Vyombo vya habari kusini mwa Afrika ,tawi la Tanzania (MISATAN)

SPIKA WA BUNGE AKIINGIA BUNGENI AKIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA MOJA YA SHUGHULI ZAO
Tukio hilo lilitokea jumatano asubuhi baada ya bunge kuwa limemaliza kipindi cha maswali na majibu, ndipo maafisa wabunge walipopita eneo walipokuwa wamekaa wanandishi na kuwakamata waandishi hao.

Chanzo cha tukio hilo ni baada ya afisa mmoja wa bunge aliyejulikana kwa jina la Ebelege kuwanyima wandishi hao vitambulisho kwa maelezo kuwa vimekwisha nakuwashauli watumie vile vya wageni.

“tuliwa na vitambulisho 60 lakini wandishi wamekuja zaidi ya 80 hivyo nendeni kule getini nitawapigia walinzi wa usalama wawapatie vitambulisho vya wageni mkatumie hadi utaratibu mwingine utakapoandaliwa”Ebelege aliwaambia wanandishi hao.

Baada ya wanandishi hao kukamatwa walipelekwa kwa afisa usalama mkuu wa Bunge aliyefahamika kwa jina la Mwanga ambapo waliwekwa chini ya ulinzi wakituhumiwa kuingia bungeni na kuandika habari bila kibali.

Mwanga alihoji uhalali wa Misa kutuma wandishi bunge hasa katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu ambapo vyombo vya habari ndio vyenye uhalali wa kutuma wandishi sio Misa.

Kufuatia wandishi hao kushikilia kwa masaa kadhaa ,Mwanaga aliwatuma askari wakamkamate Ebelege kwa tuhuma za kuruhusu wandishi bila taratibu lakini Ebelege alikana kuwatambua wandishi hao .

Aidha licha ya MisaTan kutuma mapema taarifa za kuwapeleka wandishi bunge ,ofisi ya katibu wa Bunge ilikana kufahamu taarifa hizo hivyo afisa habari wa Bunge Said Yakubu akashauri wanandishi hao wachukuliwe hatua zaidi.

Hata hivyo baada ya masaa kadhaa ya mahojiano wandishi hao waliamriwa mkuondoka katika viwanja vya bunge huku wakisindikizwa na maaskari hadi nje ya geti la bunge.

Baadaye taarifa zilibanisha kuwa wanandishi hao waliwasiliana na ofisi ya Misa ambapo baadaye ilifahamika kuwa barua ya Misa iliwasili bungeni Tangu june 10 Mwaka mhuu lakini kutokana na uzembe wa baadhi ya watendaji wa bunge walishindwa kupeana taarifa.

Hadi jana wanandshi hao walionekana wakizunguka katika baadhi ya ofisi za bunge ili kuona kama watapewa vitam,bulisho vya kuingilia bungeni kwa ajili ya kuripoti habari

Labels:

Sunday, June 7, 2009

ufisadi waitafuna Serengeti

Mkurugenzi akiri kupokea nyaraka feki

na Mwandishi wetu,Serengeti

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (DED) Kimulika Garikunga amekiri kupokea malalamiko ya wakazi wa Kata ya Issenye wakidai kuwa nyaraka za mihtasari ya vikao zilizowasilishwa kwake hatimaye kufikishwa kwenye baraza la madiwani kuonyesha kwamba wananchi wameafiki kutoa eneo lao kwa mwekezaji ni za kughushi.

Garikunga amesema kwamba katika madai ya wananchi hao wanasema kwamba hakuna mikutano ya hadhara iliyoitishwa na viongozi wa vijiji kama taratibu zinavyosema ili kupata kibali cha wananchi kutoa eneo la kuipatia kampuni ya Serengeti Holding Estate ambayo inataka eneo lenye ukubwa wa hekta 5000.

Baada ya kupokea malalamiko hayo Garikunga amesema kwamba ofisi yake imeamua kuchukua hatua za kuchunguza nakufuatilia madai ya wakazi hao ambao wameyawasilisha kwa niaba ya wenzao ili kubaini kama ni ya kweli kwamba hakuna mikutano ya wananchi iliyokaa nakuandaai nyaraka hizo.

“baada ya ofisi yangu kupokea malalamiko hayo imeanza kufanya uchunguzi kubaini kama viongozi wa kata za Natta na Issenye waliwasilisha kwangu nyaraka za kughushi kuonyesha kwamba wananchi wamekaa nakuafiki kutoa maeneo yao kwa kampuni hiyo”alisema Garikunga

Mkurugenzi huyo amesema kwamba awali diwani wa kata ya Issenye Chrismas Chabanga alimweleza kuwa taratibu zote zilizingatiwa ikiwemo kuitisha mikutano ya hadhara kwa wananchi wa Ihalala, Nyiberekera, Singisi na Mtukel ambao walikubaliana kutoa eneo hilo kwa malipo ya Milioni tano kwa Mwaka.

Kufuatia kuibuka kwa mgogoro huo tayari ofisi ya Mkurugenzi imesema kwamba itamzuia Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nyaga Mawalla kwenda kupima eneo kama alivyokuwa ameidhinishwa na baraza la madiwani hadi pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi.

Kampuni hiyo ilikuwa imepewa kibali na baraza la madiwani ambalo lilikaa Mei 8 Mwaka huu kujadili maombi ya kampuni hiyo na katika kikao hicho madiwani walilipwa posho na kampuni baada ya kupewa shilingi milioni 28 kwa ajili ya kuandalia kikao hicho.

Katika hatua nyingine baada ya kuibuka kashfa hiyo vyama vya NCCR-Mageuzi na CCM vyenye uwakilishi wa viongozi katika eneo hilo vimetoa agizo la kuchunguzwa viongozi wake waliohusika kughushi nyaraka hizo kisha kuziwasilisha katika baraza la madiwani na yakapitishwa.

Akizungumza na wandishi wa habari katika Kata ya Issenye katibu wa NCCR-Mageuzi, Wilaya ya Serengeti Mangasa Mkira

Alisema kwamba amemwita Diwani wake Chabanga aeleze jinsi alivyoshiriki kughushi nyaraka hizo na kuwasilisha mihtasari inayoonyesha kwamba wananchi walishafanya mikutano na kuafiiana kutoa eneo kwa mwekezaji.

“nimemwandikia diwani wangu afike ofisi ya wilaya ili aeleze jinsi alivyoshiriki kupitisha suala ambalo ni kinyume na taratibu za sheria ikibainika kwamba alifanya hivyo kwa maslahi ya binafsi ili kuchafua chama tutamvua uanachama wake ili kulinda heshima ya chama” alisema Mkira.

Naye Mwenyekiti wa CCM tawi la Ihalala Masoud Shashota alisema kwamba tayari wamepokea agizo kutoka wilayani wakitakiwa kuwaita na kuwahoji viongozi wote wa vijiji ambao wanatokana na Chama chake kufahamu ni jinsi gain walishiriki kuandaa nyaraka ambazo hazikushirikisha wananchi.

“sisi viongozi wa matawi tumepokea agizo kutoka CCM wilaya tukitakiwa kuwaita na kuwahoji viongozi wote wanaotajwa kuhusika na kuandaa nyaraka ambazo ni kinyume na taratibu za chama”alisema Shashota

MWEKEZAJI ALIPEWA ENEO LA MTU,

SERENGETI.

WAKATI Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Kimulika Galikunga akitafakari kufuatilia pingamizi lililowekwa na wakazi wa kata za Issenye na Natta kuhusu eneo lao kupewa mwekezaji imebainika kuwa eneo hilo alikwisha pewa mkazi mmoja wa kijiji cha Nyiberekera toka mwaka 1986.

Huo ni mtihani wa pili kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo baada ya mtihani wa kwanza kubainika kwamba hata mihtasari iliyotumiwa na baraza hilo kumpatia mwekezaji eneo lenye hekta 5000 ni ya kugushi kuonyesha kwamba wananchi wamekaa vikao wakakubali.

Hali hiyo imebainika huku bado kukiwa na mtafaruku mkubwa kutoka kwa jamii ikipinga maamzi ya halmashauri ya wilaya kujadili na kupitisha maombi ya mwekezaji huyo ya kuruhusiwa kupima eneo lao bila mchakato huo kuwashirikisha wananchi baada ya mihtasari hewa ilitumika kudanganya baraza.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari umebaini kuwa katika eneo hilo alilopitishiwa mwekezaji wa kampuni ya Serengeti holding Estate limited inayoongozwa na mwanasheria Nyaga Mawalla kuna ekari 300 zinazomilikiwa kihalali na mkazi mmoja wa kijijini hapo Moremi Mwanangwa toka mwaka 1986.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo eneo hilo alipewa na serikali ya kijiji baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa na kilichobaki sasa ni kulipia wapimaji na hakuna nyaraka zozote kutoka Serikali ya kijiji zinazotengua maamzi hayo yaliyofikiwa mwaka huo chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji Nyakanyenge Raphael.

Monangwa aliomba eneo hilo kwa ajili ya kilimo na ufugaji shughuli ambayo amekuwa akiifanya hadi hivi sasa licha ya uongozi wa kijiji hicho kuingia mengine ya kutoa eneo hilo kwa mwekezaji.

Mbali na Monangwa pia uchunguzi ulibaini kuwa eneo lingine ni makazi ya wananchi ambao wamekuwemo kwa muda mrefu hasa kundi la wafugaji ambao wanaitwa wahamiaji haramu ,huku katika shughuli za maendeleo wanashirikishwa kama wakazi halali wa kijiji hicho.

Diwani wa kata hiyo Chrismas Chabanga alikiri eneo hilo kukaliwa na wafugaji kwa muda mrefu,na kuwa wao wanawaona kama wahamiaji haramu kwa kuwa hawajapewa maeneo na serikali ya kijiji hicho.

Hata hivyo hakufafanua nia ya kutaka kumtumbukiza mwekezaji katika mgogoro wa mmiliki wa kwanza na hao wanaoishi eneo hilo ,ambao nje wanadai wahamiaji haramu na ndani wanawatambua kwa kuwa wanawashirikisha shughuli zote za maendeleo .

Baadhi ya wananchi waliwaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na wakazi wanaoishi eneo hilo kutambuliwa kuwa wapo muda mrefu ,hata mkuu wa wilaya hiyo Edward Ole Lenga katika mkutano wake wa kuhusu wahamiaji haramu alishindwa kuwaondoa .

“Toka Oktoba mwaka jana alipokuja kufanya mkutano wake hapa mkuu wa wilaya aliagiza wahamiaji haramu waondoke.lakini hawa hawajaondoka kwa kuwa tayari wanatambulika”alisema Mkazi Mmoja
.

Labels:

Sunday, January 6, 2008

Nyerere alikuwa binadamu wa kawaida au mtume?

Kila tarehe 14 mwezi wa kumi, huwa ni siku maalumu ya kukumbuka kifo cha kiongozi wa kwanza wa taifa la tanzania, hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyefariki mwaka 1999, huko london, nchini uingereza.

Kwa watu ambao si watanzania au kwa vijana wa Tanzania waweza kushangaa jinsi jina la Nyerere linavyotukuzwa na kusemwa kila kona huku likimwagiwa sifa lukuki kuanzia

mitaani, mashuleni, maofisini, vyombo vya habari na hata Kwenye nyumba za ibada kiasi kwamba kuna mchakato wa kuelekea kumtangaza mwenye heri.Nikiwa kijana wa kizazi

kipya ambaye nimesoma habari za Nyerere zaidi kwani nimepata fahamu akiwa anakaribia kufa, huwa nashindwa kuelewa utukuzaji huu, na pengine hunifanya nifikilie kwamba labda ndio

maana wanataka kumtangaza kuwa mwenye heri au mtakatifu. Hii ni kutokana na uelewaji wangu juu ya mitume mbali mbali wanaaminika kutumwa kuikomboa dunia hii.

Kwa wasomaji wa biblia wana fahamu habari za mtume mkuu ambaye huitwa mwana wa mungu aliyetumwa kulikomboa taifa la Israel ambaye Taifa hilo lilimkataa na kumsulubu mpaka kifo na alipofufuka akarudi zake mbinguni huku akiacha ahadi ya kushuka muda wowote kutoa hukumu kwa walio hai na wafu, ahadi ambayo kwa miaka zaidi ya 2000 bado inasubiliwa huku taifa alilokuja kuliokoa (Israel) likiwa kwenye machafuko ya hali ya juu.

Ukisoma vizuri vitabu (vitakatifu) utaona historia ya mtume huyu ilivyojaa kumtukuza na kumsifia tu pasipo kuangalia upande mwingine wa maisha, kwani yeye alikuja kama binadamu, na kukuna binadamu aliyekuwa mkamilifu, sasa inakuwaje mtume wa mungu nakuwa mkamilifu bila mapungufu au hata sifa nyingine za kibinadamu?

Tanaambiwa Yesu aliuwawa akiwa na umri wa miaka 36, lakini hatuonyeshwi kama ailwahi kuwa na mwenzi wa kike au na mabo mengineyo, huonyeshwa ni mtakatifu na mnyoofu tu.Hii ndivyo ilivyo na inavyoendelea kuwa kwa baba wa taifa hili hayati Julius Nyerere.

Mawazo yangu kama kijana ni kujaribu kujiuliza kwamba kama Nyerere asingezaliwa kweli taifa hili lingekuwa pabaya au pazuri zaidi ya hapa lilipo leo? Au tafa la Tanganyika/Tanzania lisinge zaliwa pia? Kuna haja ya kuangalia vizuri masuala haya na kujaribu kuachana na baadhi ya mifumo aliyotuachia Nyerere ili tuweze kuendelea mbele.

Huwa sielewi sana Nyerere anaposifiwana kueziwa kwa kuleta uhuru wa taifa hili kutoka kwa wakoloni wa kiingereza baada ya wajerumani kushindwa kututawala vizuri, hii inanishangaza kwa kuona pia bendela ya Taifa letu kutokuwa na alama nyekundu ya kuonyesha mchango wa wapiganaji walionyanyasika na kuufia uhuru wa taifa letu na badala yake tanafikiri akina Nyerere ndio waliopigania uhuru tulionao.

Historia inaonyeshi jinsi machifu kama akina Mirambo, Isike, Kimweri, Kinjenkitile Ngwale, Mkwawa, mangi meli na wengine jinsi walivyopambana na wakoloni wa kijerumani kwa nyakati tofauti na kwa ujasiri mkubwa na kuwakabili kwa kiwango cha juu zaidi, hii yaweza kuwa sababu ya waingereza kutoa uhuru haraka kwani yawezekani walijiuliza kwamba; kama wale machifu waliweza kukabiliana na wajerumani kwa kiwango kikubwa wakiwa hawana elimu na lugha moja,
je itakuwaje hawa walioonja elimu wakiamua kunzisha vita?

Si bora tuwalagahai kwa kuwapatia uhuru wa kisiasa na kuendelea kuwatawala kifikra na kiuchumi? Kwa maoni yangu kuna haja ya kuendelea kuwatukuza hawa machifu kwa kuthamini mchango wao wa kupeteza maisha kwa ajiri uhuru tulionao na sio tamtukuze

Nyerere tu na wenzake.Kama kijana unaweza labda kushangaa ni jinsi gani uchumi wa nchi kama ya uganda tuliyowahi kupiga vita inaendelea kwa kasi lakini sisi bado tunasuasua.

Tunatukuza kiongozi aliyetuwekea mifumo ambayo mpaka sasainatuongoza kuendelea kuwa masikini, tukija eti tunajisifu kwa amani aliyoipigania nyerere, hivi kweli tuna amani

a u njaa inayotunyima nguvu za kulianzisha?

Labda kumtukuza Nyerere kama nabii ndiko kunatufanya tushindwe kuendelea. Kuna haja ya kuufanyia tathimini uongozi wa Nyerere na kuangalia makosa yoote aliyoyaacha na kuyapa kipaumbele ili tuweze kuyaepuka na kujiletea maendeleo, vinginevyo tutabakia nyuma kwa kuendelea kumwona Nyerere kama Mungumtu.

Kuna mzee mmoja mtanzania aliyekuwa akiishi nchini Kenya ambaye kwa sasa ni marehemu, aliwahi kuniambia kwamba yeye aliishi kenya kwa kuukimbia unyerere. Nilipomtaka ealezee zaidi mzee huyo akuwa tayari, lakini nafikiri alikuwa na sababu zake za msingi.

Mtu mmoja aliongoza taifa lenye mamilioni ya watu kwa sera zisizoeleweka kiurahisi kwa vijana wa kizazi hiki, kwa mfano sera za ‘‘zidumu fikra za mwenyekiti”.

Inawezekanaje fikra za mtu mmoja zikadumu kwa taifa zima kama sio udikteta.Sasa kilicholipuka ni kupatia jina la Nyerere kila kitu nchi hii, utasikia uwanja wa ndege wa kimataifa unaitwa Nyerere, karibia kila mkoa una jina la Nyerere nk, je ni nyerere peke yake anayepaswa kuenziwa kati ya wapigania uhuru wa nchii?

Nyerere aling’atuka kwenye urais baada ya ujamaa kushindwa hata kama hilo halisemwi lakini ndio ukweli wenyewe, kama kweli Nyerere alikuwa tayari kuifia nchi hii kwa nini asingekaa madarakani na kusimamia mabadiliko ya kutoka kwenye ujamaa kuelekea ulibelali au ubepari (ukoloni mamboleo?) mbona maamuzi yake yanazidi kututesa mpaka leo? Angalia muungano wa Tanganyika na zanzibar, Mpaka leo bado ni tatizo, alipingana na ujinga, umasikini na maradhi, sasa vitu hivi vimekuwa maradufu.Kwa mawazo ya kijana yeyote wa kizazi kipya, nivigumu kumlinganisha Nyerere na Nkurumah au patrice Rumumba waliokufa vifo vya kutatanisha wakitetea maslahi ya watu wao.

Huyu Nyerere alidumu kutokana kutokuwa kinyume na wakooni mamboleo.
Hivyo basi wanaoendelea kumtukuza huyu jamaa basi wamtukuze kama mtume kama ilivyo kwa Yesu Kristo au mtume Muhammad ambao utukuzwaji wao haunaga maswali, ni kukubali unachoambiwa juu yao na kuamini bila kuuliza swali, ukiuliza basi wewe ni mhasi na si mwenzao.

Basi utaitwa majina ya kafiri, mfuasi wa shetani etc. Kwa Nyerere lazima tuoji sisi kama vijana na sio kukumbatia sifa tu zisizo eleweka na kwa nini tumewasahau wapigania uhuru wetu wengine.

shukrani kwa

Kamala Lutatinisibwa
Mwanafunzi-IFM
0754 771 601
jlkamala@yahoo.com
ijawebonere.blogspot.com

Labels:

Wednesday, August 1, 2007

* Dunia itatikisika, binadamu atasaga meno

Mwisho wa dunia umefika!

* Ishara za manabii zaelekea kutimia

* Uchafuzi wa mazingira nalo ni tatizo

Na Musa Ngarango

MENGI yamesemwa na yanaendelea kusemwa kuhusu tukio la kutisha la siku yenye utata ya kutoweka kwa dunia hii tunamoishi.
Je, ni kweli dunia hii kuna siku itafikia tamati? Misingi yake itavunjwa na tawala za kibinadamu nazo kuangamizwa kabisa?
Bila shaka hayo ni maswali yenye kukanganya sana ambayo kila anayeulizwa hutoa majibu tofauti. Wapo wanaosema dunia hii haina mwisho, ila mwisho ni pale binadamu anapofikwa na mauti, lakini si suala la dunia nzima.
Katika hilo, wanazuoni wa masuala ya kidini wanaikosoa sana dhana hiyo na kwenda mbali zaidi kwa kuiita dhana ya kishetani. Wanazuoni hao wanabainisha na kusema kwamba dunia hii ni lazima ifikie tamati (kiama) ambapo siku hiyo kila binadamu atalipwa kulingana na matendo yake.
“Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shamba asilejee nyuma.” Luka 17: 31. “Na atasema mwanadamu (wakati huo): Oh! Ina nini (leo hii ardhi)?” Qur’aan 99:3 Suratuz zilzal.
Aya hizi zinazopatikana katika vitabu vitakatifu vya imani, Biblia na Kurani, ni miongoni mwa aya ambazo zimebashiri mwisho wa dunia na mara kwa mara hutumiwa na wanazuoni wa kidini kuwa mifano.

Tuitazame dunia na sayari nyingine

Ukiondoa sayari ya Pluto iliyogunduliwa mwaka 1930 na mwanaanga kutoka Marekani, Clyde Tombaugh, ambayo hata hivyo iliondolewa katika mlolongo wa sayari kwa kupigiwa kura na wanasayansi waliokutana mjini Prague, Jamhuri ya Czech mwaka 2006, dunia imebaki kuwa miongoni mwa sayari nane ambazo ni Mercury, Venus, Jupiter, Mars, Saturn, Uranus na Neptune.
Katika mlolongo wa sayari, dunia ni sayari ya tatu kutoka lilipo jua ukiachilia mbali Mercury na Venus, pia ni sayari ya tano kwa ukubwa miongoni mwa sayari zote.
Wanasayansi katika utafiti wao ambao unadaiwa kufanyika miaka ya 1800 hadi 1900 kabla ya Kristo, walibaini kwamba dunia tunayoishi na sayari nyingine zinazolizunguka jua zilikuwa kitu kimoja.
Wanasayansi wanadai kwamba mwanzo wa dunia ulipatikana kwa zaidi ya miaka bilioni tano ambapo mchanganyiko wa madini, gesi na vumbi ulifanya aina fulani ya moshi uliojizungusha kwa kasi ya ajabu kwa muda wa miaka hiyo.
Ingawaje wanasayansi hawabainishi wazi kwamba vitu hivyo yaani madini, gesi na vumbi, vilitokea wapi, wanaendelea kusema kwamba kutokana na kasi hiyo ya kujizungusha, palizuka joto ambalo hatimaye lilisababisha mapande makubwa yaliyosambaratika angani na mapande hayo ndizo hizi sayari, yaani ‘Solar System’ kwa lugha ya kitaalamu.
Dunia, inakadiriwa kuwa na ukubwa wa zaidi ya maili milioni mia tano na kipenyo cha kilometa elfu 12.8
Sayari hiyo inazunguka katika njia yake kwa kasi, inatembea maili 70,000 kwa saa moja, mwendo huo kimahesabu ni sawa na wastani wa maili 1,166 kwa muda wa dakika moja, dunia hukimbia umbali wa maili 19.

Tabaka za ajabu

Wanasayansi wanasema kwamba dunia hii ina tabaka kwazo, kila moja ina umuhimu katika maisha ya binadamu. Wanabainisha tabaka hizo zipo saba ambazo ni Troposphere, Stratosphere, Ionosphere Thermosphere, Ozone layer, Exosphere na Mesosphere.
Katika makala hii nitazielezea baadhi ya tabaka hizo kwa sababu inabainishwa kwamba kila moja inatenda kazi yake katika hali ya kushangaza sana.

Troposphere: Tabaka hili lililobeba kiwango kikubwa cha aina zote za hewa zinazokadiriwa kufikia zaidi ya asilimia 90 liko umbali wa maili 13 kutoka usawa wa ardhi, limebeba asilimia 78 ya hewa ya Nitrogen ambayo husaidia kuzuia baadhi ya sehemu za dunia zisigande unapofika wakati wa usiku ambapo miale ya jua huakisi upande wa pili na kuufanya upande mwingine kukosa joto.
Stratosphere: Tabaka hili ni tofauti na tabaka la awali, lenyewe lina hali nzito ya hewa na hali hiyo huzidi kupanda kadiri unavyoelekea angani. Tabaka hili ndipo kunapopatikana njia za kitaifa na kimataifa za usafiri wote wa wa vyombo vya anga.
Ionosphere: Tabaka hili ndilo lenye hali ya umeme ambayo hutokana kwa nguvu fulani zitokanazo na jua, nguvu hizo zenye mifumo ya kiumeme husaidia utawanyaji wa mawasiliano kupitia satellite za redio, televisheni au mitandao ya simu.
Tabaka hilo ndilo husaidia sauti za vituo vya redio au televisheni kusikika hewani, kwani sauti au picha inaponaswa katika satellite ya angani, nayo hufanya kazi ya utawanyaji katika tabaka hilo.
Kama hiyo haitoshi, katika tabaka hilo ndipo inapopatikana mifumo ya radi ambayo hufanya kazi ya kuyatandaza mawimbi ya kiumeme yanayorundikana na inapotokea hali hiyo, ndipo hata mifumo ya kidunia ya mawasiliano ya redio au televisheni hutetema kwa hali ya mikwaruzo.
Ozone Layer: Tabaka hili ndilo kiungo kati ya miale ya jua na dunia. Hufanya kazi ya kuchuja miale ya jua isiakisi moja kwa moja duniani miale ambayo kama inaruhusiwa iifikie dunia moja kwa moja, itafuta kabisa mifumo ya maisha ya viumbe hai.
Kiwango kikubwa cha miale ya jua kinachohifadhiwa katika tabaka hili, kiasi chake kidogo hubadilishwa na kuwa mifumo umeme ambao ndio hutumika katika tabaka la Ionosphere.
Pia tabaka hilo huifadhi kiwango kikubwa cha hewa chafu ya Carbon dioxide ambayo huzalishwa na binadamu kwa kupumua, mifumo ya sumu itokanayo na silaha, uchafuzi wa mazingira ukiwemo wa moshi mzito utokanao na shughuli za viwanda.
Kama hiyo haitoshi, tabaka hilo pia huzuia mawe yanayotoka katika sayari nyingine yasiifike dunia ambapo mawe hayo husukumwa na upepo mkali unaorindima katika sayari hiyo kisha huunguzwa na moto mkali uliopo eneo hilo ambapo hatimaye hubakia vipande vidogo vya chuma vinavyoanguka kuelekea ardhini.

Dunia kutoweka hivi

Inaonywa kwamba kutoweka kwa dunia kutatokana na hali mbaya ya uchakavu wa tabaka la Ozone linaloendelea kuchakaa kadiri dunia inavyozidi kuzeeka na kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira.
Kama nilivyoeleza awali, kwamba miongoni mwa kazi za tabaka hilo ni kuhifadhi ziada ya hewa chafu inayotoka duniani katika hali mbalimbali kama vile, moshi wa magari, na ule utakao viwandani, kemikali za sumu zinazotoka katika vifaa vya kivita kama vile makombora ya nyuklia na kadhalika.
Inatanabaishwa kwamba kutokana na hali mbaya ya uzalishaji mkubwa wa hali ya hewa chafu unaosambaa duniani na kusafiri mpaka kwenye tabaka hilo shupavu, imefika wakati limeanza kuchakaa.
Hali hiyo mbaya ya uchafuzi wa mazingira ambayo kila kukicha imeendelea kushamiri kwa kasi ya ajabu, italifanya tabaka hilo kushindwa kuhimili na hivyo kuanza kuvujisha mionzi hatari ya jua na kuiruhusu kufika moja kwa moja duniani.
Hali hiyo itasababisha ongezeko la joto duniani na hata kuleta magonjwa ya saratni ya ngozi na damu na kusababisha kupunguza siku za kuishi kwa viumbe hai.
Wanasayansi wanaonya kwamba kama hali ya uchafuzi wa mazingira itaachwa iendelee, italifanya tabaka la Ozone kuharibika kabisa na hapo ndipo tamati ya maisha ya viumbe hai itakapowadia.
Inasemekana kwamba hewa chafu (carbon dioxed) inayohifadhiwa katika tabaka hilo, nayo itapoteza mwelekeo, hali itakayosababisha hewa hiyo kufumuka na kushuka duniani kwa kasi ya ajabu na hatimaye kusambaa baharini na nchi kavu.
Hali hiyo yenye kuogofya itakapojiri, itaharibu mifumo ya anga inayosababisha mvua kunyesha na kwa mantiki hiyo unyeshaji wa mvua utakoma.
Kutokana na mfumuko wa joto, gesi na hewa chafu, kutaifanya ardhi kuungua na kupoteza uhai wake na hatimaye kupata mipasuko na hivyo kuruhusu ujiuji (magma) utokao kwenye mwamba mgumu wenye joto kali la kuunguza kutoka chini ya ardhi na kupanda juu. Hali hiyo itasababisha hewa ya Oxygen kupotea na hivyo kuifanya ardhi ipoteze uhai wake na kupasuka vipande vipande.
Maji ambayo ni mchanganyiko wa hewa ya Hydrogen mbili na Oxygen moja (H2O) ambayo pia ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu, nayo yatapoteza hewa ya Oxygen na hapo ndipo hewa ya Hydrogen itachanganyika na hewa ya carbon dioxed na kusababisha maji kupoteza sura yake ya kawaida na kuwa katika hali ya chembe chembe ndogo na kubwa.
Kuungana kwa hewa ya Carbon dioxed na ile ya Hydrogen na miale mikali ya jua itakayoshuka sambamba na gesi, itazikoleza hewa za Hydrogen na Carbon dioxed ambapo hali hiyo itazusha mlipuko mkubwa wa moto katika maji na hapo ndipo mfumo wa mambo ya kiulimwengu utakapotikiswa na kulipuka, bila shaka kutokana na hali hiyo, maisha ya binadamu na kila kiumbe hai yatafikia kikomo.
Wanazuoni wa kidini wakinukuu maandiko mbalimbali wanasema siku za mwisho wa dunia umri wa kuishi utapungua, dunia itajaa maasi, watu watazaa katika umri mdogo, matukio ya vita yatakuwa mengi, watu watapenda pesa na kadhalika. Je, hayo hayajatimia?
Basi ikiwa ni kweli, bila shaka itakuwa kweli yenye kutisha sana, je, wewe umejiandaa vipi kukabiliana na siku hiyo ngumu?

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mitandao ya sayansi na mashirika ya habari. Mwandishi anapatikana kwa: 0754 28 30 01 E-mail: mussajr@yahoo.co.uk

MWISHO

Friday, July 13, 2007

wabunge wamshangaa mpakanjia

Wabunge wamshangaa Mpakanjia kudai kuibiwa msibani

na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa zamani wa Njombe Kaskazini, Jackson Makwetta, aliyekuwa miongoni mwa wabunge 13 waliohudhuria mazishi ya mbunge mwenzao, Amina Chifupa, amekerwa na hatua ya Mohammed Mpakanjia, kutangaza hadharani kwamba ameibiwa simu yake ya mkononi.
Tangazo la kupotea kwa simu hiyo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Darry Rwegasira, hali iliyolazimu kusitishwa kwa muda shughuli za mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Ihanjo, Tarafa ya Lupembe mkoani Iringa.

“Wananchi wa jimbo langu wamedhalilishwa, sina hakika kama huyu jamaa alikuwa na nia njema nao, kudai kuibiwa simu, wakati mara zote alionekana akiwa pweke,” alisema Makwetta.

Makwetta, alisema Mpakanjia alipaswa kutambua kuwa mahala pale ni msibani na aliyefariki alikuwa mke wake na kwamba si vyema kutoa taarifa hiyo, vinginevyo itaeleweka walioiba ni wakwe zake.

“Ni kama amekuja hapa kutudhalilisha, haiwezekani suala la simu yake binafsi linasimamisha shughuli muhimu, kuna mambo ya msingi kitaifa na kimkoa yalipaswa kuelezwa, lakini tumechukua muda kuelezwa suala la simu,” alisema Makwetta.

Mbali na Makwetta, wabunge wengine walilalamikia kauli nzito iliyotolewa na DC huyo, kwamba watu walioiba simu hiyo si waungwana kutokana na uamuzi wa kumfanyia jambo hilo mfiwa.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wabunge hao walisema kauli ya DC huyo ililenga kuwadhalilisha wananchi waliohudhuria kwenye msiba huo.

Mary Kasembe, Mbunge wa Viti Maalum, alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Mpakanjia kulifikisha kwa DC suala la kuibwa au kupotea simu, lakini baadhi ya watu wakisema yawezekana imedondoka kaburini.

“Kwa ujumla, hatua yake ya kutangaza kwamba ameibiwa simu tena kudai wakati akipokea mwili wa marehemu, tayari kwa maziko ni kukosa uungwana machoni mwa waliohudhuria mazishi hayo pamoja na waombolezaji wengine kutoka karibu kila mkoa nchini,” alisema Kasembe.

Kwa upande wake, Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango, alilalamikia suala hilo na kusema limeonyesha ni kwa kiasi gani Mpakanjia asivyoweza kuthamini maisha ya mtu na mali alizonazo.

“Kweli simu ni muhimu, lakini sisi kama wawakilishi wa Bunge na mheshimiwa Spika, tumeshangazwa kusikia kwamba simu imeibiwa wakati akiwa kaburini, kupokea mwili wa marehemu mbunge mwenzetu,” alisema Malecela.

Aidha, mbunge wa viti maalum, Janeth Massaburi, alisema pamoja na kulalamikia hatua ya Mpakanjia kudai kupoteza simu, alipaswa kutulia na kufikiria umuhimu wa Amina aliyefariki na kupata idadi kubwa ya waombolezaji kuanzia jijini Dar es Salaam, Iringa, Njombe mpaka kijijini Lupembe.

“Nchi nzima inamlilia Amina, inasikitishwa kusikia Mpakanjia akitangaza kuibiwa simu, kuna wabunge wenzetu wameibiwa simu siku ya mkesha wa msiba huu, hawakulalamika kiasi hiki, inakuwaje kama kweli alikuwa akimpenda hakutakiwa kutoa matamshi kama hayo kwa wakati ule,” alisema Massaburi.

Mbunge mwingine Aziza Ally, alisema amesikitishwa kwa kiasi kikubwa kusikia Mpakanjia akiomba msaada wa dola na kulalalamikia kupotea kwa simu yake.

Lakini pia mbunge huyo, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, alisema kuwa hatua ya DC wa Njombe kutoa matamshi mazito bila kuzingatia kama kweli simu imeibiwa ni dalili tosha kwamba aliamua kutaka kuwadhalilisha wananchi wengi waliohudhuria msiba huo.

Amina, alifariki dunia Juni 26 saa 2:45 usiku katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam, akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na homa kali na kuzikwa juzi.

Labels:

Thursday, May 10, 2007

कुली za वानासिअसा wetu

wangwe anapotsha Umma au Kapotoka?

na mobini sarya

SIKU zote nimekuwa nikiamini kuwa Siasa za Nchi yetu ndio zimeathiri
Vibaya ukuaji wa Mendeleo ya Taifa letu , hasa kutokana na kauli za
wanasiasa zinazotolewa bila vina.

hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
akiwa katika Ziara ya kawaida katika Mikoa ya kanda ya Ziwa alifika
Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema na kukagua shughuli mbalimbali za
maendeleo ya wananchi.

akiwa anahutubia wananchi wa jimbo hilo ambalo Mbunge wake ni Samweli
Chitalilo, alisikika akimwambia Chitalilo kuwa anampongeza kwa
kuchaguliwa kwake pamoja na Kelele anazopigiwa na wapinzani wake
haziwezi kumfanya kitu kwani ni sawa na kelele za mlango ambazo Daima
haziwezi kumzuia mwenyenyumba kulala.

Rais aliyasema hayo huku akijuwa kuwa Chitalilo anatuhumiwa kuwa
alighushi Vyeti vya Elimu yake na kuvitumia kugombea nafasi hiyo , jambo
linalotafasiriwa kuwa aliwadanganya wapiga kura wake kwa hiyo ni kosa.

kutokana na Tuhuma hizo aliyekuwa mpinzani wake ndani ya CCM,
Ngotezi amewaongoza wananchi wa Jimbo hilo kumfungulia mashitaka
ambapo kesi hiyo imepangwa kutolewa uamzi wa Kisheria Mwezi huu na
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kama wananchi hao waruhusiwe
kumshitaki kama mtu binafsi.

ndio maana Kikwete aliposema kelele za mlango haziwezi kumzuia
Mwenye nyumba kulala , hiyo kauli alitafsiriwa moja kwa moja kuwa ni
kujaribu kumtetea Chitalilo na kupunguza nguvu ya kesi hiyo hasa
ikizingatiwa jinsi mwendo wa uchunguzi wa tuhuma hizo ulivyoenda na
hadi kufikia hatua wananchi wenyewe wakaamua kumshitaki baada ya
kubaini kuwa CCM ilikuwa inamlinda.

ingawa Mwandishi Msaidizi wa Rais alinukukuliwa akisema kuwa Kikwete
hakumtete huyo mbunge kuhusiana na mashtaka yanayomkabili, isipokuwa
alikuwa anaeleza kelele za uchaguzi mkuu uliokuwa na upinzani mkuu,hii
kauli ya mwandishi wa Rais inaonekana kuwa ni ya kiutashi binafsi, kama
kweli Rais hakumtetea ni Vema Ikulu ingetoa Tamko.

tunasema hivyo kwa kuamini kuwa Jimbo la Buchosa halikuwa na Upinza
mkubwa kama Majimbo mwengine ya Kanda ya Ziwa mbona alipokuwa
Ukerewe hakutoa Kauli hiyo kwenye jimbo ambalo linaupinzani wa
kihistoria wa ndani ya CCM kati ya Getruda Mongella na Spika Mstaafu
Pius Msekwa mbona hakumbia hiyo kauli Mongella? kauli za wanasiasa ni za kupima!

hiyo ni Moja kauli za wanasiasa wa hapa wanapokuwa wanatawaliwa na
Utashi wa kisiasa katika kutoa maamzi ya Umma, lakini inayoonekana
mbaya zaidi kuliko zote ni hii ya Mbunge wa Jimbo la Tarime (CHADEMA)
Chacha Zakayo wangwe.

Wangwe kama anavyofahamika jimboni kwake Rasta Chacha ni miongoni
mwa wanasiasa hapa nchini waliojaa kauli zenye utata wanaodhani kuwa kila siku ni wakati wa
kampeni, hawajui kwamba kuna kipindi cha kuacha siasa na kuhudumia
jamii pasipo itikadi.

Mbunge huyo toka ameingia Bungeni Mwaka 2005 amekuwa akitoa kauli
ambazo baadaye hushidwa kuzithibitisha na kuishia kukanusha madai hayo
mbele ya Spika, miongoni mwa Madai ya hivi karibuni kabisa ni yale
aliyotoa kwenye moja ya kikao cha Bunge Dodoma
kuwa alichaguliwa kwa vitisho huku damu ikimwagwa hasa baada ya
wananchi wake kuapa kumpigia kura madai ambayo ameshindwa
kuyadhibitisha na kubadili kauli.

lakini cha kushangaza baada ya kikao cha Saba cha bunge kuahirishwa,
Wangwe alikutana na waandishi wa Habari kwenye klabu moja huko
Dodoma nakuambia kuwa mimi sikubadili kauli msimamo wangu upo pale pale kuwa watu waliuwa Tarime mlininu kuu vibaya,
wakati akiwaambia hayo waandishi alidhani walikuwa watoto kesho yake
wakaandika habari kuwa Wangwe asema madai yake yapo pale pale
amenukuliwa vibaya.

habari zingine sinadai kuwa baada ya Wangwe kuona habari ile aliwajia juu
wandishi walioandika habari ile akiwambia nilikuwa natania nyie
mmekwenda kuwaandika, kwanza kabisa wananchi wa jimbo la Tarime
sasa wammeanza kumshitukia mbunge wao wanaona kuwa Siasa imezidi
kila wakati yupo kwenye vyombo vya habari.

lakini zaidi ya yote ni hii kauli yenye mweleo mbaya aliyoitoa kwenye
vyombo vya habari wiki iliyopita akidai kuwa Harakati za vyama vya siasa
kutaka kuungana ni shinikizo la Serikali lenye nia ya kuviuwa, huku
akionya kuwa miongoni mwa wenyeviti wa vyama vya upinzani ni
mapandikizi.

Wangwe ambaye ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni hakuishia hapo
aliendelea kumwaga maneno kama mtu aliyeamshwa usingizini pale
aliposema kuwa watu kama James Bantia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ni
maofisa Usalama wa Taifa aliyeuwa Chama cha NCCR- nakumsababisha
(yeye)Wangwe kukihama akiwa Diwani kata ya Tarime mjini .

kwanza ni vema nikasema kuwa Wangwe au Rasta Chacha kama
anavyofahamika ni mbunge wa jimbo langu, Umma usingemtegemea kuwa
angeweza kusema mambo kama hayo, kwa sababu unaweza kumtuhu mtu
lakini sio kumhukumu kama alivyofanya wangwe kwa kuwataja waziwazi
akina James Batia kuwa ni maafisa usalama.

ikiwa ni kweli kuwa James Batia ni Mwanausalama sio Dhambi
kwasababu analinda nchi yake kwani ni wangapi tumewaona hata kwenye
vyombo vya habari mbona tunao lakini hawajawahi kuzuia chombo cha
habari kisifanye kazi yake, mbona wakati mwingine hao maofisa
wamekuwa wakitumika kuleta habari za Ikulu.

leo Wangwe anasema kuwa Muungano wa Vya vingi ni shinikizo la Serikali
amesahau kuwa wakati alipokuwa Diwani wa NCCR -Mageuzi alikuwa
mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Siasa Tarime, muugano uliozaliwa
hasa baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe kupita
Kanda ya Ziwa Mwaka 2002 akihuburi muungano.

ni Rasta Chacha huyu huyu alihamia CHADEMA akitokea NCCR - Mageuzi
akiwa bado Diwani kwa madai kuwa CHADEMA kimeonesha nia njema ya
kuungana na vyama vingine.

Leo anatoa kauli zinazopingana na Mtazamo wake na wa chama chake cha
sasa, bila kujua kuwa anakichafua chama hicho kinachoelezwa kuwa ni cha watu makini tangu kimeanzishwa na kimeongozwa na watu mbali mbali wakistaafu na kuachia wengine bila mapinduzi tafauti na vyama vingine.

lakini Pia madai haya aliyorushia chama cha Wanchi CUF kuwa hakifai kuungana na CHADEMA kwani uongozi wake umejikita katika upande mmoja wa Zanzibar, madai yake ni ya kupuuza na kuchekesha baada ya kulenga kukichafua amejikuta anakichafua cha kwake.

kwanza ni bora ifahamike kuwa mimi sio msemaji wa CUF na wala sio kwa kukitetea CUF lakini ninaandika kwa kutambua kuwa huu sio wakati wakampeni kwamba kunakuharibiana hapa,nikiwa kama mwanahabari ninao wajibu wa kuinua Demokrasia hapa nchini.

lazima tuambiane ukweli kwamba wangwe ni mchanga katika siasa pamoja na kupuuza madai yake apewe ushauri nasaha kama anavyoshauri Spika wake.

wangwe baada ya kuwaita viongozi kadhaa kuwa ni Vibaraka wa Serikali alikishambulia Chama cha CUF kwa kusema kuwa ni chama kilichojikita upande mmoja tu wa nchi na kukifanya kikose sura ya muungano.

"Viongozi wa juu wa CUF wote wanatoka upande mmoja wa muungano hawana hata mbunge mmoja Tanzania Bara wakati CHADEMA tunao 11 wakiwemo watano wa majimbo"Wangwe alisema maneno kama anayeropoka bila kujua akisemacho inaonekana hata viongozi wa vyama hivi hawajui.

Jamani tuwe wakweli kwa hili hivi ninani asiyejua kuwa Uongozi wa juu CHADEMA ni wa upande mmoja wa Bara, Kuanzia Mwenyekiti Freemani Mbowe Kaskazini, Makamu alikuwa DK.Kabouru kutoka Kigoma kaondoka ,katibu mwenezi Philemon Ndesamburo kutoka Kaskazini na Katibu Mkuu Dk,Slaa Kaskazini wote wanatokea upande mmoja wa bara hata wabunge wao wote 11 wanatokea upande mmoja.

wakati CUF kinauongozi uliojikita kila kona, kuanzia mwenyekiti Profesa Lipumba Kanda ya kati,Katibu Mkuu Pemba ,Naibu katibu Mkuu Bukoba mkurugenzi wa Tume ya haki za binadamu na mahusiano ya Umma Zanzibar,Naibu mkurugenzi wa Mhusiano ya Umma anatokea Morogoro hiyo ni sehemu tu fupi.

hata hii kauli ya kudai kuwa Cuf hakina mbunge Bara inamuonyesha jinsi alivyo na upeo mdogo katika siasa, huyu Mbunge kipenzi cha wakazi wa Tarime ndiye mbunge pekee katika Bunge letu anaye ongoza Jimbo na Kata baada ya kuchaguliwa na wananchi pamoja na Diwani wa Kata ya Tarime mjini nafasi zote alizigombea kwa wakati mmoja nakuwashinda wapinzani wake kwa mbali.

anaposema kuwa CUF haina wabunge bara anamanisha nini hajui kuwa zile nafasi tano za viti maalum wanawake CuF ilizigawanya katika pande tano za Tanzania bara na kwamba kila mfuatialiji wa Siasa za hapa nchini anajua kuwa baada ya CCM chama pekee kilichokamilika kinachoweza kupewa Sekali wakati wowote kikaongoza ni CUF tu hajui?kama hajui apewe ushauri

hata hivyo maisha ya wangwe mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara yamejaa utata kutokana na kauli zake, kunawakati alidaiwa kuikimbia nchi miaka ya themanini, ni vema kabla hasogelea vyombo vya habari awe na mtu wa kumpina kauli zake.

www.mobinday.blogspot.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com

Labels:

Wednesday, February 28, 2007

WASADIZI WA JK WAMECHOKA? CHEKI HIYO!

GARI la JK likionekana liko spidi kali kwa ARI,KASI NA NGUVU Mpya huku kondakta wake akiwauliza Abiria kama wanakwenda wao waqnasema yaani Gari ipo kasi halafu watapandeje?

Labels: