Monday, November 8, 2010

VITUKO VYA UCHAGUZI TARIME



Mgombea wa ubunge jimbo la Tarime Mwita Mwakwabe WAITARA akiwa amezirai katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Labels:

Sunday, May 6, 2007

तुवातुमिए मवाकाला कुवापता वाचेज़ाजी BORA


Sport
Tutuwatumie mawakala kupata vipaji vichanga mikoani

Na Mobini sarya


WIKI iliyopita nilieleza jinsi ambavyo Soka la bongo na Afrika Mashariki lisivyoweza kutegemea makocha wa kigeni ili likuwe,kwa kutumia hawa wachezaji tulionao ambao tayari kiwango chao kimekwisha fikia kikomo.

Nilijaribu kuelezea kuwa ni ukweli ulio na uwazi kuwa hapa Afrika Mashariki kuna vipaji vya wacheza Soka lakini njia inayotumika kuwapata ndio mbovu na ndio maana tumeendelea kubaki nyuma kila siku, kwa sasabubu hatuna mfumo mzuri wa kuinua vipaji vichanga.

Ndio maana nashawishika kusema kuwa ukiwaona hata hawa wachezaji wanaong’ara kwa sasa akina Mwakimba , Mkenya ,Odhiambo na wengine katika Soka hili lenye mfumo mbaya,ujue kuwa walizaliwa ni kipaji cha asili na kama wasngezaliwa nchi zinazojua maana ya kipaji cha mpira leo hii wangekuwa wanasoka bora wa Dunia.

Baada ya kutoa mtazamo wangu huo baadhi ya wasomaji walinipa maaoni yao nami naona ni vema nikayawasilisha kwa wadau wa soka kupitia njia ileile, yawasomaji ili waweze kuyafanyia kazi.

Bado narudia kusema kuwa soka letu haliwezi kukuzwa kwa kutegemea makocha wakigeni waje kufundisha hawa wachezaji waliokwisha komaa misuli ili walete ushindi ambao utazipeleka timu zetu mbali.

Kulingana na maoni ya watu wengi Soka letu ikiwemo michezo mingine kama Riadha litategemea na mifumo mipya itakayobuniwa ili kuibua vipaji vichanga kutoka mashambani na mijini ambavyo vimesahaulika hadi pale mchezaji mwenyewe anapofanya jitihada za kuibuka akiwa tayari amekwisha zeeka.

Wadau wa mpira hasa wanaongoza timu kubwa kama yanga na samba Timu zenye mitaji na wafadhili wenye Pesa, baada ya kuanzisha kambi za wa watoto wadogo pia watafute mawakala wa kupita mikoani na kuvumbua vipaji ambavyo vitakuja kuwa nyota wa baadaye.

Leo hii ni vigumu kocha anayefundisha Timu ya Yanga kufahamu kuwa kuna kipaji kipya kipo mtwara au Mpanda inakuwa vigumu kwa sababu hakuna mfumo uliosahihi wa kutafuta vipaji, hadi wamuone akichezea timu ya Polisi au hizi ambazo zinaibukia ligi kuu ambazo uwezo wake kifedha ni mdogo kwa hiyo inakuwa rahisi kuwapora wachezaji bila kelele.

Hakuna mfumo uliobora na imara wa kusaka vipaji vya watoto nakuwaanza kuwapa mazoezi wakiwa wadogo, ambapo anakuwa akijuwa kuwa mpira ni ajira na michezo kama michezo mingine.

Tukianzisha mfumo wa kutumia mawakala kuwatafuta watoto wenye vipaji kila kona ya Tanzania kisha tukawaajili makocha wakigeni kuwafundisha hapo tutakuwa tunajenga soka la baadaye lenye ushindani, ikiwa timu hizi zitafanya hivyo haitatokea wakaanza kunyang’anya wachezaji kipindi cha usajili.

Mfumo bora unaopendekeza ambao unaweza kutumiwa kuboresha soka ni kuwa baada ya mawakala kuwapata wachezaji watawakabidhi kwenye Timu zenye kambi ya vijana baada ya hapo wale wachezaji watafundishwa Soka chini ya kocha wa kigeni.

kwa kuwa wachezaji wengi wenye vipaji vichanga watakuwa wanafunzi itabidi wahamishiwe Shule iliyopo karibu na kambi yao kwa kipindi ambacho watakuwa wanafundishwa Soka baada ya hapo kocha anaweza kuona kuwa miongoni mwa wale vijana wameiva na kwa muda huo Timu husika inaweza kuwapeleka kwenye timu yoyote kwa mkataba akajeza pale kama kumpima kiwango chake.


Baada ya hapo anaweza kuchukuliwa akarudishwa kwenye timu yake baada ya kuwa amekomaa , mfano unaweza ukakuta timu ya Simba inacheza ligi kuu na kanuni za ligi kuu zinazuia machezaji chini ya miaka 15 asishiriki kwa hiyo wanaweza kumwazima timu ambayo inacheza ligi daraja la kwanza ili msimu unaofuata atakuwa na miaka 16 wanaanze kumtumia.

Lakini ili mfumo huu uweze kufanikiwa inahitajika mikakati maalumu , huu mfumo sio mgeni kwani Timu nyingi kama Chealse wanautumia kupata wachezaji wengi kutoka Afrika Magharibi, kwanza wanapeleka mawakala wao kurafuta vipaji vichanga wakishavipata wanakabidhi timu ambazo wanaingia nao mikataba ya kuwatunzia vipaji hivyo chini ya uangalizi maalum wa Kocha hadi anafika mkubwa wanakuja kuvuna walichopanda.

Inakuwa ni ajabu kuona mchezaji aliyeibukia ukubwani bila kufamika historia ya kopaji chake utamuona aking’ang’aniwa na timu hizi kuwa zinazojipata kuwa zinzawafadhili wenye hela, lakini hizo pesa mnazitumiaje ikiwa mnashindwa kuwa na kambi ya vijana wadogo ambao ni hazina ya baadaye.

Serikali imetangaza kuwaajili Kocha atakayevumbua vipaji vichanga, lakini kama kungekuwa na mfumo mzuri leo huyo kocha angekuja kufanya usaili wa kuchagua vijana watakaounda Timu ya Taifa ya Vijana kwa angewakuta vijana hao kwenye Timu kama za Yanga na Simba wapo tele.

Ingawa bado hatujapata programu yake ya kutafuta vipaji inakwendaje , lakini sasa ni kama amepewe kazi mbili kwa wakati mmoja, kwanza atafute vipaji hivyo, kisha awaweke kambini pia achague watakao ingia katika timu ya Taifa ya Vijana ,hapo sasa utaanza kuona Timu za Yanga na Simba zinaanza kunyemelea hao wachezaji.

Sasa ifikie Mahali Timu hizi kongwe zionyeshe mchango wao wa kuinua Soka la Tanzania kwa kutafuta Vipaji kwa mfumo wa kutumia Mawakala kisha wao ndio wawe wanaatoa kwa Timu kama za Kagera Sugar au Polisi Sio kuwa subiri wamepata kisha wao wanakwenda kuwapora hapo ni kudidimiza Soka,

Pia Mikataba bora ya wachezaji itazamwe upya na kuzingatiwa ,timu ziandae utaratibu mzuri wa kumiliki mchezaji huku akiwa na maslahi mazuri sio kumfunga na mikataba njaa akipata timu nyingine anazuiliwa kuhama wakati nyie mnamfanyia njaa tu.

Ikiwa Timu kama Simba itakuwa na Soka la watoto wa Chini ya Miaka 15 nsa kila mwaka iwe inawagawa kwenye timu kama kuwapima lakini wakiwa katika uangalizi maalum wa kocha tunafikili kuwa baada ya muda itaanza kuuza wachezaji kila msimu kwa Timu ambazo zitakuwa zimewapenda nakuweza kujiingizia kipato huku Soka letu likizidi kupaa ,\

Mfano kama katika Msimu mmoja wataweza kufanikiwa kuu za wachezaji 10 ambao wanachipiukia hata mkopo wa Milioni 2 haitakuwa imevuna kitita cha shilingi million 20 na wakati huo ikitarajia kuwa kwa siku za usoni itakuja kuwatumia katika timu zao,

Hiyo ndio njia pekee tutakayoitumia tuweze kuvuka vinginevyo hata huo uwanja wa mpya wa Taifa tutashindwa kuufaidi na matokeo yake utageuka tenga la kubebea magori,kwa hiyo ni vema hata hao viongozi wanakuwa wamekabidhiwa Dhamana ya kuongoza wakwa wabunifu na kueza kuelewa mbinu mbalimbali kama za afrika magharibi ili tuweze kuenenda na Soka la Ushindani.

www.mobinday.blospot.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com.

Labels:

Wednesday, March 7, 2007

Mbowe anaandaliwa kumrithi Kikwete?

Uchaguzi


Mbowe kuandaliwa au anajiandaa kumrithi kikwete ?


Na Mobini Sarya

Kwa miaka ya nyuma kwenye siasa zetu za Afrika Mashariki ilikuwa vigumu kutabili nani ataongoza baada ya kiongozi alieyeko madarakani kusitaafu lakini kwa miaka ya hivi karibuni inakuwa rahisi kufahamu ninani atayeshika dola baada ya aliyeko madarakani kutoka.

Hata kwa wenzetu Kenya kwa sasa bila shaka ukiuliza ninani atakekuwa raisi wa Jamhuri ya Kenya baadala ya Mwai Kibaki atakuambia hata kosa kukuambia ninani.

Hivyo hivyo kwa hapa kwetu Tanzania chaguzi ulipokaribia vyama vya siasa vikaanza kuitisha kura za maoni kutamtafuta mgombea kwa chama tawala watu walianza kusema bila kutafuna maneno kuwa kikwete ndiye atashinda na kweli ikawa hivyo pia ulipoanza uchaguzi mkuu walisema kwamba kikwete atakuwa Raisi na kweli ikawa.

Ndio maana na mimi na uliza kama sio kubashiri kuwa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA anaandaliwa kumrithi kikwete baada ya muda wa serikali ya awamu ya nne kufikia kikomo mwaka 2015 kama sio 2010 ?

Ninazo sababu kadhaa zinazo nifanya nihoji ambazo nafikiri hata msomaji atapaswa achangie kupata changamoto nimeamua kuhoji kwa kulingana na mfululizo wa matukio yanayo mweka Mbowe kwenye kumbukumbu ya historia.

Binafsi mimi simweelewi wapi alipoanzia siasa na sikupenda nianze kutafiti historia yake kwa sababu sielezei maisha yake wala historia yake binafsi, ila naeleza kitu kitakachotokana na masilahi ya taifa na kubadili kabisa siasa za Taifa hapo badae na Afrika nzima.

Kwa wale wanaomfahamu wanasema Mbowe kama walivyo viongozi wa vyama vingi alikuwa CCM akiwa kijana na kada wa chama alitaka atumie nafasi yake kutumikia wananchi kama Mbunge ingawa aliongoza kwenye kura za maoni lakini alienguliwa na akatangazwa aliyekuwa ameshindwa.

Kitendo hicho kilimfanya atafute chama makini ahamie ili aweze kupata nafasi ya kutumikia wananchi wa jimbo lake bila shaka chaguo lake lilikuwa Chadema na kweli alipogombea akashinda akawa mbunge wa jimbo la Hai kwa vipindi viwili mfululizo hadi alipoacha mwenyewe.

Ingawa aliacha akitaka kugombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini wananchi wake walimfuata wakitaka aendelee kugombea ubunge kwani bila yeye Jimbo litarudi mikononi mwa CCM na kweli ndivyo matokeo yalivyokuwa.

Kwani Mbowe alibaki na msimamo wake ule wa awali wa kugombea urais nafasi ambayo sasa ilimtambulisha nchi nzima na kupata umarufu wa ghafla na kutishia wanasiasa wenzake kutoka vyama mbalimbali vya siasa kikiwemo chama tawala hadi ikafikia wakati wakamvumishia kwamba amerejea CCM ilikuwavunja nguvu wafuasi wake.

Hatua ya kutumia usafiri wa anga kupiga kampeni nchi nzima ilikuwa ni hatua nyingine ya kuwatia wasiwasi mkubwa sio wapinzani wake tu hata wachunguzi wa masuala ya siasa walifikia hatua wakashindwa kufahamu ninani atakuwa wapili baada ya Kikwete na idadi ya kura atakazopata.

Kwani aliweza kwenda hadi vijijini ambako wagoimbea wengine hawakuweza kufika na kuteka makundi mbalimbali kwenye mikutano yake ya kampeni na kuzidi kuwachanganya wengi pale alipokuwa anafika kwenye jimbo ambalo mgombea ubunge kutoka chama cha upinzani ananguvu na kuamua kunadi.

Hatua hiyo ya kishujaa ambayo nilisifiwa na wasomi mbalimbali na kusema anaonyesha ukomavu wa kisiasa aliifikia kwa lengo la kuongeza idadi ya wabunge kutoka kambi ya upinzani Bungeni bila kujali itikadi.

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa alishika nafasi ya tatu lakini alishangaza watu akiwa mpinzani alipojitokeza na katika tume ya uchaguzi kisha kumkumbatia mgombea wa CCMaliyekuwa ameshinda.

Hali iliyoacha maswali mengi mitaani na kuweka histori toka uchaguzi wa vyama vingi uanze mwaka 1995 ni vigumu ilikuwa ndoto mpinzani kukaa mezani moja hasa kipindi cha uchaguzi kwani maneno yasingeisha kusema kwamba ni wakala wa CCM ameletwa ili auwe upinzani.

Pamoja na shutuma lakini pia wanasiasa nchi nyingi za Afrika hawariziki na matokeo ya uchaguzi yanapotangazwa na ukakuta aliyeshinda anatoka chama tawala kwa hiyo kitendo cha Mbowe kumkumbatia Kikwete kiliacha maswali mengi.

Wengine wakihoji na kumpongeza kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa unaoelekea kubadili mfumo wa siasa ya nchi yetu na kuleta umoja na kusahau uhasama lakini wakosoaji wake walibaki wakisema anaoonekana kutaka kujionyesha kwa kikwete ili apewe madaraka.s

Labels: