Sunday, May 6, 2007

तुवातुमिए मवाकाला कुवापता वाचेज़ाजी BORA


Sport
Tutuwatumie mawakala kupata vipaji vichanga mikoani

Na Mobini sarya


WIKI iliyopita nilieleza jinsi ambavyo Soka la bongo na Afrika Mashariki lisivyoweza kutegemea makocha wa kigeni ili likuwe,kwa kutumia hawa wachezaji tulionao ambao tayari kiwango chao kimekwisha fikia kikomo.

Nilijaribu kuelezea kuwa ni ukweli ulio na uwazi kuwa hapa Afrika Mashariki kuna vipaji vya wacheza Soka lakini njia inayotumika kuwapata ndio mbovu na ndio maana tumeendelea kubaki nyuma kila siku, kwa sasabubu hatuna mfumo mzuri wa kuinua vipaji vichanga.

Ndio maana nashawishika kusema kuwa ukiwaona hata hawa wachezaji wanaong’ara kwa sasa akina Mwakimba , Mkenya ,Odhiambo na wengine katika Soka hili lenye mfumo mbaya,ujue kuwa walizaliwa ni kipaji cha asili na kama wasngezaliwa nchi zinazojua maana ya kipaji cha mpira leo hii wangekuwa wanasoka bora wa Dunia.

Baada ya kutoa mtazamo wangu huo baadhi ya wasomaji walinipa maaoni yao nami naona ni vema nikayawasilisha kwa wadau wa soka kupitia njia ileile, yawasomaji ili waweze kuyafanyia kazi.

Bado narudia kusema kuwa soka letu haliwezi kukuzwa kwa kutegemea makocha wakigeni waje kufundisha hawa wachezaji waliokwisha komaa misuli ili walete ushindi ambao utazipeleka timu zetu mbali.

Kulingana na maoni ya watu wengi Soka letu ikiwemo michezo mingine kama Riadha litategemea na mifumo mipya itakayobuniwa ili kuibua vipaji vichanga kutoka mashambani na mijini ambavyo vimesahaulika hadi pale mchezaji mwenyewe anapofanya jitihada za kuibuka akiwa tayari amekwisha zeeka.

Wadau wa mpira hasa wanaongoza timu kubwa kama yanga na samba Timu zenye mitaji na wafadhili wenye Pesa, baada ya kuanzisha kambi za wa watoto wadogo pia watafute mawakala wa kupita mikoani na kuvumbua vipaji ambavyo vitakuja kuwa nyota wa baadaye.

Leo hii ni vigumu kocha anayefundisha Timu ya Yanga kufahamu kuwa kuna kipaji kipya kipo mtwara au Mpanda inakuwa vigumu kwa sababu hakuna mfumo uliosahihi wa kutafuta vipaji, hadi wamuone akichezea timu ya Polisi au hizi ambazo zinaibukia ligi kuu ambazo uwezo wake kifedha ni mdogo kwa hiyo inakuwa rahisi kuwapora wachezaji bila kelele.

Hakuna mfumo uliobora na imara wa kusaka vipaji vya watoto nakuwaanza kuwapa mazoezi wakiwa wadogo, ambapo anakuwa akijuwa kuwa mpira ni ajira na michezo kama michezo mingine.

Tukianzisha mfumo wa kutumia mawakala kuwatafuta watoto wenye vipaji kila kona ya Tanzania kisha tukawaajili makocha wakigeni kuwafundisha hapo tutakuwa tunajenga soka la baadaye lenye ushindani, ikiwa timu hizi zitafanya hivyo haitatokea wakaanza kunyang’anya wachezaji kipindi cha usajili.

Mfumo bora unaopendekeza ambao unaweza kutumiwa kuboresha soka ni kuwa baada ya mawakala kuwapata wachezaji watawakabidhi kwenye Timu zenye kambi ya vijana baada ya hapo wale wachezaji watafundishwa Soka chini ya kocha wa kigeni.

kwa kuwa wachezaji wengi wenye vipaji vichanga watakuwa wanafunzi itabidi wahamishiwe Shule iliyopo karibu na kambi yao kwa kipindi ambacho watakuwa wanafundishwa Soka baada ya hapo kocha anaweza kuona kuwa miongoni mwa wale vijana wameiva na kwa muda huo Timu husika inaweza kuwapeleka kwenye timu yoyote kwa mkataba akajeza pale kama kumpima kiwango chake.


Baada ya hapo anaweza kuchukuliwa akarudishwa kwenye timu yake baada ya kuwa amekomaa , mfano unaweza ukakuta timu ya Simba inacheza ligi kuu na kanuni za ligi kuu zinazuia machezaji chini ya miaka 15 asishiriki kwa hiyo wanaweza kumwazima timu ambayo inacheza ligi daraja la kwanza ili msimu unaofuata atakuwa na miaka 16 wanaanze kumtumia.

Lakini ili mfumo huu uweze kufanikiwa inahitajika mikakati maalumu , huu mfumo sio mgeni kwani Timu nyingi kama Chealse wanautumia kupata wachezaji wengi kutoka Afrika Magharibi, kwanza wanapeleka mawakala wao kurafuta vipaji vichanga wakishavipata wanakabidhi timu ambazo wanaingia nao mikataba ya kuwatunzia vipaji hivyo chini ya uangalizi maalum wa Kocha hadi anafika mkubwa wanakuja kuvuna walichopanda.

Inakuwa ni ajabu kuona mchezaji aliyeibukia ukubwani bila kufamika historia ya kopaji chake utamuona aking’ang’aniwa na timu hizi kuwa zinazojipata kuwa zinzawafadhili wenye hela, lakini hizo pesa mnazitumiaje ikiwa mnashindwa kuwa na kambi ya vijana wadogo ambao ni hazina ya baadaye.

Serikali imetangaza kuwaajili Kocha atakayevumbua vipaji vichanga, lakini kama kungekuwa na mfumo mzuri leo huyo kocha angekuja kufanya usaili wa kuchagua vijana watakaounda Timu ya Taifa ya Vijana kwa angewakuta vijana hao kwenye Timu kama za Yanga na Simba wapo tele.

Ingawa bado hatujapata programu yake ya kutafuta vipaji inakwendaje , lakini sasa ni kama amepewe kazi mbili kwa wakati mmoja, kwanza atafute vipaji hivyo, kisha awaweke kambini pia achague watakao ingia katika timu ya Taifa ya Vijana ,hapo sasa utaanza kuona Timu za Yanga na Simba zinaanza kunyemelea hao wachezaji.

Sasa ifikie Mahali Timu hizi kongwe zionyeshe mchango wao wa kuinua Soka la Tanzania kwa kutafuta Vipaji kwa mfumo wa kutumia Mawakala kisha wao ndio wawe wanaatoa kwa Timu kama za Kagera Sugar au Polisi Sio kuwa subiri wamepata kisha wao wanakwenda kuwapora hapo ni kudidimiza Soka,

Pia Mikataba bora ya wachezaji itazamwe upya na kuzingatiwa ,timu ziandae utaratibu mzuri wa kumiliki mchezaji huku akiwa na maslahi mazuri sio kumfunga na mikataba njaa akipata timu nyingine anazuiliwa kuhama wakati nyie mnamfanyia njaa tu.

Ikiwa Timu kama Simba itakuwa na Soka la watoto wa Chini ya Miaka 15 nsa kila mwaka iwe inawagawa kwenye timu kama kuwapima lakini wakiwa katika uangalizi maalum wa kocha tunafikili kuwa baada ya muda itaanza kuuza wachezaji kila msimu kwa Timu ambazo zitakuwa zimewapenda nakuweza kujiingizia kipato huku Soka letu likizidi kupaa ,\

Mfano kama katika Msimu mmoja wataweza kufanikiwa kuu za wachezaji 10 ambao wanachipiukia hata mkopo wa Milioni 2 haitakuwa imevuna kitita cha shilingi million 20 na wakati huo ikitarajia kuwa kwa siku za usoni itakuja kuwatumia katika timu zao,

Hiyo ndio njia pekee tutakayoitumia tuweze kuvuka vinginevyo hata huo uwanja wa mpya wa Taifa tutashindwa kuufaidi na matokeo yake utageuka tenga la kubebea magori,kwa hiyo ni vema hata hao viongozi wanakuwa wamekabidhiwa Dhamana ya kuongoza wakwa wabunifu na kueza kuelewa mbinu mbalimbali kama za afrika magharibi ili tuweze kuenenda na Soka la Ushindani.

www.mobinday.blospot.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home