वानोशाबिकिया Serikali kuonya Magazeti वोंय्वा ना मिस-TAN
Na mwandishi wetu
TAASISI ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN), imesema kuwa haikubaliani na onyo kali lililotolewa hivi karibuni na serikali kwa magazeti ya Tanzania Daima na MwanaHALISI.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa MISA-TAN, Ayub Rioba, aliita hatua hiyo ya serikali kuwa ni ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari.
Akizungumza kuhusu Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, inayoadhimishwa leo, Rioba alisema kuwa ni makosa kwa serikali kutishia vyombo vya habari
“Kama kweli tumeanza kwenda sehemu kama hii ya kutokubali kukosolewa, kama serikali haitavumilia kukosolewa, nawaambia tunaenda pabaya.
“Haiwezekani vyombo vya habari peke yake vikaonekana vinafanya vibaya, mbona kuna mambo mengi yanafanyika mitaani tena mabaya zaidi... kuna mikataba mingi mibovu haiko wazi kama ya Richmond, rada… hatuambiwi, nawaambia kama vyombo vya habari vinanyamazishwa hatutaendelea,” alisema huku akionyesha kusikitishwa na hatua hiyo ya serikali.
Alizngumzia hali ya upashanaji habari ambayo ilianzishwa na Rais mstaafu wa awamu wa pili, Ali Hassan Mwinyi, miaka zaidi ya 20 iliyopita na kusema kuwa hiyo ilikuwa ni hatua nzuri katika kuleta maendeleo.
“Rais Kikwete mwenyewe wakati anaingia madarakani alisisitiza kuendeleza ‘spirit’ ya Rais Mkapa kuhakikisha wanaendeleza upashanaji wa habari, lakini mambo yanakuwa tofauti… huu ni ukandamizaji.
“Hatuwezi kufagilia mazuri kila siku wakati mabaya tunayaona, zipo ‘literature’ nyingi zinaeleza hali halisi, kuna nini kwenye magazeti wakati hata hali hiyo ambayo hawataki kuambiwa ukweli imo kwenye hizo literature,” alisema.
Aidha, Rioba, ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema anafundisha somo la maadili, lakini hajaona katika maandishi ya magazeti hayo kitu kinachoelezwa kuwa ni lugha za matusi.
Alisema nchi ambazo zimeendelea na pia hali yao ya uchumi iko juu, zimeruhusu uhuru wa vyombo vya habari na wanakubali kukosolewa na kutoa mfano wa nchi hizo kuwa ni pamoja na Botswana.
Hata hivyo, alionyesha kukerwa na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo amedai vimekuwa vinavishambulia vyombo vya habari vingine.
“Tunaanza kusemana wenyewe kwa wenyewe… leo hii mimi linanigusa sana hili, tutachekwa… mimi nilifikiri tungetumia muda huo kuwasema wala rushwa!
“Mkikubali kugawanyika kwa sababu tu kuna mtu anawatumia kwa kuendeleza rushwa na kusainiana mikataba mibovu… baada ya kuwa ‘serious’ tuwasaidie Watanzania maskini tunakaa na kucheza ngoma za watu,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa wao kama MISA-TAN hawajakaa na kutoa kauli ya kiofisi, lakini kama mwelekeo wao unavyosema, hawakubaliani na serikali na huo ndio msimamo wao katika kutetea vyombo vya habari.
Akizungumzia kuhusu Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Rioba alisema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanatathmini matatizo ya kiusalama yanayowakabili waandishi, wahariri na wachapishaji ambao wanajitolea maisha yao katika kuhakikisha kuwa wanawapatia wananchi taarifa muhimu ili waweze kushiriki kikamilifu katika jitihada za kujiletea maendeleo.
Akizungumzia hali ya usalama kwa waandishi wa hapa nchini, alisema pamoja na kutishiwa mara nyingi, Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika masuala ya kiusalama na hakuna waandishi wanaouawa ukilinganisha na nchi nyingine.
Alisema kulingana na takwimu za mwaka jana za UNESCO, zaidi ya waandishi wa habari, wakiwemo wafanyakazi wa vyombo vya habari 150 waliuawa, mamia ya wafanyakazi wa vyombo vya habari walikamatwa, kutishiwa au kushambuliwa na hivyo kufanya mwaka huo kuwa mbaya zaidi kwa waandishi wa habari.
Naye Mkurugenzi wa MISA-TAN, Rose Haji, alisema kuwa maadhimisho ya siku hiyo yanafanyika leo katika Hoteli ya Peacock, ambako yatazinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib.
mwisho
Wanaodaiwa kumuua askari, mhasibu MeTL kizimbani
WATU watano wanaodaiwa kuwa vinara wa tukio la mauaji ya askari mmoja na mhasibu wa Kampuni ya Mohammed Enterprises (T) Ltd (MeTL), lililotokea katika eneo la Kiwalani, Dar es Salaam mwishoni mwa mwaka jana, wamefikishwa mahakamani.
Watuhumiwa hao waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ni mfanyabiashara, Ibrahimu Yusuph (41), Simba Simba (31) dereva, Ally Kilongozi (51) anayefahamika kwa jina la Ngosha ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Security.
Wengine ni Rajabu Mohamed (66) mkulima na mfanyabiashara pamoja na Hamis Ally (34).
Mbele ya Hakimu Mkazi, Pelagia Khaday, Mwendesha Mashitaka, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyella, akisaidiana na Inspekta Maximilian Birigi, walidai washitakiwa walitenda kosa hilo Desemba 16 mwaka jana majira saa 3:45 asubuhi, eneo la Kiwalani, jijini Dar es Salaam.
Washitakiwa hao wanatuhumiwa kumuua askari polisi mwenye namba F7091 PC Gordwin Mkumbo na Mhasibu wa Kampuni ya Mohamhed Enterprises, Aliasger Sagrrid.
Kutokana na kutokamilika kwa upelelezi wa kesi hiyo, Kenyella aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha na kuipangia tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 15, mwaka huu. Watuhumiwa ambao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi za mauaji, walirudishwa rumande.
mwisho.
Mahakama Sumbawanga yacharuka
*Watatu wafungwa miaka 90
Na mwandishi wetu, Sumbawanga
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Rukwa, imemhukumu Emmanuel Sumuni (20), mkazi wa Kijiji cha Malolwa, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi
Mwandamizi, Obediodom Chanjarika, wakati mtuhumiwa hayupo mahakamani. Mtuhumiwa huyo alitoroka baada ya kuwekewa dhamana ya sh 300,000, alipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Julai 12, mwaka juzi.
Awali, ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi, Cleophace Mpinge, kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 10, 2005 majira ya saa 4 asubuhi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa alimvizia na kumkamata binti huyo wakati anatoka kuchota maji na kisha kumvuta pembenei ya njia kabla ya kumbaka.
Upande huo wa mashitaka uliita mashahidi wanne ambao waliithibitishia mahakama hiyo kuwa, mtuhumia huyo alitenda kosa hilo na kuufanya upande wa mashitaka uiombe mahakama itoe adhabu kali.
Katika kesi nyingine, mahakama hiyo iliwahukumu Peter Mwambala (19) pamoja na Krifu Kapala (19) wote wakazi wa Kitongoji cha Bangwe katika Manispaa ya Sumbawanga kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 60 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mpinge alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Liyad Chamshama kuwa, washitakiwa hao, kwa pamoja, wakiwa na silaha aina ya panga, walitenda kosa hilo Novemba 14, mwaka jana majira ya saa 3 usiku katika eneo la Katandala ndani ya Manispaa ya Sumbawanga.
Ilidaiwa kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kumnyang’anya Rigorbert Ndegeulaya simu ya mkononi yenye thamani ya sh 30,000 pamoja na fedha taslimu sh 35,000.
Hata hivyo, watuhumiwa walikamatwa muda mfupi baadaye wakiwa wamejificha kandokando ya barabara ya Msakila.
Akijitetea kabla ya kuhukumiwa, Mwambala aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kuwa yeye ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI.
Kwa upande wake, Kapala yeye hakuwa na utetezi wowote ule na aliridhika na adhabu hiyo iliyotolewa na mahakama na ndipo hakimu alipowahukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 kila mmoja.
Mwisho

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home