Tuesday, September 11, 2007

MSANII Jhiko Manyika 'Jhiko Man'

Na Mkolo Kimenya

MSANII Jhiko Manyika 'Jhiko Man', amemaliza ziara yake katika nchi za Ulaya kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kuuza kazi zake ikiwa ni pamoja na albamu yake mpya ya Chikondi ambayo nyimbo zake zinatamba katika vituo mbalimbali vya redio nchini.

Akizungumza na Tanzania Daima, Dar es Salaam juzi, msanii huyo wa muziki wa Afro Reggae, alisema kuwa amefanya maonyesho kadhaa katika nchi za Finland, Danmark na Spain ambako pia ametumia fursa hiyo kukamilisha albu zake mbili ambazo atazizindua baadae mwaka huu.

Manyika alisema kutokana na kazi yake ya Chikondi kuwa sokoni hivi sasa ameamua kusambaza nyimbo mbili ambazo ni Kuagana na Tupendane ambao unabeba jina la albamu yake hiyo mpya ambayo anatarajia kuizindua baadae mwakani.

Alisema albamu yake hiyo ina nyimbo 10 na ameitayarisha katika nchi tofauti kwa kushirikiana na prodyuza Mikko Rossi na bendi nzima ya Suminators ya nchini Spain.

Alisema kuwa licha ya Catherine Mponda pia amemshirikisha kaka wa msichana huyo aitwae Menard Mponda ambaye anaishi nchini humo "huyu bwana amekua na msaada mkubwa katika kukamilisha albamu hiyo" anasema na kuongeza kuwa watu watarajie mambo makubwa zaidi.

Msanii huyo ambaye ana historia ndefu katika muziki wa Reggae nchini, alisema kwa hapa nchini anaisambaza albamu yake kwa kutumia kampuni yake binafsi ya muziki na mazungumzo yanaendelea baina yake na wasambazaji wengine.

mwisho..........

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home