: utamaduni wetu
Shindano la Utamaduni wa Mtanzania
1.tangulizi:
Mila na desturi ni dhana zinazomtambulisha mtu awapo pamoja
na watu wengine.
Ni muhimu kuziheshimu na kuzienzi, hata hivyo wakati inapobidi,
baadhi ya mila inapasa zichunguzwe na kurekebishwa hasa pale
mila hizo zinapoleta madhara kwa jamii moja kwa moja au kwa
kupitia kwa viumbe vingine.
Japo twapaswa kuzipiga vita mila zenye madhara, inatupasa
kuwa makini hasa tunapozungumza tukiwa nje ya afrika.
Watu wa nchi za magharibi, wamekuwa na mtazamo hasi sana
juu ya bara la Afrika, hivyo kudharau mila na desturi za waafrika
pasipokujua mila hizo ni kiungo kikubwa kwa jamii za waafrika
na kwamba kwa namna moja au nyingine zina umuhimu wake
katika jamii.
Wazo langu la msingi hapa ni kwamba japo mila fulani
zimeonekana kuwa na madhara kwa binadamu,
tunapozizungumza tunapaswa kuwa makini sana tukijaribu kwa
kila njia kuepuka kudhalilisha au kutukana utamaduni wa nchi
yetu na asili yetu kwa ujumla.
Ni muhimu kupiga vita mila potofu, lakini namna tunavyolijadili
suala zima, ina madhara au manufaa makubwa sana kwa uelewa
wa watu kuhusu nchi yetu.
KUMBUKA WAHENGA WALISEMA MDHARAU VYA KWAO NI
MTUMWA.
Kampuni ya Mobinday Tanzania Culture, Beauty and Promotion,
iliyosajiliwa kihalali kwa Msajili wa Makampuni (BRELA),
imeanzisha shindano la kitaifa linalojukana kama 'shindano la kumtafuta Malkia wa
Utamaduni wa Taifa'.
Shindano hilo litakuwa likianzia kwenye ngazi za mitaa
(vitongojini), kwa kuwashindanisha warembo wa kabila moja.
Mrembo atakayeibuka mshindi kwa kuonyesha uelewa wa
kulitangaza kabila lake vizuri nje, hasa katika mila na utamaduni,
ndiye atakayekwenda ngazi ya jimbo (wilaya). Hapo ndipo
kinyang’anyiro cha kuhusisha kabila na kabila kitakapoanza.
Wakati huo mashindano hayo yatakuwa yanasimamiwa na
mawakala watakaokuwa wamepewa kibali maalumu na kampuni
ya Mobinday inayoandaa shindano la kitaifa.
Kila shindano la kuanzia ngazi ya chini kabisa, litakuwa
linachukua mshindi kutoka wa kwanza hadi wa tatu.
Hawa watakuwa wanashiriki ngazi inayofuata hadi ngazi ya
kanda.
Ni vizuri kila kabila likawa na angalau mmoja atakayeshiriki
mashindano ya wilaya au mkoa. (Wakala kwa kushirikiana na
afisa utamaduni watakuwa na wajibu wa kuchagua waamuzi wa
shindano).
Shindano ni utaratibu wa kufanya jambo lenye ushindani wa
shughuli nyingi kwa pamoja au zinazofuatana kwa karibu.
Shughuli hizo zinaweza kuwa za aina moja au fani moja peke
yake, kama vile kuonyesha mavazi ya kubuni/asili, ngoma na
sanaa za ufundi au michezo.
pia Shindano linaweza kuwa la mchanganyiko wa fani mbili au
zaidi kwa pamoja.
washiriki – watendaji na watazamaji -hukutana katika eneo moja
lililopangwa kwa ajili ya Onyesho, katika muda wa shindano
zima.
Inasisitizwa kuwa fani zinazoshirikishwa katika shindano ziwe
zenye ubora wa asili na kila inapowezekana baadhi yake zitokane
na wabunifu au mapendekezo ya wahakiki na wahifadhi mahiri
na maarufu katika jamii au kabila husika.
Aidha utaratibu wa mashindano huweza kuandaliwa katika
sehemu na ngazi mbalimbali ili kupata fani bora za kushirikishwa
katika shindano la utamaduni.
2.0 Madhumuni ya shindano: Kwa mujibu wa dhana na
mpangilio wa shughuli, shindano huwa na mvuto wa hali ya juu
na kishindo kikubwa katika jamii. Kwa sababu hiyo shindano
linasaidia sana katika:-
2.1 Utambulisho: Utambulisho ni kitu muhimu kwa binadamu.
Wakati wote binadamu hufanya jitihada ya kujitambua yeye
mwenyewe na kubainisha wenzake.
Utamaduni ni moja ya nguzo muhimu za utambulisho wa mtu.
Shindano hutoa fursa kwa mtu binafsi na jamii kwa jumla kujua
na kukumbuka wao ni nani – kama jamii, kama taifa – na
kuendelea kuishi au kufanya mambo kwa kuzingatia jamii au
taifa lake. Kwa upande mmoja
2.Mtu hujiona kuwa mwenye fahari, heshima na nguvu. Kwa
upande mwingine utambulisho huu huwa chanzo cha kuheshimu
na kuzingatia misingi ya jamii au taifa ya maadili, itikadi,
mahusiano ya kiuchumi, kisiasa na tabia njema ya makabila .
2.2 Mshikamano: Mshikamano katika jamii hutokana na jamii
husika kuwa na kitambulisho na dhamira moja.
Shindano huwa ni kielelezo kizuri cha utamaduni na huipa jamii
ari,Utambulisho katika nafsi zao ya kuendelea kuwa na
mshikamano, umoja na ushirikiano na maelewano miongoni
mwao.
2.3 Sauti na Usawa : Katika nchi nyingi ipo hali ya baadhi ya
jamii (Kabila) kujihisi wanyonge,kudharauliwa au kudhalilishwa.
Katika hali hii usawa baina ya wananchi huwa haupo.
kushiriki kwa kabila katika shindano hili huwajengea heshima na
kujiamini mbele ya wenzao na kwa hiyo dhana ya Sauti na usawa
huendelea kuimarika.
2.4 Ushindani: Ushindani ni chachu muhimu ya maendeleo.
Washiriki katika shindano lolote huwa na nia ya kufanya vizuri.
Hali hii huamsha vipaji vya wabunifu na watunzi wa fani za
utamaduni na kuwezesha maendeleo makubwa ya fani hizo.
2.5Uzoefu wa Lugha na Ubunifu:Shindano ni mahali ambapo vitu
vingi Vitaonyeshwa, kuzungumzwa au kutolewa maandishi. Hivi
vyote huwa na fursa nzuri kwa watunzi,wabunifu, wanataaluma,
wanafunzi na wananchi kwa jumla kupata uzoefu na elimu zaidi
katika mambo ya utamaduni.
32.6 Urithishaji: Shindano hushirikisha mchanganyiko wa
mabinti wa umri wa rika ya miaka 15-25,ambao huonyesha
uzoefu wa mila na ujuzi mbalimbali wa utamaduni wao.
Kwa hiyo shindano huwa ni fursa ya wazee kuweza kurithisha
mambo muhimu ya taifa kwa vizazi vipya. Aidha shindano
huhamasisha shughuli za ufufuaji na uendelezaji wa urithi wa
utamaduni unaoshikika na usioshikika.
2.7 Ushabiki wa kitaifa: Kutokana na wingi na uzuri wa
mambo/vitu vinavyoonyeshwa katika hili shindano, ushabiki na
upenzi mkubwa kwa taifa huweza kuibuka miongoni mwa
makabila.
Tofauti zao za historia, maeneo au uhusiano huziweka kando.
2.8 Biashara na Uchumi: Kutokana na mambo au vitu vingi vizuri
kuonyeshwa katika shindano, wadau na wafanya biashara wengi
wa kazi za utamaduni huweza kuhudhuria na kubaini mwelekeo
wa biashara au shughuli zao.
Aidha sehemu ambayo shindano litafanyika kutakuwa na fursa
kubwa ya kupanua biashara kwa bidhaa mbalimbali za sehemu
hiyo kama vile vyakula na malazi.
2.9 Burudani: Binadamu ni kiumbe ambaye huwa na hamu ya
kuburudika ikiwa ni njia ya kujenga nguvu na ari zaidi katika kazi.
Kwa hiyo shindano hukidhi hamu ya wananchi ya burudani kwa
kiwango cha juu na manufaa makubwa.
43.0 Hali ya shindano:
MOBINDAY Tanzania Culture, Beauty and Promotion ni
kampuni iliyodhamiria kurejesha heshima ya Tanzania kwa
kuandaa Shindano la utamaduni litakalokuwa linatambulisha
hadhi na utamaduni wa kila kabila.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo atawachagua wajumbe watano watakaounda Body ya kusimamia na kuendesha shughuli zote za shindano.
Bodi hiyo itakuwa na kazi ya kuwatafuta waamuzi wenye sifa zitakazopendekezwa, na kuteuwa wajumbe wa kamati ndogo ya kuratibu shughuli zote za shindano.
Shindano la Kumtafuta Malkia wa Utamadauni wa Taifa ,
litakuwa likifanyika kila mwaka na kutanguliwa na mashindano
madogo madogo kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini
katika ngazi za kijiji,tarafa hadi kanda.
Shindano hilo litakaloanza rasmi mwaka huu, limetayarishwa
kwa lengo la kuulinda na kuuenzi utamaduni wetu na wa
Mwafrika kwa ujumla, kwani tunaamini kuwa utamaduni wetu ni
bora na muhimu kuliko wa mataifa mengine.
3.1Shindano hili limeanzishwa na Mzalendo Mobini (2008) ,
litakuwa linaendeshwa na kampuni ya kibinafsi ya Tanzania
Culture Beaty Co.likiwa na malengo kama yalivyoelezwa hapo
mwanzo.
litaanza kwa washiriki wasiodhidi 26 kutoka makabila
mbalimbali ya hapa nchini lakini kila Mwaka watakuwa
wanaongezeka kadri itakavyowezekana hadi kufikia washiriki
wakatoka nje ya nchi.
Shughuli zinazoendeshwa katika tamasha hilo ni:
(a)Sanaa za jukwaani za ngoma, muziki na sarakasi. (b)Sanaa za
Ufundi, uchongaji, ufinyanzi, ususi, ufumaji, mavazi.
3.2 . Lengo lake kuu ni kuonyesha fani mbalimbali za Utamaduni
wa mtanzania. Hata hivyo baadaye linatarajiwa kuwa na
washiriki ambao watatoka nje ya Tanzania .
Shindano hili litakuwa linafanyika kila mwaka nakuwahusisha
washiriki kutoka makabila mbalimbali watakaokuwa
wanaonyesha mila na desturi za makabila yao.
4.1 Ngazi ya shindano hili kitaifa itazidi kupanuka ili liwe na
hadhi ya kimataifa.
Pia mashindano madogo yanaweza kuwa mahali pa kuchagulia
washiriki wa shindano la taifa.
4.2. Kiwango cha washiriki katika shindano hili kwa kuanza
kitakuwa kidogo kulingana wingi wa makabila ,
malengo,madhumuni na mtandao wake kijiografia hadi pale .
Shindano hili la Taifa ni la Watanzania wote. Hata kama nafasi za
kushiriki haziwezi kuwaenea wote, kila mmoja atakuwa na hakiya
kushindania nafazi hizo.
4.3 Katika utamaduni husaidia kuonyesha utajiri wa utamaduni
na kujenga hali ya kupendeza. Mashindano ya jumla yana uwezo
wa kushirikisha aina mbalimbali za fani za utamaduni zenye
anuai pana zaidi.
4.4 Ingawa mashindano yote yana asili ya kuwa na mvuto
mkubwa kwa washiriki na jamii, shindano la jumla lina mvuto
mkubwa zaidi kwa wana-utamaduni, wadau, mapromota na
wafanya biashara wa ndani na nje ya nchi.
5.0. Mchanganuo wa uwezo, udhaifu, fursa na matishio katika
kuendesha Shindano la Taifa
5.1. Uwezo: (a)Maamuzi ya Kisera
* Mshiriki awe Mtanzania anayefahamu vizuri mila na desturi za
kabila lake.
* Mshiriki anatakiwa awe jasiri wa kuweza kusimama na kutetea
mila na desturi za kabila lake ili jamii imuelewe.
*
Mshiriki awe tayari kukabiliana na changamoto hasa za makabila
ya watani wao(kama yatakuwapo).
* Mshiriki afahamu vema lugha ya kabila lake na ya Kiswahili
kama lugha ya taifa, kwani ndizo zitakazotumika katika shindano.
* Mshiriki awe na umri usiozidi miaka 25.
* Jamii na familia anayotokea iwe imempa baraka zote za
kushiriki mashindano.
Wakala; ambaye ni muandaaji wa shindano eneo husika atakuwa
na mamlaka ya kumtoa mshiriki kutoka kwenye shindano
atakapobaini kuwa ana matatizo ya kijamii).
(i)Katika Sura ya Saba ya Sera ya Utamaduni ya 1997
imehimizwa kwa wananchi kushiriki na kushirikishwakatika
shughuli za utamaduni kwa kuwa ni haki yao. Hii ina maana
kuwa wananchi ni muhimu kuwawezesha kufanya hivyo kwa
kuweka mipango na mazingira mazuri.
(ii)Shindano hili linaihusisha serikali kwa maana ya taifa kwa
kutoa mchango wa kulinda maadili ya nchi na kuyafanya
makabila mbalimbali yanayochukiana kuacha vita na kushindana
kwa utamaduni, jambo litakaloleta mshikamano na amani
pamoja na kuwapatia watu mbalimbali ajira.
(b)Katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala, CCM, imeelekezwa
kuwa Serikali itaboresha shughuli zamaendeleo ya utamaduni,
hususani kwa kuanzisha na kusimamia mashindano na
matamasha yatakayowashirikisha wananchi wengi katika
michezo na sanaa kwa lengo la
11;Lengo la shindano hili ni kutangaza mila na tamaduni za
makabila mbalimbali kwa kuyaenzi na kuyahifadhi.
kuna makabila yaliyo hatarini kutoweka,Kwa hiyo mshiriki
atakayetokea katika mojawapo ya hayo atakuwa najukumu la
kuyatetea na kuhakikisha anatangaza tatizo hilo kwa jamii ili
wasaidiwe.
12• Kutokana na jinsi sekta ya Utamaduni itavyopokelewa ndani
ya jamii , upo urahisi wa Makampuni ya biashara kutumia
washiriki katika shughuli na matangazo ya kibiashara.
(d) Fani, shughuli, au vitu vya kuonyeshwa katika tamasha hili
vipo kwa wingi. Hii inatokana na utajiri mkubwa wa utamaduni
wetu.Cha muhimu ni kuwa makini katika uchaguzi ili kuwa na
shindano lenye anuai pana.
5.2. Udhaifu
(a) Ufinyu wa bajeti itakayokuwa imetolewa na wadhamini
ambao ni mtu yeyote, inaweza kuwa sababu ya kupunguza
washiriki wa shindano la utamaduni.
(b) Tatizo la upungufu wa watumishi katika ngazi za Mkoa na
Wilaya ni kubwa.Shindano hili linaweza kutumika kuleta
changamoto kwa Serikali kuwaajiri maafisa wengi kila sehemu ili
waweze kusimamia utamaduni wa eneo husika.
13Wilaya na Miji zilizo nyingi zinao Maafisa utamaduni. Hata
hivyo baadhi ya Halmashauri hazina maafisa hawa. Ni muhimu
kuzingatia hali hii na kuandaa utaratibu utakao washirikisha ili
kufanikisha shindano.
5.3. Fursa
(a) shindano hili litatumika kulinda na kuendeleza mazingira
ikitiliwa maanani kwamba kuna makabila mbalimbali yenye mila
zisizoruhusu kukata miti ovyo.
Jambo hilo litaisaidia serikali na kuitangaza nchi kwa
kushirikiana na vituo vya utamaduni.
Shindano litakuwa likiboreshwa kadiri miaka inavyokwenda na
kadiri inavyowezekana. Na hili litatokana hasa na jinsi jamii
itavyolipokea.
(b) Maamuzi ya kisera ya Serikali na Chama Tawala yanayounga
mkono kuwepo kwa shindano hili yanapaswa kutekelezwa.
(c)Vigezo vya kushinda
Ili mshiriki awe mshindi na kutangazwa kuwa mrembo wa
utamaduni wa Tanzania atatakiwa aeleze namna atakavyoisaidia
jamii yake.
Je, mavazi aliyovaa mshiriki yanaitambulishaje jamii yake,
yanavutia au ameiga?
Ni kwa jinsi gani mshiriki ameweza kujieleza mbele watu na
kujibu maswali anayoulizwa kuhusu kabila lake, mila na desturi.
Mshiriki anatakiwa ashiriki katika mashindano ya utangulizi
kabla ya shindano kubwa la kumpata mshindi wa jumla.
Kila mrembo atapita katika jukwaa liliotayarishwa na kuonyesha
mavazi yanayovaliwa nyumbani - jina la vazi, muda wa kuvaa vazi
hilo na sehemu vazi kama hilo linapovaliwa.
Mrembo atakapokuwa jukwaani ataeleza historia ya kabila lake,
lilikotokea, liliko hivi sasa na kama kabila hilo limesambaa katika
mikoa mbalimbali; aina ya maisha wanayoishi na utamaduni
wao kwa ujumla.
Mrembo aeleze ubora wa utamaduni wa kabila lake na kuutetea
kwa swali lolote atakaloulizwa huku akionekana mchangamfu
mwenye uso wa furaha.
Mrembo aonyeshe mavazi ya ubunifu. Vazi litakaloonekana zuri
litatangazwa kuwa la taifa kwa kipindi cha mwaka mzima. Katika
kila hatua mshindi atapata alama mwishowe zitakajumlishwa na
waamuzi na kisha aliyepata kura nyingi atatangazwa mshindi wa
jumla.
(d) Wapo wataalamu wa kutosha hadi ngazi ya wilaya ambao
watakuwa wanatumiwa katika shughuli mbalimbali za
maandalizi na uendeshaji wa tamasha. Suala la msingi ni
tamasha kuwa la wadau badala ya vyombovya serikali pekee.
(e)Udhamini wa Makampuni na asasi za biashara binafsi una
uwezekano wa kukubali kuingia katika masuala ya utamaduni
kwa kiwango kikubwa zaidi.
5.4. Matishio
(a)Muda wa kufanya Shindano la Utamaduni wa Taifa ungefaa
kuwa mmoja kwa miaka yote. Lakini kulingana na matukio
mengine,italazimu kila mwaka kuchagua tarehe maalumu.
Kimsingi miezi yakiangazi ndiyo inayofaa, yaani Julai hadi
Novemba.
(b)Ukosefu wa fedha, ikiwa pamoja na udhamini, ni tishio
kubwa.Ingawa kuna uwezekano kwa baadhi ya wadau
wakajitokeza kwa dhati kulidhamini shindano hili , washiriki
wengine wazuri watashindwa kushiriki kutokana na kukosa
nafasi.
(c)Baadhi ya makabila yatashindwa kabisa kuwa kujitokeza
katika shindano hili kutokana na wengine kupoteza utamaduni
wao ulioathiriwa na mwingiliano wa tatmaduni za nje.
(d)Hali iliyopo hapa nchini ya ulimbukeni wa kuthamini
utamaduni wa nje inaweza kupunguza msisimko na kishindo
kinachotarajiwa au hata kuibua vikundi vya wapinzani wa
utamaduni wetu kulisemea vibaya shindano hili.
Baada ya mshindi kupatikana
Baada ya kuwa mshindi kuonekana kuwa amekidhi vigezo
vilivyohitajika na kuwazidi wenzake kwa alama, atangazwa kuwa
ndiye Malkia wa Utamanduni wa Taifa.
Kuanzia muda huo, mila na tamaduni za kabila lake zitaanza
kutangazwa kwenye vyombo vya habari huku aina ya mavazi yake
yakichaguliwa kuwa ‘mavazi ya kitaifa kwa mwaka mzima’ hadi
atakapopata mrithi.
Mshindi wa kwanza hadi wa tatu watapewa zawadi mbalimbali
zitakazokuwa zimependekezwa na waandaaji wa tamasha na kwa
mwaka husika.
Mshindi atawezeshwa kwa kila hali kufanya shughuli zake
atakazotaka ikiwa ni pamoja na kuutangaza utamaduni wao.

Labels: Kweli tupo gizani?

<< Home