Monday, November 15, 2010

Ripoti kamili ya Mradi wa umwagiliaiji, kilimo kwanza Mara

Na Mobini Sarya,Mara
ULE mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji unaolenga kuwahamazisha wakulima mkoa wa Mara waanze kulima kilimo cha kisasa ambacho kitawaletea tija umewaletea hasara kubwa wakulima badala ya faida.
Maelezo ambayo yametolewa na wadau mbalimbali wanaohusiana na mradi huo yameweka wazi ufisadi ulioghubika mradi huo nakuusababishia uwaletee hasara wakulima wa Nyatwali Kata ya Kunzugu Wilayani Bunda.

mashamba ya mpunga yaliyokauka baada ya mazao hayo kukosa maji, sasa ekari moja imekuwa ikitoa gunia tatu za mpunga
Vigogo Bunda wajigawia mashamba nakuacha wakulima hoi
Mradi huo ulipangwa uwe mfano wa kupigiwa chapuo katika kuhamasisha wakulima wa maeneo mengine mkoani hapa waanze kujifunza kulima kilimo cha umwagiliaji.
Hali hiyo imeleezwa kuwa ni baada ya wizara ya Kilimo na umwagiliaji kununua mashine ambazo zimeshindwa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kupeleka kwenye mashamba yalipo mita 200 kutoka ziwani.
Awali mradi huo ulipaswa uanze kuzalisha mazao Mwaka jana lakini viongozi wanaohusika na mradi huo kushindwa kutumia vizuri zaidi ya Shilingi Milion.100 kununua mashine nzuri mradi huo ulikwama.
Kufuatia hatua hiyo zaidi ya ekari 200 za mazao ya chakula ambazo zilikuwa zimelimwa eneo la Nyatwali wilayani hapa zilikauka nakusababisha hasara huku Halmashauri ya Bunda ikitumia zaidi ya sh. Mil. 10 kuwalimia mashamba hayo.
Licha ya Mashine hizo ambazo zimenunuliwa kampuni ya Davis Shartliff ya jijini Dar es Salaam, kununuliwa kwa zaidi ya shilingi Milion.100 huku mradi mzima ukigharimu ,milioni ya poesa bado wakulima wameshindwa kuvuna tena kwa mara nyingine Mwaka huu.
Hali hiyo imesababisha kauli mbiu ya Kilimo kwanza ingiwe dosari huku wananchi wa Kata ya Nyatwali wakimtaka Waziri wa Kilimo na Ushirika Steven Wassira ambaye ni mgombea wa jimbo la Bunda, aeleze ni kwanini wizara yake imeshindwa kusimamia mradi huo kikamilifu umewaletea hasara.
Wananchi hao walimweleza Wasira kuwa waliambiwa kuwa mradi huo umekamilika hivyo kwalima mashamba lakini mazao yake yameanza kukauka baada ya kukosekana maji.
Wasira ambaye ni mbunge wa hapa aliwambia wananchi hao kuwa hata yeye hajui kilichotokea hivyo amewaagiza wataalam, wa umwagiliaji wafuatilie kuona kama mashine zingine zinapatikana ili kuweza kufanikisha mradi huo unaolenga kuwanufaisha wakulima wa mashamba hayo ambayo yapo ekari 500.
“Tulitegemea kuwa mradi huu ungefanikiwa ili kuweza kuwakomboa wakulima na umasikini kwa kulima kilimo cha umwagiliaji lakini sasa unaona yametokea haya”Wassira aliyasema hayo Mwishoni mwa Mwaka jana jambo majimbo yaliyoibua maswali upya.
Huku wakulima hao wakitaka awaeleze ni lini mradi huo utakuwa tayari kwani wamekuwa wakidanganywa huku wakiingia hasara ya kulima na kumwaga mbegu ambazo zimepotelea mbali.
“Mhe. Waziri wewe unasema kuwa unagombea tena ubunge na mradi uliotuahidi bado haujakamilika muda wa kampeni unakaribia tuhakikishie ni nilini mradi huo utakuwa tayari”alihoji mwananchi moja nakufanya watu washangilie
Katibu wa kikundi wa wakulima Nyatwali, Malongo Mashimo anasema kuwa baada ya kutengenezwa mashine hizo,mapema Mwaka huu halmashauri iliazimia zilimwe ekari 170 tu kati ya 500 kama majaribio.
“wakulima tuliajanda kwa kuchangia gharama lakini baadaye walibaini tena kuwa mashine hizo hazina uwezo wa kumwagilia ekari zote hivyo wakapunguza hadi ekari 100”anasema Mashimo.
Lakini katika hali inayoonyesha kuwa mradi huo umeshindwa kuwakomboa wananchi kati ya ekari 100 zilizopandwa mazao ya mpunga ni ekari 60 tu zilipata maji nyingine zilikauka kabisa, huku wakulima wakiwa wametumia zaidi ya shilingi 90,000 kuandaa mashamba.
Hali hiyo imeleezwa kuwa ni baada ya wizara ya Kilimo na umwagiliaji kununua mashine ndogo ambazo zimeshindwa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kupeleka kwenye mashamba yalipo mita 200 tu kutoka ziwani.
Kufuatia hatua hiyo hata hizo ekari 60 za mpunga ambazo zilitarajiwa kunwa septemba Mwaka huu zilikauka hivyo wameambulia ekari 42 ambazo hata mazao yaliyopatikana hayaridhishi.
“Ni mkulima mmoja tu ndiye amefanikiwa kupata gunia 28 za mpunga, mwingine gunia 23, watatu gunia 18 ambapo wakulima wengine waliambulia magunia matatu huku wengine wakikosa kabisa”anasema Katibu huyo.
Baadhi ya wakulima wamesema kwamba walitumia zaidi ya shilingi laki tano kuandaa mashamba hayo lakini wamekatishwa tama na serikali kuwapelekea mashine ambazo haziwezi kumudu uwendeshaji.
“mara ya kwanza halmashauri ilitulimia ekari 200 hiyo ilikuwa ni Agosti Mwaka 2009 lakini baada ya mashine kuharibika ,ikabidi walime upya Mwaka huu ekari 100 ambazo tumeambulia 40 tu huku zingine zikikauka”anasema mkulima Marko Okebe.
Hata hivyo wakulima hao wanadai kuwa mradi huo hivi sasa umevamiwa na viongozi wa Halmashauri ambao wamejikatia maeneo yanayofikiwa na maji huku wakulima wakipewa amaeneo ambayo hayana maji.
Miongoni mwa Viongozi wanaomiliki mashamba katika maeneo hayo na wamefanikiwa kupata mazao ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda,Mkurugezi maafisa kilimo na watendaji wengine, huku mkuu wa Mkoa wa Mara akijitoa baada ya kuona ubabaishaji umezidi.
Hata hivyo, Lukiko anasema kuwa viongozi waliamua kuchukua maeneo hayo ili kuwahamasisha wakulima nao walime baada ya kuona wamesusia kilimo hicho.
Madai hayo yanapingwa na katibu wa kikundi cha wakulima hao ambaye alisema kuwa
“tumewakubalia walime hapa ili waweze kutusaidia kulipa umeme kwa mfano sasa hivi kila mwezi tunalipa umeme Milioni mbili ambazo halimashauri inatuapa ,unadhani kama wasingekuwa na maeneo hapa wangeulipia umeme huo?”alihoji Mashimo
Alipoulizwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sprian Oyer kama hamashauri yake inalipia umeme kwasababu anamiliki shamba kule alisema,
“kazi ya Halmashauri ni kuhakikisha wananchi wanapata faida, hatuwezi kuacha mazao yateketee kwa kukosa umeme…halmashauri inalipia gharama za umeme kwa wastani wa shilingi Mil.1,200,0000 kwa mwezi.
Afisa Mazao wa Bunda Balisamaki Shija anasema kuwa mradi huo ulikuwa ukabidhiwe kuanzia April Mwaka huu jambo ambalo halijatekelezwa licha ya Bwana shamba kudai kuwa mradi huo tayari umekabishwa halimashauri
Naye mlinzi anayelinda mradi huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Michael alishangazwa na wataalam,wa Serikali kukubali kufungiwa mashine ambazo ni ndogo kuliko uwezo wa mabomba yaliyotandazwa hapo hivyokushindwa kuvuta na kusukuma maji kutoka ziwani haidi mashambani.
“tatizo la mashine hizi ni ndogo kuliko uwezo wake mara ya kwanza walipozifunga waliwasha zikaungua zote wakasafirisha kwenda kutengeneza Dar es Salaam, waliporudi kufanya majaribio tena zikaungua sasa unaona wamekwenda kimoja”alisema Mzee Michael.
Mhandisi wa Kampuni ya Davis, Eng.Shayo Denis anakiri kupewa tenda ya kusambaza mashine hizo na wizara ya Kilimo na Umwagiliaji kitengo cha kanda lakini akasema kuwa wenye majibu zaidi ni kitengo hicho.
“Ni kweli sisi tulipewa kazi ya kuleta mashine hizo na kufunga …nakumbuka tuliwauzia takribani shilingi Milioni 100 lakini tulipokwenda kufunga tulikuta wameweka vipuri vingine (Non return Valve) zingine hivyo kukatokea matatizo hayo naamini wao wanamajibu mazuri”alisema Shayo

Labels: