Friday, January 14, 2011

Mhindi kuwafadhili wastaafu JWTZ

WANAJESHI wastaafu nchini wameanzisha Muungano wa unaojulikna kama MUWATA utakaosaidia kuwaweka pamoja na kutambua shughuli zao.

Akitambulisha muungano huo leo Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Muwata, Ancety Mayuge amesema kuwa wamepata wanachama zaidi ya 8000 kutoka Mikoa 22 ya Tanzania Bara.

Bwana Mayuge amesema kuwa Lengo la Muungano huo ni kuwatambua wanajeshi wastaafu walipo na shughuli wanazofanya ili kuwa rahisi kusaidiana
Amesema kuwa kesho wanajeshi wastaafu zaidi ya 300 wanaokaa jijini Dar es Salaam watakutanana mfadhilili wao mkuu ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Bajaji kutoka India Bwana Sunil ili waone namna anavyoweza kuwasaidia.

Aidha Mayuge amewaonyesha wanandishi wa habari cheti cha usajili wa muungano huo kilichotolewa Disemba 27 Mwaka huu kinachodhibitisha kuwa wanatambuliwa na Serikali.

Labels:

Thursday, January 6, 2011

Dowans S.A kulipwa dolla Milioni 65

na Mobini Sarya

HATIMAYE serikali imekubali kuilipa Kampuni ya Dowans S.A zaidi ya dolla Milioni 65 sawa na Takribani Bilioni 70 pesa ya Tanzania kama fidia baada ya shirika la Umeme tanesco kuvunja mkataba wa kufua umeme.

Waziri wa Nishati na Umeme William Ngereja amesema jumatano hii kuwa pesa hiyo inalipwa baada ya mahakama ya utatauzi wa migogoro ya kimataifa ICC kuamru.

Ngereja aliwaambia wandishi wa habari kuwa awali Dowans walitaka walipwe Dolla za kimarekani Milioni 149 lakini uamzi wa mahaka hiyo kuamua ilipwe Milioni 65 u.s $.

Aidha katika mgogoro wa pili tanesco wanatakiwa kuilipa kampuni ya Richmond Dolla 50,000 badala ya Dolla 169 zilizokuwa zinadaiwa na Richmond kwa kukashifiwa.

Kutokana na uamzi huo richimond yenyewe imeamriwa kuilipa Tanesco Dolla Milioni 1.2 kama nusu gharama ya uendeshaji wa kesi ilitumiwa na mawakili.

Hata hivyo waziri huyo amesema kuwa serikali ipo tayari kuilipa kampuni ya Dowans kiasi hicho endapo itasajili hukumu hiyo katika mahakama kuu ya Tanzania na taratibu zote kufuatwa.

Kabla ya waziri kuwaleza wandishi wa habari matukio hayo ilikuwa imezagaa taarifa mitaani kuwa serikali inatakiwa kuilipa Dowans takribani shilingi milioni 185 jambo ambalo waziri amelikanusha vikali.

Labels:

Sunday, June 7, 2009

usafiri wa kivuko Kigamboni