watanzania watakiwa kupenda kula korosho
Watanzania wahamasishwa kula korosho
Na Mwandishi wetu
WATANZANIA wameaswa kujenga utamaduni wa kupenda kula
korosho kwani zinajenga afya hususani
kwa akinamama wajawazito na watoto wadogo,ambao huwezeshwa katika
makuzi bora.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Kilimo na
Chakula,Malima wakati akizindua siku ya kuonja korosho kwenye banda la bodi ya
korosho lililopo kwenye maonyesho ya sabasaba.
Waziri Malima alisema
kuwa Tanzania inasifika du niani kwa kulima korosho safi na bora lakini
wananchi wake hawana utamaduni wa kula hizo kororosho badala yake wanapendelea
kula biskuti jambo ambalo ni kinyume na
nchi zingine.
![]() |
| mmoja wa wafanya Bodi ya korosho akigawa korosho siku ya kuonja korosho iliyofanyika jana Sabasaba,jijini Dar es Sam.Picha na Tanpress |
“Watanzania hatupendi kulakorosho wakati zinapatikana kwa wingi hapa nchini ,nawaasa wazazi wajitahidi
kila wanapoandaa chakula korosho iwe pembeni kwa sababu ni nzuri hata kwa watoto…..pia naiagiza bodi ya korosho
kutengeneza vipindi vya kuhamasisha ulaji wa korosho vichezwe kwenye redio na
televisheni”amesema Waziri Maalima.
Naye katibu mtendaji katika mfuko wa kuendeleza korosho nchini (CIDTF)
Suleman Lenga amewashauri wakulima
kutambua kuwa hapa nchini kuna soko kubwa la korosho badala ya kutegemea soko la nje wanaweza kuuza hapa.
“kwa kutambua hilo mfuko wa
CIDTF umeambua kuwalipia gharama za kubangua korosho wakulima wadogo ili
waweze kuziongeza thamani wakati wa kuuza hivyo wananchi wanapaswa kuanza
kulakorosho kwa wingi ziweze kuletwa sokoni kwa wingi pia”amesema Lenga.
Labels: Zilizokiki



