Thursday, May 10, 2007

माम्बो या katiba

HARAKATI za Viongozi wa Vyama vya Upinzani kuona katiba mpya inapatikana kabla ya uchaguzi wa Mwaka 2010 huenda zikagonga Mwamba baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Mary Nagu kusema kuwa kwa sasa madiliko ya katiba sio Mhimu.

waziri Nagu aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Karimjee wakati akitoa Hotuba ya kufungua Semina ya Siku mbili ya Kuwawezesha wanawake katika Siasa hapa nchini.

Semina hiyo iliandaliwa na umoja wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni (TDC) , kufadhiliwa na umoja kama huo kutoka nchini Finland ' DEMO Finland' ambapo kila chama kiwatuma wajumbe 18 , kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi wakiwemo waandishi wa Habari.

katika hotuba yake waziri Nagu aliwataka wanawake ambao walikuwa wanatokana na vyama vya siasa, kuachana na harakati za kudai mabadiliko ya katiba mpya kwani sio ya kazima baadala yake waendelee kuongeza bidii ya kupigania usawa katika kila idara hadi bungeni ili wawe nusu kwa nusu.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home