Maonesho mavazi ya utamaduni Mei 27
Maonesho mavazi ya utamaduni Mei 27
ASASI ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Tanzania (MMAWATA), imeandaa maonesho ya mavazi ya kitamaduni yatokanayo na Maliasili ikiwemo magome ya miti na migomba yatakayovaliwa na vijana wa kike na kiume.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa asasi hiyo, Hilda Bandio amesema kuwa maonesho hayo yatafanyika Mei 27 mwaka huu saa 2:00 usiku katika ukumbi wa Ubungo Plaza.
“Mavazi haya kama ya mababu zetu yanatokana moja kwa moja na maliasili zilizofanyiwa matengenezo madogo na yanatokana na magome ya miti ya Miluba, kamba za migomba, kamba za matete, mikeka, vifuu vya nazi, vibuyu, shanga, katani, manyoya ya ndege, magunia, ngozi za kondoo na simbi,” alisema.
Alisema mavazi hayo ya aina mbalimbali yanavaliwa kwa nyakati na shughuli husika kama sherehe, ufukweni na mengine ya matembezi ya kawaida ambapo kwa upande wa wanaume itakuwepo migolole, kanzu, makoti, mashati, bukta, kofia na suruali na kwa wanawake yatakuwepo magauni, sketi, blauzi, bukta, sidiria, kofia, mitandio na mashuka.
Alisema kuwa katika maonesho hayo yatakuwepo mapambo yatokanayo na maliasili kama vile vibanio vya nywele, hereni, cheni za shingoni na bangili pamoja na sanaa nyingine za utamaduni ikiwemo mikoba ya wanawake, fimbo za wanaume na viatu.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home