KAMPUNI YA SBC YASHEREHEKEA MAFANIKIO YA MIAKA 10

Meneja Masoko wa Kampuni SBC Tanzania Ltd. Rashid Chenja akizungumzia maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni ya SBC inayozalisha vinywaji Pepsi, Mirinda, Seven Up, Evervess Soda Water, Evervess Tonic Water na Mountain Dew ambapo wamechangia shilingi Bilioni 28.8 katika uchumi wa Tanzania. Kulia ni MKUU wa mahusiano ya kampuni Foti Nyirenda Kushoto ni Corporate Affairs Officer Emmanuel Musiba.

KAMPUNI ya vinywaji baridi ya SBC Tanzania Ltd, imetenga Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kununulia dawa za kupambana na kifua Kikuu nakuzisambaza kupitia kitengo cha Kifua Kikuu (TB), ili kusaidia kutoa huduma za dawa na matibabu kwa wagonjwa wa kifua kikuu.
Kwa kuanzia, kampuni itakuwa ikitoa Sh milioni 50 kila mwaka kwa ajili ya kuchangia dawa na matibabu ya wagonjwa hao.
Mpango huo utaanzia Dar es Salaam na kisha kuendelea katika mikoa mingine. Mkuu wa Uhusiano wa SBC, Foti Nyirenda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu kuelezea maadhimisho ya miaka 10 tangu kampuni hiyo ilipohama kutoka Fahari Beverages na kuwa SBC mwaka 2001.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home