UMEME wapanda kinyemela
ueme wapanda kinyemela
Na Mobini Sarya
SIKU chache baada ya Mamlaka ya udhibiti nishati na Madini (EWURA) iruhusu shirika la umeme (TANESCO) kupandisha gharama ya umeme, imebainiaka kuwa, Shirika hilo limeongeza tena gharama hizo kinyemela.
uchunguzi uliofanywa katika vituo vya mawakala wa kuuzia umeme wa LUKU, imebainika kuwa mawakala hao wamekuwa wakiwatoza wateja bei kubwa nje ya ile inayokatwa kwenye mashine za Maxcom.
baadhi ya mawakala wamekuwa wakiwadai wateja pesa za ziada kama malipo yao ya uwakala,ili waweze kuuza umeme huo , ambapo wanakata shilingili 300 kwa mtu anayetaka umeme wa Shilingi 5000 na Shilingi 500 kwa mtu anayetaka umeme wa Sh.10,000.
mawakala hao maarufu kama Maxumeme, walisema kuwa, wamepewa maelekezo kutoka Tanesco kuwakata wateja pesa ya uwakala,kama kazi ya kuwadumia badala ya kudai shirika hilo.
Msemaji wa Ewura,Titus Kaguo alipoulizwa kama Tanesco wameomba kibali cha kuongeza gharama ya kuwalipa mawakala wao, alikataa na kusema kuwa taarifa hizo ni mpya kwake.
“Subiri hapa hapa ngoja niwapigie simu Tanesco wanipe majibu…..”alisema na kumpigia simu Badra Masoud ambaye ni msemaji wa Tanesco na kujibiwa kuwa, Shirika hilo halina habari kama mawakala wameongeza hiyo bei badala yake wamekuwa wakiwalipa asilimia tano ya mauzo.
wakati Tanesco wakisema kuwa hawajaruhusu wateja wanaonunua LUKU kukatwa pesa za ziada kama malipo ya mawakala Mwandishi w etu alimuonyesha vielelezo vya risti zinazoonyesha wateja waliotoa shilingi 5000 na kuuziwa umeme wa 4700.
kwa mfano katika kituo kimoja cha banana Ukonga wakala alikuwa akiwauliza wateja maswali, ‘unataka umeme wa 5000 nipe 300 kama huna nitakata humu nikupe wa 4700 na kama unataka wa 10000 tutakata 500”alinukuliwa.
mteja mmoja aliyenunua juzi umeme katika kituo cha wakala mmoja wa Uwanja wa ndege nusura arushe ngumi baada ya kuomba umeme wa Shilingi 30,000 nakuatakiwa atoe shilingi 1500 kama pesa ya wakala, hali iliyozua malalamiko kwamba hiyo pesa ya wakala ilipaswa ilipwe na Tanesco.
kufuatia malalamiko hayo Ewura imesema kuwa wataindikia Tanesco barua kwa haraka ili waweze kupatiwa majibu kabla hawajachukua hatua za kisheria “Hii taarifa tunaifanyia kazi haraka na leo tutawaandikia barua Tanesco ili watupe majibu ya haraka kwanini wameongeza mzigo huo”alisema Kaguo.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home