Friday, March 4, 2011

Wakristo na Waislam ‘wamuasi Mengi

Wakristo na Waislam ‘wamuasi Mengi


JITIHADA za Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Regnal Mengi kuwaunganisha Wakristo na Waislam waishi kwa amani zimegonga mwamba licha ya kugharimia mkutano wao na kuwapatia posho nono kila mmoja.

hatua hiyo imetokana na Wakristo kutangaza rasmi kuwa kuanzia sasa watapambana na waislam, jino kwa jino hadi Serikali ingilie kati na kumaliza uhasama huo.

“Tumechoka kunyanyaswa na Waislam…sasa tunasema basi tutajibu mapigo kwa njia ile ile watakayotumia, wakimtukana askafu na sisi tunamtukana Sheikh lakini tutaongeza busara hadi serikali itakapoingilia kati”

kauli hiyo imetolewa wiki hii na Mwenyekiti wa umoja wa Wainjilisti wa Kikristo nchini (UWAKITA) Samson Bullegi, ikiwa ni siku chache tangu, Mfanyabiashara Mengi awakutanishe Mashekh na maaskofu jijini Dar es Salaam, kuzungumzia namna ya kuwa wamoja.

katika mkutano huo uliofanyikia hotel ya Moven Pink na kufunguliwa na mfanyabishara huyo, baadaye kufungwa naye mchana, viongozi hao walijadili mambo mbalimbali yanayohusiana na imani zao na kutoa matamko mazito.

Miongoni mwa mazimio walisoma kwenye tamko lao ni kwamba kuanzia sasa viongozi wa Kikristo na kiislam watashikiana kutatua migogoro kwa pamoja badala ya kutumia jazba au machafuko.

aidha waliazimia kuwa viongozi wa dini hizo watakuwa wanakutana kila mara kutatua matatizo yanayoibuka kwenye jamii na kumaliza migogoro kwa njia ya amani kabla ya machafuko.

baada ya mkutano huo viongozi wao walipokewa posho zilizotolewa na mfanyabishara huyo kabla, hajafunga mkutano huo na kuondoka kila mmoja akiwa na furaha.

Mwinjilisiti Bullegi alipoulizwa kwanini wakristo wameamua kutoa tamko kali hilo badala ya kutumia ile kamati ya viongozi waliounda kwenye mkutano ule alisema kuwa ilishavunjika.

“Kamati gani? siku ile ile viongozi wametoka kwenye mkutano zilisikika kauli kutoka kwa waislam wakilaani yale matamko ya mkutano huo, huku wakiwabeza wenzao kwa kusema walio hudhuria mkutano huo ni Masheikh njaa na kweli kesho yake wakafanya mkutano Mwanza wakakashifu viongozi wetu”anasema Bullegi

alisema kuwa Wainjilisti wameamua kutoa tamko hilo kwa niaba ya wakristo wote kama njia ya kukabiliana na waislam ambao wamekuwa wakiwanyanyasa wakristo kwasababu serikali iliyopo madarakani ni ya kiislam.

Mwinjilisto huyo akiwa ameongozana na viongozi wenzake akiwemo Katinu mikuu wa UWAKITA Cecil Simbaulanga, alisema kuwa kwa muda mrefu waislam, wamekuwa wakivamia mikutano ya wakristo na kufanya fujo lakini badala ya kukamatwa wanaokamatwa ni wakristo.

“Hii inatokana na serikali iliyopo madarakani ni ya Kiislam, ukiangalia Wizara ya mambo ya ndani,Waziri,naibu, mkuu wa Polisi IGP,wote ni Waislam…ndio maana juzi waislam walipovamia mkutano wa Wakristo lakini waliokamatwa ni waijilisti”anasema Bullegi

wainjilisti hao wameitaka serikali kuwaachia huru mara moja wahubiri waliokamatwa mto wa Mbu mkoani Arusha na baadala yake, Polisi wawajibike kwa kushindwa kuwapelekea ulinzi wakati walipewa taarifa.

Uwakita umesisitiza kuwa kuanzia sasa wakristo hawatanyamaza pale waislam watakapowachokoza kwani watapambana nao kwa njia ile ile hata ikiwa ni kwa kuchoma misikiti na makanisa ili Serikali iingilie kati na kukomesha uhasama huo.

walitaja baadhi ya matukio ambayo Waislam, wamewahi kuvamia kwenye mikutano yao, lakini waliokamatwa na kufungwa ni viongozi wa kikristo licha ya kuhalibiwa mali zao na kupigwa.

aidha jitihada za kumpata Mwekikti wa jukwa la amani,lililoundwa na viongozi hao katika mkutano wa Mengi, Sheikh Musa Salum hazikuweza kufanikiwa.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home