Wednesday, December 1, 2010

Ukeketaji Mara kukomeshwa sasa?

KITUO CHA Sheria na haki za binadamu,LHRC KIMEITAKA Serikali kukomesha Mara moja vitendo vya ukeketaji vinavyoendelea wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.

Akizungumza na wanndishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,mkurugenzi wa kituo hicho Francis Kiwanga amesema kuwa wamepata taarifa kutoka wilayani humo zikionyesha kuwa kila siku wasichana 100 wanakeketwa tangu Novemba Mwaka huu

Alisema kuwa Licha ya vitendo hivyo kufanyika hadharani lakini Polisi wameshindwa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kwa madai kuwa sio kosa jambo l;inaoonyesha kuwa Polisi wanaupungufu wa ufahamu.

Kiwanga alissema kuwa mkoa huo unatarajiwa kuwakeketa watoto 5000 hadi kufikiwa januari 15 Mwaka huu kama hatua za haraka hazitachukuliwa kukabiliana na kile alichoita ukatili wa kike.

Ameongeza kuwa taarifa za leo asubuhi ambazo wamepata kutoka kwa wasaidizi wao waliopo wilayani taarime zinaonyesha kuwa kwa siku ya Novemba 30 Mwaka huu watoto 100 walifanyiwa ukeketaji.

Amesema kuwa kwa mjibu wa shetria ,ukeketaji ni kosa chini ya sheria ya kanuni adhabu sura namba 16 ya sheria za Jamhuri ya Tanzania ,pia imeelezwa kuwa ni uvunjaji wa haki za binadamu na watoto wa Kike.

Aidha wizara ya maendeleo ya jamii Jinsia na watoto imetakiwa ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya wanaohusika na ukeketaji huo kutoka na sheria iliyopitishwa na bunge kukabidhiwa katika wizara hiyo.

Naye afisa Jinsia na watoto katika LHRC ,anna Henga alisema kuwa Mkoa wa Manyara unaongza kwa kukeketa wasichana sawa na mara kwa asilimia 85 ukifuatiwa na Arusha 72, Singinda 65 na Dodoma ni 54.

Taarifa hiyo imekuja siku chahche baada ya mkuu wa mkoa wa Mara Kanal enos Mfuru kusema kuwa anakusudia kuendesha zoezi la kuwatahiri wanaume wote wa mkoa huo hasa wafanyakazi wa jimbo la Rory kama njia ya kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home