Bunge lakwama Richmond
*Sitta atangaza mjadala kufungwa
*Pinda amfuta ‘machozi’ Lowassa
*Hoja ya Rostam ya majaji yazimwa
*Mwenyewe amgeuzia kibao Spika
Na Rahel Chizoza, Dodoma
BUNGE la Jamhuri ya Muungano limelazimika kuifunga hoja ya Richmond baada ya juhudi zake za miaka miwili za kuibana serikali itekeleze maazimio yote 23 ya Bunge kugonga mwamba.
Hatua hiyo ya Bunge kuufunga mjadala huo kinyume cha matarajio ya wengi ilitangazwa na Spika wa Bunge Samuel Sitta.
Kufungwa kwa mjadala huo ambao ulihusisha Kampuni yenye utata ya Richmond Development Company LLC kumekuja wakati Watanzania wakiwa na kumbukumbu ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Mbali ya Lowassa, mawaziri wengine wawili waliojiuzulu baada ya majina yao kutajwa katika sakata hilo ni Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.
Kabla ya Spika Sitta kutangaza kufungwa kwa mjadala huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo, alitangaza taarifa ya mwisho ya utekelezaji wa serikali wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu Richmond na ile ya mgodi wa makaa ya mawe ya Kiwira.
Akizungumza bungeni jana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliahidi kuwa maazimio yote yaliyoachwa mikononi mwa serikali yatashughulikiwa kikamilifu, likiwamo la hatima ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.
Alisema kuwa mapendekezo mengine ya kamati yatakayopewa uzito wa pekee ni pamoja na kuwasilishwa bungeni kwa muswada wa kutenganisha shughuli za siasa na masuala ya biashara na kujipanga kikamilifu katika kuhakikisha kuwa mikataba inayosainiwa inazingatia masilahi ya nchi.
Alisema kazi iliyofanywa na Bunge ni kubwa na inastahili kupongezwa huku akiunga mkono jitihada zilizofanywa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika kukabiliana na suala hilo.
“Suala la Richmond lilikuwa gumu sana wote hapa mnafahamu mpaka likaipitisha nchi kwenye historia mpya ya kisiasa, kwa kujiuzulu kwa mawaziri wawili na waziri mkuu pamoja na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri,” alisema.
Akizungumzia kuhusu hatua ya kujiuzulu kwa mawaziri katika sakata hilo, Pinda alisema uamuzi wao ulichukuliwa katika misingi ya kuwajibika kisiasa na haukutokana na kuwa kwao na makosa.
Pasipo kufafanua, Pinda ambaye alionekana kurejea kauli aliyoitoa siku chache baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, Februari 2008, aliposema lilikuwa ni tukio la ajali ya kisiasa, alikwenda mbele na akawataka mawaziri waliojiuzulu katika sakata hilo kutulia, kwani ipo siku wanaweza wakarejea tena katika madaraka ya umma.
Awali akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa (CHADEMA), alisema kushindwa kwa Bunge kumuwajibisha Dk. Hoseah ni kutotimiza wajibu uliotakiwa kutekelezwa na Bunge, kwani kuchunguzwa kwa wabunge hakuhusiani na tuhuma zilizopo dhidi ya mtendaji huyo.
“Hapa Bunge linakwepa majukumu, maana ukiangalia hoja ya Richmond ilitangulia na hii ya posho mbili ilikuja nyuma yake, inakuwaje tunaacha kilichotangulia kwa ajili ya kuhojiwa kwa posho mbili?” alihoji mbunge huyo.
Naye Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema kuwa waliokuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi walipewa majina mengi na kuandikwa katika magazeti.
Mbunge huyo pia alipongeza hatua zilizochukuliwa na kuunga mkono utekelezaji unaofanywa na serikali huku akiitaka kushughulikia kikamilifu maazimio hayo.
Katika hatua nyingine, Spika wa Bunge Samuel Sitta, alimtaka Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kufunga hoja yake ya kutaka kuundwa kwa jopo la majaji watatu kwa ajili ya kupitia maamuzi ya Bunge.
Alisema hoja ya mbunge huyo inakwenda kinyume cha Katiba na kanuni za Bunge, ambapo mhimili mmoja hauwezi kufanyiwa maamuzi na mhimili mwingine.
Alisema kuwa mbunge huyo alikuwa na muda wa miezi 12 wa kuwasilisha jambo hilo bungeni lakini hakupeleka, hivyo amechelewa mwenye na hakuna haja ya kuundwa hicho alichokitaka.
“Mjadala huu nimeufunga hapa bungeni na yeyote atakayejitokeza kujadili tena kanuni zitafuata mkondo wake,” alisema Spika.
Akizungumza na Tanzania Daima baadaye jana jioni kuhusu hoja hiyo ya Spika, Rostam alisema suala la Richmond limefungwa baada ya miaka miwili, huku wananchi wakiwa hawajui ukweli halisi kuhusu suala hilo.
“Nakubali yameisha, jambo hili lisingechukua zaidi ya wiki moja na badala yake limechukua miaka miwili kulimaliza, kwa kuwa lilijaa siasa zaidi. Ni bahati mbaya kwa kuwa tumewanyima wananchi kujua ukweli zaidi kama tungeruhusu tume ya majaji.
Rostam alieleza kushangazwa na kauli ya spika kusema kwamba alikuwa na miezi 12 ya kujitetea, ilhali akijua kwamba yeye ndiye aliyemzuia kufanya hivyo ndani ya Bunge.
Akiwasilisha taarifa ya kamati yake jana, Shellukindo alisema kuwa kamati imeshindwa kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya Dk. Hoseah kutokana na kuwepo kwa mchakato wa wabunge kuchunguzwa na taasisi anayoiongoza.
Alisema azimio namba nane la Bunge liliitaka serikali kuwawajibisha Hoseah na maofisa wengine wa mamlaka hiyo waliohusika katika zoezi la uchunguzi na kuandaa taarifa ya Richmond Development Company LLC kwa manufaa ya umma.
“Kwa sasa kamati imeona haitakuwa haki kutolewa maelezo au majibu kwa serikali kuhusu azimio hili, kwa sababu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru ameanzisha zoezi la kuwachunguza wabunge, kwa mntiki hii kamati inaliomba Bunge likubali suala hili liachwe kwenye mamlaka ya juu ya Bunge,” alisema Sellukindo.
Kujiondoa kwa kamati ya Bunge katika suala hilo ni kuepuka kuwepo kwa mgongano wa masilahi baina ya Bunge ya taasisi hiyo.
Mbali na hatua hiyo, pia mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kuhusu azimio namba 18 lililoitaka serikali kuwafungulia mashitaka ya jinai wamiliki wa Kampuni ya Richmond kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia serikali, alisema kamati imezingatia hatua zilizofikiwa na serikali za kuunda kamati maalumu ya vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola vya kimataifa.
Alisema pamoja na hatua hizo zilizofikiwa na serikali, bado kamati inasisitiza kuwa wamiliki hao wafikishwe mahakamani na serikali itoe taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Mwenyekiti huyo wa kamati alisema kuwa kuhusu azimio la 8 na lile la 14 ambayo yalitaka serikali iwawajibishe viongozi wenye dhamana ya kisiasa waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, kamati imezingatia mchakato uliofanywa na serikali wa kuvihimiza vyombo vya dola kukamilisha suala hili.
Aidha, alisema kuwa kamati imeridhika na maamuzi ya mamlaka za nidhamu za kuwafutia mashitaka jumla ya watumishi watano ambao walifunguliwa mashitaka ya nidhamu yasiyowahusu ambapo wawili kati yao walikuwa ni watumishi wa sekretarieti ya kamati ya wataalamu.
Alisema watumishi wengine watatu walionekana kuwa hawakuhusika moja kwa moja kwenye mchakato wa zabuni hiyo, ambapo walitumika kwa nyakati tofauti katika kutoa ushauri kwa Wizara ya Nishati na Madini kuhusiana na suala hilo.
Alisema kamati imezingatia maoni yaliyotolewa katika ripoti ya serikali kuhusiana na uwajibikaji uliofanywa na viongozi wa siasa kwa hiari yao.
Shellukindo alisema kuwa katika azimio namba 10 lilitaka Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) pamoja na bodi ya wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada ya dola 4,865,00 yaliyofanywa na Kampuni ya Dowans iliyorithi majukumu ya Richmond na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya uchunguzi kuhusu suala hili, alishauri kwamba kwa kuwa dola za Marekani 30,696,598 ambazo serikali ilizitoa kama malipo ya awali zilikuwa zimezingatia usafirishaji wa mitambo kwa njia ya meli, ulibaini kuwapo kwa utaratibu huo.
Wakati huo huo, Mbunge wa Mkanyageni ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, alisema kuwa anashangazwa na serikali kutumia muda wa miaka minne kuwatafuta wamiliki wa Richmond, jambo ambalo alisema kuwa ni utaratibu mbaya unaotumika.
Akitoa mchango wake, mbunge huyo alisema kuwa kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilipewa muda wa mwezi mmoja na nusu na ilifanikiwa kukamilisha kazi yake katika kipindi hicho.
Alishangazwa na kauli za serikali za michakato katika mambo muhimu yanayohusu masilahi ya taifa, huku akihoji sababu za kucheleweshwa kwa utafiti huo, ikizingatiwa kuwa serikali ina mkono mrefu wa kuweza kufika mahali popote kiuchunguzi.

<< Home