Wanatumia umasikini wetu kujinufaisha wao
Na Mwandishi wetu.
MWAKA 2002 kampuni ya Grumeti game Reserve ambayo imewekeza mahoteli makubwa ya kitalii pamoja na vitalu vya uwindaji katika hifadhi ya Taifa Serengeti ilianzisha mfuko wa kusaidia jamii unaofahamika kama Grumet Game reserve Fund.
Mfuko huo maarufu kama Grumeti Fund ulianzishwa na Kampuni hiyo kwa malengo mawili moja likiwa ni kuwasaidia wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo kutokana na kwamba kampuni hiyo ilichukua maeneo yao na kuyageuza vitalu vya uwindaji.
Awali wananchi walikuwa wanayatumia maeneo hayo katika uwindaji wa kiraia ili kujipatia kipato na kitoeo lakini Kampuni ikayageuza kuwa vitalu vya uwindaji na shughuli za kitalii.
Pia mfuko huo ulikuwa na lengo la kusaidia jamii hiyo ijiletee maendeleo iachane na uwindaji haramu pamoja na kupambana na ujangili kwa kutumia askari wake.
Hata hivyo tangu mfuko huo uanzishwe miaka saba iliyopita uendeshaji wake umegubikwa na utata hasa kutoka na vyanzo vyake vya mapato na shughuli zinazofanywa katika jamii husika ya wakazi wa Bunda na Serengeti Mkoa wa Mara.
Ingawa Mfuko wa Grumeti Fund unadai kuwa unasaidia kusomesha watoto wa familia Masikini kufadhili miradi ya Kilimo na kuwachimbi visima wakazi wa vijiji hivyo, lakini wenyeji ambao ni walengwa wanaupinga wakitaka serikali ichunguze mwendendo wake kwani umeanzishwa kwa manufaa binafsi ya kampuni hiyo.
Miongoni mwa sababu wanazotoa ni kwamba mfuko huo umekuwa ukitumika vibaya kukusanya pesa za watalii kwa nia ya kusaidia jamii masikini lakini michango inayopatika imekuwa ikitumika kuwahudumia wanasiasa wanaotembelea kampuni hiyo ndio maana hawakosi hoteli hiyo.
“kila Waziri anayechagulia katika Wizara ya maliasili tunafikri huyo ndiye atatusaidia kusikia kilio chetu kuhusu manyanyaso ya ‘jeshi’ la Mwekezaji huyo lakini akishafika kwenye hoteli hiyo akahudumiwa na huo mfuko hatumuoni tena kwetu”anasema Mkazi wa Kihumbu wilayani Bunda
Ingawa kampuni hiyo inakiri kwamba askari wake wanalalamikiwa na jamii hiyo lakini mkuu wa kitengo cha kuhudumia jamii kwenye mfuko huo,Richard Ndaskoi anasema hakuna mtu aliyejitokeza wazi akadhibitisha kwamba amebakwa.
“ni kweli malalamiko ya wananchi kubakwa tumekuwa tukiyasikia lakini hajawahi kujitokeza mtu yeyote akasema nimebakwa na askari wenu zaidi ya kulalamikia pembeni”anasema Ndaskoi
Anapoulizwa kiasi cha Pesa zinazotengwa kila Mwaka na kampuni hiyo kwa ajili ya kuhihudumia jamii kupitia mfuko huo Ndaskoi anakosa jibu zaidi ya kusema kwamba zile ni pesa za kutoka mfukoni mwa mmiliki wa kampuni hivyo hazina hesabu.
“ninachoweza kukuambia ni kwamba sisi tukitaka kufanya mradi wa jamii tunamuomba mwenye kampuni pesa ndipo anaziingiza kwenye mfuko huo kwa kujitolea wala hakuna mtu mwingine anayechangia”anasisitiza Ndaskoi ambaye anapinga madai kwamba mfuko huo unachangiwa pesa na watalii halafu haziendi kwenye jamii.
Lakini wananchi wa eneo hilo wanasema kuwa misaada hiyo hawaioni zaidi ya matesa wanayopata kutoka kwa askari wa kampuni hiyo maarufu kama askari wa ‘VIP’ ambao wamekuwa wakituhumiwa kuwapiga watu na kuwabaka akinamama.
Wananchi hao wanasema kuwa wanashangazwa na serikali kuiachia uhuru Kampuni hiyo kuunda mfuko huo ambao umekuwa ukitumika kukusanya pesa za watalii halafu haziingii kwenye malengo yalikusudiwa kama inavyoelezwa.
“Watu wanaojua utamu wa kampuni hii ni viongozi kwani wapo wanaosomeshewa watoto wao kwa maelezo kuwa ni watoto masikini kumbe ni wa kwao ndio maana ukiizungumza vibaya kampuni hii utajikuta matatani”anasema mwananchi mmoja
Wakazi wa kijiji cha Nyichoka kinachopakana na eneo la kitalu cha Kampuni hiyo, wanasema kuwa wanataka kumuona Waziri mkuu atembelee kijiji chao ili wamweleze uozo huo.
“tunamuomba Waziri mkuu au Rais afike huku tumweleze matatizo yake tunaokumbana nao kutoka kwenye kampuni hii tangu nchi hii ipate uhuru hatujawahi kumuona kiongozi hapa katika eneo letu ”anasema mkazi mmoja ambaye ni mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho.
Mjumbe huyo ambaye amechaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita ni miongoni mwa wananchi wanaolalamika kuwa mfuko wa Grumet Fund umeanzishwa kwa lengo la kukusanya ya wahisani kwa manufaa ya kampuni hiyo.
“Wageni wakitembelea hoteli hiyo wanawambia kuwa ,pia tuna mfuko wa kuisaidia jamii hii ya hapa ambayo ni masikini, tunasomesha watoto wao hivyo mnaweza kuchangia, lakini wakichangia hizo pesa hakuna chombo kinachoziangalia”anasema kiongozi mmoja wa Kijiji.
Msimamizi wa mfuko huo Ndaskoi anapinga madai kwamba wageni wanachangia mfuko huo lakinik katika mtandao wao huo wanaeleza bayana kuwa wageni wanashiriki kikamilifu kuchangia mfuko huo pamoja na sehemu ya mapato inayopatikana kutoka katika biashara ya utalii inawekwa kwenye mfuko huo.
Madai hayo pia yanadhibitishwa na mfanyakazi mmoja wa mfuko huo ambaye alisema kuwa mara nyingi wanapata pesa msimu wa utalii unapoanza ambapo wageni wengi huchangia mfuko huo.
“Mara nyingi tunapata pesa kutoka kwa wageni, kama unavyojua wageni wanaotembelea hoteli zetu ni matajiri hivyo tunawaambia kuwa tunamiradi tunayosadia jamii nao huchagia”anasema mfanyakazi huyo Vicent Nyamasagi
Nyamasagi anasema kuwa mfuko huo ambao ulimsomesha na yeye unasomesha watoto ambao wamefaulu lakini familia zao ni masikini, ingawa alishindwa kubainisha wanavyoepuka udanganyifu.
Wakati kampuni hiyo inaongeza kuwa lengo mhimu la mfuko huo ni kusadia kuboresha biashara ndogo za wanajimii na kuzalisha ajira zaidi jamii husika inasema kuwa hakuna biashara inayofanywa katika meneo yao zaidi ya kilimo na ufugaji ambao ni wa kienyeji.
Biashara ndogo inayozungumzwa na kampuni hiyo ni kilimo cha kisasa na kuhakisha wanapunguza mbinu zozote zinazoweza kutumiwa na wawindaji haramu kwa kuifanya jamii hiyo ibadilike na kuangalia kitoeo kingine badala ya kutegemea wanyama.
“Kilimo gani cha kisasa tunacholima hapa zaidi ya kutunyanyasa ,hii kampuni kwa kutuchukulia maeneo ya kuchunga nasikia watalii wakija huwa wanawaambia wanamfuko wa kutuhumia sisi ,sasa wanachangiwa pesa halafu wanafanyia mambo yao”anasema Simon Mtura mkazi wa Singisi
Mtura anasema kuwa hata madai kuwa Grumeti Fund imewapatia mafunzo ya wajasilimali na upeo wa kuendesha biashara pamoja na kuwasaidia mitaji ya ufugaji wa samaki ,kilimo cha Mboga, ufugaji wa nyuki ,kilimo cha alizeti na kuzalisha mafuta ni uongo.
Wakati mfuko wa Grumeti unadai kuwasaidia huduma nzuri ya maji ,kilimo cha biashara ,ufugaji wa nyuki na uvuvi pamona na kuku wa mayai huku wenyeji wakipinga misaada hiyo kwamba haipo kwa upande mwingine viongozi wa Halamashauri ya Bunda na Serengeti wanaisifu kampuni hiyo.
Akizindua tanki la Maji lililojengwa na kampuni hiyo kwa ushirikiano na Halamashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo John Ng’oina aliwaasa wakazi wa kijiji cha Park Nyigoti wasikubali kukosana na kampuni hiyo kwani ni jirani mzuri.
Ngoina alisema kuwa uwekezaji wa kampuni hiyo ni mhimu katika mkoa huo kwani imesababisha wilaya yake imejulikana duniani hivyo haipaswi kubezwa au kulaumiwa kutokana na uwekezaji wake.
Kwa mfano wanadai kuwa ni watoto wa viongozi peke yao ndio wanasomesha watoto wao kwa kisingizio cha kuwalipia watoyo wa masikini ada ya shule ambayo hadi sasa hakuna aliyenufaika nao.
Uchunguzi uliofanywa na tanzania Daima umebaini kuwa kunaudhaifu mkubwa wa kufuatilia malengo na namna ya inavyoendeshwa mifuko inayosajiliwa na wageni.
Uchuchunguzi uliofanywa katika ofisi ya msajili wa mifuko Wizara ya mambo ya ndani umebaini kuwa hakuna ofisa anayefuatilia mifuko hiyo kubaini pesa zinazoingia kwenye mifuko hiyo zinatoka wapi.
Ingawa msajili wa taasisi mifuko hakuweza kupatikana kwa urahisi lakini mmoja wa wazaidizi wake alipoulizwa kama wanafuatilia kwa ukaribu pesa zinazoingia na kutoka kwenye mifuko hiyo alisema hawana bajeti hiyo.
“sisi tunasubiri watuletee taarifa ofisini kila Mwaka kwa kweli hatujui wengi wao wanapotoa pesa na kama wanatimiza malengo yaliyokusudiwa lakini tukibaini wametudanganya kwenye taarifa yao tunaweza kuwashtaki”anasema afisa huyo.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home