Ripoti kamili,ufisadi kilimo kwanza mara-2
*aliyelima ekari moja apata gunia tatu za mpunga,wakulima walaani,
*viongozi wajikatia maeneo nakuacha wakulima hoi.
“tutawanyang’anya mashamba wale wote ambao hawakufikisha magunia hata nusu ya wale waliopata mengi inaonekana ni uzembe na hawakuzingatia utaalam wa kilimo cha mpunga”kauli ya Afisa Kilimo Bunda Lukiko

Serikali yatumia milioni 650 wakulima wambulia gunia 150 tu.
Trekta ambayo imetolewa na mwekezaji uchwara ili apate eneo la kulima baada ya serikali kshindwa kusimamia mradi wa umwagilaji huku vigogo wakitafuna peza zilizotengwa bila kuguswa
HATIMAYE imethibitika kwamba Serikali imetumia zaidi ya shilingi Milioni 650 na kuambulia gunia 150 katika ekari 170 imebainika wazi.
Hatua hiyo inatokana na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mradi huo kushindwa kununua mashine zinazokidhi mahitaji.
Hali hiyo imeleezwa kuwa ni baada ya wizara ya Kilimo na umwagiliaji kununua mashine ambazo zimeshindwa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kupeleka kwenye mashamba yalipo mita 200 kutoka ziwani sawa na milimita 100 usawa wa bahari.
Pamoja na hali hiyo kujitokeza Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo Chibunu Lukiko ametishia kuwanyanganya mashamba wakulima wote waliopata hasara akidai kuwa ni wazembe.
Akizungumza na gazeti hili alisema kuwa “tatizo sio mashine inaonekana wakulima walioshindwa kuvuna hawakufuata maelekezo ya kitaalam kwahiyo tutaangalia huo ni uzembe tunaweza kuwanyanyanya tukawapa wengine”anasema Lukiko
Mradi huo wenye jumla ya ekari 500 upo katika kijiji cha Nyatwali Kata ya Kunzugu nje kidogo ya mji wa Bunda.
Uchunguzi wa wazi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba hadi sasa mradi huo umekumbwa na utata baada ya wizara ya maji kuikabidhi halmashauri mradi huo kimya kimya bila hata wakulima wenyewe kujua.
Utata unaojitokeza katika mradi huo ni baada ya mashine zilizofungwa kwenye mradi huo ,kuungua zote hivyo kusababisha ekari 200 zilizokuwa zimepandwa mazao Mwaka jana kukauka hivyo kusubiri hadi zilipotengezwa jambo lililosababisha mazao kuungua yote.
Baada ya tukio hilo kila mmoja alianza kumtupia lawama mwingine kuwa ndiye anahusika kuagiza mashine mbovu kati ya halmashauri ya Bunda na umwagilia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Bunda, Oyer amasema kuwa hadi sasa halmashauri yake imetumia zaidi ya shilingi Milini .230 ambazo zilitolewa kutoka mfuko wa maendeleo wa umwagiliaji wilaya (DIDF).
Mara ya kwanza walipokea kiasi cha shilingi Milioni 130,000,000 Kwa Mwaka 2007 hadi 2008 na Mwaka 2009 kuelekea 2010 zilitolewa shilingi Milioni 100,000,000.
Oyeri anasema kuwa pesa hizo zote zimetumika kupima na kusanifu mashamba,kukarabati nyumba ya mashine (ambayo hata hivyo haikuonekana)kufunga umeme na kulipia gharama za umeme.
Aidha mkurugezi huyo alisema kuwa pesa zingine zilizobaki zililima mashamba,kununulia mbegu za mpunga na kutoa mafunzo kwa wakulima.
Hata hivyo alisema kuwa Serikali ilitoa shilingi milioni 5 kwa ajili ya kulipia umeme na pesa hizo zilipokwisha ndipo halmashauri ikaanza kuchangia ili kunusuru mazao ambayo sasa wengine wameambulia gunia tatu.
Baada ya hasara hiyo kujitokeza wakulima wa eneo hilo wameamua kukodisha ekari 50 kwa tajiri
Hata hivyo, Lukiko anasema kuwa viongozi waliamua kuchukua maeneo hayo ili kuwahamasisha wakulima nao walime baada ya kuona wamesusia kilimo hicho. mmoja ambaye amewapelekea trekta kuu kuu moja kwa mkataba wa miaka mitano.
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bunda Chibunu Lukiko anasema kwamba watu wanaopaswa kuajibika kutokana kutelekezwa kwa mradi huo ni maafisa wa umwagiliaji kanda kwasababu mradi huo upo chini ya wizara ya maji na umwagiliaji.
Lukiko anasema kuwa ofisi yake ya Wilaya haijui lolote kuhusiana na mradi huo kwani watu waliohusika na utangazaji tenda hadi kusimamia mradi huo ni kitengo hicho cha kanda na ofisi yake haina hata wataalamu wa kufunga mashine hizo.
“kama ni kuwajibika ni hao watu wa kanda waulize walipotoa hizo mashine ambazo zimefungwa na kutengenezwa mara tatu zikiungua , sisi tulichohusika nacho ni kulipia gharama za kulimia trekta ambazo ni Milioni 12 tu”aliwahi kusema Lukiko wakati mashine zilipoharibika.
Katibu wa kikundi wa wakulima Nyatwali, Malongo Mashimo anasema kuwa baada ya kutengenezwa mashine hizo,mapema Mwaka huu halmashauri iliazimia zilimwe ekari 170 tu kati ya 500 kama majaribio.
“wakulima tuliajanda kwa kuchangia gharama lakini baadaye walibaini tena kuwa mashine hizo hazina uwezo wa kumwagilia ekari zote hivyo wakapunguza hadi ekari 100”anasema Mashimo.
Lakini katika hali inayoonyesha kuwa mradi huo umeshindwa kuwakomboa wananchi kati ya ekari 100 zilizopandwa mazao ya mpunga ni ekari 60 tu zilipata maji nyingine zilikauka kabisa, huku wakulima wakiwa wametumia zaidi ya shilingi 90,000 kuandaa mashamba.
Hali hiyo imeleezwa kuwa ni baada ya wizara ya Kilimo na umwagiliaji kununua mashine ndogo ambazo zimeshindwa kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kupeleka kwenye mashamba yalipo mita 200 tu kutoka ziwani.
Kufuatia hatua hiyo hata hizo ekari 60 za mpunga ambazo zilitarajiwa kuvunwa Septemba Mwaka huu zilikauka hivyo wameambulia ekari 42 ambazo hata mazao yaliyopatikana hayaridhishi.
“Ni mkulima mmoja tu ndiye amefanikiwa kupata gunia 28 za mpunga, mwingine gunia 23, watatu gunia 18 ambapo wakulima wengine waliambulia magunia matatu huku wengine wakikosa kabisa”anasema Katibu huyo.
Baadhi ya wakulima wamesema kwamba walitumia zaidi ya shilingi laki tano kuandaa mashamba hayo lakini wamekatishwa tama na serikali kuwapelekea mashine ambazo haziwezi kumudu uwendeshaji.
“mara ya kwanza halmashauri ilitulimia ekari 200 hiyo ilikuwa ni Agosti Mwaka 2009 lakini baada ya mashine kuharibika ,ikabidi walime upya Mwaka huu ekari 100 ambazo tumeambulia 40 tu huku zingine zikikauka”anasema mkulima Marko Okebe.
Hata hivyo wakulima hao wanadai kuwa mradi huo hivi sasa umevamiwa na viongozi wa Halmashauri ambao wamejikatia maeneo yanayofikiwa na maji huku wakulima wakipewa amaeneo ambayo hayana maji.
Miongoni mwa Viongozi wanaomiliki mashamba katika maeneo hayo na wamefanikiwa kupata mazao ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda,Mkurugezi maafisa kilimo na watendaji wengine, huku mkuu wa Mkoa wa Mara akijitoa baada ya kuona ubabaishaji umezidi.
Madai hayo yanapingwa na katibu wa kikundi cha wakulima hao ambaye alisema kuwa
“tumewakubalia walime hapa ili waweze kutusaidia kulipa umeme kwa mfano sasa hivi kila mwezi tunalipa umeme Milioni mbili ambazo halimashauri inatuapa ,unadhani kama wasingekuwa na maeneo hapa wangeulipia umeme huo?”alihoji Mashimo
Alipoulizwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sprian Oyer kama hamashauri yake inalipia umeme kwasababu anamiliki shamba kule alisema,
“kazi ya Halmashauri ni kuhakikisha wananchi wanapata faida, hatuwezi kuacha mazao yateketee kwa kukosa umeme…halmashauri inalipia gharama za umeme kwa wastani wa shilingi Mil.1,200,0000 kwa mwezi.
Afisa Mazao wa Bunda Balisamaki Shija anasema kuwa mradi huo ulikuwa ukabidhiwe kuanzia April Mwaka huu ili uweze kutumika kumwagilia ekari 200 zilizokuwa zimeandaliwa kama majaribio lakini mashine zilizofungwa zilishindikana kuashwa.
mhandisi wa Kampuni ya Davis, Eng.Shayo Denis anakiri kupewa tenda ya kusambaza mashine hizo na wizara ya Kilimo na Umwagiliaji kitengo cha kanda lakini akasema kuwa wenye majibu zaidi ni kitengo hicho.
(Ni kweli sisi tulipewa kazi ya kuleta mashine hizo na kufunga …nakumbuka tuliwauzia takribani shilingi Milioni 100 lakini tulipokwenda kufunga tulikuta wameweka vipuri vingine (Non return Valve) zingine hivyo kukatokea matatizo hayo naamini wao wanamajibu mazuri” anasema Shayo
alipotafutwa Kaimu Mkurugenzi wa Kanda umwagilaiji (zone Irrigation) Eng.William Karumuna, ambaye kitengo chake kinadaiwa kuusimamia kupitia wizara ya maji alikataa kwa nguvu zote ofisi yake kuhusika na mradi huo.
Karumuna aliitupia mzigo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwamba mradi huo ni wa kwao ndio wanajua walipopata mkandarasi aliyeshindwa kuleta mashine za kuvuta mashine na kusukuma katika mashamba ya wakulima mita chache kutoka ziwa Victoria.
“ sisi hatusimamii miradi ya umwagiliaji ni kazi ya halmashauri hiyo, kwenye kitengo chetu hapa hatuna hata wataalam, wa kufunga mashine lakini wao wanao wale wa Idara ya maji waulize kwanini hawakuwatumia”anasema Kurumuna.
Alisema kuwa ofisi yake kwanza haina hata bodi ya Zabuni hivyo hairuhusiwi kufanya manunuzi yanayozidi shilingi Milioni 20 wakati ule mradi ni wa mamilioni ya shilini na wao wanaruhusiwa kisheria kutangaza tenda kubwa kama hiyo.
Kamuruma naye kama wenzake alitupia mzigo ofisi ya Mkurugenzi ya wilaya hiyo kwamba ndio ilihusika na masuala yote na wao walihusika kwa sehemu ndogo tu ya kuchora michoro ya eneo lakini watu waliohusika kuagiza hizo mashine mbovu ni Halmashauri.
Kauli hiyo inapingwa vikali na Afisa ugavi wa Halmahauri hiyo Dinawe Samweli anayesema kwamba ofisi yake haijawahi kutangaza hiyo tenda kwani shughuli zote za manunuzi zilifanyikia kanda na wao wakawaletea hizo mashine tena siku ambayo ni ya mapumziko.
“ninachokuambia Mwandishi katika ofisi yangu hapa kuna kitabu cha makabidhiano ya hizo mashine kutoka umwagiliaji kanda , wao ndio wanajua walipozitoa na bei walizonunua sisi walitukabidhi wala hatuhusiki na huo mradi wasikwepe”alisema Samweli
Alipoulizwa kuwa huo mradi upo chini ya nani, Samweli alijibu kwa haraka kuwa upo chini ya Wizara ya Umwagiliaji ambapo hicho kitengo cha kanda ndio wanahusika na kila kitu, kwani ipo miradi mingi wanasimimamia hata ile ambayo ipo kwenye halmashauri.
Aidha katibu wa kikundi hicho alisema kuwa katika msimu wa kilimo ambao umeanza mwezi huu wameazimia kulima ekari 40 tu na kati ya hizo zipo ekari 18 za viongozi wa Halmashauri ili kupunguza hasara zaidi.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home