Kuzama kwa Meli Z. kumetufumbua macho wananchi
Uzembe Uliosababishwa Kuzama kwa meli Ziwa Victoria Tumewafahamu Viongozi wa Serikali.
• Ni watu wanaopenda kutumia Maafa ya watanzania ili kujitangaza.
• Ghorofa iliporomoka Dar viongozi walikatisha vikao mhimu Arusha na kuwahi makamera kwenye tukio.
“ waziri mkuu alikimbilia nini kuja Dar es Salaam aliposikia kuwa Jengo la Hoteli limeporomoka na kuacha kikao kilichokuwa kimeishwa na Rais kinaendelea Jijini ,Arusha wakati aliposikia Meli imepotea na kuhofiwa kuuwa watu zaidi ya 28 Ziwa Victoria hakujaribu kwenda kutia muguu ,ili apate habari ni kanini Chombo kilichokuwa na Binadamu kipotee wiki nzima bila serikali kuarifiwa’’?
Wananchi wa kanda ya ziwa wangependa waelewe thamani yao katika serikali hii iko wapi ,kama mtu mmoja amajeruhiwa kiongozi anakatisha ziara kwa aajili ya hilo iweje wafe watu miamoja serikali imtume naibu waziri ,kwenda kwenye tukio ,tena lenye utata?
Takribani wiki tatu zimepita toka tangu Taifa limepata Msiba mkubwa wa kuzama kwa meli ziwa Victoria ,lakini tukio hilo likiwa limechukuliwa kama jambo dogo na watu wakiendelea kupiga siasa kama hakuna tukio baya la maafa liikumba Taifa na Kupoiteza roho za watu zaidi ya 28 ambao miili yao imeshindikana kupatika.
Sitaki na mimi nionekane kuwa ni mzembe kwa kuchelewa kuandika hilo tukio leo najitikeza hata bora msomaji nibainishe kabla hujaanza kusoma kuwa kila nilipokuwa najaribu kulifuatilia hilo tukio ili nipate data za kuandika makala nilikuwa nashindwa kutokana na jazba iliyokuwa inanishika hasa kutokana na tukio linavyosimuliwa na jinsi lilivyo shughulikiwa na mamlaka husika.
Ni kweli nilikuwa nakumbwa na Jazba ambayo mara zote nilikuwa naishia kulaaumu vyombo vya habari jinsi vilivyolipoti tukio hilo na kufanaya viongozi wa serikali waone kama hakuna maafa ya kitaifa na kuendelea kula kuku kwa mlija kwenye ziara zao za kawaida walizokuwa wameandaa.
Hata baada ya kuona hasira zangu zimeishia nimekaa chini nikatafakari nikaona stakuwa nimewatendea haki watanzania hasa wakazi wa kanda ya Ziwa kama sitatumia taaluma yangu niliyopewa na Mwenyezi Mungu kuwakemea na viongozi wababaishaji wanaopenda kutumia maafa kujitaza wanapoona kunawaandishi wa habari na kamera zao.
Kwanza ni bora nianze kubainisha sababu iliyofanya iliyofanywa nishikwe na hasira iliyoambatana na Jazba nikashindwa kuandika kila nilipojaribu kuandika mara zote machozi yalikuwa yanaziba macho.
Kuanzia juanuari Mwaka huu hadi Machi 31,Ripoti kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya usafiri wa Anga na Majini (SUMATRA) ilitoa takwimu zilikuwa zinaonyesha kwa kipindi hicho kifupi zaidi ya watu 61 walikuwa wamefariki Dunia ziwa Victoria ,kulingana na maeneo yaliyotajwa ni kama na uzoefu wangu kwenye hilo ziwa Ajali nyingi zililekodiwa mkoa wa Kagera na Moja Kibara Bunda.
Ingawa hizo takwimu zilitolewa na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Majini SUMATRA, King Chirangi niliingiwa na wasiwasi juu ya utendaji wao wa kazi hasa baada ya kumuuliza maswali kadhaa, nay eye kujibukuwa walikuwa hawajajiimalisha kwani walikuwa ndio kitengo hicho kimeondolewa kwenye Wizara ya maji!
Wakati huo tunaongea naye ilikuwa ni siku chache tangu boti ya mizigo iliyokuwa imebeba abiria kuzama Machi 31 mwaka huu na kuuwa watu zaidi ya 36 , baada ya kuzama na miili haijaanza kuibuka tulitangaziwa ni watu 21 wamekufa maji lakini baada ya miili kupatikana matokeo yalikuwa ya kushangaza na na namna miili hiyo ya watanzanaia ilivyozikwa hatukuelezwa !
Maana nilisikia kiongozi mmoja kutoka mkoa wa kagera anasema ni vigumu kutambuliwa kulingangana ilivyokuwa imeharibika ,na tatizo lingine ambalo hakulitaja hapakuwepo na majina yaliyokuwa yameandikwa ambayo yangetumiwa kutangaziwa ndugu na jamaa wafike kutambua miili yao ndugu kama ilivuyoadhimiwa miaka 10 nyuma baada ya kuzama Meli ya MV Bukoba na kuleeta maafa ya kitaifa.
Siku chache baada ya Mkurugenzi huyo wa Ulinzi na Usalama wa Majini King Chirangi atoe takwimu hizo akimaanisha kwamba ni za ziwa lote, Mkuu wa Wilaya ya Mleba aliitisha kikao cha wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo na kutoa takwimu zilizonishangasha kwani alisema kuwa hicho kifupi watu zaidi ya 60 walikuwa wamezama maji kati ya januari na machi katika wilaya hiyo.
Hapo ndipo utata wa Takwimu ulizidi kunichanganya kwani SUMATRA watu 61 ndio wamekufa ziwa viktoria kwa Ajali ambazo Chirangi anakiri zingeweza kuepukwa kama uangalizi ungekuwepo wakati huohuo na kipindi hicho hicho walaya ya Mleba inasema imepoteza watu zaidi ya 60 je SUMATRA wanapata wapi hizo takwimu za kudanganyia Umma ?!
Nimetangulia kuonyesha wasiwasi wangu jinsi viongozi wanavyotumia maafa kujinufaisha ,na kuelezea jinsi nilivyopata wasiwasi na hizo takwimu hasa kwa kuwa naelewa mazingira ya ziwa vikitoria ,kwani wakati ananipa hizo takwimu hazikuhisha Ajali zinazotokea mkoani mara hasa vizinga vya Kinesi ,bwai ,paris na kukiri n.k sio kwamba ni salama hapana takwimu hawana uliza !
Wala hizo Takwimu hazikutaja kabisa mitmbwi ya wavuvi wanakufa wakati wanavua bila kutumia maboya au kugongwa na meli ya MV. Victoria , Serengeti na Mv .Butiama ambazo mara kwa mara zimekuwa zikisababisha mauaji kwa kugonga mitumbwi ya wa uvuvi usiku wanapokuwa wametega halafu wamelala.
Maana inaeelezwa Nahodha huwa wanalala wanaacha chombo kinasafiri chenyewe hujikuta wanawagonga wavuvi kila mara na hizo takwimu hubakia palepale ,na maisha ya wavuvi hubaki kuwa kama machoizi ya Samaki kwenda na Maji ! Ndio maana naendelea kuwasakama Sumatra kuwa utendaji wao wa kubakia Ofisini hawana hata Takwimu za Ajali mkoani Mwanza ,kama Magu.
Ndio maana wanategemea takwimu kutoka wilaya ya Muleba kuzitumia kuakilisha maisha ya wavuvi ziwa zima kwa kuwa serikali wilaya ya Muleba ipo macho inalekodi matukio yote yanayowakuta wavuvi wake kwa kujali faida na kipato wanachowaingizia.
Ndio maana leo nashawishika kusema kuwa Ajali nyingi zinazotokea ziwani humo uzembe wa viongozi toka serikali yetu ambayo imejenga utamaduni kuwa hadi yatokee maafa ndio waanze kukemea.
Nasema hivyo kwa sababu Mei 21 mwaka 96 miezi mitano baada ya serikali ya awamu ya tatu kuwa imeingia madarakani ,Taifa lilishuhudia maafa makubwa ya kitaifa baada ya meli ya MV Bukoba kuzama Ziwa Victoria na kuuwa watu takribani 12 kwa makosa yanayodaiwa kuwa ni ya kuzembe ambayo yangeweza kuepukwa.
Tulishuhudia viongozi wakuu wa kitaifa wakifika kule kusikia maelezo ya tukio na kukemea vikali kasha kutoa tamko kali kuwa yeyote yule anayemiliki chombo cha usafiri majini ahakikishe anaweka vifaa vya uokoaji na kuandika majina ya abiria wote wanaosafiri.
Lakini baada ya muda tamko hilo lilikosa wafuatiliaji na wahusika kulipuuza wakendelea kufanya wawezalo hadi kusababisha ajali za mara kwa mara kana kwamba serikali imekwenda likizo na wahusika walioteuliwa kuangalia maisha ya watu yanakuwa salama wanaendelea kugawana mrahaba ofisini kama hawapo.
Wakati viongozi wa serikali wakizi kuanya uzembe maisha ya wavuvi yanateketea kama vile hawaiingizii serikali kipato kikubwa kinachotokana na kuuza minofu nje na kupata pesa nyingi za kigeni matajiri nao wameendelea kutumia mwanya huo kwa kucheza ‘dili’ na viongozi wa serikali kwa kumaliza watu.
Tukio la juzi la Meli ya Mv Nyageni kuzama na watu zaidi ya 28 katika ziwa Victoria kwa muda wa wiki nzima bila wahusika kufahamu wala Serikali kutarifiwa ni la kustaajabisha linalotakiwa maelezo ya kina tena serikali ikiwa imekunja uso kabisa.
Kwa wale waliwahi kutumia usafiri katika ziwa hilo watakubaliana nami bila kigugumizi kuwa watu walipoteza roho zao ni zaidi ya 28 kwa wale tunaofahamu shida ya usafiri na nauli yake hasa ukilinganisha kuwa chombo hicho kilikuwa kinatoza nauli ya chini.
Tukio hilo ni la kustaaajabisha kwasababu kama Jiji la Mwanza lenye wandishi wengi Serikali likashindwa kufahamika hadi wengine tulilisikia kwenye vyombo vya kimataifa kama BBC radio je yanayotokea huko ziwa Tanganyika ambako wandishi hawafiki inakuwaje ?
Ni watanzania wangapi wamekwishapoteza maisha kwa aajili ya uzembe huo katika ziwa Nyasa na Rukwa ,je tuendelee kuisifu serikali pale inapoona tukio limefanyika katikati ya jiji la Dar es Salaam, pale inapokuwa imebomoka nyumba ndio viongozi wanajipnga kila mmoja anakoromea wahusika ?
Staki tundelee kusifiana wakati tunapokuwa tunaweka maisha yetu rehani ni Majuzi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa amewaita Mawaziri wote Arusha kuwafundisha maadili nya kazi lakini lilipoporomoka jingo la hoteli jijini Dar na kuuua mmoja na kujeruhi mwingine Waziri Mkuu Edward Lowassa alikimbia toka Arusha kuja kushudia.
Baada ya Lowasa kushuhudia lile tukio watu wengi walimsifu na baadhi ya vyombo vya habari vikafikia hatua kuponda waziri mkuu mstaafu Eti kipindi MV Bukoba ilizama aliacha msiba akaenda ziara nje, lakini huyu amekatisha vikao na kuja kusimamia oparesheni na kuamuru mkandarasi wa jengo akamtwe haraka.
Kumbe pamoja na hizo sifa Lowassa alikuwa anajua anachofanya yeye ni Mwanasiasa alijua kule kuna vyombo vya habari vya kimataifa na makamera ataonekana na kusika kilahisi, kwenye tukio hilo lilikuwa limeuwa mtu mmoja na kuacha kelele nyingi za kuanza kuchunguza majengo mengine.
Kelele hizo inasadikiwa zimehifadhiwa uvunguni zinasubiri tena Jengo la mafuta hause liporomoke waanzee tena kupiga kelele eti wanachunguza mkandarasi aliyelijenga na kuangalia majengo mengine kama ni salaama, wakati tayari likiwa limeuwa.
Juzi wakati Meli ya Mv Nyamgeni ilipozama wakazi wa kanda ya ziwa tulitegemea kumuona Waziri Mkuu akirudi kwa kasi kama alivyokwenda jijini kuwahi tuykio kabla mapaparazi hawajaondoka ,na kufika huku kuwaamuru wahusika ambaye ni mmiliki wa chombo,
TRA,na SUMATRA mkoa wa Mwanza na Bukoba wakamate!
Lakini kumbe haikuwa hivyo matokeo yake ikawa kinyume na matarajio yetu kwani kwenye tukio hata waziri anayehusika na Wizara hakufika matokeo yake alitumwa Naibu waziri ambaye tulimsikia akihojiwa na BBC akishindwa kutoa maelezo yenye kueleweka kama waziri.
Hazi nazo zikawa hasira na machungu kwa wakazi wa kanda ya ziwa Huku waziri mkuu na waziri husika wakiona maisha ya watanzania yaliyopotea kwa uzembe hayana thamani wakaamua kwenda kula kuku mikoa ya kusini kwa kutembelea barabara zianzo limwa huko.
Kwa sehemu tukio la Mwanza linafanana kidogo na tukio la Jijini kwani ,tukio la jijini ilidaiwa mkandarasi alijenga lile ghorofa lililoporomoka Kijitonyama bila kibali na lilikuwa limesimamishwa
na, katika ile ajali iliyotokea Mwanza ilidaiwa kuwa ilikuwa imesimamishwa ,kwakuwa ilikuwa mbovu tangu mwaka 2004 lakini ikaendelea kutembea.
Maswali yanabaki palepale ni nkwanini serikali imeshindwa kuamuru wahusika wakamatwe mara moja na kupata jibu aliyeiruhusu ile Meli ikaanza kutembea na je kazi ya SUMARA ni nini au kungoja mapato ofisini,ilikuwaje meli ikazama wiki nzima bila serikali kutarifiwa ,kwati wahusika walifahamu kuwa imeondoka lakini imeshindwa kufika kama ratiba inavyoonyesha.
Kuna maelezo kuwa meli hiyo ilikuwa hainha mawasiliano ,ndio lakini je wahusika kutoka Bandari ya bukoba walishindwa kuwasiliana na wa mwanza kuwaeleza kuwa meli imeoondoka ili na wale wakingoja ispofika kwa mdu ulopangwa watoe taarifa mamlaka husika ?
Hapa kuna ajenda ya siri roho za watu haziwezi kupotea hivihivi siamini kama Nahodha na wasaidizi wake hakuna ambaye hakuwa na simu ya mkononi ambayo wahusika walikuwa wanajua namba zake,kama sio kulijua tukio halafu kunyamaza nalo.
Nimeanza kwa kusema boti ilizama wakatuambia watu 21 wamekufa lakini miili ilipoopolea walipatikana 36 ndio maana sikubaliani na idadi ya watu hao 28 tunaoambiwa wakati inafahamika MV Nyamgeni ni kwa ajili ya kusafirishia watu na mizigo!
Serikali isilishugulikie tatizo hilo kiusanii kwakuwa labda vyombo vya habari jijini humo haviangazi macho yake ziwani kama vile vya bukoba, nakucha roho za wavuvi zikiendelea kutekketea kwa manufaa ya wachache, tunawaomba waache kucheza na maisha ya watu watupatie maelezo ya kina ninani aliyehusika kukiruhusu chombo kusafiri bila kuandika watu majina na bila kuwa na maboya.
Viongozi wa serikali acheni hizo za kusubiri tukio lipokatikati ya waandishi ndio mnakwenda kujitangaza kila mmoja kuonyesha hasira zake huku pale pengine wanakwepa kama hakuna tukio wakati hili ni la maafa ,na mamlaka zinazohusika ziwajibike mara moja.
Kuna mwandishi mmoja aliandika katika makala yake wakati Raisi kikwete alipokuwa ametimiza siku miamoja kuwa ni mapema kuisifu au kuhikumu serikali hii mbayo imetimiza siku miamoja lakini isipoangalia yaweza kujirudia yale ya Mkapa,na mimi namaliza kwa kusema ikiwa msomaji ataona nimeongeza chumvi nay eye aongeze maji kisha aonje aone ladha yake,s
0743 339 579 mobinsons @ yahoo. com

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home