Wednesday, March 7, 2007

Mwenyekiti Chadema apongezwa

Na mwandishi wetu

WANANCHI wamempongeza Mwenyekiti wa Taifa, wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa kupata mualiko wa kufanya ziara ya siku 10 nchini Uingereza.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima, wananchi hao walisema kwa hatua hiyo Mbowe sasa atakuwa mwanasiasa wa kimataifa.

“Mzee wa Helkopta kwa sasa si mwanasiasa wa Taifa peke yake bali kwa sasa amevuka mipaka mpaka kufikia mwanasiasa wa kimataifa,” alisema Hassan Kamau.

Wakati mkazi mmoja wa Tandika, Kabuche Nyakira alisema endapo Mbowe atapata ujuzi zaidi wa vyama vya nje ataleta upinzani mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2010.

Mbowe amemwagiwa sifa hizo baada ya juzi kupata mwaliko wa ziara ya siku 10, kutoka katika Chama cha Conservative cha Uingereza.

Imeelezwa kuwa katika ziara hiyo Mbowe ataongozana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe.

Katika ziara hiyo watapata fursa ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho utakaofanyika jijini Manchester.

Aidha atatambulishwa rasmi kwa Mwenyekiti mpya wa Conservative, David Cameroon.

Ziara hiyo itakuwa ya pili kwa Mbowe kufanya tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini mwaka jana.

Mwisho.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home