WILAYA YA TARIME YAKABILIWA NA MIGOGORO YA ARDHI.
• VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI WA NORTH MARA VIMEATHILIKA ZAIDI.
• MABARAZA YA ARDHI YA VIJIJI, WENYEVITI VYANZO VYA MATATIZO.
• UZEMBE WA SERIKALI KUPIMA KUTOPIMA VIWANJA UNACHANGIA .
Na Hellena Magabe Tarime.
TATIZO la migogoro ya ardhi ni moja ya matatizo ambayo kwa sasa yanashika nafasi kubwa katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara ukichia mbali matatizo mengine kama wizi wa mifugo.
Upungufu wa ardhi na ongezeko la watu inasemekana kuwa ndio hasa chanzo kikuu cha migorogoro na vita vya mara kwa mara.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya watu wenye uelewa mdogo kufikiri kuwa Wilaya ya Tarime inaongoza kwa mauji,wizi wa mifugo ukatili wa kijinsia ,ukeketaji na mengineyo mengi,bila kufanya kwanza utafiti na kubaini chanzo chake.
Hali hiyo imenisukuma kufanya uchunguzi wa muda mrefu na kugundua kwamba wenye viti wa vijiji pamoja na mabaraza ya ardhi ya vijiji na serikali ni chanzo cha migogoro hiyo isiyoisha.
Migogoro ya ardhi wilayani hapa imegawanyika mara tatu ipo ya Serikali na Wananchi ya wananchi wenyewe kwa wenyewe , mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi huo wa North Mara.
Migogoro yote ya aina mbili ni sugu na hasa kwa kuzingatia kwamba chanzo cha ugomvi wa muda mrefu unaotokana na vita ya koo wilayani hapa umebainika kuwa chanzo ni ardhi.
Sehemu zote zenye ugonvi wa ardhi ukiuliza hazijapimwa watu wanaishi kienyeji na nyingie mabaraza yanalaumiwa kutowatendea haki wananchi.
Pia Wenyeviti wanalalamikiwa kwa kushuirikiana na mabaraza kugawa viwanja kiholela kitendo kinachozidisha utata kwani kwa karne hii serikali ilitakiwa kupima maeneo yote ili kila mtu amiliki eneo lake kihalali.
Nikianza na mfano wa kwanza wa mgogororo baina ya jeshi la IWTZ na wananchi katika kijiji cha Ronsonti mjini Tarime ambapo zaidi ya kaya 31 zimezuiliwa na jeshi kuendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji tangu Mwaka 2008 .
Chanzo cha mgogoro huu unaotishia amani wakazi wa hapa ni wananchi kuribisha jeshi kwa muda katika eneo lao mwaka 1979.
Jeshi liliomba hifadhi kwa muda katika kijiji cha Rosonti baada ya Mvua kubwa kunyesha na kushindwa kuvuka mtoni kwajiri ya kwenda nga’mbo ya pili kwajili ya mahitaji wakadai wakijenga daraja wataondoka.
Hata baada ya daraja kukamilika hawakuondoka ingawa walikuwa wanakaa Nyandoto ingawa bado wako huko na ng’ambo ya pili wameteka eneo la kijiji cha Rosonti na kuzuia shughuli zote kufanyika huo mgogoro unaendelea kufukuta hadi leo bila kutatuliwa.
Mfano wa pili ni wa Waziri wa ajira na ajira na kazi Gaudesia Kabaka ambaye anamgogoro na mzee Ally Mrimi na kesi yao iko katika baraza la ardhi na makazi la wilaya chanzo ni waziri huyo kumega kisehemu kidogo cha Mrimi na kutengeneza barabara ya kuingilia kwake bila ridhaa yake.
Mfano mwingine ni mgogoro wa wananchi na Serikali nilibahatika kukutana na watu watano ambao wameshinda kesi yao ya ardhi katika baraza la ardhi la wilaya nje ya baraza hilo wakiwa nafuraha kwa kushinda kesi yao dhidi ya mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Murito Nyamongo ambaye aliamua kumtumia wakili wake Bw.Patric Makinda Mohere lakini akashindwa.
Marwa Masero pamoja na Sephani Mahati Chacha ni miongoni mwa watu watano walioshida kesi iliyoanza kuunguruma katikabaraza la ardhi October 2010 na kufanikiwa kushinda Julai 14 Mwaka 2011 ambapo waliisifu Serikali na mahakama hiyo kwa madai kuwa imewatendea haki.
Walidai kuwa Mwaka 1994 aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji kwa jina Joseph Mwita Muhori kwa kushirikiana na baraza la ardhi la kijiji aligawiwa watu wapatao 61 eneo ambalo ni la wazi kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo watu hao wakiwa wanatoka katika kijiji kimoja.
Lakini baada ya mwenyekiti mwingine kuchaguliwa mwaka juzi 2009 kwa jina Joseph Mangwe aliwazuia wao jambo ambalo hawakuridhika nalo kwani wengine hawakuzuiliwa na wakati wanazuiliwa walikuwa wame lima tayari kwa kupanda mbegu walipojaribu kugoma mkutano wa kijiji uliitishwa na mwenyekiti kwa lengo la kupiga kura.
Wanaeleza kwamba kura zikapigwa zikawaangukia walewale watano ambao mwenyekiti aliwazia kulima ikaonekana ni mpango umepangwa kwa kuwa hawakuwa na maeneo mengine waliamua kufika katika baraza kupata msaada wa kisheria.
“ Tulitaka tuanzie kwenye barazala ardhi la kijiji lakini tukaona kwamba mwenyekiti wa baraza la ardhi la kijiji ni baba yake na mwenyekiti wa kijiji anayetushtaki hivyo tukaona hatutasikilizwa na tunapoteza muda wetu bure tukaona bora tuje kwenye sheria” anasema Masero
Migogoro ya aina hii ni michache ukilinganisha na ya wananchi wenyewe kwa wenyewe pamoja na ya mgodi na wananchi ambayo ni tatizo kubwa na lina changamoto nyingi.
Bila Serikali kuingilia kati hatima itakuwa mbaya sana hata hivyo washindi wa kesi hii walihisi mwenyekiti wao anataka kuwapora eneo hilo kwa kwa nia ya kuuzia mgodi ambao unaendelea kupora ardhi nyingi kwa udanganyifu.
Ndani ya eneo la Nyomongo kijiji cha Nyangoto kwa upande wa mgogoro wa wananchi wenyewe kwa wenyewe nilikutana na Mkazi mmoja kwa jina Mangwe Ntwega siku hiyo hiyo naye alipewa eneo ekari 20 mwaka 1994 akawa amepakana na Bi. Ghati Ryoba bila mgogoro wowote aprili mwaka huu mama huyo akamshtaki kuwa amemwingilia eneo lake.
Alidai kuwa mama huyo alimfikisha katika baraza la ardhi la kijiji ambapo amri ilitolewa amgawie ardhi yake nusu kwa nusu jambo ambalo hakuliafiki kugawa ardhi yake ambayo ameimiliki kwa muda mrefu hivyo ameamua kufikisha malamiko yake katika baraza la ardhi.
“ Najua anataka eneo langu ili akauzie mgodi nashangaa kuona ananga’anga’ania eneo langu wakati ana eneo kubwa sana kuliko langu miaka yote hiyo tumekaa kwa amani mbona hakuwahi kulalamika” alisema.
Ukiangalia mifano ya wakazi wa Nyamongo katika migogoro hiyo miwili tofauti utakuwa umegundua jambo kuwa baraza la vijiji na wenyeviti na serikali za vijiji ni tatizo vilevile mgodi nao unahusishwa.
Nikija kwenye mgogoro baina ya wananchi na wananchi ni mingi ukiwemo mgogoro sugu ambao ulishasababisha maafa katika koo ya Wanchari na Warenchoka ambao ulisababisha watu kadha kupoteza maisha lakini nitatolea mfano kwa mtu mmoja ambaye ameshida kesi mara mbili lakini badaye imefufuliwa tena baada ya miaka kadaa kupita.
Joseph Opija ana ekari 3 ambayo wanaigombea na Obimbo Ondogo ambapo Opinga alidai kuwa mwaka 1995 alishtakiwa na Ondongo kuwa amemuingilia ardhi yake kumpatia mtu akajenga katika eneo hilo aitwaye Athony Okey alipeleka malalamiko kwa mtendaji wa kata akashindwa hivyo wakamua kwenda mahakama ya mwanzo na kushinda ambapo hakimu alikuwa N.M.Nyamhanga.
Mwaka 1997 Opinga aliamua kwenda mahakamani kwa hakimu Salum Manyango na kushinda kesi hiyo lakini Ondogo alipeleka malalamiko kwenye baraza la ardhi la kijiji na mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Joshua Adrea ambaye aliamua Odonge apewe ardhi hivyo Opinga ameamua kufungua kesi Mwaka huu june 24.
Tatizo hili kwa upande wa vijiji vinavyozunguka mgodi ni kubwa kwa kiasi kikubwa na jambo ambalo limechangia ni viwanja kutopimwa mgodi umekuwa ukifanya tathimini zake pindi unapohitaji eneo kwa kukadilia kwa hatua na kuwalipa watu fidia ndogo sana.
George Gabriel ni mkazi wa Nyakunguru anaelezea tatizo hilo lilivyo kubwa katika kijiji chao ambacho ni moja ya kijiji kinachozunguka mgodi ambapo adai wenyeviti wa vijiji na baraza la ardhi wamekuwa watu wa tamaa wanagawa kiwanja kimoja hata zaidi ya watu watatu.
“ Utakuta kiwanja kimoja wanakigawa kwa watu zaidi ya mmoja huyu akija akitoa hela anapewa hatimaye sasa unakuta kiwanja kimoja kinagombaniwa na watu wanne na hata kuna wanadugu wawili wanagombania kiwanja kimoja na watu wengine waligonganishwa kiwanja ni Nyamokwe Gibere pamoja Chawari Wambura Chawari” alisema.
Ghati Methusera ni mkazi wa uwanja wa ndege kijiji cha Nyakunguru, ameporwa ardhi yake na mgodi tangu mwaka 2005 , mgodi kwa kutumia njia ya udanganyifu kwa kumrubuni mume wake na sasa amejibana kwenye kieneo kadogo.
Anasema kuwa mgodi ulifanya tathmini katika ardhi yake yenye ekari 79 akiwa hayupo ambapo ulimlipa mume wake shilingi million 30 pesa ambayo ililipwa kwa ajili ya katani na miti ambapo ardhi haikuhesabiwa hivyo haikulipiwa mpaka leo.
“ Badaye wakaja tena wakapora ekari 80 eneo jingine bila mkataba eneo ambalo mpaka sasa waling’ang’ani na walikuja kulipora mimi nikiwa Dar es salaam yaani sina pakulima hata bustani ya mboga tunaomba serikali itusaidie jamani” alisema
Wakazi wengi wa Nyakunguru wanakabiliwa na tatizo hilo na mwezi ulioisha ilifanyika tathimini ya kinguvu nguvu kwenye ardhi zao na wanalazimishwa kulipwa fedha kidogo kulingana na ukubwa wa aridhi zao.
Nilipomwuliza afisa ardhi wa wilaya ya Tarime kwanini tatizo hili ni kubwa wilayani hapa aliniambia chanzo kikubwa ni tatizo la viwanja kutopimwa pili kwamba ongezeko la wakulima na wafugaji.
“ Unajua hata hivyo watu wanazaliana kila siku lakini ardhi haiongezeki tangu uhuru ni ile ile kwahiyo lazima tatizo la ardhi liwe kubwa lakini..mkoa unampango wa kupima viwanja vyote na tutaanzia wilaya ya Bunda” alisema.
Jambo jingine anasema ni tamaa ya wanandugu kugombania ardhi za mirathi pindi ndugu zao waapofariki dunia na kuongeza kuwa wengine wana tamaa za kutaka maeneo makubwa kwajili ya kuendesha shughuli zao za kilimo.
Pia anasema kuwa jambo jingine ni uelewa mdogo wa watu juu ya utunzaji wa ardhi ambapo hakuweza kutaja takwimu ya watu ambao wanakabiliwa natatizo hili angalau kwa mwaka jana hadi sasa.
Nilibahatika kupata takwimu kwa mwaka huu pekee tangu mwanasheria wa haki za binadamu wilayani hapa Bw. Bonny Matto ambapo anasema kuanzia January mpaka aprili watu wapatao 114 wamefika kituoni kwake kuomba msaada na miongoni mwao wamepeleka kesi zao mahakamani zinaendelea kushughulikiwa.
Bonny Matto anatupia lawama wenyeviti wa vijiji na mabaraza ya vijiji kwa kuvunja sheria za ardhi namba 5 ya mwaka 1999 kifungu 8:(1) kisemacho kuwa, Halmashauri ya kijiji kwa kuzingatia masharti ya sheria hii itawajibika kusimamia ardhi yote ya kijiji.
Anamaliza kwa kusema kuwa kifungu kingine 5;(5) kisemacho Halmashauri ya kijiji haitagawa au kutoa hati miliki ya kimila bila ya kwanza kupata idhini ya mkutano mkuu wa kijiji, jambo linalowakwazawatu kupima maeneo yao.
0758997070,0782 997070,0655997071

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home