Wednesday, January 9, 2013

Inakuwaje Wajawazito Buchosa wajifungua bila kupimwa?




Na Mobini Sarya

ZAHANATI tegemeo pekee ambayo ni tegemeo kwa wakazi 25000 wa visiwa vya Sengerema iliyopo katika kijiji cha Lushamba,Buchosa mkoani Mwanza haina vipimo vya maabara wala ukimwi kwa wajawazito.

Zahanati hiyo ambayo kimsingi ilipaswa kuwa kituo cha afya imekosa vipimo mhimu vya kupimia upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) na malaria jambo linalowazimu akimama wanaohudhuria kiliniki  kujifungua bila kupimwa.

Mganga muuguzi wa zahanati hiyo,Bi.Yasinta Midale ameliambia nipehabari kwamba wana zaidi ya miezi mitatu hawajapata vipimo hivyo jambo linalowalazimu akinamama kujifua katika mazingira hatarishi.

“Ni hatari kwa mjamzito kujifungua bila kupimwa kama ana maambukizi ya ukimwili ili aweze kupewa ushauri namna ya  kumkinga mtoto atakayezaliwa asipate maambukizi ya Ukimwi”anasema Midale.

 Kwa mjibu wa takwimu zilizotolewa na mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba,Deus Bugumba ameliambia Tanpress kwamba kijiji chake kina wakazi zaidi ya 25000 wakiwemo wavuvi wanaokalia visiwa saba hivyo wote wanategemea zahanati hiyo.

“wote wanakuja kutibiwa hapa Kanyara ndio kuna zahanati wakazidiwa inaitwa gari kutoka mjini sengerema Km.80 ni kama mwendo wa masaa matatu hivi kwa gari ya wagonjwa hadi hapa kijijini”anasema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kama mzee Jonathan ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho amedai kuwa zahanati hiyo licha ya kuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wa hapo lakini haina huduma yoyote ya kiafya.
“kwanza sisi tulitakiwa kuwa na kituo cha afya eneo hili sio zahanati…hatuna madaktari hata wa kuweza kuzalisha mjamzito kama anatatizo…mimi mkamwana wangu alitaka kujifungulia hapa ikashindikana ikabidi niingie gharama za kumsafirisha hadi sengerema”anasema mzee Jonathan

Anatolea mwito kwa serikali kuwajengea kituo cha uhakika ili waweze kupata huduma za afya kama walipa kodi wengine tafauti na sasa ambapo hupoteza maisha kila  mara.    
 

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home