MASAI KSHINNDA GARI LAKINI VIPI ANGESHINDA NG'OMBE
Joseph Sakaya: mshindi wa gari la Celtel aliyeshindwa kuamini ukweli wa mambo
*Alihofia kuporwa simu mara baada ya kutaarifiwa kuwa ni mshindi
*Aliibuka mshindi baada ya kutuma ujumbe mara mbili
* Mwenyewe ataka kulikodisha, wakeze wadai liuzwe wanunue 'vipanya'
Na Joseph Zablon
'NILIKUWA narudi kutoa shamba na wenzangu kunako saa tano za asubuhi, simu iliita katika namba nisiyo ifahamu, nilipokea, tofauti na simu zingine, niliulizwa mimi ni nani? lakini nilishindwa kuelewa, kwani nilisikia sauti za watu wengine pembeni wakicheka.
Upo wapi?, lilikuwa swali jingine ambalo Sakaya hakulipenda "Kina nani hawa, wanipigie simu yangu kisha waniulize mimi nani? kutokana na mila zake za Kimasai aliona kuwa anadhihakiwa lakini alikuwa na subira kidogo ndipo alipoambiwa kuwa anaongea na watu wa Celtel mbele ya vyombo vya habari na yeye ndiye mshindi wa promosheni kushinda gari ya 'endesha ndoto yako'.
Anasema kuwa hakuamini lakini kusikia nje ya mazungumzo na mtu huyo wa Celtel watu wanashangilia, alizidi kuamini na kubaki katika mshangao ni vipi ameweza kuwa yeye ndiye mshindi. "Siamini hadi hivi sasa" alisema wakati akiwa njiani na waandishi wa habari ndani ya gari hilo aina ya Nissan X-Trail, lenye thamani ya shilingi milioni 40, akielekea kijijini kwake, Matui, Kiteto mkoa wa Manyara.
Mshindi huyo anahadithia zaidi kwa kusema kuwa alibaki na habari hizo moyoni hakutaka watu aliokuwa nao wafahamu kumetokea nini jambo ambalo anasema alifanikiwa kwa kiasi kikubwa na hofu hiyo anasema kuwa ilitokana na ukweli kuwa ushahidi pekee ambao alikuwa nao ni simu yenye kadi (namba), yake.
Sakaya anasema kuwa alibaki na jambo hilo lakini siri haikuweza kufichua na alifanikiwa kiasi fulani kutokana na ukweli kuwa ni wachache ambao wanamfahamu kwa jina la Joseph na zaidi siku iliyofuata, habari zikasikika katika vyombo vya habari, vikimtaja na kuelezea kuwa ni mkazi wa kijiji hicho cha Matui. "niliwakatalia kuwa sio mimi labda Sakaya mwingine, anasema na kuongeza kuwa hiyo ilimsaidia ingawa si sana.
Anasema Sakaya kuwa alipigiwa simu na kuelezwa utaratibu ikiwa ni pamoja na kwenda Dar es Salaam, na watu wake wawili wa karibu akwa ajili ya kukabidhiwa gario lake. Kuwasili na gri hilo kiojijini kwake si tu kunaiobua ari na udadisi wa kutaja kujua ni jinsi gani watu wanashiriki mchezo huo na wapo ambao walidai vipi mbnoa sisi tunacheza kila siku toka ianze promosheni lakini hatupati..!
Wanasema mengi lakini ukweli unabaki kuwa Sakaya ndiye mshindi wa kwanza wa bahati nasibu hiyo kubwa ya namna yake nchini hivi sasa na kuwasili kwake kijijini hapo na gari hilo kulizua shangwe ya namna yake kutoka kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mapokezi yalianzia kilometa kama mbili hivi kabla ya kufika nyumbani kwake ambapo wanaume wa kimasai wa rika lake na kinamama walijipanga mistari miwili pembeni ya barabara kumlaki Sakaya na gari lake wakiimba na kucheza kwa stahili ya namna yake.
Msafara ulipokelewa kwa mbwembwe za namna yake hadi nyumbani kwake katika eneo kubwa kiasi lenye vibanda vitatu vya udongo na zizi kubwa la ng'ombe kutokana na ukweli kuwa Sakaya ni mkulima na mfugaji wa ng'ombe na mbuzi.
Sherehe kubwa ilifanywa ikiwa ni pamoja na kumpongeza kijadi kwa kufuata utaratibu maalum na shughuli hiyo ilihudhuriwa na watu wa namna mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali ya kijiji na watu wengine wa jirani.
Awali Sakaya baada ya kukabidhiwa gari hilo akiwa Dar es Salaam, alipata kuelezea kuwa nia yake ni kulikabidhi gari hilo katika kampuni ya ukodishaji wa magari ya Tours and Safari lakini wake zake wana mawazo tofauti.
Mke mkubwa wa Sakaya ambaye ni Rahel, anasema kuwa gari hilo ni fahari kubwa kwao lakini watazungumza na mume wao ili ikiwezekana waliuze na kununua gari jingine hususani ya biashara kama vile mabasi madogo 'Vipanya' au yanayofanana na hilo.
"Tutamshauri aliuze na kunua gari jingine la biashara ikiwezekana Toyota Haice" anasema mke wake mkubwa kauli ambayo inaungwa mkono na mke mdogo, Momoi ambao wanakiri kuwa maisha kwao sasa yamebadilika na ni kipindi kwao kuishi vizuri zaidi ya mwanzo.
Anasema Momoi kuwa sasa maisha yamebadilika kutokana na ukweli kuwa kwa kuwa na chombo hicho cha usafiri kila sehemu hivi sasa imekuwa karibu, "hospitali sasa ipo karibu na kila sehemu tutakayohitaji kwenda, tutafanya hivyo, tunawashukuru Celtel' anasema na kuongeza kuwa hawakutarajia lakini imekuwa kweli.
Miongoni mwa watu ambao wameguswa na zawadi hiyo ni pamoja na Waumini wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Masai Kusini, Usharika wa Namerok, Matui, Kiteto, Manyara, muinjilisti Joseph Tsunnay na mchungaji wa kanisa hilo, Issaya Ole Lee.
Ole Lee anaeleza wakati wa ibada ya kuliombea gari hilo iliyofanyika kanisani hapo kuwa ile ni neema ya mtaa, litawasaidia wote hivyo ni wajibu wa waumini wa kanisa hilo kutoa msaada wa hali na mali kwa Sakaya na anaeleza kuwa iwapo wakipatikana kina Sakaya wanane katika kijiji hicho basi ni dhahiri maendeleo ya eneo hilo yatakuwa kwa kasi kuliko ilivyo sasa.
Mdogo wa Joseph Sakaya ambaye ni mtumishi wa umma mjini Moshi ambaye alikuwepo katika hafla ya kijadi ya kumpongeza mshindi huyo, baba wa watoto nane na wake wawili, anaeleza kuwa hajui aseme nini lakini ukweli ni kuwa ukoo wao umepata bahati ya ajabu kupitia Joseph Sakaya.
Anasema kuwa hakuamini alivyosikia kupitia vyombo vya habari na akalazimika aombe hudhuru kazini kwake ili aweze kusaidiana na ndugu yake huyo kuhakikisha kuwa gari hilo linatua kijijini hapo na pamoja na mamo mengine kumsaidia kuliendesha kutoka Dar es Salaam hadi kijiji cha Matui, Kiteto.
Pamoja na yote ukweli unabaki kuwa Joseph Sakaya ni mtu mwenye bahati ya namna yake ambayo si tu imewashangaza watu wa kabila lake bali pia imebadili fikra za watu wa eneo hilo kuhusu michezo ya kubahatisha na promosheni zingine.
Awali kulikuwa na fikra kuwa pengine kuna kujuana l;akini walio wengi wanaomjua Joseph Sakaya wanakiri kuwa ilikuwa bahati yake na wanakiri kuwa mkulima na mfugaji huyo muda mrefu hakuwa na simu na aliinunua Juni mwaka huu na ajabu miezi isiyozidi mitatu baadae imebadili maisha yake.
Atafanyaje na gari hilo itakuwa vipi uamuzi anao mwenyewe lakini wakati umefika wa watu wengine kujaribu bahati zao katika kila jambo kwani waswahili wanasema kuwa hata bahati huwa inatafutwa haiji yenyewe.
mwisho.........

<< Home