Sunday, September 23, 2007

BIASHARA YA WATOTO YASHAMIRI JIJINI

Watoto

Na Mobini Sarya

SIKU chache baada ya wanafunzi wa Daraza la saba kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi nchi nzima, Biashara ya kusafirisha watoto wakike kutoka mikoani maeneo ya vijijni na kuwapeleka mjini hususani jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyizwa kazi za ndani imeibuka.

Katika uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kwa siku kadhaa tangu wanafunzi hao wamalize elimu ya msingi wiki iliyopita limebaini kwamba mamia ya watoto wakike na kiume wamekuwa wakisafirishwa na baadhi ya watu wanaojiita mawakala wa kutafuta wafanyakazi wa ndani.

Mawakala hao ambao wengi wao ni wanawake wa makamo wamekuwa wakipita katika majumba mbalimbali ya watu wakiwauliza kama wanataka wafanyakazi wa ndani kutoka kijini na mara wanapokubaliana huomba nauli ya kuwaletea wafanyakazi hao ikiwemo na ujira wa kazi hiyo.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliozungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki walithibitisha kuwepo biashara hiyo na kueleza kuwa ni ya muda mrefu na huu ndio msimu wake, kutokana na watoto wengi kumaliza shule jambo linalokuwa rahisi kuwapata.

Wanasema kuwa wamekuwa wakipenda watoto wanaotoka mashambani kwani unakuta bado hawajajanjaruka na kulijua Jiji “ukipata katoto kanakotokea kijiji bado kashamba unakuwa na uhakika katakufanyia kazi kwa kipindi kirefu kabla hakajaelewa jiji hata gharama za kumlipa ni ndogo sio kama za hawa ambao w amezoea Jiji”anasema mkazi mmoja

Baadhi ya mikoa ambayo imeonekana kuwa kinara kwa kusafirisha watoto kwenda Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Iringa, watoto hao wamekuwa wakisafirishwa hadi stendi ya Ubungo ambapo mhusika hupigiwa simu kwenda kuchagua mfanyakazi wake, na watoto wanaobaki hutafutia kazi zingine ikiwemo kutembeza bidhaa.

Katika uchunguzi huo imeoneka kwamba watoto wengi wakike wao hutumikishwa majumbani na wakiume ndio hupewa kazi ya kuuza maji na kutembeza bidhaa mbalimbali kwa ujira unaoelekea kuwa sawa ,kati ya shilingi 5,000 na 10,000.


Aidha katika uchunguzi huo imebainika kuwa sababu ya watoto wengi kumbilia mjini ni hali ngumu ya maisha kijijini wanapokuwa wamemaliza shule kwani wengi w ao unakuta bado umri ni mdogo w a kuweza kujitegemea ,hali hiyo huchangiwa na wazazi wao wenyewe kuwasukuma kwenda mjini baada ya kuahidiwa na mawakala wa biashara hiyo kuwa wakiruhusu watoto wao kuja mjini watapata maisha bora.

kama mototo mmoja alivyoeleza kuwa mzazi wake alimwabia akatafute kazi mjini kwani hata akifaulu hana uwezo wa kumsomesha.

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home