Serikali ina ubavu wa kuadhibiti wahaini Zanzibar?
Na Mobini Sarya
SERIKALI ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ina ubavu wa kuwadhibiti wanasiasa wanaoipinga kwa kivuli cha kutaka kuvunja muungano?
Ndio.naanza kwa kuuliza swali hilo kutokana na hali ya mambo inavyo kwenda kwani inaoonekana kuna watu sasa wanajiita wanaharakati wa muungano kumbe ndani ni wahaini.
Kwa mjibu wa tafsiri mbalimbali mhaini ni mtu mdanganyifu, mwenye hila, mjanja, msaliti, mwenye maneno ya fitina na kisiasa ni mtu anayepinga serikali halali iliyopo madarakani akiwa na nia ya kuipindua.
Hicho ndicho ninacho maanisha na hiyo ndio hali inayojitokeza sasa kwa wanasiasa uchwara wa Zanzibar ambao wamejivika vazi la udini na uanaharakati wa muungano.
Hawapingi wazi wazi serikali ya jamhuri bali wanajidai kupinga muungano waziwazi wazi, kumbe hicho ni kivuli tu na lengo lao hawaitaki serikali kitu ambacho ni uhaini.
Kwani hawajui kuwa kukataa muungano ni kukataa kwanza serikali ya Muungano? Na ili muungano uvunjike ni lazima kwanza serikali igawanyike, wabara na wa visiwani?
Je kusababisha serikali ikavunjika sio uhaini?kwanini watu hao waachiwe wavuruge muungano kwa tamaa zao tu za kutaka kujitawala?
Ni vema na haraka ni kasema wazi kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaundwa na kuongozwa na viongozi wahaini dhidi ya serikali tukufuku ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kabla sijaenda mabali ni vema ni kasema kwa haraka bila kificho kuwa duniani hakuna taifa la Zanzibar bali kuna nchi ya Zanzibar yenye dola butu isiyo na nguvu ya kujilinda nje ya mpaka yake wala ndani bila kutegemea mamlaka ya taifa la Tanzania.
Serikali ni serikali hata bara kuna serikali za vijiji hivyo eneo kuwa na serikali hakumanishi kuwa hiyo ni jamhuri kamili wala kuwa na baraza la wawakilishi hakunaminishi kuwa ni taifa kwasababu hata maeneo ya bara kuna baraza la wawakilishi.
Hivyo wasijivunie kuwa na Serikali wakaudharau muungano wa Tanzania kwani bila kupokea ulinzi kutoka bara watajikuta wapo chini ya himaya ya Oman.
Ikitokea hali hiyo watakuwa wamejiweka mateka wenyewe watakuwa wamejirudisha utumwani walikokombolewa Januari 1964 na wazalendo wa kiafrika kabla ya kuomba ulinzi kutoka kwa Mwalimu nyerere ambaye aliwaambia njia nzuri ni kuunganisha mataifa hayo kuwa taifa moja lenye utambulisho mmoja.
Ndio maana waungwana wanasema visiwa vya Zanzibar ni sehemu ya mikoa ya Tanzania hilo halina ubishi hadi ikulu ya Zanzibar, ndio maana kimeibuka kikundi cha wahaini wachache lakini chenye nguvu ya fedha kikipinga serikali halali ya muungano.
Wanapinga eti kwa madai kuwa hawataki kuwa chini ya serikali ya Tanzania, madai kama hayo yaliwahi kutolewa Mwaka 1984 na Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe kabla ya kuibiwa nyaraka zake na Makamu wa sasa (SMZ) Maalim Seif na kumpelekea mhandisi wa muungano, Mwalimu Julias Nyerere.
Lakini ni Maalim Seif huyu huyu ambaye baada ya kupita Miaka 28 ameanza kuhoji anataka kuvunja muungano amekwenda mbali zaidi hadi kukisaliti chama chake cha CUF.
Kwa mjibu wa sera ya chama cha wananchi CUF, kinatambua muungano wenye serikali tatu tafauti na CCM yenye kutambua muungano wa serikali mbili lakini Malim Seifa licha ya kuwa Katibu mkuu wa CUF yeye amekuja na hoja ya muungano wa mkataba.
Maana yake ni kwamba tunaweza kuingia makubaliano ya muungano wa kimkataba baada ya muda fulani mkataba ukimalizika tunavunja muungano kila mtu anashika lake.
Anafanya hivyo bila kujua kuwa duniani hakuna muungano wa mkataba, huwezi ukatoka kwenye muungano kamili ukaenda muungano wa mkataba utakuwa na nia ya kuvunja muungano wa awali kilichopo unaweza kutoka muungano wa hiari ukaingia muungano rasmi.
Hata hivyo kitendo cha viongozi wa umma kujiingiza kwenye siasa na kuanza kuwashawishi wananchi na wafuasi wao waukatae muungano kinathibitisha wazi kuwa katika serikali ya SMZ kuna wahaini wanaopaswa kushughulikiwa kama Jumbe alivyofanywa Mwaka 1984
Hapo ndipo tunapoanza kuhoji kama kweli viongozi wa serikali wana uwezo wa kudhibiti kikundi hicho, kwasababu viongozi wake wapo ndani ya serikali ya Zanzibar na katika baraza la wawakilishi.
Lakini wahaini hao hali wakipenda madaraka wameamua kujifungamanisha na kikundi cha kidini kinachojulikana kama jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislam Zanzibar.
Kikundi hiki kwenye katiba yake sehemu ya nne kipengele ( d ) inatamka wazi kuwa Jumuiya haitakuwa na uhusiano wowote na chama chochote cha siasa’lakini licha ya katazo hilo wanasiasa wahaini wamekuwa wakikitumia kikundi hiki kama vuvuzela la kufikisha ujumbe wanakotaka.
Mmoja wa kikundi hicho alinukuliwa akisema kuwa wanasakamwa na serikali kwasababu wamekuwa wakihamasisha wakazi wa visiwa vya unguja na Pemba wakatae muungano.
Madai hayo yanafanana nay ale yanayotolewa na viongozi waliopo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) hivyo kuzua hoja kuwa inakuwaje kikundi cha uamsho kilichosajiliwa kwa malengo ya kusambaza dini ya kiislam kijiingize kwenye siasa?
Kuna watu wamefikia hatua wanatamka wazi wazi kuwa hoja za uamsho ni zile zile zilizokuwa zinasimamiwa na viongozi wa CUF kabla hawajaingia madarakani hivyo kutoa nguvu kwamba nyuma ya kundi la uamsho kuna wanasiasa.
Hoja hiyo inaweza kuwa kweli ikikumbukwa kuwa hivi karibuni Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar alihojiwa na shirika la utangazaji BBC akatamka wazi kuwa licha ya chama chake kuridhia muungano wa serikali tatu lakini yeye na wafuasi wake wanapendekeza muungano wa mkataba.!
Maana yake ni nini? Ina maana Seif haamini hata sera za chama chake, huyo ni kiongozi wa aina gani? Anataka nini mbona amezeeka hata leo muungano ukivunjika atanufaika na nini?
Tuna weza kuhoji tukapata majibu lakini lililo mbele yetu kwamba pengine Seif kama walivyo wengine wanaopinga muungano wameahidiwa jambo huko uarabuni kama wakifanikisha kuvunja muungano huo.
Hiyo hali ikiachwa hivi hivi ikue itakuja kutugharimu, ndio maana wengine wanahoji je serikali inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete ina ubavu wa kwashughulikia mapema wahaini waliojichimbia katika serikali ya SMZ.
Wanasiasa wa namna hiyo wakiachwa kuendelea kujenga mizizi ya fitina wataligharimu taifa hivyo ni bora waanze kuchunguzwa miziz ya uasili wake maana wengine hata makazi yao inadaiwa kuwa wamekwisha jengewa oman wanachosubiri Moto uwake wakimbilie kule.
Nimalizie kwa kuhoji kuwa Mwaka 1984 Mwalimu Julias Nyerere alimtimua kazi Aboud Jumbe kwa kutaka kuleta uhaini wa muungano je serikali ya sasa inayooongozwa na ndugu Rais Jakaya Kikwete itadhubutu kuwaita wahaini hao mjini Dodoma?
www.mobinday.blogspot.com.0753 399 579 mobinsons@yahoo.com

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home