TAMKO LA JUKWAA LA HABARI (TANEF)KUHUSIANA NA KIFO CHA MWANAHABARI
TANZANIA NEWS FORUMS
Jukwaa la habari-Tanef
S .L.P 12261, break.news@yahoo.com,0656 938315, 0753399579, Dar es Salaam, Tanzania
September 10. 2012
TANPRESS YAIKITISHWA NA UKIMYA WA RAIS KUSHINDWA KUTUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MWANDISHI
TANPRESS ni shirika huru la habari ambalo linaendeshwa chini ya jukwaa la habari nchini (TANEF),shirika hili linalenga kuweka mazingira huru kwa wandishi wa habari ili waweze kufika vijijini kwa lengo la kukusanya na kusambaza habari kwa jamii hususani iliyopo maeneo yaliyosahaulika.
TANPRESS ni shirika linalolenga kutoa uwanja mpana zaidi kwa wandishi huru wa habari kuweza kufika maeneo mbalimbali kwa lengo la kupata taarifa kwa wakati,hivyo wanahabari waliopo maeneo ya vijijini ni wadau wakuu wa shirika hili.
Hivyo kwa mara ya kwanza shirika hili linatoa masikitiko makubwa kutokana na kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi ambaye aliuwawa na Polisi Septemba 2 Mwaka huu mkoani Iringa wakati akitekeleza majukumu yake ya kukusanya habari maeneo ya vijijini,tukio linalotishia uhuru wa habari.
Hata hivyo pamoja na kutolewa matamko mbalimbali ya kulaani tukio hilo la kikatili, kinachotusikitisha ni jinsi ambavyo viongozi wa Serikali na taasisi zake walivyolichukulia kwa dharau kubwa tukio hilo,ambalo pengine ni tukio kubwa na baya lililotokea nchini Mwaka huu katika Tasnia ya habari.
Hakuna kiongozi yeyote kutoka taasisi mhimu ya serikali aliyejitokeza hadharani kutoa hisia zake hata Pole kwa ndugu na family ya marehemu achilia mbali vyama na kituo cha habaari cha chanel 10 ambacho marehemu alikuwa anakitumikia enzi akiwa hai.TANPRESS imesikitishwa sana na ukimya wa rais Jakaya Kikwete kushindwa kutuma salam, za rambirambi kama ambaavyo amekuwa akifanya kwenye misiba mingine na wakati mwingine hufika kutoa pole moja kwa moja.
Tumemuona akifanya hivyo katika misiba mbalimbaali,alijitokeza kumjulia hali Mkurugenzi wa Halihalisi Publishers,Sued Kubenea alipomwagiliwa tindikali na maadui wa uhuru wa habari,pia alijitokeza kumjulia hali mbunge wa Rombo Selasini alipolazwa baada ya kupata ajali mbaya iliyogharimu ndugu zake.
Kubwa zaidi Rais Kikwete alijitokeza nyumbani kwa msanii nguli wa filamu,Steven Kanumba alipofariki dunia jijini Dar es salamu,akatoa pole kwa familia ya marehemu kabla ya kupishana na waziri wake akipeleka pesa za rambirambi zinazofikia shilingi milioni 10.kwanini kimya kwa mwangosi.
Inamaana Rais Kushindwa kutuma salam, za rambirambi wala wizara ya habari kushindwa kufanya hivyo anajiweka katika kundi la waovu waliohusika na ukatili huo,jambo ambalo linadhidi kumjengea ziki aendapo kustaafu,kwasababu anaonekana kuwa ni kiongozi anayenyamazia maovu kwenye utawala wake.
Tunalojiuliza ni kwa namna gani Rais ameshindwa kutolea tamko hata la kulaani tukio hilo,hivyo kupingana na waziri wake wa mahusiano,Seteven Wassira aliyetangazia umma kupitia shirika la TBC kuwa kila binadamu anathamani sawa.
TanPress tunapinga kauli hiyo kwani Kama kauli ya Waziri ingekuwa sawa leo Rais angetuma mwakilishi kwenye msiba huo au salam za rambi rambi kwa kituo cha televisheni cha Chan.10 alichokuwa anafanyia kazi marehemu pamoja na Klabu ya wandishi ya Iringa (IPC)kama ambavyo Rais amefanya kwa misiba mingine.
Waziri Wassira amesema kuwa misiba yote inayotokea inalingana tusiupe uzito zaidi huu,sawa lakini Wassira hajatuambia mbona serikali yake imekaa kimya kwenye msiba huu,tafauti na misiba mingine ambayo wamekuwa wakitoa ubani kama ule wa marehemu Steven Kanumba au tuamini kwamba serikali imehusika moja kwa moja na kifo hicho.
Baada ya TANPRESS kuona kimya cha Rais na serikali yake katika kashfa hii,tunashauri yafuatayo;1.Kwanza Rais Kikwete amfukuze kazi Mkuu wa Polisi na Waziri wa Mambo ya ndani baada ya kushindindwa kuwajibika kutokana na ukatili wa Polisi wao.
2.Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamhanda akamatwe kwa kushiriki oparesheni haramu iliyosababishwa na amri yake hivyo kuleta maafa ya aibu.
3.Serikali kupitia kwa wizara ya habari itoe ufafanuzi ni kwanini imedharau msiba au kifo cha mwandishi huyo kwa kushindwa kutoa msaada wowote licha ya kwamba Polisi walihusika kuuwa kama walivyofanya Tarime kwa kuuwa watu watano kisha wakatoa ubani kwa familia zao.
5.Mwisho tunaomba nchi wafadhili wanaotoa misaada inayolenga ukuaji wa demokrasia na utawala bora kama ina umhimu kwasasa kutokana na nchi wanayoifadhili kutoheshimu utawala bora.
…………………………
Sir Mobini Sarya
Mkurugenzi.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home