Sunday, November 11, 2007

TAIFA LENYE WALIMU WALIOKATA TAMAA

Na Stephen Ishengoma

Kwanza napenda niipongeze HAKIELIMU kwa namna ilivyoweza kueleza ukweli kuhusu sekta ya elimu ilivyo hapa Tanzania. Mkurugenzi mwanzilishi na timu yake wanastahili pongezi za dhati.

Ukweli wa kile wanachokisema HAKI ELIMU kuhusu ELIMU katika nchi yetu unabaki palepale ingawa serikali za nchi maskini kama Tanzania zinapoambiwa ukweli au kukosolewa huchukua na hata kuamua kuchukua hatua kali dhidi ya wanaozikosea serikali hizi. Hii inatokana na viongozi kuzoea kuimbiwa nyimbo za sifa hata kwa mambo yasiyohitaji kusifiwa.

HAKIELIMU wameonyesha kasoro na mapungufu mengi katika wa vyumba vya madarasa uhaba wa madawati na ofisi za walimu, uendeshaji mbovu wa watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia sekta hii kuanzia ngazi ya shule husika mpaka wizarani, uhaba wa nyumba za walimu, ucheleweshaji wa mishahara ya walimu, maslahi duni ya walimu , usafiri duni wa wanafunzi kwenda na kurudi kutoka shuleni na uhaba wa vitabu mashuleni.

Matatizo yote haya yamesababishwa na viongozi na watendaji wengine waliopewa dhamana ya kuliongoza TAIFA hili kushindwa kutambua ni maeneo yapi yanastahili kupewa kipaumbele. Kiini cha yote haya ni mmomonyoko wa maadili ya viongozi wa TAIFA hili ambalo mwenyezi mungu alilijalia rasilimali za kila aina . ukweli huu umejidhihirisha katika mikataba ya kinyonyaji ambayo ilisainiwa na viongozi waliomomonyoka kimaadili na wasiokuwa na uchungu na nchi yao.

Mabilioni ya fedha ambazo zingeboresha ELIMU na hali za walimu katika nchi hii yamekwishapote ana yanazidi kupotea kutokana na kukosekana viongozi makini.

HAKIELIMU si chama cha siasa ingawa baadhi ya wabunge wa chama chako mheshimiwa Rais wanamewahi kunukuliwa wakiishutumu kuwa inajiingiza kwenye mambo ya siasa na kuitaka ijisajili kama chama cha siasa. Pia walionya kwa ikichiwa iendelee na matangazo yake inaweza kusababisha serikali yako kuanguka.

Hakika kama haya ndo mawazo ya wabunge wetu wanaolipwa fedha nyingi kutokana na kuwepo kwao bungeni bosi ipo haja ya kulivunja bunge kuokoa fedha za wlaipa kodi. Au ipo haja ya akili za wabunge wa aina hii na elimu yao kuchunguzwa.

Napenda niseme HAKI ELIMU ni wazalendo na matangazo yao ndo yaliyoiamsha serikali iliyokuwa imejisahau na kuanza harakati za kujenga mashule. Nilidhani serikali ya awamu ya nne itaifungia kama ilivyofanya ile ya awamu ya tatu chini ya waziri wa wakati huo ambaye alidiriki kufuta baadhi ya masomo akidhani anaboresha kumbe ndo anaangamiza ELIMU. Lakini pamoa na kasoro hizo ambazo hata wewe mheshimiwa Rais uliziona bado umeendelea kumkumbatia.

Ukweli wa kile wanachokisema HAKI ELIMU unabaki pale pale na serikali yako inatakiwa kuufanyia kazi. Mheshimiwa Rais jitahidi kuwa mtu tofauti wa kufikiri kwa mapana na marefu ya ukwlei unaoletwa mbele yako na kuufanyia kazi ili uweke historia kama ya ndugu ye Joachim Chisano na hayati baba wa taifa.

Mkurungenzi mwanzilishi wa HAKI ELIMU katika moja ya mahojiano yake na kitu kimoja cha Televisheni alinukuliwa akisema tunaweza kuboresha elimu katika nchi hii iwapo rasilimali za n chi hii zitatumiwa vizuri na kuangalia ni maeneo yapi yapewe kipaumbele. Huu ndio ukwelil na uwazi.

Sasa hivi kila kiongozi anaimba wimbo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa karibu kila kona na kujisifu kuwa serikali imeboresha elimu. Nakubaliana na suala la ujenzi wa vyumba hivi lakini naomba nihoji akili ya viongozi hawa wanaodhani elimu imeboreka nchini baadhi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa. Hii ni tatizo katika akilil ya viongozi.

Tunaichotakiwa kujiuliza ni je, huko madarasani kuna walimu kwanini tatizo la ukosefu wa walimu limeuwa endelevu lisilopata ufumbuzi? Huko madarasani kuna viti vya walimu na wanafunzi? Je, huko mashuleni kuna nyumba za walimu? Huko mashuleni kuna vitabu? Kuna maabara? Je hata hao walimu waliokohuko wana nguvu na ari ya kufanya kazi hiyo au wapo kwa sababu walisomea kazi hiyo au kwasababu hawajapata sehemu nyingine ya kwenda yenye maslahi mazuri? Je ni mbunge yupi au waziri yupi au Rais yupi ambaye yuko tayari kuacha kazi yake hiyo akaenda kufundisha darasani ? Jibu linaeleweka kwamba huko hakuna kipato bali umaskini. Huu ndio ukweli.

Tuache siasa za kipuuzi za ualimu ni kazi ya wito na walimu waache kufikiria pesa. Viongozi wnaongea hivi wanatakiwa wakemewe na kuogopwa kama UKOMA. Utawala wa mwalimu Nyerere ulikuwa na vipaumbele. Ni katika kipindi hiki watu wote walitibiwa bure na chuo kikuu. Na wakati wa utawala huu migodi ya dhahabu ilikuwa bado haijaanza kuchimbwa. Lakini watu walisoma na kutibiwa bure.

Wakati mwingine najiuliza ni kirusi gani kimeingia katika akili za viongozi wa bara la Afrika? Nilitarajia Tuzo kama ya Mo Ibrahimu ije Tanzania. Lakini pamoja na kuwa ni taifa lenye watu waliotulia kwa miaka yote hiyo na kujihusisha vema katika ukombozi wa mataifa mengine ya Afrika bado tumeonekana kuboronga . Mabalozi wan chi wahisani wamekwishaliona hilo. Wameona hili ni taifa la viongozi wababaishaji viongozi wala rushwa.

Viongozi wanatakiwa kujiuliza maswali ya msingi ya nini kinaisibu sekta ya elimu badala ya kujigamba majukwaani kwa mafanikio ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakati watoto wanaozalishwa huko hawawezi kushindana katika soko la ajira wale wanaotoka katika hizi shule zinazojiita Academy au International.

Ushindi wowote ule, uwe wa kilimo, ufugaji, viwanda, michezo na biashara unategemea elimu waliyoipata wananchi wake kutoka kwa walimu wanaothaminiwa na si hawa waliokata tama. Ninyi kama viongozi kuwapeleka watoto wenu nje ya nchi si suluhisho la kuliondoa taifa katika umaskini wa elimu. Kuwapeleka vijana pale vyuoni wakachukue mafunzo ya miezi mitatu au sita kasha waende wakafundishe hakutaboresha elimu wala kuondoa tatizo la uhaba wa walimu kuwashawishi vijana waliofaulu vizuri kwenda kusomea ualimu.

Katika kuonyesha kuwa mwalimu hathamini hata taarifa ya serikali kuhusu viwango vipya vya mishahara katika sekta binafsi walimu hawakuguswa. Mheshimiwa Chiligati aliyataja maeneo mengine yoe lakini hakuongelea walimu. Lakini huko kwenye sekta binafsi zipo shule pia.

Mwalimu ambaye ni tegemeo la maendeleo katika sekta nyingine bado anaendelea kudhalilishwa. Ninaposema kuadhalilishwa simaanishi walimu za binafsi. Na huko nadhani hali ya udhaliilishaji ni ya kiwango cha juu. Haitafutiani nay ale yaliyojiokeza katika mgodi wa Bulyahulu ambapo rimeripotiwa mfanyakazi alitishiwa na kuuuawa mzungu na kumwambia hata kama mfanyakazi huyo anngeshitaki kwa Rais asingefanywa lolote.

Mfano mzuri wa shule chafu zinazoendeshwa kwa ubabaishaji wa hali ya juu huku ikiwa na uhusiano mzuri na watendaji wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ni hii ambayo iko jirani na makazi ya Rais mstaafu inayomilikiwa na wahindi na ile iliyo karibu na kituo cha polisi cha surrender bridge ambaye elimu yake ni kidato cha nne au sita.

Ukitazama shule hizi kutokea nje unaweza kudhani kuwa hizi ni shule bora kumbe ni bora shule. Walimu na wazazi wanaozielewa shule hizi watakubaliana na mimi kuwa hapo mwalimu mwenye asili ya Tanzania hana thamani. Watakubaliana na mimi kuwa nidhamu ya wanafunzi wa shule hizi ni mbaya na walimu hawana ubavu na nidhamu hii chafu. Ukiangali viwango vya mishahara katika shule hizi na nyingine za namna hii zinazomilikiwa na wahindi. Kinachosikitisha zaidi hawa walimu ambao si wahindi ndio wachapakazi. Ndio injini za shule hizi. Huu ndio ukweli na hawa ndio wawekezaji katika sekta ya elimu .a wizara husika zinayofahamu haya.

Nilishangaa kusikia mwalimu mswahili m wenye shahada na diploma ya ualimu “take home” yao ni kati ya laki mbili na laki mbili na elfu arobaini wakati binti wa kihindi ambaye anafanyakazi maktaba “take home” yake ni shs lakini tano na nusu hadi sita. Mwalimu wa kihindi ambaye hajasomea ualimu mshahara wake ni mara mbili zaidi ya ule wa mwalimu mswahili aliye na shahada ya ualimu. Je, waziri wa serikali ya viwango, ya kasi mpya na nguvu mpya, aliyehudhuria mafunzo pale Ngurdoto na kulipwa posho nono anayaelewa haya? Shule kama hii inathaminiwa mwalimu au kinadhalilisha mwalimu?

Mheshimiwa Rais hizi ndo shule ambazo wanao wanasoma au wamewahi kusoma. Ni shule zenye ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa kijinsia ambazo walimu waswahili wanahamu kila kukicha kama kuku wa kineyeji. Hili ndo eneo ambalo waziri Chiligati hakutaka kulizungumzia wakati akiwaslisha taarifa ya nyongeza za mishahara katika sekta bianfsi.

Nimeambiwa wakaguzi wa wizara wanapokwenda katika shule hizi wanayona yote haya na idadi kubwa ya walimu ambao hawana vyeti wala hawajasomea ualimu lakini wanajua mwisho wa kazi yao ya ubaguzi watapewa bahasha na kutoa alama na ripoti nzuri kwa shule husika.

Walimu katika shule hizi wanaambiwa wawapo watoto maeneo ambayo ndo maswali ya mitihani yatatoka ili wafaulu vizuri. Waziri Sitta unayafahamu haya? Mwalimu mmoja mswahili katika shule hizi zinazojifanya ni za kidini na kutoa misaada ya hela kwa watoto wenzao kule Lebanon alifukuzwa kazi alipokataa utaratibu huu mchafu wa kuwaonyesha watoto maeneo yatakayotoka maswali yamtihani. Hizi ndo shule zako mheshmiwa Rais. Ndo shule wanasoma wanao. Ndio wawekezaji katika elimu.

Nimeambiwa kuwa walimu katika shule ya kihindi iliyoko kule makumbusho waliwahi kuambiwa na mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo kuwa kama mshahara huo wanaoupata waache kazi kwani walimu hawaridhiki wamejaa kariakoo watawaita kuchukua nafasi za wale walioacha. Hebu pima kauli hii ya mwekezaji huyu. Hii ni kauli ya unyanyasaji na udhalilishaji wa fani ya ualimu na walimu wenyewe katika taifa hili. Mwenye shule huyu mhindi haelewi kuwa ameweza kuwekeza hapo kwa sababu ya mazingira mazuri ambayo muasisi wake ni mwalimu, marehemu baba wa taifa. Ananilinganisha mwalimu na nyanya zinazouzwa kariakoo. Uwepo wa shule kama hizi ni matokeo ya rushwa. Na shule hii ya wahindi inayongozwa na watu wasio na sifa za ualimu. Wakaguzi wanapokwenda pale wanapewa rushwa.

Je tutegemee nini kama walimu wanafananishwa na nyanya zinazopatikana kariakoo? Walimu wanafokewa na wanafunzi katika shule hizi za binafsi. Wenye shule wanawafokea walimu mbele ya wanafunzi je , hapa kuna elimu bora au bora elimu? Nina mashaka kama kanuni na taratibu zinafuatwa dkatika kutoa vibali vya kuanzisha shule hizi. Na hata kama taratibu zilizokuwepo hazijapitwa na wakati. Lakini ni ukweli uliio wazi kuwa kuna udhaifu mkubwa katika eneo hili. Ndio maana shule hizi zimegeuka kuwa biashara badala ya kutimiza lengo lililokusudiwa la kusaidia serikali kutoa huduma hii. Walimu katika shule hizi wamekuwa kama kuku wa kienyeji wanaohamahama kutoka shule moja kwenda nyingine. Wamiliki wazazi na haujui kama hali hii inawaathiri watoto. Wamiliki wanaifanya ni kuchuma hela. Kundi la wamiliki wa aina hii linatakiwa kushitakiwa kwa kuhujumu nchi na watoto wanaolipa karo.

HAKI ELIMU bado wanapewa changamoto la kuanika uoza huu ili wananchi waone na waelewe taifa linavyoangamia. Katika hali kama hii elimu bora haitakuwepo na tatizo la uhaba wa walimu halitakwisha. Waziri sitta peke yake hawezi bila msaada wa viongozi walio juu yake na wabunge. Ninasema hawezi kutyhubutu kwa sababu baadhi ya wamiliki wa shule hizi ni viongozi wa serikali, viongozi wastaafu, watendaji wakubwa serikalini, wanajeshi wenye vyeo vya juu na wabunge. Hawa wote wanashiriki kudhalilisha mwalimu, kumnyanyasa mwalimu na kuwafanya waendelee kuishi maisha duni kupitia shule wanazozimiliki. Ndio maana wamesita kutaja mshahara mpya wa mwalimu katika shule binafsi.

Hesabu ya haraka haraka kwa shule inayotoza karo nafuu kwa muhula mmoja ni shs 300,000. hivyo mwanafunzi huyu katika mihula yote mitatu analipa shs. 900,000/= darasas moja linalofundishwa na mwalimu mmoja lenye watoto 30 shule hizi za binafsi hususan darasa la kwanza, la pili na la tatu linazalisha shs 27,000,000 kwa mwaka. Mwalimu huyu anaambulia shs 210,000 au chini ya hapo kwa mwezi ambao ni sawa na shs 2,532,000/= kwa mwaka. Hapa mwalimu huyu hana kitu chochote anachonufaika nacho baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kuisha isipokuwa michango yake ya NSSF ambayo nayo mnyonyaji na mnyanyasaji huyu aamue kuipeleka NSSF.

Hali hii ya kuendelea kuwadhalilisha walimu ni dhahiri itazaa

Kwa sababu viongozi wenye uchungu na mataifa haya ya Afrika wameshatangulia mbele ya haki na waliobaki hawana muda tena tutarajie taifa la sasa na kesho lenye viongozi na wataalamu matapeli ambao hawajui wafanya nini ili taifa hili lisonge mbele wanasiasa wajinga wasioweza kuchambua upi ni mchele na zipi ni pumba. Tutajie wawakilishi itakuwa ni kupiga makofi kwa kila hoja inayoletwa mbele yao. Wawakilishi ambao wanajadili kupigiwa saluti na kupewa magari ya kifahari badala ya mambo muhimu ya kuliendeleza taifa. Tutarajie viongozi ambao watasaini mikataba ya kijinga na kinyonyaji kwa sababu wamefundishwa na walimu waliokata tama. Tatarajie wahandisi ambao watajenga magorofa na muda mfupi magorofa hayo kusababisha madhara kwa wananchi.tutarajie viongozi watakaojihusisha na mihadarati kwa sababu elimu walioipata ni duni.

Mwisho tutalazimika kuingia mikataba ya kukagua hesabu za halmashauri zetu. T utajikuta tuna mawaziri wanaosaini mikataba ya kuendesha wizara na hata ikulu yetu.

Haiwezekani mtu yeyote kwasababu ana pesa zake apewe kibali cha kuanzisha shule. Tena wengine ni wauza madawa ya kulevya na wameshiriki kutoa taifa hili katika umaskini mkubwa tunatakiwa kuwa makini katika elimu kwani kila hatua inategemea elimu. Tuangalie sifa na elimu ya huyu mtu anayeanzisha shule, tuangalie CV yake na histori yake. Kitabia na kitaaluma, tuangalie mazingira tuangalie menejimenti ya shule kuanzia mkuu wa shule, misaidizi, makarani na walimu atakaoajiri wana sifa zipi.

Tuziangalie bodi za shule hizi na uwakilishi wa walimu katika bodi hizo, tuchunguze na kubaini jinsi walimu katika shule hizi kama wanalipwa mishahara inayolingana na sifa, uzoefu na kazi wanazozifanya. Mikataba ya walimu inatakiwa ifanane na isiyo ya kinyonyaji na inayotoa haki kwa walimu. Wamiliki wa shule hizi wanaonyeshe jinsi wanavyosaidia kuinua hali za maisha ya walimu na si kutajirika kupitia migongoni mwao. Mwisho namalizia kwa kuwakumbusha HAKIELIMU kwamba mapungufu ya elimu yaonyesha katika matangazo yao si katika shule za serikali tu bali zipo kasro nyingi sana katika shule binafsi. Shule hizi zinamilikiwa kupita kiasi. Walimu hawathamini, walimu wanahamahama kwa sababu ya unyanyasaji na maslahi duni. Shule hizi zina ubaguzi wa rangi katika mishahara na maslahi mengine. Utapele ni mwingi sana. Watoto katika shule hizi hawawaheshimu walimu

Mungu ibariki Tanzania


JK atakiwa kuomba radhi

MZOZO MAHAKAMA YA KADHI

na Agnes Mlundachuma

S
UALA la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini linazidi kupanuka, na kwa mara ya kwanza tangu mjadala huo uanze, jina la Rais Jakaya Kikwete limeanza kuingizwa katika mzozo huo.
Rais Kikwete ametajwa katika sakata hilo pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, wakidaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika mgogoro huo, ambao sasa unazidi kuchukua sura tofauti.
Kwa upande wake, Rais Kikwete ametajwa akitakiwa kuwaomba radhi Watanzania, kwa kile kinachodaiwa kuwa, dhamira yake ya kutaka kuigeuza Tanzania kikatiba kuwa nchi ya Kiislamu na hivyo kuirejesha katika mzozo wa miaka ya mwanzo ya 1990 uliohusisha juhudi za baadhi ya viongozi kuiingiza katika kundi la nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).
Aidha, IGP Mwema amepewa siku 21 kumuomba radhi Mchungaji Christopher Mtikila, kutokana na kitendo chake cha kuwatuma askari wamkamate (Mtikila), kumhoji na hatimaye kumfungulia mashtaka ya uchochezi wakati hana kosa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mchungaji Mtikila, ambaye ndiye aliyeibua mjadala unaoendelea kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, alitaka tamko la Rais Kikwete la kuomba radhi liambatane na hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi wote wa umma, waliohusika kwa namna yoyote katika kitendo hicho cha kuingiza Uislamu katika ilani yake ya uchaguzi, serikali na Bunge.
Aliongeza kuwa sambamba na hilo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho alidai ni kikundi cha maslahi ya kibinafsi cha watu fulani, nacho kifutwe kama inavyoagiza katiba.
Mtikila alisema, Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Halmashauri ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), walikutana na walitaka kutoa tamko la kupinga mapinduzi hayo ili kulinda katiba ya nchi, lakini serikali iliwahadaa wasifanye hivyo bali wangojee tume yao ilifanyie kazi suala hilo.
Hata hivyo, Mtikila alisema, inashangaza kuwa tofauti na ahadi iliyotolewa na serikali kwa taasisi hizo nyeti za kidini nchini, harakati zilianzishwa ili muswada kuhusu Mahakama ya Kadhi upelekwe bungeni bila Wakristo kujua, mpaka Mungu alipowafunulia na kuwawezesha kuwahisha ulinzi wao wa katiba mahakamani.
Alisema yeye hapingi kuanzishwa kwa mahakama hiyo, bali anachopinga ni kuingizwa katika katiba ya nchi ambayo kimsingi inapingana na suala hilo.
“Tunachopinga vikali sisi ni kuingizwa kwa dini ya Kislamu au Mahakama ya Kadhi katika katiba ya nchi yetu,” alisema na kuongeza kuwa hata kama kutakuwa na harakati za kutaka kardinali, askofu au paroko wa Kanisa Katoliki kuingizwa katika katiba ya nchi, atapinga kama atakavyopinga kuingizwa mtandao wowote wa kidini katika katiba.
Aliwataka Waislamu wasidanganywe kwa kuwa Mahakama ya Kadhi ni mradi wa watu wachache, na kuongeza kuwa, kuna nchi kadhaa za Kiislamu zimekataa mahakama hiyo kwa sababu sharia zake ni kinyume cha haki za binadamu.
Alisema hoja ya kuwa mahakama hiyo itashughulikia mirathi, hija na ndoa tu, ni ulaghai ili iingizwe katika katiba, baadaye makadhi waue watu wasiokubali dini ya Kiislamu na kuangamiza Wakristo na Wayahudi na kuchinja Waislamu watakaoiacha dini yao.
Alisema hivi sasa nchi haina Mahakama ya Kadhi, lakini Waislamu wanaoa, wanaolewa, wanapata mirathi na kesi zao za mirathi zinashughulikiwa na pia wanakwenda hija na kuhoji mahakama hiyo italeta mabadiliko gani katika masuala hayo yanayodaiwa kuwa itayashughulikia.
Aidha, Mtikila alisema kitendo cha baadhi ya Waislamu kupinga ziara ya Papa ni kutofahamu kwamba mbali ya Vatican kuwa makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, pia ni nchi huru ingawa ipo ndani ya nchi ya Italia.
Alifafanua kuwa Vatican ni sawa na Swaziland na Lesotho ambazo zimezingirwa na nchi ya Afrika Kusini.
Alisema Papa atatembelea Tanzania kiserikali sawa na kiongozi mwingine wa nchi na kwa kuwa kuongoza kanisa ni huduma ya kiroho, hawezi kuiweka roho pembeni anapokuwa katika ziara ya kiserikali.
Akifafanua kauli zake za awali kuhusu kupinga kwake utaratibu unaotaka kutumiwa kuanzisha Mahakama ya Kadhi, Mtikila alikanusha kutamka kuwa Uislamu ni ugaidi na kusisitiza kuwa Mahakama ya Kadhi ndiyo chombo cha ugaidi ndiyo maana hata baadhi ya nchi za Kiislamu zinaikataa.
“Uislamu wa Watanzania usio na ukatili wa Mahakama ya Kadhi hauwezi kuitwa ugaidi kamwe,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine, alisema mbinu ya kamati inayotetea mali za Waislamu iliyotangaza azma yake ya kumkata kichwa, ni hasira tu, kwa kuona pesa walizokuwa wanataka kupewa hazitakuwepo na suala hilo halitazungumziwa bungeni wala serikalini kwa kuwa lipo mahakamani.
Aliongeza kuwa, yeye hawakatalii Waislamu kuabudu, lakini si kuliiingiza suala hilo la kidini ndani ya katiba.
Kauli hiyo ya Mtikila inakuja wakati taifa likipita katika kipindi kigumu cha msigano wa hoja zinazokinzana kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi jambo lililogusa hisia za makundi mbalimbali ya Wakristo na Uislamu kiasi cha kutishia amani.
Baadhi ya kauli za waumini wa dini hizo mbili, ndizo ambazo kwa upande fulani zilisababisha taasisi za dola kuamua kuingilia kati na kuchukua hatua za kisheria.