म्बुंगे अवावेका वानांची क्वेन्ये karantini
mbunge adaiwa kuwaweka wananchi kwenye karantini
Na Mobini Sarya.
WAKAZI wa Kijiji cha Ruhita kata ya Rugu wilayani Karagwe, wamelalamika maeneo ya Makazi yao kuchukuliwa na kikundi kimoja cha wafugaji, na kutakiwa kuhama bila kulipwa fidia.
Wakazi hao zaidi ya 1000 kutoka vitongoji vya Miliro ,Chamengo na Kigasha wamedai kuwa Mbuge wao Begumisa Blandes, Diwani wa kata ya Rungu na Mwenyekiti wao Cylidion Mgeni pamoja na watu wengine wanne wamepora eneo lao kwa madai kuwa wameuziwa na kijiji kwa lengo la kufuga bila kuwalipa fidia wakazi hao.
“kinachoonekana sasa huenda ukazuka mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji kwani inaonekana kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe anaegemea upande wa Mbunge kuwa serikali ya kijiji inaouwezo wa kuuza ardhi, Mkuu wa Wilaya anapoulizwa swala la fidia anatoa majibu ya kukwepa” ilisema sehemu ya nakala waliyotumia Tanzania Daima.
Wanadai kuwa Agoust 12 Mwaka jana kikundi cha watu saba akiwemo Mbunge na Diwani wakishirikiana na Mwenyekiti wao ambaye naye ni mwana kikundi waliitisha kikao cha Serikali ya Kijiji cha Ruhita ,wakalipa kiasi cha shilingi M.2,500,000 na wkapewa stakabadhi namba .S.V.376369 ya Agoust 12 Mwaka 2006 na wajumbe wa serikali ya kijiji wakaidhinisha kuwa wapewe ardhi ya Hekta 45,000 ambayo ni ya vitongoji vitatu.
Katika moja ya vielelezo ambavyo vimetumwa Tanzania Daima inaonyesha kuwa Pesa hizo zililipwa katika kikao hicho kama fidia kwa maliasili ziliopo eneo husika na kuekeshwa katika chama cha msingi cha Misha yenye kumbukumbu namba KN 2965 51.
Wakazi hao wanasema kuwa Baada ya kulipa fedha hizo,ikapita miezi mitano kikundi hicho ambacho hakina jina kikapeleka wapimaji wa ardhi kutoka wilayani Karagwe wakapima na kuweka vigingi baada ya hapo wamekuwa wakipelekewa Polisi kutoka kituo cha Nyakahaga wakitishwa ili wahame eneo hilo.
Pamoja na hali hiyo wakazi hao wanadai kuwa hawezi kuondoka katika eneo hilo kuwapisha wajanja hao bila kujua nani atawalipa fidia ya Mali zao kama nyuma na mashamba na tena hawajui waende kuishi wapi kwani baadhi yao wanadai kuwa wameishi hapo kwa miaka hamsini.
Hata hivyo wakazi hao wanapanga kutuma ujumbe kwa Waziri wa ardhi na nyumba John Magufuli ili aweze kuwasaidia kilio chao kwani hata mbunge wao ameshiriki ikiwa ni miezi nane tu tangu achaguliwe.

Labels: ne3s

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home