म्बुंगे akabiliwa na तुहुमा
Tuhuma zamkabili mbunge anayedaiwa kuweka wananchi chini yake
Na Mobini Sarya
MBUNGE wa Jimbo la Karagwe Gozibert Begumisa Blandes anatuhumiwa na wananchi wake kujipatia Ardhi yenye Ukubwa Hekta 45,000 katika kijiji cha Ruhita kata ya Rugu Mkoani Kagera ambayo ni makazi ya watu nakudaiwa kubadili eneo hilo kuwa lanchi yake ya kufugia.
Kutokana hatua hiyo wakazi wa vitongoji vitatu, Chamengo ,Miliro na Kigasha zaidi ya 1000 wamemtuhumu kuwa hatua yake ya kubadili makazi ya watu kuwa eneo la kufugia wanyama, wakazi hao wamejikuta amewaweka chini ya himaya yake wasijue la kufanya.
Wakazi hao wanadai kuwa Mbunge huyo alifanikiwa kujipatia eneo hilo wanaloona sio halali kwani ni makazi ya watu baada ya kuuda kikundi cha watu saba akiwemo Diwani wa kata ya Rugu Cleophace Gerevaz na kumshirikisha Mwenyekiti wa Kijiji hicho Cylidion Migeni ambaye hata hivyo ni miongoni mwa wanakikudi.
Baada ya Mbunge huyo kuunda kikundi hicho ambacho hakijafahamika jina walimshawishi Mwenyekiti huyo kuitisha kikao cha Serikali ya Kijiji Agoust 12 Mwaka jana ambapo katika kikao hicho alikabidhi madaraka kwa muda Eyustadi Raphael Chuma ili kupitia maombi ya kikundi chake.
Katika moja ya Vielelezo ambavyo Tanzania Daima imetumiwa vinaonyesha kuwa siku hiyo kikundi hicho kilijiyambulisha kuwa cha watu wafugaji walikuwa wanaoomba eneo la kufugia wanyama lenye ukubwa wa hekari 45000 na kupanda miti, ambapo walipitishwa maombi yao na kulipa shilingi Milion 2.5 ikaidhinshiwa wapewe hatimiliki.
“baada ya miezi mitano kupita tangu wakabidhiwe eneo hilo Mbunge huyo na wenzake waliwaleta watu wa idara ya ardhi kutoka wilayani karagwe wakapima na kuwekewa vigingi kisha wameanza kupeleka Polisi kutoka kituo cha kidogo cha Nyakanga wakiwatisha wakazi wa maeneo hayo kuwa wahame katika eneo lao waliouziwa”inasema sehemu ya malalamiko.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa hawezi kuhama katika eneo hilo kwa sababu hajui nani atawalipa fidia ya Nyumba na mashamba yao wala hawajui waende kuishi wapi kwani baadhi yao wameishi yao wameishi hapo kwa miaka zaidi ya hamsini kwa hiyo hawawezi kuhama bila fidia.
“Kinachoonekana kwa sasa huenda ukazuka mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji kwa inaonekana kuwa mkuu wa wilaya karagwe anaegemea upande wa mbunge kuwa serikali inao uwezo wa kuuza ardhi hata anapouliwa swala la fidia anatoa majibu ya kukwepa”inasema taarifa yao.
Hata hivyo moja ya sehemu ya vielelezo vya kikao cha kuridhia kutoa eneo hilo inaonyesha kuwa wajumbe waliomba kikundi hicho kuwa wakulima ndani ya vitongoji hivyo waheshimiwe, kikundi kilinde usalama wao na mali zao.
na kikundi hicho kikalipa pesa ambazo zemewekezwa Chama cha msingi Kasiki, K/Misha M.S.LTD yenye kumbukumbu namba KN 29651 na wakapewa stakabadhi yenye kumbu.na S.V.376369 ya Agoust 12 Mwaka jana.
Hata hivyo Mbunge huyo anadai kuwa eneo hilo ameliomba kama mwananchi wa kawaida na kupewa kihalali ili afugiwe wanyama wake kwani eneo hilo lilikuwa la malambi ya wakimbizi sasa wameondoka.
Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusi tuhuma hizo awali Mbunge huyo alikana kufahamu taarifa zozote kuhusiana na eneo hilo huku akidai kuwa hajapokea malalamiko yoyote lakini baadaye alikiri kupewa eneo hilo ingawa alikana kutoa pesa yoyote wala kununua.
“unasikia Mwandishi ukitaka kuandika taarifa nzuri muone Diwani atakueleza mimi sijapokea malalamiko yoyote wala sihusiki”alise Blandes lakini alipoambiwa mwandi yupo Dar es Salaam na anavielelezo vyote alisema
“napenda kukuambia kuwa eneo hilo lilikuwa makazi ya wakimbizi nimeomba kama mwananchi wa kawaida ili nifugie nimepewa kama vile angekodishwa mwanchi mwingine anayesema nimeuziwa ameona huo mkataba”?alihoji huku akikana kuunda kikundi wala kitoa malipo yoyote kama vilelezo vinavyoonyesha.
Aidha wakazi hao wamedai kuwa hata walipompelekea kilio chao hicho kwa mkuu wa wilaya yao kuhusu kulipwa fidia majibu yasiyoridhisha, kutokana na hali hiyo wakazi hao wanapanga kumuona Waziri wa ardhi John Magufuli wamweleze kwani wanadai mbunge wao ametumia madaraka yake kuchukua eneo hilo ikiwa ni miezi minane tu baada ya kushunda ubunge.

0 Comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home