Thursday, June 14, 2007

सुMATRA बलाज़ा LA USHAURI

OCS Trafic wa Dodoma M/S Mary akichangia hoja za wadau wa usafiri katika mkutano uliofanyika Dodoma hivi karibuni.






Katibu mtendaji wa Baraza la Usahuri la SUMATRA, Oscar Kikoyo akiwasilisha Mada katika mkutano wa kutoa Elimu ya awali kwa wadau mbalimbali wanaotumia vyombo vya Usafiri wa Nchi kavu na majini uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.



Baraza la Ushauri wa la watumiaji wa huduma za SUMATRA kiboko cha Makondakta na madereva wakorofi.

Katibu wake asema aliyepata ajali akashindwa kulipwa akifika kwao atalipwa.

Na Mobini Sarya.

“WANANCHI wanatakiwa kubadilika wajifunze kudai haki zao kwani sasa kila sehemu mabaraza ya kuwatetea walaji wanaonyanyaswa na wafanybiashara yameannzishwa na Abiria akishaingia katika chombo cha usafiri huyo ameingia mktaba na mwenye chombo ili amfikishe salama ,mwenye chombo asipofanya hivyo amevunja masharti lazima amlipe fidia” hiyo ni kauli ya katibu mtendaji Oscar Kikoyo wa baraza jipya la kutetea wasafiri na kuwashauri SUMATRA.

Baraza la Ushauri kwa Watumiaji wa huduma zinazosimamiwa na Mamlaka ya udhibiti na ukaguzi wa vyombo vya usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA Consumer Counsultative Council) lilianzishwa Februari 13 Mwaka 2005 chini ya sheria ya namba 9 ya mwaka 2001 na kifungu cha 29 kilichoanzisha Mamlaka ya Udhibiti na utoaji leseni wa vyombo hivyo.

Katibu mtendaji wa Baraza hilo Kikoyo anasema kuwa jukumu kubwa ya Baraza hilo ni kuwa kiungo kati ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na SUMATRA kama watoa huduma za Daladala, Basi na Meli, SUMATRA yenyewe na Serikali mkazo mkubwa ikiwa ni kuhakikisha kuwa maslahi ya watumiaji yanawasilishwa ipasavyo.

Kikoyo anasema kuwa baraza ni chombo kinachotetea maslahi ya wasafiri kwa hiyo anawaomba ushirikiano ili baraza hilo liweze kutimiza malengo yake kwa ufanisi ambayo ni kuwaelimisha watumiaji wa huduma za usafiri wan chi kavu na majini juu ya kudai haki zao , wajibu wa watoa huduma , na njia muafaka ya kutatua migogoro ambayo inaweza kujitokeza wakati wa kutoa huduma hizo.

pia baraza hilo linakazi ya kuongeza ushawishi wa haki za watumiaji wa haki za watumiaji wa huduma za usafiri kwa kuchangia maendeleo ya watumiaji wa huduma hizo kwa kuhamasisha vitendo vinavyoweza kuimarisha nafasi ya watumiaji wa huduma za usafuri wan chi kavu na majini.

Malengo mengine ya baraza hilo ni kufuatilia taarifa za hali halisi ya usafiri wan chi kavu na majini ,kushughulikia kero mbalimbali zinazohusu usafiri wa barabara ,majini na reline zikiwemo za mabasi ya mikoani na daladala, kushiriki kikamilifu katika kufuatilia hali ya usafiri wa nchi kavu na majini hatimaye kutoa ushauri jinsi ya kuboresha usafiri huo.

Kuishauri SUMATRA , Wizara na Serikali juu ya hatua zinazofaa kuchukuliwa ya kuboresha usafiri wa nchi kavu na majini, kujitangaza katika vyombo vya habari ili majukumu yake yaweze kufahamika kwa wananchi wote.

Pia baraza hilo liliundwa kwa lengo la kusimamia walaji ‘wasafiri’ kama wakili katika kutetea haki zao wanapokuwa wanadai, hadi sasa baraza hilo limekwisha toa Elimu ya awali katika mikoa minne ambayo ni Mbeya ,Dodoma ,Dar es Salaam na Pwani ili wananchi wafahamu namna ya kudai haki zao wanapokuwa wamepata matatizo katika vyombo hivyo vya usafiri.

Baraza hilo na ushauri na usuluhishi wa migogoro linasema Mtu anayefupisha ruti ya safari anakuwa amefunja mkataba wake wa Leseni kwahiyo anapaswa kuchukuliwa ikiwamo na kunyimwa leseni kwa kipindi kingine.

Sheria namba 9 inalipa Baraza mamlaka ya kushughulikia malalamiko ya abiria na kuishauri SUMATRA kuchukua hatua dhidi ya wahusika “unajua hao wamiliki wa vyombo vya usafiri ni wafanyabiashara na siku zote wamekuwa wakitafuta namna ya kupata faida kuliko kumjali mteja, hata ule msemo kwamba mteja ni mfalme hapa Tanzania haupo” anasema Kikoyo.

Kutokana na hali hiyo abiria wote wanashauriwa kuwa kila wanapopata ajali au matatizo kwenye safari wahakikishe kabla ya kwenda kutibiwa wanapitia Polisi kupewa Fomu namba 3 PF3 ili baada ya matibabu alipwe haki yao, pia mtu aliyeumia anashauriwa asipeleke malalamiko yao Mahakamani kwani anachelewa kulipwa, wapeleke malalamiko yao moja kwa moja Sumatra na watoe nakala kwenye Baraza ili kusimamia hayo madai.

Wananchi wanashauriwa kuwa njia rahisi ya kupata fidia baada ya kupata matatizo katika usafiri ni kupeleka PF3 Sumatra na kutoa Nakala katika hilo baraza kama mtetezi kisha Sumatra itamwita mwenyechombo itakaa itasikiliza malalamiko kisha itaamua pamoja na PF3 pia unatakiwa uwena Tiketi ya Basi ,Treni au Meli lakini kwa Daladala sio lazima kwani tiketi zao ni ndogo wala haziachi vilelezo kondakita anapochana.

Uamzi ukitolewa na Sumatra muathilika asiporidhika anakata Rufaa katika kamati ya rufaa inayochaguliwa na Sumatra ikiwa na wajumbe kutoka nje pia nakala inatolewa katika baraza kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi kamati inakaa kusikiliza pande zote mbili ikitoa maamzi kama kuna mtu ambaye hakuridhika tena anakata Rufaa baraza la usuluhishi wa ushindani kibiashara ambaye mwenyekiti wake ni Jaji wa Mahaka kuu kwa hiyo uamzi unaotolewa unakuwa ni wa Mahakama kuu ya Tanzania.

Kwahiyo wananchi wanashauriwa wakipata matatizo masuala yao yapitie sekta husika ili kuwahi kupata haki zao na sio Mahakamani kwani Kesi huchelewa kutokana na wingi wa majalada pia Baraza hilo linawatolea wito kama kuna mtu ameshindwa kulipwa haki yake baada ya kupata ajali anashuriwa kufika katika baraza hilo kwa ajili ya utaribu wa kupata haki zake.

Pia kutokana na ajali kuongezaka mara kwamara Baraza hilo linaandaa utaratibuwa wa kuwalazimisha wenyevyombo kuandika majina abiria wao wote kabla ya safari ili inapotokea ajali iwe rahisi kuwatambua ,ili kuona kazi hiyo inatekezwa kwa ufanisi Baraza hilo lipo mbioni kupeleka Ofisi zake mikoani ambapo zitakuwa chini cha Mkoa.

Kazi nyingine ya Baraza hilo ambalo watu wengi hushindwa kulitafautisha na SUMATRA ni kuhakikisha linasimia kwa dhati ,kutetea , kushauri na kuhimiza usafiri salama na bora wenye kuzingatia nidhamu na maslahi ya kila mmoja na kuhakikisha wanapigania kutopandishwa holela kwa nauli.

Kiutendaji baraza linaongozwa na katibu mtendaji ambaye majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha baraza linafikia malengo yake, linakuwa na wajumbe saba wanaoteuliwa na waziri wa miundombinu na wanakaa kwa miaka mitatu kabla ya kubadilishwa, baraza lililopita mwenyekiti wake alikuwa Alhaj Said El-Maamry, wajumbe wapya wanatarajiwa kuteuliwa wakati wowote na waziri.

“Abiria wakielimika wakadai haki zao hata hizi vurugu za daladala zitakwisha, hakuna tajiri atakaye kulipa kulipa faini kila wakati” anasema Oscar Kikoyo Katibu mtendaji wa baraza hilo ambaye anasema litakuwa kiboko cha wamiliki wa vyombo wakorofi.

Hili baraza la ushauri ni miongoni mwa Mbaraza manne ambayo yameundwa kwa ajili ya kuwatetea walaji mabaraza hayo ni Baraza la ushauri wa watumiaji huduma za angani ,baraza la ushauri watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRCCC) Baraza la ushauri wa watumiaji wa nishati na umeme na hilo la Wasafiri wa Nchi kavu.

Webste;www.mobinday.blogspot.com 0753 399 579 mobinsons@yahoo.com.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA NDUGU

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home